Hivi kwanini wanasheria huwa wanaitana wakili msomi

Hivi kwanini wanasheria huwa wanaitana wakili msomi

Naona wanasheria wameacha uzi utembee wenyewe na kuzalisha kejeri na dogoso zisizo za lazma.
Naomba mpokee jibu hakika.
Ikumbukwe kutunga na kutafsiri sheria ni fani ya kale sana na ina tabia ya kutunza ukale huo hadi leo katika utekelezaji wake.
Sasa mwanzo sheria ilikuwa haisomewi bali kupokezana kwa vizazi kwa kuchagua watoa maamuzi wenye uaminifu na maelekezo vyema umri ukiwa kigezo kimojawapo.
Baadae wakawepo watafsiri sheria wa kusomea wakifanya sambamba na waliorithi ujuzi huo.
Katika kujitambulisha ikawa wa kusomea wanaitwa wanasheria wasomi ili kujitofautisha na wale waliopokea maarfa kwa wazee.
Utamaduni ukaenea hivyo hadi leo.
Mengine ni porojo!
Yapo mengi tunayofanya leo katika fani nyingine ambayo hata hayana maana sana. Had miondoko. mavazi, gestures n.k.
 
Ni hivi, mfano, wewe ni Engineer maana yake wewe unafahamu sheria za ujenzi kwa undani.

Halafu mimi ni mwanasheria, maana yake ninazifahamu sheria zifuatazo:

1. Sheria za ujenzi.

2. Sheria za mazingira

4. Sheria za kazi

5. Sheria za uvuvi

6. List inaendelea.

Sasa hilo gap nililokupiga hapo, ndipo usomi wa mwanasheria unapoingia.
 
Lugha ya kazi hiyo ili wapate wateja wawapige hela nyingi...
Dalali msomi
Dereva fund
Beki kitasa
Dokta matelephone n.k n.k
Ukianza kuona hayo majina, jua bei utakayopigwa hapo
 
Hawajiiti, wanaitwa.

Wakili Msomi sio cheo cha kujivika, ni jina wanalopewa kutokana na historia ya fani ya sheria.

Zamani wanasheria walihudumu katika makasri ya kifalme na waliwajibika kumuongoza mfalme katika njia inayostahili kwa mujibu wa miongozo.

Taaluma yao ilikuwa ni ya kifalme zaidi, na walithaminika mno. Ndio maana wakaitwa LEARNED BROTHERS.

Walijifunza mambo mengi sana ili kumuwezesha mfalme aendeshe nchi kwa ufanisi.

LEARNED maana yake ni jina la heshima linaloakisi ujuzi wa mambo mengi. Ni utamaduni baina ya wanasheria kuitana kwa heshima kubwa sana.

Hata walimu pia hawajakatazwa kujiita WASOMI. Unaweza ukajiita MWALIMU MSOMI.

Au jiite MFANYABIASHARA MSOMI, AU FUNDI MSOMI, AU DOKTA MSOMI, FUNDI CHEREHANI MSOMI, WAZIRI MSOMI nk.

Hii ni nchi ya kidemokrasia, hata ukitaka kujiita BWABWA pia ni RUKSA.

Cc Lamomy
 
Mwenye kufahamu naomba anifahamishe hivi kwanini wanasheria mnaitana wakili msomi 🤔 kwani kuna mawakili sio wasomi ?
Ushamba tu,wakili msomi kuna wakili hajasoma?
Hana confidence.
Ukiona mtu anajipakia mavyeo kibao mahd sijui jua hii ndaza hii
 
Nakazia wengi wao ni ma bush loya tena Kuna fala mmoja kaniharibia kesi yangu 😏😏😏😏😏
Kesi yako yenyewe ya ubakaji unalawiti watoto wadogo unafikiri kuchomoka ni mchezo mchezo tu??

Vielelezo vyote viko ngangari, ukichungulia ripoti ya daktarii iko ngangari, ukiangalia ushahidi wa macho uko ngangari, ukiangalia maelezo ya polisi yako ngangari, UNACHOMOKAJE KWA MFANO?

NGANGARI NGUNGURI, ni nyundo tuu.

Miaka mia saba jela.
 
Katika taaluma za wapenda ujiko basi hao wa Sheria ni wenyewe.

Mpaka kwenye misiba ya wenzaosiku hizi wanavaa yale majoho Kenyatta huwa anayaita magauni.
 
Mwenye kufahamu naomba anifahamishe hivi kwanini wanasheria mnaitana wakili msomi 🤔 kwani kuna mawakili sio wasomi ?
Hapana hiyo ni misemo tu ilizuka mtaani na hasa hasa ilitokea kwa vijana wa chadema kipindi kile Tundulisu alivyopata umaarufu kwa kuendesha kesi mbalimbali akawa anashinda.
Sasa kwa furaha yao vijana wa chadema ndio wakawa wanamshangilia na kumuita Wakili msomi na msemo ukapata umaarufu na kuenea mitaani.
Ni kama tu Mange kimambi wanavyomuita dada wa Taifa kwani yeye ndio dada mkubwa kuliko madada wote wa Tanzania?
Au ni sawasawa na Fatma Karume wanavyomwita Shangazi wa Taifa kwani yeye ndio shangazi mkubwa kuliko mashangazi wote wa Tanzania?
 
Ushamba tu,wakili msomi kuna wakili hajasoma?
Hana confidence.
Ukiona mtu anajipakia mavyeo kibao mahd sijui jua hii ndaza hii
Wakili Msomi ni jina la Kihistoria. Hawajiviki tu.

Enzi hizo za zamani, taaluma ya uanasheria ilikuwa inarithishwa kama mapokeo. Haikuwa elimu ya darasani.

Baadaye wafalme wakaanza kuwatumia wanasheria katika falme zao, na ikabidi waanzishe elimu rasmi ya sheria ili ku-formalize.

Ndio hiyo sababu, wanasheria wa darasani wakataka kujitofautisha na wanasheria waliopata ujuzi wa sheria kwa kurithi. Wakajiita WANASHERIA WASOMI.

Hawa ni wasomi wa kusomea. Na kiukweli kati ya taaluma ambazo ni CROSS-CUTTING basi ni SHERIA.

Ukiwa mwanasheria unajifunza kila kitu katika ulimwengu. Angalau miongozo ya KILA KITU.

KILA KITU kimewekewa sheria, hakuna jambo lisilo na sheria kwa hiyo unajikuta unasoma mambo yote.

WAKILI MSOMI sio cheo, ni jina la kihistoria.

Na wewe jiite FUNDI CHEREHANI MSOMI au DOKTA MSOMI.

Hata kudunga sindano za machanjo ni USOMI pia, kwanini hamjiiti??
 
Sababu wakili (advocate ) maana yake ni mtetezi, na mtu yeyote anaweza kuwa mtetezi, hivyo lazma kutofautisha mtetezi aliyesomea na ambaye hakusomea, pia kazi ya mwanasheria inahitaji KUSOMA KILA SIKU HADI UNASTAAFU, tofauti na taaluma nyingine vitabu vya taalluma vinaachwa shuleni na vyuoni na ukiwa navyo ni mapambo.
 
Wakili Msomi ni jina la Kihistoria. Hawajiviki tu.

Enzi hizo za zamani, taaluma ya uanasheria ilikuwa inarithishwa kama mapokeo. Haikuwa elimu ya darasani.

Baadaye wafalme wakaanza kuwatumia wanasheria katika falme zao, na ikabidi waanzishe elimu rasmi ya sheria ili ku-formalize.

Ndio hiyo sababu, wanasheria wa darasani wakataka kujitofautisha na wanasheria waliopata ujuzi wa sheria kwa kurithi. Wakajiita WANASHERIA WASOMI.

Hawa ni wasomi wa kusomea. Na kiukweli kati ya taaluma ambazo ni CROSS-CUTTING basi ni SHERIA.

Ukiwa mwanasheria unajifunza kila kitu katika ulimwengu. Angalau miongozo ya KILA KITU.

KILA KITU kimewekewa sheria, hakuna jambo lisilo na sheria kwa hiyo unajikuta unasoma mambo yote.

WAKILI MSOMI sio cheo, ni jina la kihistoria.

Na wewe jiite FUNDI CHEREHANI MSOMI au DOKTA MSOMI.

Hata kudunga sindano za machanjo ni USOMI pia, kwanini hamjiiti??
Sawa Wakili msomi
 
Mwenye kufahamu naomba anifahamishe hivi kwanini wanasheria mnaitana wakili msomi 🤔 kwani kuna mawakili sio wasomi ?
Ingia
Humu imeshajadiliwa..

 
Mwenye kufahamu naomba anifahamishe hivi kwanini wanasheria mnaitana wakili msomi 🤔 kwani kuna mawakili sio wasomi ?
Hii ni taaluma inayohitaji kusoma Kila wakati. Sio tu kusoma sana wakati unaadaliwa Bali hata wakati unatekeleza majukumu yako. Fikiria kwa mfano kwa kipindi Cha miaka 5 tu, Sheria ngapi zimebalika na kuterekebishwa? Ni kesi ngapi (precedents) zimeandikwa? Na kwanini? Hivyo kama wewe sio Mtu wa kuji update kwa kusoma na kuresearch Kila wakati lazima upate shida sana. Hasa unapokuwa Mahakamani.

Ndio maana inaitwa LEARNED PROFESSION. Sidhani kama Kuna taaluma yenye kusoma kwingi kama Sheria.
 
Wakili Msomi ni jina la Kihistoria. Hawajiviki tu.

Enzi hizo za zamani, taaluma ya uanasheria ilikuwa inarithishwa kama mapokeo. Haikuwa elimu ya darasani.

Baadaye wafalme wakaanza kuwatumia wanasheria katika falme zao, na ikabidi waanzishe elimu rasmi ya sheria ili ku-formalize.

Ndio hiyo sababu, wanasheria wa darasani wakataka kujitofautisha na wanasheria waliopata ujuzi wa sheria kwa kurithi. Wakajiita WANASHERIA WASOMI.

Hawa ni wasomi wa kusomea. Na kiukweli kati ya taaluma ambazo ni CROSS-CUTTING basi ni SHERIA.

Ukiwa mwanasheria unajifunza kila kitu katika ulimwengu. Angalau miongozo ya KILA KITU.

KILA KITU kimewekewa sheria, hakuna jambo lisilo na sheria kwa hiyo unajikuta unasoma mambo yote.

WAKILI MSOMI sio cheo, ni jina la kihistoria.

Na wewe jiite FUNDI CHEREHANI MSOMI au DOKTA MSOMI.

Hata kudunga sindano za machanjo ni USOMI pia, kwanini hamjiiti??
Wataanza kulia kwa kwikwi.Wape nyongeza.
 
Lugha ya kazi hiyo ili wapate wateja wawapige hela nyingi...
Dalali msomi
Dereva fund
Beki kitasa
Dokta matelephone n.k n.k
Ukianza kuona hayo majina, jua bei utakayopigwa hapo
Hahaha... hakuna kitu kama hicho.

Hata majaji wanaitwa JAJI MSOMI, au HAKIMU MSOMI, au WAKILI WA SERIKALI MSOMI.

A learned judge, a learned magistrate, a learned state attorney, a learned counsel.

Haya sio majina ya ujiko au ya kutafuta fedha, ni majina wanayoitana watu wa fani ya sheria kwa malengo ya KUHESHIMIANA na si vinginevyo.

Hata Jaji akitaka kumuita Wakili lazima aseme WAKILI MSOMI. Wanapeane heshima kwa namna hiyo.

Unaweza pia ukajiita POLISI MSOMI.

Kama unajiamini umesoma kwani unaogopa nini? Msomi akijiita msomi kuna tatizo?

Jiite POLISI MSOMI, ukichekwa shauri yako. Au MGAMBO MSOMI.

MKURUGENZI MSOMI, SEKRETARI MSOMI, MKUU WA WILAYA MSOMI.
 
Back
Top Bottom