Hivi kwanini wanasheria huwa wanaitana wakili msomi

Hivi kwanini wanasheria huwa wanaitana wakili msomi

Engineer baki hivyo hivyo kuna watu wamesoma sociology, community development wanaandika projects wanapata hela sana, ww baki na engineering yako
Hahah we unadhani ningekuwa sina hela ningejivunia uinjinia?
 
Hata engineer anakuwa anazijua kwa sababu ndiye mtekelezaji wa hizo sheria. Kuzijua sheria siyo lazima uwe mwanasheria au wakili.
Issue ni kwamba Sheria zipi anazijua?
Hata sisi cpa tunazijua Sheria za kodi, lakini hatuwezi kusema tunajua sheria
 
Ni hivi, mfano, wewe ni Engineer maana yake wewe unafahamu sheria za ujenzi kwa undani.

Halafu mimi ni mwanasheria, maana yake ninazifahamu sheria zifuatazo:

1. Sheria za ujenzi.

2. Sheria za mazingira

4. Sheria za kazi

5. Sheria za uvuvi

6. List inaendelea.

Sasa hilo gap nililokupiga hapo, ndipo usomi wa mwanasheria unapoingia.
Hiyo sio sababu ya kujiita msomi.

Mfano mimi injinia na nnajua sheria ya ujenzi, manunuzi, mazingira, sheria ya mikataba nk nk je na mimi ni wakili msomi?
 
Mwansheria ni mtaalamu wa kila sekta.

Kila sekta ina sheria, na hivyo mwanasheria anawajibika kuzifahamu.

Pia sekta zote zina kesi na hivyo mwanasheria anahusika nazo.

Ina aminika kwamba, mwanasheria ni mtaalamu anayeongoza kwa kuwa na elimu pana kuliko taaluma zote duniani.

Hii ndiyo sababu sisi Wanasheria kuitana wasomi yaani Learned lawyer/Advocate.
Kabisa, kwa akili yako unaona mwanasheria anaifahamu kila sekta, hence, kwa mfano, tuseme anaweza akafanya kazi za daktari, mhandisi, mkemia etc?
 
Issue ni kwamba Sheria zipi anazijua?
Hata sisi cpa tunazijua Sheria za kodi, lakini hatuwezi kusema tunajua sheria
Hiyo ni wewe tu wengine wanajua sheria nyingi nyingine. Hata wakili hajui sheria zote. Sheria zipo nyingi sana hawezi kuzijua zote. Linapojitokeza jambo linalohusu sheria fulani ndipo anaitafuta hiyo sheria, anaisoma na kujiandaa kwa ajili ya jambo hilo. Na engineer vivo hivyo. Huwezi kuisoma sheria fulani kujifurahisha tu bila kuwa na matumizi ya hiyo sheria wakati huo. Isitoshe siyo lazima usome sheria yote bali unasoma vipengere vya hiyo sheria kwa jambo lililojitokeza wakati huo.
 
Mtu kama ni msomi ni msomi tu. Huwezi kumuondolea hilo.

Usomi siyo kukariri na wala haupimwi kwa vitisho.

Huyo konda mwenyewe elimu yake inafahamika na kila Mtanzania, kwa hiyo hana kigezo cha kumpima aliyesoma.

Kama wewe unajiona umesoma na una uhakika, basi jiite msomi tu maana hakuna kizuiIzi.

Punguzeni makasiriko.
Yule jamaa ambae ni WAKILI tena memba wa TLS ambae hajui kusoma ulimsikia?.....
 
Kabisa, kwa akili yako unaona mwanasheria anaifahamu kila sekta, hence, kwa mfano, tuseme anaweza akafanya kazi za daktari, mhandisi, mkemia etc?

Nimesema anafahamu kanuni na taratibu za sekta mbalimbali. Sijasema anajua kazi ya udaktari.

Mbona una kichwa kigumu aisee!

Mfano, mimi kwenye Tort Law nimejifunza medical negligence pale ambapo mtaalam wa afya anapofanya kazi zake na kusababisha madhara kwa mteja.

Hapo ndipo msomi wa sheria inapoingia kutatua changamoto hiyo na kuamua je, kuna kosa au lah..
 
Hiyo sio sababu ya kujiita msomi.

Mfano mimi injinia na nnajua sheria ya ujenzi, manunuzi, mazingira, sheria ya mikataba nk nk je na mimi ni wakili msomi?

Hapana. Ni Injinia Msomi. Wewe jiite hivyo wala usiapate tabu
 
Back
Top Bottom