Hivi kwanini hununui na kusoma vitabu?

Napenda kusoma vitabu vya riwaya tu, yan napenda haswa. Ila viwe kwa kiswahili MF. Damu na machozi, Rais anampenda mke wangu, mfadhili, Vuta nkuvute, Takadini and the like....

Hongera sana mkuu. Riwaya zinaburudisha, fikirisha na kufundisha pia.

Hivyo vitabu vya kiingereza navyo ni riwaya au vya kitaaluma? Unahisi shida ni nini hadi hivyo unashindwa kuvimaliza na kuwa bored?
 
Binafsi ishanipita hiyo ila ntakomaa na machalii wangu wasome vitabu
Mbona unakata tamaa mdau! Usomaji wa vitabu hauna umri. Kujifunza ni mchakato usio na mwisho.

Tunaomba tujue kwa namna gani unadhani unaweza kuhamasika kusoma ili uweze kukomaa vizuri na machalii wasome vitabu. Ni rahisi zaidi wakikuona unasoma pia!
 
Daah vitabu pekee niliwahi kusoma ni james Hadley hand me the fig leaf job na cha gamba kikosi cha kisasi baasi nina soft copy nying ila daah sisomi aiseee.

Kimsingi sijakuzwa kusoma vitabu yanahitajika maamuzi ya makusudi.
 
Daah vitabu pekee niliwahi kusoma ni james Hadley hand me the fig leaf job na cha gamba kikosi cha kisasi baasi nina soft copy nying ila daah sisomi aiseee
Kimsingi sijakuzwa kusoma vitabu yanahitajika maamuzi ya makusudi

Ulijisikiaje wakati unasoma hivyo vitabu mkuu? Burudani pekee au vilikupa mawazo/maarifa mapya?

Tunaamini hayo maamuzi ya makusudi unaweza kuyachukua kwa kurejea hisia na faida ulizozipata kiakili wakati unamsoma James Hadley na Gamba.

Au kwako kikwazo ni kipi?
 
Mkuu utamaduni wa kusoma vutabu umeharibika tangu zama za shule za msingi. Sasa mtu anasogea npaka levels za juu tayari tabia inakua imeshajijenga. Suala jingine ni uhaba wa maktaba mahala watu wanapoishi au kufanyia kazi.
 
Binafsi sikukuzwa hivyo ndio maana nashindwa kusoma, ila kununua nanunua kimtindo, huku nilipo boss wangu anasoma sana vitabu, amenishawishi nisome nikamwambia anilipe kwa kila kitabu ntakachosoma akaniona hamnazo
Hukukuzwa hivyo kivipi? Kama umepitia ahule basi umekuzwa kusoma vitabu. Shule zinahimiza kusoma vitabu na hasa kuanzia awamu ya mkapa mpak Magufuli, vitabu vya kiada na ziada ni vingi hivyo kutlkusoma ni tabia uliojijengea na si kukuzwa.Pamoja na mapungufu ya elimu yetu serikali inajitahidi kuleta vitabu vya kiada, labda vya ziada.

Basi jitahidi kuwahimiza watoto wako wasome vitabu.Kati ya citu mwafrika amevikataa ni kusoma vitabu na kuandika vitabu. Kuna mambo yetu mengi sana hayajaandikwa vitabuni.
 
Hukukuzwa hivyo kivipi? Kama umepitia ahule basi umekuzwa kusoma vitabu. Shule zinahimiza kusoma vitabu na hasa kuanzia awamu ya mkapa mpak Magufuli, vitabu vya kiada na ziada ni vingi hivyo kutlkusoma ni tabia uliojijengea na si kukuzwa.Pamoja na mapungufu ya elimu yetu serikali inajitahidi kuleta vitabu vya kiada, labda vya ziada...
Mzee unahisi wote tuliposoma hivyo vitabu vilikuwa vinafika? Hata ikitokea vimefika ni vitabu vinne kwa wanafunzi zaidi ya mia mbili, kweli elimu yangu iliisha kupindi cha utawala wa marehemu mkapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom