Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,513
- 167,150
MAMBO KUMI(10) YA KUZINGATIA KWENYE USOMAJI VITABU
NA: NAAMALA SAMSON
1. SOMA kitabu kinachohusisha kitu unachokipenda. Kama unapenda mapishi/uongozi/IT/ushairi, saka kitabu cha mapishi/uongozi/IT/ushairi soma. Utaenjoy kukisoma. Sio unasoma mambo yanahusu "roketi" wakati hata huyapendi,utakuwa unajilazimisha na utaishia njiani😀
2. Anza na kitabu kifupi. Ukitaka kuona raha ya kusoma na kumaliza, saka hata chenye 50 pages ama 100 pages. Vipo vingi tu. Na utakimaliza hata ndani ya wiki. Hapo ndo ukisema kila siku usome 20 pages. Ila wasomao fasta, 100pages ndani ya siku moja hadi mbili kakimaliza. Mimi niliwahi kumaliza kitabu cha 84 pages ndani ya nusu saa! Yes! Nusu saa kimeisha. Na nikaelewa kila kilichomo na kushare kwenye group. Wenzangu hata page ya 30 walikuwa hawajafika! Yote ni UKIZOEA kusoma kwa speed. Inakuwa ni tabia. Haikwepeki.
Halafu itakusaidia sana ukiwa kiongozi/meneja mradi/mfanyabiashara mahali ukapewa ripoti, unaisoma mwanzo mwisho. Hata iwe na 2000 pages ama zaidi. Kama zile ripoti za CAG!😀 Maana usipozipitia,hautagundua makosa.
3. Saka kitabu chenye maandishi na michoro. Hasahasa kama u mpenzi wa kujifunza kwa picha. Hujawahi jiuliza vitabu vya watoto vingi kwanini vina picha? Vinamsaidia msomaji ku-visualize kirahisi sana. Na anaelewa kwa haraka sana.
4. Tumia muda ukiwa idle, foleni, lunch, safari ndefu (ndege, treni, boti), na mapumziko yoyote kujisomea. Kuna mtu anasema hana muda wa kusoma ila anakuwa masaa manne kwenye foleni akiwa anatokea na kurudi nyumbani kutoka kazini. Sasa badilika. Anza kubeba kitabu ukiwa unaenda kazini, soma kwenye gari/daladala (Acha wakutanie eti mzungu😀 usijali). SOMA! Hautajipunguzia lolote bali utajiongezea maarifa.
5. Kama hupendi maandishi, siku hizi unaweza kuona vitabu vimewekwa kwa njia ya audio na video/film/animation. Ni njia nyingine ya kuelewa sana kitabu. Mfano film ya THE GIFTED HANDS, HARRY POTTER, A MAN OF THE PEOPLE, JESUS na films kibao zingine zimetokana na story za vitabu. Ukiona huelewi maandishi, saka movie yake utazame. Ndani ya lisaa limoja na nusu ukimaliza kuona movie unaelewa kitabu kinahusu nini. Ama audio version yake kupitia podcasts.
Wakati wengine wanasikiza nyimbo ya DODO ama JEJE, wewe Umeweka zako earphones unasikiliza "100 WAYS TO MOTIVATE PEOPLE".
6. Usisome kushindana. Hili ni kosa ambalo wengi tunalifanya. Unashindana kusoma? 😀 shindana na nafsi yako sio na mtu mwingine. Jiwekee lengo ndani ya wiki kumaliza kimoja walau. Ukimaliza unajipongeza kwa kujinunulia zawadi. Jipongeze! Ni hatua kubwa sana.
7. Usisahau kuandika summary ya ulichosoma. Wengine wanatumia "highlighter" kuainisha main points. Ni sawa pia. Inakusaidia kujua ulichojifunza kirahisi na kukumbuka. Na kufanyia kazi.
8. Ukiweza pia jiunge na makundi ya wasomaji wenzako. Whatsapp, Telegram, na mitandao mingine kuna groups kuhamasisha usomaji. Kama hili pia. Ambapo inakusaidia kupata kuelewa vitabu vilivyopo na mbinu mbalimbali za usomaji. Inakusaidia kutoondosha ari ya usomaji. Na kuna libraries nyingi siku hizi,tuzitumie kusoma na kwenda kukaa na kuandika pia.
Wengine wanasema usomaji ni wito!😀 Na huo wito pia nawe unao. Usijidharau.
9. Kama uendavyo gym kusaka six packs, kitabu ni gym ya ubongo. Yani ukitaka kujua mtu ana uelewa kiasi gani, usiombe kukutana na aliyesoma vitabu vingi na akavielewa. Hata maongezi ya anayesoma vitabu na asiyesoma huwa ni tofauti. Usikubali kuwa na ubongo usio na six packs,kisa hausomi😀 Ubongo utakuwa na kitambi!! SOMA uushughulishe! Kwa kutafakari na kung'amua la kufanya. Unakuwa smart na mbunifu sana katika uyafanyayo.
Na anayesoma utaona hata style ya uandishi wake- imekuwa influenced/imechagizwa na style ya waandishi wengine.
10. Tumia device uipendayo kusomea. Japo inashauriwa zaidi kusoma hardcopies(kuna raha yake ya kushika kurasa na kuzifunua,na haiumizi macho kama devices nyingine), lakini chagua device inayokufaa. Wapenda kwenye simu? Tablet?Laptop? Kindle(hii tablet maalum ya kusomea yenye vitabu lukuki)? Unaweza jaribu kikufaacho na ukakitumia.
Kumbuka: Kusoma ni kwa faida yako na taifa lako. SOMA usiwe mzigo kwa nafsi yako. Soma usiwe mzigo kwa jamii yako.
Tuendelee wasiliana na kuzidi kuhamasishana kujisomea.
Kama umeweza kusoma hadi hapa mwisho, basi unaweza kusoma kitabu chochote na ukakielewa. Safari njema ya usomaji.