Kwanini ni muhimu kusoma?

josephdeo

Member
Nov 23, 2015
95
196
Rais wa awamu ya tatu Hayati Benjamini Willliam Mkapa aliwahi kusema, ukitaka kumficha mtanzania kitu chochote mfiche kwa njia ya maandishi. Sisi binafsi tunaungana na kauli hii kwa asilimia 100. Asilimia kubwa ya Watanzania hawapendi kusoma kabisa jambo ambalo linatufanya kuwa nyuma sana kwa baadhi ya mambo. Wanasema kuwa mambo yote yapo kwenye maandishi na maandishi pia ndio yana elimu kwani kila jambo ni lazima liwe kwenye maandishi na kunazo faida nyingi na kubwa sana kwenye kusoma. Hii inapelekea kuwa na watu wenye ufinyu wa maarifa kwani hakuna mtindo ambao ni madhuti wa kujisomea maandiko mbalimbali. Tumekuwa kama wasindikizaji kwani tunashindwa kujifunza kwa kusoma na matokeo yake tunataka kuwa kama wao kwa kuwatazama tu jambo ambalo aliwezekani hasa hasa kwenye ulimwengu wa sasa ambao umejaa hadaa nyingi sana. Ni muhimu kusoma na kama kijana au mtu wa kariba nyingine ni muhimu sana kutenga mda ambao unaweza kujisomea hasa hasa vitabu na makala kama hizi hii itasaidia kupanuka kwa ubongo wako katika kufikiria.


Mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema ili uwe msemaji bora duniani lazima uwe msomaji mzuri sana pia lazima uwe msikilizaji mzuri sana. Ukweli ni kwamba watanzania tulio wengi hatuyazingatii Haya masharti, wengi wetu ni wasemaji na hawapendi kusikiliza pia wengi hatupendi kusoma. Jambo ambalo linapelekea kutokuwa na wataalamu wengi kwenye tasinia mbali mbali na hii inatoka chini kabisa wakati wa makuzi ya watoto hapa ndipo wazazi hufanya kosa hili na pengine kwa kutokujua kwa maana utaratibu huu wa kusoma sio wa kwetu kabisa. Unapaswa kuanza kufundisha mtoto kusoma akiwa mdogo kabisa kati ya miaka 3 mpaka 5 hii itasaidia kufahamu kuwa kusoma ni sehemu ya maisha na badala ya kutizama luninga kwa mda mrefu wewe mletee vitabu vya hadithi na kujifunza ili aweze kufahamu kuwa mambo mengi katika dunia hii ya leo yapo katika maandishi. Mtengenezee mazingira haya ili akija kukua awe moja kati ya watu ambao wameelimika na sio msomi na wenye uwezo wa kujenga hoja zenye mashiko mbele za watu na kuweza kuwa na fikra yakinifu katika mambo yake ya kila siku. Maandizi ya baadae hufanyika sasa hivyo anza kumfundisha mtoto wako kusoma vitabu mbalimbali hili kuweza kutengeneza uwezo mzuri wa kufikiri.


Wenzetu wa mataifa mbali mbali wametupiga hatua kubwa sana kuliko sisi kwa sababu ni wafuatiliaji wazuri sana wa hizo kanuni. Matokeo yake sisi tumekuwa tukitafuta utatuzi wa matatizo yetu kwao kwa kukosa watu ambao wanaweza kuyatatua na hii ni kushindwa kuwa wasomaji wazuri wa majirida na vitabu. Moja kati ya watu walikuwa na uwezo nchini kwetu marehemu Ruge aliwahi kusema kuwa sisi tunayafahamu matatizo yetu vyema kuliko mtu mwingine yoyote lakini cha ajabu ni kuwa tunataka watu wasioyafahamu matatizo yetu kuja kuyatatua na hii ilitokea wakati wa kampeni yake ya fursa kupitia kituo cha redio alichokuwa akikiongoza Clouds fm. Hii inatokana na ukweli kwamba sisi hatujawahi kutafuta suluhisho la matatizo yetu zaidi ya kumtafuta wa kumbebesha lawama hizo na hii inatokea kwa kukosa maarifa ya utatuzi maarifa hayo ambayo yanapatikana kwa kusoma vitabu. Maneno ya MUNGU yanasema kuwa "watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa" na hii nikutokana na kushindwa kusoma vitabu na maandishi mengine. Leo hii tunaona matatizo makubwa ya kimkataba ambavyo yanawavuruga watu wengi na hii yote ni kwa sababu hawakusoma na kuelewa ila wakajikuta tu wameweka sahihi yao na hata tukizungumza tu ukweli huwa unasoma vigezo na masharti ambavyo unapewa kabla ya kuanza kutumia App yoyote ile au huwa unakubali tu bila kusoma.


Watu wengi wamekuwa wavivu kusoma na kuona kana kwamba wanapoteza muda kufanya hivyo bila kufikiria kuwa muda ambao wangeutumia kusoma wangeongeza maarifa ambayo yangesaidia kutatua matatizo yao kwa urahisi sana kuliko kuona wanapoteza mda kisha wanautumia huo mda kuangaika pasipo kuwa na maarifa. Jiwekee utaratibu wa kusoma ili sasa uweze kuwa na maarifa ya kutosha kukabiliana na changamoto za maisha ni vyema mno kusoma kuliko kutazama luninga yako tenga huo muda ambao unatakiwa kutazama luninga wewe jifunze kusoma na unaweza kuanza kusoma makala hizi na kisha kupata ujuzi ili sasa uweze kusoma vitabu. Tunakuomba na kukusisitizia kuwa kusoma ni muhimu na ni vyema kwa afya yako ya akili kwani yote ambayo unayaona sasa yapo kwa maandishi na ikiwa kama unataka mabadiliko ya kifikra basi anza kusoma vitabu ili uongeze uwezo wako wa matumizi ya akili yako.



Shukurani nyingi ziende kwa MWENYEZI MUNGU kwa kutujalia sisi kukuletea haya wewe. Kwa maoni na ushauri tafadhali wasiliana nasi kupitia nambari +255766604683 au kupitia email josephdeogratius70@gmail.com au kupitia mitandao yetu ya kijamii kama vile: Facebook JOSEPH DEOGRATIUS, Twiter JOSEPHDE14, Instagram JOSEPHDEO70. Asante!

IMG_20220325_102121.jpg
 
Nimesoma nikataka kuishia njiani, roho ikanisuta nikamalizia….. jitahidi kutuletea makala zaidi na zaidi hapa jamvini.

Kwa kuwa umemtaja Mungu, niongezee tu hapo kuwa Mungu ndiye muasisi wa maandishi….. ndiyo maana aliweka neno lake kwenye maandishi ili watu wasome.

Maandishi ni muhimu sababu ni mtu mwenye akili timamu tu anayeweza kuandaa na kuandika kitabu, tofauti na vipindi vya luninga ambavyo hata kilaza anaweza kuongoza kwa kubwabwaja na kuuza sura.
 
Sikupingi ila niliwahi kufanya uchunguzi kwa sisi waafrika kukaa na kutenga muda kwa ajili ya kujisomea ni Jambo gumu wanalomudu wachache.

Vijana wengi endapo utakaa mahala na kusikiliza maongezi yao ni mada za ngono, ipi dawa nzuri ya nguvu za kiume na vitu kama sex position za kufikia vilele.

Niliwahi kaa sehemu tangu nimefika mpaka naondoka vilivyokuwa vinazungumziwa nilisikitika sana hii yote katika makuzi wazazi hawakutupa mazoea hayo kama ulivyogusia.

Kuna familia niliwahi kufika kuishi hapo kwa muda nilikuta bwana mdogo anafuatilia kipindi cha Air crash investigation cha National Geographic nilifurahi sana na nilimchunguza mara kwa mara channel zake ni Kama discovery nikagundua haya mambo yanaanzia chini.
 
Maoni,

mafupi tu natoa...
Hizo aya zako atleast zipunguze uvutie hata wavivu kusoma wasome, watu ni wavivu ndio ila usiwakomeshe sasa

Kusoma ni chakula cha ubongo, kama ilivyo msosi na tumbo

Toka nilijue hilo nimeweka utaratibu wa kusoma baadhi ya vitabu kila mwaka.
Ni rahisi kumshawishi mtu aendelee kusoma kitu ukiandika aya ambazo haiztishi

Nimeandika maneno mengi kiasi ila si umesoma bila kuboreka 😅...ona juu nilivyoanza
 
Back
Top Bottom