Hivi kwanini hununui na kusoma vitabu?

Hivi kwanini hununui na kusoma vitabu?

Ulijisikiaje wakati unasoma hivyo vitabu mkuu? Burudani pekee au vilikupa mawazo/maarifa mapya?

Tunaamini hayo maamuzi ya makusudi unaweza kuyachukua kwa kurejea hisia na faida ulizozipata kiakili wakati unamsoma James Hadley na Gamba.

Au kwako kikwazo ni kipi?
Kiukweli ukiwa unasoma soma vitabu kuna u sharp flani unakua nao akilini ambao saizi nikiji analyze najiona kabisa uwezo umepungua
Roho inaniuma, plus maarifa unayo yapata ni mazuri sana
Nikisoma vitu watu wanaandika humu nasema daah hawa jamaa ni kusoma tu ndio wamejua aya
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Unafurahisha na kusikitisha at the same time

Kwahiyo maarifa yamekutosha mkuu?
Yamenitosha sanaa aisee...sikuhiz elimu ni more of visual na sio maandish...najifunza kwa kuona kitu kinafanywa ama kusimuliwa..sio kusoma maandish..nna alergy..maaana nmesoma saaaana..na havijanisaidia kihiiivyo
 
Kama sababu ni kuchoka na kazi, vipi kujisomea kwa siku za mapumziko?
Siku za mapumziko niko na familia...outing za hapa na pale....mkuu.skuhiz elimu is more of visual...najifunza kwa kuona kwa macho na kusikiliza.na ndomana wenye platforms za visual na kuskilizaa ndio wana survive dunia ya sasa...najifunza meng youtube..tv n radio...kusoma maandish karne hii ni ngum mno.so waandish mngebadilika kuendana na dunia inavyotaka
 
Kuna audio books,visualization za vitabu kibao kwenye youtube kote huko unapata vitabu hivyohivyo vilivyoandikwa ila usiseme kwamba umetosheka maarifa cause haya maisha yanahitaji skills nyingi so ni vizur katika maisha yako yote ukajifunza either kupitia watu, matukio ,na vitabu lakini vitabu ni best kwa sababu mwandishi ameandika kile alichopitia kwenye nyanja fulani kwa undani zaidi na lazima amefanya uchunguzi kwenye hilo suala

A person who doesn't read has no difference with a person who can't read
 
Mdau MR BINGO umeiweka vizuri sana hii. Asante.
 
Kiukweli ukiwa unasoma soma vitabu kuna u sharp flani unakua nao akilini ambao saizi nikiji analyze najiona kabisa uwezo umepungua
Roho inaniuma, plus maarifa unayo yapata ni mazuri sana
Nikisoma vitu watu wanaandika humu nasema daah hawa jamaa ni kusoma tu ndio wamejua aya

Ni kweli. Akili ya mtu anayesoma sana ipo sharp na ina majibu ya maswali mengi kwa haraka. Kuna maajabu kwenye hili.

Sasa una mpango gani? Unadhani kitu gani kinaweza kukuhamasisha ukarudi tena kwenye kusoma vitabu?
 
Halafu wengi ni choka mbaya, watu wa fantasies. Yaan nitoke kibaruan nmechoka nisilale nisome kitabu? Vitabu nilivyosoma toka darasa la kwanza mpaka namaliza chuo kikuu miaka mi4 vinatosha sana kwa maarifa.

Kwa mujibu wa bilionea wa Zimbabwe ndugu strive masiyiwa anasema hii tabia ya waafrica kuamini kwamba kusoma kunaishia unapomaliza chuo ndio sababu kuu bara la Africa kuendelea kuwa maskini

Watu wengi miongoni mwetu hatuji update kimaarifa ndio maana bara letu limedumaa kimaendeleo
 
Me sisomi vitabu kwa sbb ya umaskini tu ndugu wamezidi kunipiga mizinga so nkichanganya na matumizi yangu kwa kweli sioni bsjeti ya kununua vitabu.
Ila nkipata Natoma, kwa mfano nshasoma kile cha Sugu "From the Street to the Parliament " nlikiotea mahali. Vitabu vya online havivutii kusoma.
Ni ngumu pia kusoma vitabu akati huna uhakika wa kula.
 
Salaam,

Tunaendelea kutatua changamoto na kutoa elimu kwa umma katika nyanja mbalimbali.

Uzi huu tutautumia kujua sababu za watu kutosoma vitabu hasa hapa nchini Tanzania. Lazima kuna shida mahali!

Wataalamu wameshaeleza na kuthibitisha kuwa usomaji wa vitabu husaidia kunoa ubongo, kubadilisha tabia za mtu/jamii, kumsaidia kudhibiti mazingira, biashara na faida nyingine lukuki ikiwemo burudani na kusafiri kimawazo, kihisia na kujifunza.

Pia mtu anayesoma na asiyesoma vitabu utofauti wao mkubwa upo kwenye namna ya kufikiri na kutatua changamoto.

Labda tukuulize wewe ambaye huna utaratibu wa kujisomea vitabu; Kwanini hununui kitabu na kusoma? Je, hupendi au basi tu? Nini kifanyike upate ari ya kusoma vitabu?

Funguka, tuzungumze.
Muda ila nasomag vitabu
 
Nikiongelea kwa mtazamo wangu swala la kusoma vitabu ni utamaduni, kwa watanzania tulio wengi swala la kusoma kitabu au vitabu tena vya kuelimisha ni mtihani bora hata kiwe cha mapenzi au cartoon, hili ni kutokana na utamaduni wetu tuna penda sana story za kuhadithiwa au kuhadithiana yalio jiri kuliko kukaa na kusoma ndio mana mtu na weza kaa kijiweni kutwa kupiga story bila kuona shida ila ukimuliza chanzo cha taarifa zake unakuta na yeye alisikia hawezi kuambia alisoma kitabu au gazeti hata siku moja.
 
Salaam,

Tunaendelea kutatua changamoto na kutoa elimu kwa umma katika nyanja mbalimbali.

Uzi huu tutautumia kujua sababu za watu kutosoma vitabu hasa hapa nchini Tanzania. Lazima kuna shida mahali!

Wataalamu wameshaeleza na kuthibitisha kuwa usomaji wa vitabu husaidia kunoa ubongo, kubadilisha tabia za mtu/jamii, kumsaidia kudhibiti mazingira, biashara na faida nyingine lukuki ikiwemo burudani na kusafiri kimawazo, kihisia na kujifunza.

Pia mtu anayesoma na asiyesoma vitabu utofauti wao mkubwa upo kwenye namna ya kufikiri na kutatua changamoto.

Labda tukuulize wewe ambaye huna utaratibu wa kujisomea vitabu; Kwanini hununui kitabu na kusoma? Je, hupendi au basi tu? Nini kifanyike upate ari ya kusoma vitabu?

Funguka, tuzungumze.
Mimi ni mnunuzi na msomaji mzuri na kweli nimefaidika hata namna ya kufikiri,kuongea na nifanye nini pale ninapopata changamoto mbalimbali katika maisha japo kadri ninavyoishi naona uwezo wa kununua na kusoma umepungua kutokana na kuongezeka kwa majukumu mengine ya maisha.Kusoma Vitabu ni moja ya jambo muhimu sana katika maisha kwa sababu unapata mawazo mbalimbali ya watu ya kukusaidia katika maisha.
 
Issue ni kusoma vitabu au ni lazima tuvinunue kwanza hivyo vitabu? Mpangilio wa maneno katika kichwa cha uzi wako unaonesha msisitizo ni kununua (biashara) na si kusoma.
Niliacha kununua vitabu one decade ago. Saiv ni mwendo wa soft copy tu (tena bure kabisaaaa).
Namshangaa mleta mada ni kama anasisitiza tununue vitabu badala ya kusisitiza "tuongeze juhudi Ya kusoma vitabu".
 
Kwa mujibu wa bilionea wa Zimbabwe ndugu strive masiyiwa anasema hii tabia ya waafrica kuamini kwamba kusoma kunaishia unapomaliza chuo ndio sababu kuu bara la Africa kuendelea kuwa maskini

Watu wengi miongoni mwetu hatuji update kimaarifa ndio maana bara letu limedumaa kimaendeleo
Vice versa is the truth...watu wanaosoma soma sana vitab huwa wama excuse nying katika uthubutu....nenda kkoo kwa matajir wafanya biashara uone hata wanaa muda huo...go getters weng huwa hawasom som vitab..wao ni utekelezaj.sis somasoma sasa..ndo waongeaj sana wa mirad ya watu..motivational speakers weeng ndo soma soma....wapoteza muda...ukishasoma vitab kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kikuu..umemaliza..mengneyo ni ziada tuu kutoboa...sema weng hamjiamin ma elimu zenu ndo mana mnasoma mnasoma na kuendelea kusoma..
 
Back
Top Bottom