Hivi kwanini hununui na kusoma vitabu?

Hivi kwanini hununui na kusoma vitabu?

Nasoma na kununua sana vitabu...
Ngoja waje kutoa muongozo...
 
Halafu wengi ni choka mbaya, watu wa fantasies. Yaan nitoke kibaruan nmechoka nisilale nisome kitabu? Vitabu nilivyosoma toka darasa la kwanza mpaka namaliza chuo kikuu miaka mi4 vinatosha sana kwa maarifa.
Huna likizo ya mwaka, mbona mnatafuta visababu, yani huendagi vacation wewe ukose kusoma hata vitabu, mnajifanya mpo busy na kazii na bado mnachechemea, muda upo sana wa kuongeza maarifa, muda unaonda bar huo muda huwezi tumia kusoma kitabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasio penda kusoma au kununua vitabu, huwa nawashangaa sana kama baadhi yao wanavyo tushangaa sisi.

Kwangu mimi kusoma vitabu na kununua vitabu ni sehemu ya maisha yangu, haipiti siku au siku mbili bila kusoma vitabu, kadhalika haipiti wiki au wiki mbili bila kununua kitabu au vitabu.

Mara ya mwisho kama mwezi umepita hivi, niliulizia kitabu fulani kina volumes (Juzuu 42,kila juzuu ina kurasa zisizo pungua 600) nikaambiwa bei ni zaidi ya milioni, nikawaambia ngoja nijipange kwanza nitawatafuta. Hapo hapo muuzaji ananiambia kuna watu tayari wameshaweka oda ya kitabu hicho hicho, yaani huwa kinakuja kwa oda, kuna watu wanapenda vitabu asikwambie mtu.

Kwanini nisiwashangae wasio penda kusoma au kununua vitabu ?
 
Wasio penda kusoma au kununua vitabu, huwa nawashangaa sana kama baadhi yao wanavyo tushangaa sisi.

Kwangu mimi kusoma vitabu na kununua vitabu ni sehemu ya maisha yangu, haipiti siku au siku mbili bila kusoma vitabu, kadhalika haipiti wiki au wiki mbili bila kununua kitabu au vitabu.

Mara ya mwisho kama mwezi umepita hivi, niliulizia kitabu fulani kina volumes (Juzuu 42,kila juzuu ina kurasa zisizo pungua 600) nikaambiwa bei ni zaidi ya milioni, nikawaambia ngoja nijipange kwanza nitawatafuta. Hapo hapo muuzaji ananiambia kuna watu tayari wameshaweka oda ya kitabu hicho hicho, yaani huwa kinakuja kwa oda, kuna watu wanapenda vitabu asikwambie mtu.

Kwanini nisiwashangae wasio penda kusoma au kununua vitabu ?
Naomba jina la hicho kitabu hicho na mwandishi.
 
Wengine kawaida, ila nadhani ni malezi na utashi wa mtu, kama hujafundishwa umuhimu wake ni shida sana kuwa hivyo
 
Naomba nisaidiwe kitabu cha kusoma kinachohusu maswala haya haya ya maisha yetu katika upande wowote
 

Mhu 12:12 SUV​

Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili.
 

Mhu 12:12 SUV​

Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili.
Nakazia mstari wa mwisho kusoma sana huuchosha mwili
 
Huna likizo ya mwaka, mbona mnatafuta visababu, yani huendagi vacation wewe ukose kusoma hata vitabu, mnajifanya mpo busy na kazii na bado mnachechemea, muda upo sana wa kuongeza maarifa, muda unaonda bar huo muda huwezi tumia kusoma kitabu

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaan niache kwenda bar nisome kitabu..hiv mtoa comment unaakili sawa sawa.
 
Kusoma vitabu na kununua vitabu ni hobby mbili tofauti
 
  • Tatizo 'theory' za kwenye vitabu ukipeleka kwenye maisha halisi zinagoma
  • Kitabu kina kurasa labda 5000, na mwaka una siku 365; nikiamua kusoma kila siku kurasa mmoja,itanichukua miaka 13 na nusu kukimaliza;swali, je hicho kitabu kimenisaidia nini katika kuniongezea kipato?
 
Mimi mtumish wa kawaida natoa wapi hela ya kununua vitabu, field yangu ni sayansi and education, vitabu vyake ni gharama sana, dola 100+ .Mshara wangu700,000 Bado NMB loan+ boom loan. Je, nawezaje kununua vitabu ndugu?

Acha vitabu tu kwa mwanasayansi anatakiwa awe na home laboratory ndogo ya kuchunguza mambo madogo madogo lakini ni ngumu.
Umenifanya niwaze Sana, kwa kawaida natakiwa kama msomi niwe na bar ndani yenye vinywaji vikali. Sio pombe, spirits pekee. Maana walev wanawaza bia tu. Sis watu wa russia tunakua unakuwa na kabaa uchara nyumban unaweka juice za box na spirits. You know what I mean... Yaani hapo ni mtoto hatakiwi kuonja ulevi..vodka, konyagi, kei vant, amarula nk
 
Nadhani watu wengi wakisikia kusoma kitabu wengi hudhani lazima viwe vya "motivation speakers".. hii inawafanya watu hata wasitamani kujua huu ulimwengu wa kusoma vitabu unavitu vya aina gani.

Binafsi vitabu ni sehemu ya maisha yangu... Ila so called "motivational books" havijawahi kunivutia
 
My iBook store. Haijawahi kuniangusha iwe safarini au kwenye mapumziko.

Maarifa na taarifa za kutosha.
JPEG_20210225_223027_4401351621853083481.jpg
JPEG_20210225_223048_7925726680870407487.jpg
JPEG_20210225_223127_4072510941977189625.jpg
JPEG_20210225_223215_257755391003995503.jpg
JPEG_20210225_223237_1832771121169713031.jpg
JPEG_20210225_223316_2703597539565388128.jpg
JPEG_20210225_223338_6527678235220917189.jpg
JPEG_20210225_223402_7657570308514117413.jpg
JPEG_20210225_223429_5550116903681649448.jpg
JPEG_20210225_223453_7572936623387220923.jpg
JPEG_20210225_223520_7246758126996751800.jpg
JPEG_20210225_223541_5153688962518064439.jpg
JPEG_20210225_223647_4563372230087833460.jpg


Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kusoma vitabu ni hobby kama zilivyo hobbies nyingine tu. Binafsi sikuwaga na hiyo hobby kabisa nlikua kila kitabu nnachosoma naishia katikati

Ugonjwa wangu mkubwa ulikua ni movie, nlikua natumia muda mwingi kwenye movies na ukizingatia mi sio mshabiki wa mpira

Huu uraibu wa kusoma vitabu ulianza mwaka juzi tu na hii ni baada ya kukutana na kitabu cha jamaa mmoja anaitwa James Clear (Atomic Habits), hiki ndo kitabu cha kwanza kufanikiwa kukimaliza chote bila kuishia katikati, kilikua na pages 680+

Hiki kitabu kwa kiasi flani kilianza kubadilisha lifestyle yangu, baada ya hapo nikaanza kutafuta vitabu vingine... nasoma vitabu vya aina zote...fiction na non fiction, kwa mwaka jana pekee nimefanikiwa kumaliza vitabu 7

Niko selective kwenye kuchagua vitabu vya kusoma maranyingi huwa naangilia vile ambavyo vimekua recommended na watu wengi kwenye magroup ya wanaopenda kusoma vitabu hata humu jf kuna nyuzi kibao za vitabu

Vitabu vyote huwa nadownload kutoka torrent sites kwa format ya .epub afu navitumia kwa app ya Media365 sijawahi nunua hardcopies

Kuhusu muda wa kuvisoma hii kwangu ni rahisi ukizingatia natumia simu so naweza ku visomea popote pale, wakati mwingine hata niko kwenye foleni ndani ya bank nimeboreka nafungua tu app napitia hata page 10 fasta, huwa natenga dakika 20 - 30 asubuhi na jioni karibu kila siku nasoma page za kutosha, siku hizi ule muda wa kuchek movies nimeuhamishia kwenye vitabu

Nimekuja kugundua vitabu vina fantasy flani kama movies tena naweza kusema kwangu imekua zaidi ya movie kwasabu na-enjoy na pia naongeza maarifa ya kutosha, Vitabu vinatoa maarifa in detail. Hata kingereza changu cha kuandika naona kabisa kime improve, siku hizi zile memo za kiofisi naziandika kiufundi sana naona mpaka boss wangu ame notice hii kitu ameniambia

Hapa kilichobaki ni kuwa develop tu wanangu na hii tabia ya kupenda kujisomea najua watajifunza mengi sana
Kuna kitabu kimoja cha huyu mwamba anaitwa Mark Manson - The Subtle Art Of Not Giving A Fu*k natamani kama kila mtu angekisoma ili tuishi kwa kuheshimiana
 
Kusoma vitabu ni muhimu sana ili kukujenga kifikra
 
Back
Top Bottom