Faida Kuu 6 za kusoma kila siku na umuhimu wa kusoma kila siku baada ya kuhitimu shule au chuo

Gelion Kayombo

Senior Member
Feb 17, 2018
149
193
Kusoma vitabu na machapisho mbalimbali ya kujenga kuna manufaa mengi kwa msomaji kuliko mtu wa kawaida anavyoweza kudhani. Hapa ieleweke pia, sizungumzii kusoma kwa kawaida ambako kila mtu anapitia. Nazungumzia kusoma vitu nje na vitu tulivyo soma/tunavyosoma darasani.

Watu wengi huhitimisha safari ya kusoma na kujifunza siku wanayohitimu shule au chuo. Wengi hudhani safari ya kujifunza huishia siku ile wanapohitimu shule au chuo. Wanasahau kuwa kumbe, siku wanayohitimu shule au chuo ndiyo kwanza, mwanzo wa kusoma na kujifunza vitu vipya ambavyo kwa miaka mingi hawakupata nafasi ya kusoma na kujifunza wakiwa shuleni huanza.

Watu wachache wanaelewa kuwa mabadiliko makubwa duniani katika kila nyanja yaliletwa au yanasababishwa na wasomi ambao waliamua kuendelea kujifunza vitu vipya ambavyo hawakusoma shule au chuo. Wewe mwenyewe msomaji unaweza kutafuta taarifa za wanamabadiliko wakubwa ambao waliwahi kuishi au wanaoishi sasa hivi ambao wanaendesha na kuongoza dunia kwenye kila sekta na wote hao utakuta ni watu ambao wanasoma na kujifunza kila siku.

Wanasoma na kujifunza kila siku kwa sababu wanajua faida za kusoma vitu vipya ambavyo hawakusoma na kujifunza shule au chuo. Zifuatazo ni faida utakazopata kama utaanza kusoma na kujifunza vitu vipya baada ya kuhitimu shule au chuo. Kuna faida nyingi utakazopata ila hizi ni baadhi tu ya faida hizo.

Kusoma kutakujengea uwezo wa kufikiri.

Kusoma kunahusisha akili nyingi, hivyo kwa mtu kujijengea tabia ya kusoma na kujifunza vitu vipya baada ya kuhitimu shule au chuo hufanya akili yake iwe inafikiria kisawasawa. Ieleweke pia kwa binadamu kitu pekee kinacho mtofautisha na viumbe wengine wote ni akili yake tu. Na binadamu anaweza kuijenga akili yake kwa kujifunza vitu vipya kila siku. Atafanya hivyo kwa njia ya kujisomea kila siku vitu ambavyo hakuwahi kusoma shule au chuo.

Kusoma kunaimarisha afya yako.

Binadamu ana vitu vitatu ambavyo vinamfanya awe vile alivyo na ili awe mwenye afya njema. Binadamu ana akili, nafsi na mwili. Kila kitu kina mahitaji yake na mahitaji hayo lazima yatimizwe kwenye kila kitu kama binadamu atakuwa mwenye afya njema. Hapa leo nitazungumzia hitaji la akili na siku nyingine tutaangalia mahitaji mengine kwa ujumla. Akili ya binadamu inahitaji kusoma, kujifunza vitu mbambali kama binadamu atakuwa mwenye afya njema.

Kusoma kuta kusaidia kukupa maarifa ya kutatua changamoto zako

Changamoto zinazotokea kwetu sisi ni changamoto ambazo watu wengi walishapitia na walizitatua na waka andika aidha mtandaoni au kwenye vitabu. Ili na sisi tupate kuelewa namna ya kutatua changamoto hizo tunahitaji kusoma ili tupata maarifa ya namna ya kutatua changamoto hizo.

Kukufungulia dunia kwa namna ya kipekee

Mfumo wetu wa elimu hautufundishi maarifa ya namna ya kuweza kuiona dunia kwa jicho la tatu. Kupitia kusoma vitu vipya ambavyo mtu hakusoma shule hupata maarifa ya kumwezesha kutambua fursa zinazo mzunguka.

Kusoma kunaburudisha

Mtu anaweza kupata burudani ya kutosha na kusahau changamoto zake za kimaisha kwa muda kwa njia rahisi ya kujisomea. Kusoma humburudisha na kumfanya mtu ajifunze pia.

Kusoma kutakufanya ujitambue

Kujitambua ni changamoto sana kwa watu wengi na huchukua muda mpaka mtu ajitambue. Ndiyo maana binadamu inamchukua miaka 20 kukua lakini bado asijitambue. Mazingira tunayo kulia hayatufanyi tujitambue. Kuanzia nyumbani mpaka shuleni hatufundishwi jinsi ya kujitambua. Wachache wanaojitambua hutokea kutokana na mazingira ambayo aidha yamewafanya wajitambue au wao wenyewe wamejifunza vitu ambavyo vinawafanya wajitambue.

Hitimisho

Kusoma ni jambo muhimu hata baada ya kuhitimu shule au chuo. Unaweza kuwa mtu mwenye maarifa ya kutosha, yatakayo kuwezesha kubadili maisha yako kwa kuanza kujisomea na kujifunza vitu vipya baada ya kuhitimu shule au chuo. Kuna vitu vingi muhimu hatukufundishwa nyumbani au shuleni. Lakini tunaweza kujifunza wenyewe kwa kujisomea. Jambo la msingi hapa ni kusoma vitu ambavyo vitakujenga na kubadilisha mtazamo wako wa maisha na kuanza kuiona dunia katika pembe nyingine.

Anza kujijengea tabia ya kujisomea sasa hivi. Anza taratibu kujisomea na baadae utazoea. Tembelea website hii yangu ambapo utajifunza mambo mengi ambayo hukusoma shule.

Gelion Kayombo.

Iringa Tanzania

Kwa mawasiliano zaidi: Tuma ujumbe Whatsapp kwenye namba hii:0769770288 au kwenye email hii:
 
Naona unatokea Iringa naomba utumie elimu yako kupunguza matukio ya ubakaji mkoa wako ni kinara.
Kweli mkuu? Mimi sina taarifa kama mkoa wa Iringa unaongoza kwa matukio hayo ya ubakaji. Hata hivyo shukrani kwa kushiriki jukwaani. Karibu na wewe tuelimishane namna tutakavyo ondoa hizo tabia chafu ambazo zinazidi kuharibu jamii yetu
 
Teeh! tehee! Matanzania, yotee! mataahira kweli kweli!! na hayana Dawa! nilitegemea huu uzi utapata wachangiaji kweliiiii lkn holaaa!!...watoe na mbinu mpya zisizo chosha za kupenda kusoma! vitu vikakaa lkn mweee!

ndo walivyo wabongo! udaku fakuu tuuu
 
Ha ha ha mkuu umechafukwa?
 
Teeh! tehee! Matanzania, yotee! mataahira kweli kweli!! na hayana Dawa! nilitegemea huu uzi utapata wachangiaji kweliiiii lkn holaaa!!...watoe na mbinu mpya zisizo chosha za kupenda kusoma! vitu vikakaa lkn mweee!

ndo walivyo wabongo! udaku fakuu tuuu
Mama Said tunakuheshimu ujue ooh!
 
Me nasoma humu humu JF, maana napata madini ya hii dunia mpaka nashangaaa... Shukran founder
 
Kusoma vitabu na machapisho mbalimbali ya kujenga kuna manufaa mengi kwa msomaji kuliko mtu wa kawaida anavyoweza kudhani. Hapa ieleweke pia, sizungumzii kusoma kwa kawaida ambako kila mtu anapitia. Nazungumzia kusoma vitu nje na vitu tulivyo soma/tunavyosoma darasani.

Watu wengi huhitimisha safari ya kusoma na kujifunza siku wanayohitimu shule au chuo. Wengi hudhani safari ya kujifunza huishia siku ile wanapohitimu shule au chuo. Wanasahau kuwa kumbe, siku wanayohitimu shule au chuo ndiyo kwanza, mwanzo wa kusoma na kujifunza vitu vipya ambavyo kwa miaka mingi hawakupata nafasi ya kusoma na kujifunza wakiwa shuleni huanza.

Watu wachache wanaelewa kuwa mabadiliko makubwa duniani katika kila nyanja yaliletwa au yanasababishwa na wasomi ambao waliamua kuendelea kujifunza vitu vipya ambavyo hawakusoma shule au chuo. Wewe mwenyewe msomaji unaweza kutafuta taarifa za wanamabadiliko wakubwa ambao waliwahi kuishi au wanaoishi sasa hivi ambao wanaendesha na kuongoza dunia kwenye kila sekta na wote hao utakuta ni watu ambao wanasoma na kujifunza kila siku.

Wanasoma na kujifunza kila siku kwa sababu wanajua faida za kusoma vitu vipya ambavyo hawakusoma na kujifunza shule au chuo. Zifuatazo ni faida utakazopata kama utaanza kusoma na kujifunza vitu vipya baada ya kuhitimu shule au chuo. Kuna faida nyingi utakazopata ila hizi ni baadhi tu ya faida hizo.

Kusoma kutakujengea uwezo wa kufikiri.

Kusoma kunahusisha akili nyingi, hivyo kwa mtu kujijengea tabia ya kusoma na kujifunza vitu vipya baada ya kuhitimu shule au chuo hufanya akili yake iwe inafikiria kisawasawa. Ieleweke pia kwa binadamu kitu pekee kinacho mtofautisha na viumbe wengine wote ni akili yake tu. Na binadamu anaweza kuijenga akili yake kwa kujifunza vitu vipya kila siku. Atafanya hivyo kwa njia ya kujisomea kila siku vitu ambavyo hakuwahi kusoma shule au chuo.

Kusoma kunaimarisha afya yako.

Binadamu ana vitu vitatu ambavyo vinamfanya awe vile alivyo na ili awe mwenye afya njema. Binadamu ana akili, nafsi na mwili. Kila kitu kina mahitaji yake na mahitaji hayo lazima yatimizwe kwenye kila kitu kama binadamu atakuwa mwenye afya njema. Hapa leo nitazungumzia hitaji la akili na siku nyingine tutaangalia mahitaji mengine kwa ujumla. Akili ya binadamu inahitaji kusoma, kujifunza vitu mbambali kama binadamu atakuwa mwenye afya njema.

Kusoma kuta kusaidia kukupa maarifa ya kutatua changamoto zako

Changamoto zinazotokea kwetu sisi ni changamoto ambazo watu wengi walishapitia na walizitatua na waka andika aidha mtandaoni au kwenye vitabu. Ili na sisi tupate kuelewa namna ya kutatua changamoto hizo tunahitaji kusoma ili tupata maarifa ya namna ya kutatua changamoto hizo.

Kukufungulia dunia kwa namna ya kipekee

Mfumo wetu wa elimu hautufundishi maarifa ya namna ya kuweza kuiona dunia kwa jicho la tatu. Kupitia kusoma vitu vipya ambavyo mtu hakusoma shule hupata maarifa ya kumwezesha kutambua fursa zinazo mzunguka.

Kusoma kunaburudisha

Mtu anaweza kupata burudani ya kutosha na kusahau changamoto zake za kimaisha kwa muda kwa njia rahisi ya kujisomea. Kusoma humburudisha na kumfanya mtu ajifunze pia.

Kusoma kutakufanya ujitambue

Kujitambua ni changamoto sana kwa watu wengi na huchukua muda mpaka mtu ajitambue. Ndiyo maana binadamu inamchukua miaka 20 kukua lakini bado asijitambue. Mazingira tunayo kulia hayatufanyi tujitambue. Kuanzia nyumbani mpaka shuleni hatufundishwi jinsi ya kujitambua. Wachache wanaojitambua hutokea kutokana na mazingira ambayo aidha yamewafanya wajitambue au wao wenyewe wamejifunza vitu ambavyo vinawafanya wajitambue.

Hitimisho

Kusoma ni jambo muhimu hata baada ya kuhitimu shule au chuo. Unaweza kuwa mtu mwenye maarifa ya kutosha, yatakayo kuwezesha kubadili maisha yako kwa kuanza kujisomea na kujifunza vitu vipya baada ya kuhitimu shule au chuo. Kuna vitu vingi muhimu hatukufundishwa nyumbani au shuleni. Lakini tunaweza kujifunza wenyewe kwa kujisomea. Jambo la msingi hapa ni kusoma vitu ambavyo vitakujenga na kubadilisha mtazamo wako wa maisha na kuanza kuiona dunia katika pembe nyingine.

Anza kujijengea tabia ya kujisomea sasa hivi. Anza taratibu kujisomea na baadae utazoea. Tembelea website hii yangu ambapo utajifunza mambo mengi ambayo hukusoma shule.

Gelion Kayombo.

Iringa Tanzania

Kwa mawasiliano zaidi: Tuma ujumbe Whatsapp kwenye namba hii:0769770288 au kwenye email hii:
Ndio maana mawakili wanaitwa "wakili msomi" hii ni kwasababu husoma kila siku na sheria hutungwa kill siku na mabadiliko yapo kiiiiiila iitwayo leo
 
Back
Top Bottom