Possibles
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 1,898
- 2,335
Useful comment. Barikiwa sanaKusoma vitabu ni hobby kama zilivyo hobbies nyingine tu. Binafsi sikuwaga na hiyo hobby kabisa nlikua kila kitabu nnachosoma naishia katikati
Ugonjwa wangu mkubwa ulikua ni movie, nlikua natumia muda mwingi kwenye movies na ukizingatia mi sio mshabiki wa mpira
Huu uraibu wa kusoma vitabu ulianza mwaka juzi tu na hii ni baada ya kukutana na kitabu cha jamaa mmoja anaitwa James Clear (Atomic Habits), hiki ndo kitabu cha kwanza kufanikiwa kukimaliza chote bila kuishia katikati, kilikua na pages 680+
Hiki kitabu kwa kiasi flani kilianza kubadilisha lifestyle yangu, baada ya hapo nikaanza kutafuta vitabu vingine... nasoma vitabu vya aina zote...fiction na non fiction, kwa mwaka jana pekee nimefanikiwa kumaliza vitabu 7
Niko selective kwenye kuchagua vitabu vya kusoma maranyingi huwa naangilia vile ambavyo vimekua recommended na watu wengi kwenye magroup ya wanaopenda kusoma vitabu hata humu jf kuna nyuzi kibao za vitabu
Vitabu vyote huwa nadownload kutoka torrent sites kwa format ya .epub afu navitumia kwa app ya Media365 sijawahi nunua hardcopies
Kuhusu muda wa kuvisoma hii kwangu ni rahisi ukizingatia natumia simu so naweza ku visomea popote pale, wakati mwingine hata niko kwenye foleni ndani ya bank nimeboreka nafungua tu app napitia hata page 10 fasta, huwa natenga dakika 20 - 30 asubuhi na jioni karibu kila siku nasoma page za kutosha, siku hizi ule muda wa kuchek movies nimeuhamishia kwenye vitabu
Nimekuja kugundua vitabu vina fantasy flani kama movies tena naweza kusema kwangu imekua zaidi ya movie kwasabu na-enjoy na pia naongeza maarifa ya kutosha, Vitabu vinatoa maarifa in detail. Hata kingereza changu cha kuandika naona kabisa kime improve, siku hizi zile memo za kiofisi naziandika kiufundi sana naona mpaka boss wangu ame notice hii kitu ameniambia
Hapa kilichobaki ni kuwa develop tu wanangu na hii tabia ya kupenda kujisomea najua watajifunza mengi sana
Kuna kitabu kimoja cha huyu mwamba anaitwa Mark Manson - The Subtle Art Of Not Giving A Fu*k natamani kama kila mtu angekisoma ili tuishi kwa kuheshimiana