Hivi kusudi la maisha ni nini?

Hivi kusudi la maisha ni nini?

Kwani kusudi la maisha ni nini?

Miaka 80-120 ijayo hatutakuwepo hapa duniani, tutakufa, tutazikwa na kuwa mavumbi. Kitu kitakachobaki labda ni skeleton zetu chini ya ardhi kama ushahidi kuwa tulikuwepo.

Watu wanasoma, wanapata ajira, wanakuwa na familia halafu mwisho wa siku wanakufa 🙄
Wakifa wanakuja wengine wanazaliwa, wanaishi, wanapata familia halafu wanakufa. Wakifa hao pia wanakuja wengine wanazaliwa wanaishi halafu wanakufa, na hao wakifa wanazaliwa wengine halafu wanaendeleza mzunguko uleule. Ili iweje? Hii cycle ya existence ina maana gani?

Sio sisi tu, kuanzia kuku, mbuzi, samaki, simba yani viumbe vyote vinakuja duniani, vinaishi halafu vinakufa. Vikifa vinakuja viumbe vingine kuendeleza mzunguko uleule.

Cha kushangaza kuna hadi small creatures kama bakteria ambavyo navyo vinaishi vinakufa nk, ili iweje 🧐🙄

Aliyetengeneza huu mfumo ni nani, na lengo lake lilikuwa ni lipi haswa? Nashindwa kuelewa kabisa hii cycle. It feels so meaningless
Majibu huwezi pata Mkuu labda ni kubadilishana kwamba yanayoonekana ni maendeleo Leo hii yametokana na huo mbadilishano.

So kusudi la maisha ni kubadilishana uwezo
 
Duh 🙄
Hongera yenu mliotafuta imani thabiti na kuishikilia, ni vizuri sana for mental health
Binafsi kila nikifikiria wazungu na waarabu walivyonyanyasa waafrika, kuwaibia rasilimali na kuwafanya watumwa halafu haohao ndio wakatuletea dini kwa kipindi hicho, nawaona kama matapeli

Kwa mfano Mungu anataka tufanye ibada ili iweje
Ukichagua kuwa mjinga na mvivu wa kufikiria lazima ukumbatie dini.

Watu wa dini watakwambia tumeletwa Duniani kumuabudu Mungu.
 
Kama binadamu kaumbwa kuja kufanya ibada, kwa nini asiachwe aishi milele ili azifanye ibada vizuri???
Dunia ni sehemu ya mtihani wa mwanadamu sasa tunakufa as if ndo tumemaliza mitihani yetu halafu tunaenda kuhesabiwa siku ya kiama kama ulitenda mabaya au maovu

Yni ni mfano wa maisha ya shule tu
 
Hatuwezi kujua tusivyo vijua. Ila tunaendelela kupunguza tusivyo vijua kwa utafiti, udadisi, uchunguzi na majaribio zaidi.

We cannot solve the ultimate mysteries of nature because we ourselves are the part of mystery we are trying to solve.
Ikiwa sisi ni sehemu ya mystery yenyewe, je kuna njia yoyote ya kuangalia au kuelewa asili kwa usahihi kabisa, au kila tafiti itakuwa na mipaka isiyoepukika?

Ikiwa sisi ni sehemu ya mystery yenyewe, je inawezekana kabisa kufikia ufahamu wa mwisho wa asili, au kila mtu atabaki na mambo yasiyoelezeka milele?
 
Hilo swali nilijiuliza siku moja nikiwahi hospital nimelazwa.

Nilijiuliza; kwahiyo nilizaliwa ili mwisho wa siku nije nife? Kama ni hivyo bora nisingezaliwa kabisa, maana nisingepitia hayo maumivu niliyokuwa nayapitia.
Kwa kinachoendelea hapa Duniani kama kungekuwa Kuna kujua au kuona sidhani kama Kuna mtu angetamani kuzaliwa.

Ila Sasa uzuri ni kwamba kama ambacho hukupanga kuzaliwa huna sababu ya kuhofia kufa.

Tunahofu Kwa sababu tumelishwa pumba na watu wa dini na dini zililetwa Ili kusaidia au ku neutralize harshness ya mwanadamu ambae hana tofauti na wanyama isipokuwa utashi.

Sasa huu utashi ndio umeleta gage,ume set standards za kibinadamj na reasoning au judgement ya kusema hikli tuite baya na hili zuri adhabu yake ni a au b na Kwa kuwa hatujua tulikotoka kabla basi ndio ikaletwa hiyo narration ya uwepo wa Mungu na adhabu zitakazofuatia baada ya kifo.
 
Yeah , halafu watu hawaulizi kabla ya kuzaliwa walikua wapi 🤔
 
Yeah , halafu watu hawaulizi kabla ya kuzaliwa walikua wapi 🤔
Hakuna mtu angeogopa kufa kama sio vitisho vya hadithi za dini.

Ilifaa tusikitike kuacha wapendwa wetu,Mali zetu nk na sio kuhofia tuu kufa eti Kuna adhabu.

Standards of judgement ziishie hapa hapa Ili kuwesesha ustaaarabu sio kutosha watu Kwa stori za kutunga.
 
Ikiwa sisi ni sehemu ya mystery yenyewe, je kuna njia yoyote ya kuangalia au kuelewa asili kwa usahihi kabisa, au kila tafiti itakuwa na mipaka isiyoepukika?

Ikiwa sisi ni sehemu ya mystery yenyewe, je inawezekana kabisa kufikia ufahamu wa mwisho wa asili, au kila mtu atabaki na mambo yasiyoelezeka milele?
Tunavyo vijua ni vichache sana kuliko tusivyo vijua.

Kuna vitu vingi sana bado hatuvijui. Universe ina vitu vingi sana ambavyo hata bado havijagunduliwa.

Hatuwezi kujua na kufikia ufahamu wa kila kitu katika asili.
 
Kama haiwezekani huu ulimwengu uwe ume exist from nowhere, Iliwezekana vipi kwa huyo Mungu ku exist from nowhere?

Kama kila kitu kilichopo kitahitaji uumbaji, Hata huyo muumbaji wa kila kitu atahitaji uumbaji wake.

Muumbaji huyo, hawezi kuwepo tu, from nowhere.
Mwenye kuumba kisicho umbwa hana muumba
 
Kabla ya kujiuliza ukifa unaenda wapi, hebu tujiulize kabla ya kuzaliwa, ulikuwa wapi? Hivyo wakati mwingine tuache tu mambo yaende ki nature
 
Back
Top Bottom