Hivi kucheza muziki ni kutikisa kiuno tu.!

Hivi kucheza muziki ni kutikisa kiuno tu.!

Safety last

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2011
Posts
4,242
Reaction score
1,429
Wanajf nimekuwa nikiona watu wengi wanaosakata rumba na miziki mbali mbali wanatikisa kiuno tu, hii ndo aina pekee na maalum ya kucheza muziki tu au ni kutofahamu aina za kucheza mziki , hapa tz wapi kuna course ya music dance !
 
May be wanachanganya uzoefu wao na uchezaji wa ngoma za asili.
 
I mean i second your words and really interested in the answers of other members...
oooh yeah cause nowday everyone dance in way that kiuno must shake and im tired of that ,i want to see guys dance in otherway thats why im looking for the music course sometime we can go there for testing other steps
 
oooh yeah cause nowday everyone dance in way that kiuno must shake and im tired of that ,i want to see guys dance in otherway thats why im looking for the music course sometime we can go there for testing other steps
Ifanyie modernisation sindimba
 
May be wanachanganya uzoefu wao na uchezaji wa ngoma za asili.
kila mziki ukipigwa nimekuwa nikiona watu wanatikisa kiuno tu haijalishi ni Rock ,country,salsa kwaya jamani we cant dance in otherway
 
duh hii ni ngoma ya wapi kwanza ?
Ndio hapo sasa, hata ngoma za makabila bado kuelewa, ndio maana mnaona kucheza dansi ni viuno tu. Mi nadhani kila mziki unaendana na asili ya watu wanavyo cheza huo muziki.

Tamaduni nyingi au tuseme makabila mengi ya Tanzania miziki au ngoma zao za asili uchezaji wao ndio huo, kukata kiuno, na ndio sababu hata wanao cheza muziki wa dansi ni vigumu kuondokana na asili yao.
 
Mie napenda sana kucheza Salsa nadhani ntachukua kozi one day!
 
Na bora sie kule kwetu kwa akina muraa, yetu Kichwa kifua mabega na miguu
 
Ila kweli....watu wengi huwa wanakata tu viuno, mi nahisi ni mazoea tu kuanzia kwenye ngoma zetu za asili. Lakini na miziki yetu mingi ya kibongo inatupelekea kwenye mauno zaidi! Leo hii utamkuta mwanaume anacheza kiduku huku kiuno kinatikisika.
 
Ni vibumu kuitikisa mikono na kichwa bila kutikisika kiuno. Au uitikise miguu bila kiuno kutikisika. Kwa wabongo tulipata sifa kwa wamakonde uchezeshaji wao wa kutikisa kiuno. Kule kupendwa ikawa ni kuiga. Pia afrika ya magharibi wanayo hiyo aina ya kucheza wakitikisa kila kiungo. Ilikua ngumu kuiga ikawa kwa hapa kwetu ni kama ngoma ya kizaramo au mnanda(mchiriku). Lakin wa kongo wao waliboresha zaidi kukata mauno hadi wanaume so imekua ndio muendelezo. Dance hata ukitikisa mguu au mkono ni poa.
 
hata kwenye kwaya siku hizi badala ya kucheza kichwa mwisho mabega utakuta watu wanakata viuno bila mpangilio.
 
Back
Top Bottom