Hivi ile michezo ya watoto wa enzi hizo sasa hivi bado ipo?

Chakorii

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
18,586
50,683
Habari zenu jamani. Natumaini nyote mko salama kabisa. Mimi niko poa kabisa😊😊

Turudi kwenye mada. Hivi mnajua michezo ya zamani ilikuwa inahimarisha akili na ubongo kwa kuwa mwili unakuwa unafanya kazi?

Mdako
Ukicheza mdako lazima utumie akili ya namna ya kumfunga adui yako. Hapo unacheza hutakiw kugusa tetere hata moja zaidi ya zile unazotakiwa kuziingiza shimon tu (inaitwa makali makuu)utoto raha sana nyie😁😁

AE11AB77-5E7D-451D-889D-D1D1E8C0B3D8.jpeg



Kujipikilisha
Hii kwa watoto wa kike ilikuwa utafanya juu chini uhakikishe unakaa na mama jikoni ili ujue namna anavyopika kesho yake ukawaringishie watoto wenzio kuwa unajua kupika(hili ni funzo)😁😁nimejipikilisha sana pilau na nafikiri hii imenipelekea kupenda sana kupika kuliko kitu kingine.hata kama nitapika maji mimi nina furaha muda wote wa upishi🤣🤣(mbona kupika majiii..)😁😁

B07769C0-46B2-4E2A-871E-7AB73691AA60.jpeg


Tikri
Kilimanjaro ,Arusha,Manyara na Tanga kwa wengi hili neno sio geni. Huu mchezo unakufanya unakuwa mkakamavu mzembe mzembe hutouweza huu mchezo maana unakufanya uruke sana kama vyumba vingine vimeshachorwa chorwa (kufunga) so inabidi kuruka kama umekutana na mchezaji mwenzio anahuruma basi atakupa njia (ukiomba)

Nakumbuka nilikuwa naruka kama sungura😁😁kwa sasa sidhani kwakweli maana naweza kuruka nikajikuta siagani na nyonga🤣🤣Bwana Yesu

76FB607F-C734-45FE-A3DF-18216DF2E3D3.jpeg


Kuruka kamba.
Hii ni kama hiyo 👆juu ukifanya huu mchezo unakuwa mkakamavu sana na huwezi pata manyama uzembe kipuuzi.hivi nilikuwa aruka kamba kipindi hicho ee😁😁Sina kumbukumbu wala hata lakni kwa sasa na ubonge wangu huu naruka kamba mguu mmoja mpka 50😁😁

93F344AB-1EBC-4588-800B-087A86813C9C.jpeg


Mchezo wa baba na mama
😁😁😁huu siuzungumzii saaaaana lakini ulikuwa ukifanyika kwanzia jion kwenda usiku.wahenga wanaujua lakini pia ilikuwa inakuandaa na kujua majukumu ya familia(hili ni funzo pia)

Tule tumbakishie baba😁😁jamani
Mbona tule tumbakishie babaaa.

Mnaweka kifusicha mchanga na mtu katikati mnakaa chini na kukizunguka hicho kijifusi mnaanza kula taratibu kabisa(table manners hapa zipo)(funzo lingine tena hili)atakae kidondosha kijiji atapigwa mangumi sana tu mpaka achoke hata ukikimbia utakimbizwa mpaka ukamatwe(funzo lingine hili kuuchangamsha mwili,akili kuendelea kuimarika pia..lakini kukuandaa kuwa mwanariadha wa mbio za shule😁😁umitashumta sijui kama nimepatia vizuri)

Kumbukumbu zangu zinaniambia nilikuwa nikipigwa sana mangumi maana andunjez hawana hatua kali😁😁sijui ni aina nyingine ya ulemavu huu sielewi

Mpira wa miguu
nakumbuka enzi hizooooo, nilikuwa nasakata kabumbu mbaya mbovu mheshimiwa msomaji naomba nikwambie hizo ndoto za kuja kuwa mwanakabumbu mashukuri wa kike sijui kimeyeyukia wapi.
Kwa mtoto inampa ukakamavu,uhodari na pia kujijua vipaji vyao na mengineyo.

Kwa leo niishie hapa maana michezo ni mingi sana na mingine nimeisahau wapenzi wasomaji wa leo.

Kama unaikumbuka michezo ya zamani tafadhali tukumbushane.

Swali la msingi ni Je hii michezo bado inachezwa mtaani kwako?au watoto wanacheza na Tablets, cartoons kwa TV na mengine yafananayo na hayo?

Naomba kuwasilisha.

Chakorii
 
Kwenye mpira wa miguu hapo ilikuwa 🔥🔥🔥

Sisi huku tulikuwa tunacheza tobo bao
Unapigwa chenga weeee ukizubaa mpira ukapita katikati ya miguu tu!!...hehehehhh inabidi ugeuke mwanariadha kuukimbilia 'mwembe'/mti wa maembe ukaushike ili kujinasua na mabao ya wadau
 
Hii michezo kwasasa haipo watoto wanakuwa na kukuta nyumbani kuna kila kitu mfano Tv ambazo zinawa keep busy na kusahau michezo pendwa kama hii,yote kwa yote Jennifer na Suzanne asanteni sana kwa ushirikiano hakika mchezo wa Baba na Mama niliutendea haki naweza kusema "irudiwe irudiwe" ndio haiwezekani tena kila masika na mbu wake
 
Nishapigwa sana kwa kuiba mchele kwenda nao kwenye vichochoro kujipikilisha

Mdako umenichelewesha shule sana ila umesahau na wa kuchezesha vichupa
 
Michezo yote ipo na inachezwa kama ilivyokuwa ikichezwa hapo awali.

Nimeenda mara kadhaa kijijini kwetu, maisha ni yale yale, hali ni zilezile kama kipindi cha ukuaji wangu.

Kwa ufupi maisha ambayo mimi niliyaishi, kuna watoto wengine hiyo michezo yote wanaicheza.
 
Mchezo wa kivita, hapo kunakua na 2 sides ya majambazi na wanajeshi au polis kw jina pendwa tuliwaita ( stelingi ) nhc imetokana na utohoaji wa jina la kingereza apo ni balaa Dadek ni full mikimbizano na kujificha ukitoka apo mwil lazm uchoke
 
Enzi tunakua tulikua active sana kwenye hyo michezo bila kusahau Kombolela na ilikua raha sana.
Watoto wa sikuhizi busy na cartoon + games za kwenye simu/tablet, wachache sana mjini wanacheza hyo michezo
 
Mchezo wa kujificha mbona hamuusemi wajameni!....wadada wakubwa wakubwa kidogo wanachukua vivulana wanajificha nabyo! mbaaali weee!! halafu utasikia nimejitokezaaa!! nimejitokezaaa!,..... halafu ule wa baba na mama mnacheza kimama!! mama!! kibaba...

na hapo mnakuwa familia na watoto!.......nani ana kmbuka mchezo wa kubebana ule halafu me unabewba na ke tuuuu! jamanii aaah!
 
Back
Top Bottom