Mji wa Karamay, Xinjiang wabarikiwa kuwa na mvuto wa aina ya kipekee

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
微信图片_20230725083502.jpg


Wahenga wanasema tembea ujionee. Ikiwa hii ni mara ya pili kutembelea mkoa wa Xinjiang Uygur, nimebaini kwamba hata utembee mara ngapi katika sehemu mbalimbali za mkoa huu, basi hakika hamu haitakwisha na kizuri zaidi ni kwamba utagundua mambo mengine mengi mapya. Nasema hivi kwasababu huu ni mkoa uliobarikiwa vivutio vya aina mbalimbali. Lakini licha ya vivutio, kutokana na mkoa huu kusheheni makabila mengi madogo, umeufanya kuwa na tamaduni za aina nyingi zinazoambatana na mila na desturi tofauti.

Katika matembezi yangu ya mara hii, kituo changu cha kwanza kabisa kilikuwa ni mji wa Karamay, moja ya miji maarufu sana ya mkoa wa Xinjiang. Ilinichukua takriban saa nne na nusu kwa ndege hadi kufika katika mji wa Urumqi kutoka Beijing, mji mkuu wa China na baadaye kupanda ndege nyingine ambayo ilitufikisha katika mji huo tuliodhamiria kufanya matembezi yetu, mji wa Karamay.

Labda niseme tu kwamba mji huu umenifumbua macho, hasa baada ya kutembelea maeneo yake mbalimbali. Kilichonivutia zaidi ni pale nilipofika katika Korongo Kuu la Dushanzi na kujionea namna Korongo hilo linavyoingiza mamilioni ya pesa kwa mwaka. Mara nyingi tumezoea kuona maeneo kama hayo yakitajwa kijiografia tu, yaani kuelezewa namna yalivyojiunda katika maelfu ya miaka iliyopita. Lakini kuamua kuyatumia maeneo hayo yaliyo mbali na yenye hatari na kuyageuza kuwa kivutio cha utalii, hili ni jambo linalopaswa kusifiwa na kupigiwa mfano.

Korongo Kuu la Dushanzi, ukiliangalia kwa karibu lina michirizi mingi ambayo inatoa sura ya kuvutia sana. Kwa mujibu wa muongozaji wetu, michirizi hii huwa inaleta mandhari nzuri hasa wakati ambao theluji kutoka Milima ya Tianshan inapoyeyuka na kufanya maji yake yatiririke kwenye michirizi hii. Korongo hili likiwa na upana wa mita 100 hadi 400 chini kabisa na kimo cha mita 200, limesheheni michezo ya aina mbalimbali ambayo kwa mtu wa kawaida anaweza kuona ni michezo ya hatari. Hata hivyo, kwa watalii wanaotembelea korongo hilo ama hata watu kama sisi tunaofanya matembezi ya kujua kwa kina maeneo kama haya, tunaona ni miongoni tu mwa michezo ya kusisimua ambayo inakupa hamu ya kutaka kuthubutu ili kuona kama utaweza ama la.

Michezo hiyo ni pamoja na kupita kwenye daraja la kioo, ambalo linatoka upande mmoja wa Korongo hadi upande mwingine. Daraja hili lenye urefu wa mita 186 na kimo cha mita 150 linaweza kukutia hofu, lakini mimi niliamua kuwa na ujasiri na uthubutu wa kutembea na hatimaye nikamaliza kulitembea lote. Daraja hili limetengenezwa juu ya korongo kwa ajili ya watalii kupata fursa ya kujionea kwa karibu zaidi kimo cha korongo hilo na mandhari yake ya kuvutia.



Sambamba na daraja hilo, kuna mchezo mwingine maarufu sana ujulikanao kama Dawazi. Hii ni sarakasi ya jadi ya kutembea juu ya kamba. Kawaida wachezaji wanatembea juu ya kamba bila ya kuvaa vifaa vya kujikinga, Isipokuwa wanabeba jiti moja tu mkononi ikiwa kama njia ya kujishikilia wakati wanapopepesuka ili wasidondoke chini. Dawaz kwa lugha ya kabila la Wauygur maana yake ni kutembea kwenye kamba, mchezo huu wa jadi umeanza kuchezwa zamani sana katika sehemu za kaskazini magharibi mwa mkoa wa Xinjiang nikimaanisha katika mji huu wa Karamay. Mchezo huu wa hatari sana, ambao una historia ya miaka zaidi ya 2000 umeorodheshwa na UNESCO kama urithi wa utamaduni usioshikika wa China.

Kwa wachezaji wapya yaani wale wanaojifunza wanatakiwa kutembea kwenye kamba yenye urefu wa sentimita 50 tu chini, kabla ya kuendelea kujifunza Dawaz ambayo inahitaji mwanasarakasi kutembea kwenye kamba yenye urefu wa mita 20 juu kabisa. Adili Wuxor ni mchezaji maarufu sana na nguli wa sarakasi ya aina hii, ambapo amevunja rekodi nyingi za Guiness kwa sarakasi hiyo. Nikiwa miongoni mwa watu wenye bahati, niliweza kuona akifanya maonesho ya kutembea juu ya kamba, akipita kwenye Korongo Kuu la Dushanzi. Mwanzoni nilikuwa nikiogopa sana kwani kimo cha korongo ni kikubwa na yeye alionekana kutembea juu kabisa tena umbali mrefu. Hivyo licha ya woga na hofu iliyonitawala, nilipiga moyo konde na kuamua kuangalia hadi akavuka kutoka upande mmoja kwenda mwingine. Hivi sasa asilimia 30 ya watu wa China, hasa wanaotoka mkoani Xinjiang wanajua mchezo huu unaorithishwa kizazi baada ya kizazi. Kwa mjibu wa Adili, lengo lake ni kuongeza idadi hii kwa kutoa mafunzo ya mchezo huu katika mji wake wa Karamay na nje ya mkoa wa Xinjiang.
 
Back
Top Bottom