Hivi hii ni sawaa?

Hivi hii ni sawaa?

kwani wanalala naye chumbani? au anaona anammalizia vyakula? kama mimi ni mme wako upo na mimi faragha chumbani kwangu tunajadili yetu na pengine tunamjadili hata bimkubwa mwenyewe na kupanga yetu, tukitoka asubuhi tunamkuta sebuleni au jikoni, tunamwaga vizuri hao kazini, hadi jioni, kuna shida gani?.....anakuibia nini, upendo? kwani chumbani kwenu mnalada watatu? wewe, mama mkwe na mmeo?
Ni utovu wa nidhamu na ukwepaji majukumu ya kifamilia kwa mwanamke kutelekeza mume na kukimbilia kwa watoto kuishi huko miezi. Maandiko kwa wakristo hayaruhusu kabisa.
 
Ana kwake na ni pazuri tu kajengewa na wanae,pia ana mme wake ye anataka akae kwa wanae tu
Kama haumwi na vyote anapata akiwa kwake na mume anae mwenye Afya njema... Bado anakuja kukaa Makali miezi sita...

Mkwe mbea utamjua tu.....
 
Akisema nimekuja kutembea utamuuliza atakaa muda gani?
No... hapo sasa ndipo penye mkanganyiko inategemea na nidhamu ya mzazi.

Halafu bro hii ni ligi familia zinatofautina na malezi yanatofautina. Kila mmoja anaongea kwa experience ya familia na jamii iliyomzunguka. Ila binafsi nipo against na sio against ni aibu kwake kukaa kwangu aibu saana.
 
Nadhani mleta mada ndio muhusika. Naomba nikuulize: Angekua ni mama ako mzazi ungesema hivo? 2. Kati ya wewe na mumeo nani anatoa matumizi?? 3. Anaetoa mahitaji ya familia na anayehudumiwa nani anatakiwa kulalamika?? 4. Kumpikia mama kwe wako unaona kazi sana???? 5. Mumeo amechukua kitanda mlichokua mnalalia kampa mama ake alalie na wewe unalala chini???? 6. Umewahi kusikia mama mkwe wako ni mchawi???. Ukijijibu haya uatagundua kwanini watu husema HAKUNA KAMA MAMA. Angelikua baba mkwe wako ningepata mashaka maana wanaume hatuaminiki (maana ni ngumu mkamwana kumtongoza baba mkwe) lakini MAMA, MAMA, MAMA, MAMA. Hiyo ni chata nyingine. Usirudie huu upuuzi
Sio mimi, kwanza mimi atakaenioa atapata bahati sana mim nikimpenda Mwanaume napenda na ndugu zake ndio fomula niliyonayo ,,,kwa upande wangu naweza kuishi na mama wa mme wangu na namlea tu vyemaa,ila haswaaa nikiwa nampenda huyo mme ,,,lazima nipende anachopenda mme wangu
 
Ni haki yake jmn hujui wanawe kawalea kwa shida gn. Sasa leo wamepata manufaa wanufaike wengne, looh me mwanangu akioa naenda kuhamia kabisa, shida nnayoipata Sasa kumtengenezea nice future naijua mm na ole wake uyo mkamwana alete vijineno atajuta...
Sawa mkuu lakini sasa ndio umwache baba watoto miezi 6 peke yake ati ulipata shida na mwanao? Nani hakupata shida na mwanae????
 
Ni waolewaji wa sasa tunajifanya wazungu tunaishi kizungu hatutaki wazazi wala ndugu, lkn hiyo sio haki kabisa.
Aysher sio waolewaji wa sasa....

Aseeh jamii zinatofautina saana.
 
Wengi mnawatetea wamama lakini niseme si vibaya ila kuna baadhi ya makabila wamama ni kero kwenye ndoa za watoto wao, nimeshuhudia dada mmoja akikosa raha mama mkwe na ma wifi hawakatiki nyumbani, alafu hawamsaidii kazi wananyosha miguu tu, hii si sahihi kabisa.
Mfano huyi binti alijifungua mama mkwe ana nguvu kabisa bado alikuwa hamsaidiii chochote , binti wa kazi afanye kila kitu,adeki,apike,afue,kila kitu afanye mama mkwe hata kuogesha mjukuu hakuna,,hapo mama yake mzazi akashindwa kuja kwa sababu mama mkwe wa mwanae yupo,binti ikabidi akomae tu asaidizane sasa hivi anaumwa kiuno haswaa kwa ajili ya kufanya kazi kiuno hakijakomaa kwaajili ya kujifungua
 
Mimi sioni shida akae mwaka sawa ila kwa wamama wanaojielewa hustahili kuishi kwa mwanao zaidi ya mwezi labda kama unaumwa.

Hii tabia wanayo wasukuma haumwi mwaka huyo kwa mwanae haifai.

Kwetu hawawezi tena kamani mama wa binti anakuja kama kuna jambo la maana au ugonjwa.

Hivi mama mkwe kumwacha mmewe kuja kwa mwanae miezi hiyo yote ni heshima? Inatoa somo gani?

Binafsi kama kaja matembezi mwezi au miwili sina shida kama mstaarabu hata miaka kumi naishi nae ila kuna wale midomo kama chiriku hapo ndo shida.

Inshort hakuna shida yeyote kuishi nae.la muhimu heshima
 
Sawa mkuu lakini sasa ndio umwache baba watoto miezi 6 peke yake ati ulipata shida na mwanao? Nani hakupata shida na mwanae????
Na yy uyo baba watt km anaona yuko peke yake na aje hajafukuzwa ati..!! Tutahamia sote kwa mtt wetu Ni haki yetu
 
No... hapo sasa ndipo penye mkanganyiko inategemea na nidhamu ya mzazi.

Halafu bro hii ni ligi familia zinatofautina na malezi yanatofautina. Kila mmoja anaongea kwa experience ya familia na jamii iliyomzunguka. Ila binafsi nipo against na sio against ni aibu kwake kukaa kwangu aibu saana.

Haa haa haa nmecheka sana hapo
 
Hivi unajua wanawake wakikaa sehemu moja,naomba kama umeoa mlete mama ako akae na mkeo muda mrefu utaniambiaa,kuna vitu unaweza fanya ni kawaida tu halaf mama mkwe akaona umemtendea vibayaa
Oh, ni nadra sana hayo mambo kumkuta baba mkwe kamfanyia mkwewe
 
Kama mkwe mstaarabu, anayajua mipaka yake na anaheshimu nyumba ya mwanae,hawezi kukaa muda wote huo kwa mwanae na hawezi kuanza kuleta shida kwa ndoa ya mwanae.
Haya ameona mkwewe ana shida, si arudi kwake.
Tatizo wengi hawajui mipaka yao
 
Na yy uyo baba watt km anaona yuko peke yake na aje hajafukuzwa ati..!! Tutahamia sote kwa mtt wetu Ni haki yetu
Ha! Ha! Ha! Mkuu hamieni tu. Lakini siyo ustaarabu kabisa.... Kazi Yangu kubwa itakuwa ni kukarangiza hadi sufuria zitoboke...
 
Mfano huyi binti alijifungua mama mkwe ana nguvu kabisa bado alikuwa hamsaidiii chochote , binti wa kazi afanye kila kitu,adeki,apike,afue,kila kitu afanye mama mkwe hata kuogesha mjukuu hakuna,,hapo mama yake mzazi akashindwa kuja kwa sababu mama mkwe wa mwanae yupo,binti ikabidi akomae tu asaidizane sasa hivi anaumwa kiuno haswaa kwa ajili ya kufanya kazi kiuno hakijakomaa kwaajili ya kujifungua
Halafu unakuta dada wa watu anasemwa na mama mkwe mpaka basi
 
Back
Top Bottom