Hivi hawa wanaokula kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan na Kwaresma ni hawana dini au ndo wanajiendekeza?

Hatujiendekezi ila wengine tunanyonyesha na ndio umetuona tunakula na kumimina juice.
 
KUFUNGA SIO UTAKATIFU AU USAFI. KUNA WATU WAKIFUNGUA WANAFANYA MAMBO ZA AJABU KULIKO HATA SHETANI. KIPINDI HIKI HATA SHOGA KAFUNGA, AKIFUNGUA ANAENDELEA NA YAKE
 
Sisi hatutaki kumkwaza Mtu. Nadhani nimeeleweka
IMG-20230324-WA0043.jpg
 
Wana jamii kwema?. Leo nikiwa kwenye mizunguko yangu. Nikakutana na sahani za misosi zinapitishwa mchana kweupe watu wanapiga misosi fresh yani. Kabla macho hayajatulia vizuri naona juisi zina miminwa.

Sasa nikawa najiuliza hivi huu mwezi si Waislam na Wakristo funga imetukuta sote kwa pamoja. Sasa hawa wanaokula na kunywa mchana kweupe ni kina nani?

Muwe na mfungo mwema wa Ramadhan na Kwaresma.
Funga pekee haiwezi kumpeleka mtu peponi. Kuiona Pepo ni mjumuisho wa mambo mengi sana ya kiroho.

Kwanza wanaofunga katika roho na kweli ni wachache sana, wengi wanaigiza (wanashinda njaa tu).

Wapo wanaofunga ili wasionekana wanakinzana na watu wengine wa imani yao. Kwahiyo usipokula au kunywa tena kwa siku 40 tu (kwa Wakristo) au siku 30 tu (kwa Waislamu) haimaanishi ndiyo umemaliza kila kitu.
 
Kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan ni nguzo ya 4 ktk uislam ,Na Amesema Bwana Mtume amani Iwe juu yake kwamba Mwenye kufunga ktk Njia ya MwenEnzi Mungu basi MwenyEnzi Mungu humuweka mtu huyo (Muumini/Muislam) mbali na Moto wa Jehanam kwa umbali wa miaka 70 Pia faida ya wafungaji Siku ya hukumu/kusimama hesabu/Kiama wataingia ktk mlango maalum unaoitwa Rayyan kuingia ktk Pepo ya MwenyEnzi Mungu ni hayo tu machache kiimani/kinafsi ktk kupandisha watu ktk Darja ya UchaMungu lkn pia kuna Faida nyingi kiafya anazopata mfungaji kama kuchoma /kupunguza mafuta mwilini na kumpumzisha tumbo kwa umeng'enyaji/usagaji wa chakula .
 
Wana jamii kwema?. Leo nikiwa kwenye mizunguko yangu. Nikakutana na sahani za misosi zinapitishwa mchana kweupe watu wanapiga misosi fresh yani. Kabla macho hayajatulia vizuri naona juisi zina miminwa.

Sasa nikawa najiuliza hivi huu mwezi si Waislam na Wakristo funga imetukuta sote kwa pamoja. Sasa hawa wanaokula na kunywa mchana kweupe ni kina nani?

Muwe na mfungo mwema wa Ramadhan na Kwaresma.
Acha unafiki !! Kama kweli mnafunga, sasa iweje bajeti ya chakula iwe kubwa kupita kipindi ambacho hamjafunga ??! Mfano kabla ya mfungo unatumia 200,000/= ya chakula kwa mwezi, halafu ukifunga unatumia 500,000/= kwa mwezi badala ya kushuka hadi 20,000/= au 15,000/= kwa mwezi ??!
 
Sabato hatuitambui hii Kwaresma wala pasaka ya tar 30, ni mchongo flan mwaisa
 
Back
Top Bottom