Kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa wa COVID19 wakati wa mfungo wa Ramadhan kwa Waislam

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,874
Ikiwa zimebaki siku chache waumini wa dini ya kiislamu kuingia katika mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhan. Shirika la Afya Duniani (WHO-World Health Organization) wametoa muongozo wa muda (Interim Guidance) tarehe 15/April /2020,muongozo huo ukipewa jina "Safe Ramadan Practices in the Context of the COVID-19" .

Chama chetu cha ACT wazalendo, viongozi na wanachama tumekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu,miongozo,ushauri, mapendekezo kwa serikali pia wananchi na jamii kwa ujumla namna ya kujikinga na ugonjwa huu ili kupunguza maambukizi.

Ngome ya Vijana Act wazalendo tumeona ni jambo jema kutafsiri muongozo huu wa WHO kwa ufupi kwa lugha ya kiswahili kutoka lugha ya kingereza.

WHO katika muongozo huu wanasema mwezi mtukufu wa Ramadhan ni mwezi ambao familia za kiislamu,marafiki na ndugu wanakuwa pamoja ,kukutana na kufuturu pamoja (Breaking their fast together) au kula daku pamoja (Suhour), kukutana kwa wingi katika nyumba za ibada (misikitini) na kuhudhuria sala tano za faradh na za muda mrefu katika ibada za sunnaah kama Taraweeh na Qiyam.

Pia waislam wengine hubaki msikitini mchana na usiku kwa sala na maombi katika siku kumi za mwisho wa mwezi wa Ramadhan (I'tikaf).Yote haya ni tamaduni na utaratibu kwa waislam wote Duniani kipindi cha Ramadhan.

Mwezi mtukufu wa Ramadhan unaangukia mwishoni mwa mwezi April hadi mwisho wa mwezi Mei . Kipindi ambacho maambukizi ya ugonjwa wa COVID19 bado yanaenea kwa kasi,hivyo kuna haja ya hatua muhimu na mahususi kuchukuliwa.

WHO wanasema katika kipindi hiki kuna haja kubwa ya kuepuka mikusanyiko ya aina yeyote ,na tathimini ya kutosha inapaswa kufanyika hasa mamlaka za serikali na viongozi wa dini kuangalia namna kuhairisha,kubadili, kuendelea, kuboresha au kuzuia mikusanyiko baada ya kupima tathimini ya hatari (Risk assessment).

Maamuzi yeyote baada ya tathimini yajikite katika sala ambazo ni hiari /Sunna zinazosaliwa baada ya sala ya Isha.Sababu mara nyingi inahusisha mikusanyiko mikubwa.Kama kutakuwa na katazo lolote la makusanyiko kipindi hiki cha Ramadhan basi njia mbadala za kidigital zinaweza kutumika Kama Tv ,Radio na mitandao ya kijamii.

Kama mikusanyiko kipindi hiki cha Ramadhan itaruhusiwa kuendelea.Basi hatua madhubuti za kujikinga na kupambana na maambukizi zinapaswa kuchukuliwa kikamilifu ili kuepuka maambukizi ya COVID19.

Mambo ya kuzingatia.

1.Kuepuka kukaribiana/Physical distance
#Kukaa mbali mita 1 au futi 3 kati ya mtu na mtu au watu muda wote.
#Kuepuka kupeana mkono ,watu wapeane ishara (Nodding) au kupungiana (Waving).
#Kuzuia idadi kubwa ya watu kukusanyika sehemu ya mauzo au madukani.

2.Makundi yenye hatari (High-risk groups)
#Watu wanaojihisi vibaya au wenye dalili za COVID19 waepuke kuhudhuria matukio yeyote,wafuate miongozo na watoe taarifa kwa mamlaka za afya haraka.
#Watu wenye umri mkubwa(wazee) au yeyote ambaye anasumbuliwa na magonjwa ya awali kama kisukari,kansa,magonjwa ya upumuaji wasihudhurie shughuli au matukio yeyote sababu makundi haya ni rahisi kwao kupata maambukizi hata kifo kutokana na COVID19 sababu ya kinga zao kuwa dhaifu.

3.Sehemu /Mazingira ya tukio (event au ibada)
#Kama inawezekana tukio lolote lenye idadi ya watu lifanyike nje,Kama ni ndani kuhakikishwe kuna hewa ya kutosha inapita (Ventilation and air flow).
#Kufupisha urefu wa tukio au shughuli husika ili kuzuia uwezekano wa kuzidisha uwezekano wa maambukizi.
#Kufanya tukio au shughuli inayohusisha watu wachache kuliko idadi ya watu wengi.
#Kuwe na uratibu wa kuelekeza watu wanaoingia na kutoka katika ibada ili kuzingatia umbali (Physical distance) miongoni mwao muda wote.
#Kuwe na hatua mahususi za kurahisisha ufuatiliaji (Contact tracing) katika tukio ,ibada au shughuli ambapo mgonjwa ametambuliwa miongoni mwa wahudhuriaji au washiriki.

4.Kuzingatia na kuhimiza usafi
Waislam kabla ya kusali huchukua udhu(Kunawa /usafi wa viungo) hivyo:
#Kuwe na vifaa vya kutosha vya kurahisisha udhu, maji ya kutosha na sabuni ya kupakaa mkononi.
#Kuwe na tissues pia Dustbin ya kuhifadhia tishues hizo.
#Kuhimiza waumini kuwa na misala binafsi ya kutandika juu ya kapeti.
#Kuwe na Screen au Tv ambayo mara zote itakuwa ikionesha ushauri namna ya kujikinga ,usafi wa mikono na ujumbe wa jumla wa kujikinga na ugonjwa wa COVID19.

5.Usafi wa mara kwa mara katika sehemu ya ibada ,Jengo na maeneo mengine
#Kuweka safi vifaa vyote vya kuchukulia udhu msikitini.
#Kuweka safi mitaro au mikondo yote ya kupitishia maji baada ya kuchukua udhu.
#Kusafisha mara kwa mara vifaa au sehemu zinazoshikwa sana au mara nyingi (Often touched- objects) kama vile vitasa vya mlango ,swichi,vyuma vya ngazi (Stair railings ) vyote visafishwe na dawa za kuuliwa bakteria au virusi (Detergents au Disinfectant).
#Kuhimiza usafi wa mara kwa mara katika sehemu na maeneo yanayotumiwa kwa kusali na ibada kila baada ya tukio la sala au ibada .Dawa za Detergents na Disinfectant zitumike pia mara zote.

6.Utoaji wa misaada (Sadaqat /Zakah). Unapaswa ufanyike kwa uwangalifu mkubwa kwa kuzingatia Physical distance ,pia kuepuka mkusanyiko wakati wa kufuturu au kufuturisha,pia sadaka au chakula kinapaswa kifungwe katika Packages (vifungashio) ili iwe rahisi katika ugawaji.Ni vyema taasisi ndio ipewe jukumu la kuandaa,kufunga, kuhifadhi na kugawa chakula au sadaka hizo kwa kuchukua tahadhari zote za Physical distance.

7.Saumu kwa wagonjwa wa Corona

#Kama ilivyo ada ni watu wenye afya imara ndio wanapaswa kufunga kipindi cha Ramadhan.Mgonjwa mwenye maambukizi ya Corona au COVID19 anaweza kutofunga Saumu kwa mashauriano ya daktari wake.Kama ilivyo kwa mgonjwa yeyote.

8.Lishe na Mlo
#Mlo mzuri na unywaji wa maji na juice nyingi ni jambo muhimu sana kipind hiki cha Ramadhan.
#Watu wale na kutumia sana vyakula ambavyo ni fresh na unprocessed kama matunda na vingine.

9.Matumizi ya (Tumbaku) Sigara

#Matumizi ya tumbaku/Sigara ni hatari sana kwa mazingira ya kila siku ,hasa kipindi hiki cha Ramadhan na ugonjwa wa COVID19.Kwa kawaida mtumiaji wa Sigara anaweza kuwa tayari ana matatizo au magonjwa ya mapafu ambayo hufanya utendaji kazi wa mapafu kuwa dhoofu au chini Sana hivyo hali hii inachangia Sana hatari ya kupata na kuathirika na ugonjwa wa Corona kwa urahisi sana .
#Pia kuvuta Sigara kwa kugusa lips kwa vidole huongeza uwezekano mkubwa wa kupata COVID19 kupitia mifumo ya hewa na upumuaji.

10.Himiza utulivu wa kiakili na afya
#Mbali na kuchukua hatua zote zote hizo juu waumini bado wanaweza kuwa na uwezo wa kuwa na mahusiano na ndugu ,jamaa na marafiki kwa kuzingatia masharti ya wataalamu (Physical distance),kutumia njia za mitandao kuwasiliana (digital platforms),kufanya maombi kwa wagonjwa na pia kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara kwa kufuata hatua za kujikinga na kuchukua tahadhari.

Chama chetu cha ACT wazalendo , viongozi na wanachama tutaendelea kuhimiza wananchi wote na sisi wenyewe kwa ujumla kuchukua tahadhari juu ya kujikinga na ugonjwa huu.Pia tunawatakia waislamu wote maandalizi mema ya mwezi mtukufu wa Ramadhan. Ramadhan Kareem.

Shukrani,
Imetafsiriwa na kutolewa na Ngome ya Vijana ACT wazalendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu kwenye kwarezima mlitoa mwongozo ama kwa kuwa mmejinasibu na lichama lenu kama viongozi wa Madrasa.
 
~ muongozo alishautoa mtume Muhammad s.a.w kitambo sana yanapotokea magonjwa ya mlipuko ya kuambukiza waislam wafanye....hao mabeberu hawana jipya.
 
Back
Top Bottom