Hivi Gerson Msigwa yupo sawa? Baba wa Rihanna akistaafu atakuja kuishi Zanzibar itasaidia nini Watanzania?

Hata angetuambia Elon Musk, Jeff Bezos, Warren Buffet hata Rihanna mwenyewe wanakuja kuwekeza, Uwekezaji wa ukweli tungeona anaongea vitu vya maana.

Sasa baba wa Rihana nani anamjua duniani kuisaidia Tanzania kwa viwango vyovyote vya maana?
 
Kwa hiyo sasa hivi hizo gharama ambazo Tanzania isingeweza kuzimudu huko nyuma, sasa tumezimudu vipi?

Baba wa Rihana anatusaidia nini sisi?

Hivi Msingwa anaelewa kua baba wa Rihana ni mwizi na tapeli mkubwa hadi binti yake alimfungulia mashtaka ya utapeli na wizi kwa kutumia jina la binti yake?

Huu uongo wa kumpa sifa Samia za kijinga hautatusaidia chochote.

Samia nae alivyo muongo eti alikua na wasiwasi kama filamu itakubalika Tanzania ila amepokea text meseji zaidi ya 300,000 kwa pongezi alipofika tu Tanzania.

Hivi Samia anafikiri sisi ni wakalia maji kama yeye na wenzake aa kule kwenye maji ambao unaweza kuwadanganya tu, namba ya simu binafsi ya rais inajulikana na circle ya watu wachache wasiozidi 1,000. Hizo text laki tatu zilitumwa na nani?

Hii nchi alieturoga.
 
Maza president akiendeleza hivi vijimambo vyake vya kitumwatumwa baada ya muda wasaidizi wake wote watageuka mazombi.
 
Binafsi sijaona alipokosea Msigwa

Alichotamka ni kikubwa na cha muhimu kwa kila anayemfahamu Rihanna lakini haifahamu Tanzania
 
Mtashangaa sana ila katiba mpya iko wazi ni lazima hawa wateule wanaoteuliwa bila merits zozote lazima wawe hivyo.
 
Back
Top Bottom