Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 304
- 518
Baada ya Gerson Msigwa kutoa Elimu kuhusu azimio la Bunge na Uwekezaji wa Bandari ya Dar, Wananchi sasa wamejua ukweli.
Ni Jukumu letu Watanzania kuunga Mkono Juhudi zake kwani waliokuwa wanapotosha kuhusu Uwekezaji wa Bandarini sasa wameelewa ukweli. Watu walidanganywa kwamba Bandari zote za Tanzania zinachukuliwa na mwarabu kwa mkataba usio na kikomo. Sasa watu wote wameelewa zilikuwa propaganda za kuzua taharuki na uongo kutoka kwa watu wanaoitakia Mabaya Tanzania.
Kila Mtanzania anapaswa kuunga Mkono juhudi zinazo fanywa na Gerson Msigwa, vita ya kiuchumi haijawahi kuwa nyepesi.
Gerson Msigwa
Leo asubuhi nimesoma post ya Kigogo wa Twitter akimshambulia Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa na Kitengo cha Mawasiliano cha Mamlaka ya Bandari (TPA) kuwa wamezembea kutoa elimu kuhusu mkataba wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu uwekezaji katika bandari.
Nimeshangaa sana kwamba kwa zaidi ya wiki mbili hata kabla mkataba huu haujasomwa Bungeni ina maana Kigogo alikuwa haoni jinsi Msigwa alivyokuwa akitoa maelezo kuhusu mkataba huu na umuhimu wake kwa Taifa?
Nimeshangaa zaidi kwamba wakati Msigwa akitoa taarifa kuhusu mkataba huu wengi walikuwa wanambeza kwamba hajui anachokifanya akiwemo Kigogo mwenyewe na kushinikiza aondolewe, leo ukweli umejulikana kuwa Msigwa alikuwa sahihi ndio Kigogo anakuja na makala ndefu ya kudai Msigwa hajatimiza wajibu wake? Uonezi mkubwa.
Namkumhusha Kigogo kuwa Msigwa amezungumzia uwekezaji wa bandari ya Dar es Salaam mara nyingi katika mikutano yake ya Waandishi wa Habari na alieleza dhamira ya Serikali ya kutafuta wawekezaji kwa ajili ya kongeza ufanisi wa bandari hii.
Nikiwa mmoja wa wanaofuatilia kazi zinazofanywa na Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali nadiriki kusema shambulizi hili ni uonezi mkubwa na Kigogo anapaswa kujua anaotuandikia pia tuna akili za kujua mambo.
Nani asiyejua mageuzi makubwa ya Idara ya Habari wakati wa Dk. Hassan Abbas na mageuzi makubwa zaidi alitoyafanya Gerson Msigwa.
Ina maana Kigogo amesahau kuwa ni katika kipindi cha Msigwa Idara ya Habari imeanzisha taarifa za Msemaji Mkuu wa Serikali ambazo zilianza kutoka kila wiki kiasi cha kuonekana zinachosha na mikutano ya taasisi za Serikali ambayo hufanyika mfurulizo katika kipindi ambacho Bunge halikutani?
Nani asiyejua kuwa Msigwa kaja na kitengo cha Idara ya Habari MAELEZO kinachorusha matangazo mbashara kama ilivyo Ikulu na sasa vyombo vya habari vinapata matangazo ya shughuli mbalimbali za Serikali moja kwa moja kwenye newsrooms zao?
Ni Msigwa huyuhuyu kaanzisha Clubhouse ya Msemaji Mkuu wa Serikali ambapo anawaleta Mawaziri na wanaulizwa na kujibu maswali papo hapo.
Ni Msigwa huyu huyu ametengeneza studio na yupo mbioni kuanzisha Kipindi Maalum cha Ongea na Waziri, na amewaonesha Waandishi wa Habari wa Dodoma gari la matangazo kwa ajili ya kufanya matangazo ya nje.
Nimejiuliza sana ina maana Kigogo hasikii jinsi Msigwa anavyopambana kukabiliana na uposhaji mbalimbali unapotokea? Kwamba Kigogo hamuoni Msigwa kwenye vyombo vya habari na mitandaoni.
Kwamba Kigogo haoni majarida ya Nchi Yetu kutoka Idara ya Habari MAELEZO ya Mtandaoni na nakala ngumu?
Kwamba Kigogo haoni Makala ya Kazi Iendelee inayorushwa na TBC
Kwamba Kigogo haoni clip za video zinazotengenezwa na Idara ya Habari kila siku na kusambazwa mitandaoni tena nyingine hata yeye huwa anapost
Kwamba Kigogo haoni pages za Msigwa na za Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali za Mtandaoni na jinsi anavyoipambania Serikali ya Rais Samia?
Kwamba hamsikii Msigwa akiwa kwenye matukio mbalimbali?
Lakini Je, Kigogo anajua kazi zingine anazozifanya Msigwa ambazo pengine hazionekani machoni.
Nadhani kwenye hili Kigogo kachemka, na ni vizuri atafute shutuma zingine dhidi ya Msigwa na Idara ya Habari. Hii hapana, mwacheni kijana afanye kazi.
Tena kibaya zaidi anagombanishwa na aliyemteua yaani Rais. Hili jambo linakwaza sana.
Nikiwa ni mmoja wa vijana wanaojifunza kutoka kwa Msigwa, sijafurahishwa na post ya Kigogo na nimeona niandike hapa.
Msigwa piga kazi, Watanzania tunaona unachokifanya kwa ajili ya Serikali yetu na Rais wetu.