saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,173
- 6,158
SAMAHANINI SANA WANA JF HASA MKUU WA WILAYA YA RORYA, NILIMAANISHA MKURUGENZI MTENDAJI WA WILAYA YA RORYA MOKANI MARA NA SI MKUU WA WILAYA KM NILIVYOANDIKA AWALI, HATA HIVYO NIMESHINDWA KU-EDIT HEADING
Jana ktk taarifa ya habari ya jioni Channel Ten kiongozi wa mwenge wa uhuru kitaifa alilalamika kuwa mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Rorya alionesha dharau kwa mwenge wa uhuru, hakutaka kutoa ushirikiano wowote ikiwa ni pamoja na kukata kutoa documents kuhusu miradi mbalimbali iliyoko ktkt wilaya hiyo ya Rorya. Tangu nikiwa shule ya msingi miaka ya 80 mwanzoni sijawahi kusikia jambo km hili. Tulikuwa tunaamka alfajiri saa 11 km ndio muda mwenge unapita ktkt eneo letu. Navyojua mwenge wa uhuru ni kitu kinachoheshimiwa sana ktk nchi yangu ninayoifahamu.
Kiongozi wa mwenge wa uhuru ni mwakilishi wa Rais wa Nchi na mwaka huu mwenge alikabidhiwa na Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mkoani Mtwara. Hivi mkurugenzi wa wilaya ni nyau wa aina gani kuudharau? Kwa maana nyingine amemdharau Rais wa jamhuri ya muungano pamoja na waziri mkuu. Mwenge wa uhuru unatumika kuunganisha nchi yetu, unapelekea ujumbe wa kitaifa ktk maeneo yote ya nchi yetu, unamulika ufisadi wa aina yoyote ktkt miradi yetu, nyau km mkurugenzi wa wilaya amepata wapi ujasiri wa kuudharau? Bado hajakamatwa na kuwekwa ndani?, bila shaka huyu siyo raia wa nchi hii. Hivi siku hizi vetting zinafanyikaje, huyu bwana amepataje nafasi ya ukurugenzi wa wilaya? Huyu siyo aondolewe tu bali afanyiwe uchunguzi wa kutosha. Lazima tuwe wazalendo kwa nchi yetu