Ngoja warudi tujue kipi ni sahihi au vipi.
Kwa alie wahi kufika kambi hii ya JWTZ KABOOYA
Kuna mnara wa kumbukumbu ya mashujaa pamoja na vifaaa vilivyotumika vitaani .
Cha ajabu zaidi mnara huo una majiiina ya askari woote waliokufa vitani ni weengi saaaana kupita maelezo .
 
Askari wrote waliokufa vitani ni 614 ikiwa nipamoja na askari wa kigeni waliokuka kutupa msaada angalalia vizuri mnara wa mashujaa wa vita ya Uganda kaboya uliopo mkoani kagera
 
#HISTORIA_NA_KUMBUKUMBU_YA_VITA_YA_KAGERA:

Jeshi la Tanzania JWTZ laingia mji mkuu wa Uganda Kampala.

#Sehemu_ya - 21.

Katika toleo lililopita tuliona maandalizi ya Jeshi la wananchi wa Tanzania namna lilijidhatiti kuuvamia,kuuteka na kuukamata mji mkuu wa Uganda wa Kampala.

Tuliona namna hali ya hewa ilivyokuwa mbaya sana,lakini askari wetu walifanikiwa kukabiliana nayo kibishi katika mazingira magumu ya mvua.

Brigedi za 201, 207 na 208 zilijipangwa kwa kazi muhimu.
Wakati mipango ya kuiteka Kampala ikifanyika katika Ikulu ya Entebbe,Iddi Amin naye alikuwa mjini Kampala na maofisa wa jeshi lake wakipanga namna ya kuulinda mji huo,hata hivyo mipango yao haikufanikiwa na Kampala ilitekwa.

Endelea…

Ingawa Iddi Amin alijiandaa kikamilifu kuilinda Kampala isitekwe na Tanzania,lilikuwa ni suala la muda tu kabla majeshi ya Tanzania hayajauteka mji huo.

Brigedi ya 208 ilikuwa ikisonga mbele kuelekea kati kati mji huo kutokea Kusini ma jiji la Kampala.
Luteni Kanali Benjamin Msuya alikuwa akiongoza mapambano hayo akiwa na askari kiasi cha 800.

Hawa walikuwa wakielekea katikati ya Kampala,wakati huo Brigedi ya 207 ilikuwa inashambulia kutokea Magharibi mwa Kampala, wakati Brigedi ya 201 ikiweka vizuizi Kaskazini kuwakabili wanajeshi wa Amin waliokuwa wanakimbia.

Upande wa Mashariki uliachwa kuruhusu Walibya kukimbilia Jinja na kuondoka Uganda.

Mashambulizi ya mji wa Kampala yalianza asubuhi ya Jumanne ya mwezi Aprili 10, 1979.
Majeshi ya Tanzania yalifanikiwa kushinda kila aina ya upinzani wa majeshi ya Amin waliokutana nao,licha ya kukabiliana na hali mbaya ya hewa.

Aprili 10 ni siku ya kihistoria kwa Tanzania na Uganda na Dunia pia.
Inapaswa kuandikwa katika vitabu vya historia kwa ajili ya vizazi vijavyo vya Waganda.
Majeshi ya Iddi Amin yaliyojaribu kupambana na majeshi ya Tanzania yalijikuta yakielemewa vibaya sana katika medani ya kivita.

Kwa mfano,katika eneo moja la Barabara ya Jinja, wanajeshi wa Amin waliojaribu kupambana na majeshi ya Tanzania kuvuka vizuizi vilivyowekwa na Brigedi ya 201 iliyokuwa ikiongozwa na Brigedia Imran Kombe,walidhibitiwa.
Hadi kufikia jioni askari wengi wa Amin walikuwa wameuawa na magari yao kadhaa yaliharibiwa.

Kutokea upande wa Magharibi mwa Kampala, Brigedi ya 207 iliyokuwa chini ya Brigedia John Butler Walden maarufu kama "BLACK mamba" ilikuwa inaukaribia mji wa kampala.
Ilipofika asubuhi kikosi cha Brigedia John Walden kikawa tayari kimeteka mji wa Natete na sasa kilikuwa kinaelekea Rugaba.

Maeneo ya Kilima cha Kasubi na makaburi ya Kabaka nayo yakawa yametumbukia mikononi mwa majeshi ya Tanzania na washirika wake.

Wakati Luteni Kanali Benjamin Msuya akijiandaa kupeleka vikosi vyake kupitia barabara kuu ya kuelekea Kampala kutokea Kusini,vikosi vingine vya Brigedi ya 208 tayari vilikuwa njiani kuelekea Kampala kupitia Port Bell na gereza lililokuwa na sifa mbaya la Luzira.

Wakati huo mvua ilikuwa imepungua na angalau mawingu mazito nayo yalikuwa yameanza kupungua na anga kufunguka.

Kadiri Kampala ilivyokaribiwa ndivyo kwa mara ya kwanza raia walivyokuwa wakiongezeka na kuwa makundi makubwa barabarani huku wakiwa na majani na matawi ya miti wakiwapungia wanajeshi wa Tanzania waliokuwa wakielekea katikati ya jiji la Kampala.
Walijua kuwa mara baada ya Kampala kutekwa,enzi ya utawala wa Iddi Amin wa Uganda ingekuwa imefikia mwisho.

Luteni Kanali Benjamin Msuya alikuwa na wasiwasi kuwa katikati ya Jiji la Kampala kwenye majengo marefu huenda kungekuwa na wadunguzi au wadunguaji.
Hata hivyo hakuwa na la kufanya kwa sababu raia wengi walikuwa wanaingia mitaani kuwalaki wanajeshi wa Tanzania.

Walipokaribia mzunguko wa Makindye,karibu na Gereza la Makindye lililotumiwa na Iddi Amin kama kambi ya mateso kwa raia wake na watu wengine,umbali wa kama kilomita mbili kutoka katikati ya kampala,adui walishambulia.
Wakati makundi ya raia wakishangilia,ghafla zilisikika risasi za SMG.

Katika hali ya kushtukiza namna hiyo ilikuwa ni vigumu kwa raia na wanajeshi kupata mahali pa kujificha.
Kwa hiyo raia walibaki wakishangaa kinachoendelea.

Wanajeshi wengi waliwahi kujificha kwenye mitaro ya maji machafu.
Milio ya risasi iliendelea kuongezeka,pamoja na mashambulizi hayo,mara moja Luteni Kanali Msuya alitoka na mkuki wake kwa kasi kuelekea mbele bila kujikinga.

Alipofika mstari wa mbele kabisa alielezwa kuwa risasi hizo zilielekezwa kwa wanajeshi wa Tanzania kutokea nyuma ya soko lililokuwa eneo hilo.
Hata hivyo,hakuna mwanajeshi wala raia aliyepatwa na risasi hizo.

Wakiwa wanatafakari hilo, mara wakaona gari aina ya Mercedes Benz likija kwa kasi kuingia barabarani kuelekea walipokuwa wanajeshi wa Tanzania.

Ndani ya gari hilo kulikuwa na askari watano waliokuwa wamevalia kiraia,mmoja ndiye aliyekuwa akiendesha na wengine wakiwa wamening’inia kwenye madirisha ya gari huku wakifyatua risasi.

Ni dhahiri kwamba askari hao walikuwa wamejitoa mhanga,na haikujulikana hasa kwa nini hao wanaume watano waliamua kupambana na jeshi la zaidi ya askari 800 lenye vifaru na silaha nyingine nzito za kivita.

Hata hivyo ndani ya sekunde chache walikuwa tayari wameuawa na wanajeshi wa Tanzania kabla hata hawajaufikia mzunguko wa Makindye kwa gari lao kulipuliwa katika mapigano yaliyodumu kwa dakika 10 tu.

Muda mfupi baadaye askari wachache walitumwa kwenda kupekua eneo la soko ambamo gari lile lilitokea.
Lakini hawakukuta chochote cha kutiliwa shaka.

Wanajeshi wa Tanzania wakaanza kuimba “Kamata Kampala” ... “Kamata Kampala”, kisha wakaanza tena kutembea kuelekea katikati ya Jiji la Kampala. Raia walirejea tena kwenye makundi yao na kuungana na wanajeshi wa Tanzania na ‘gwaride’ likaanza tena kuelekea Kampala kana kwamba hakuna lolote lililotokea.

Kabla ya kufika katikati ya Kampala kulikuwa na matukio kadhaa ambayo askari wa Amin katika maeneo fulani fulani walijaribu kuwarushia risasi askari wa Tanzania kabla ya kukimbilia mafichoni,lakini katika matukio yote haya hakuna risasi iliyompata hata mmoja.

Ilipofika saa 11 jioni askari wa JWTZ wakafika eneo la Clock Tower katikati ya Kampala,hili ni eneo ambalo Septemba 1977 Amin aliwaua kwa kuwapiga risasi watu 12 wa kabila la Langi na Acholi akiwamo Askofu Janani Luwumu akiwatuhumu kula njama za kuipindua serikali yake.

Luteni Kanali Benjamin Msuya na wapiganaji wake hawakuwa na ramani ya kampala,na sasa zilikuwa zimebakia saa mbili tu kabla giza halijaingia.

Jambo la kwanza ambalo alipanga kulifanya ni kukiteka kituo cha Redio ya Taifa ya Uganda (UBC).

Katika hatua hii tumeona namna majeshi ya Tanzania yakifanikiwa kuingia katikati ya jiji la Kampala,baada ya Brigedi ya 208 chini ya kamanda Benjamin Msuya kuongoza mapambano na uvamizi huo wa mji mkuu wa Uganda.

Itaendelea….
 
#HISTORIA_NA_KUMBUKUMBU_YA_VITA_YA #KAGERA:

Brigedia Benjamin Msuya ashangilia kuiteka Kampala.

#Sehemu_ya_22.

Toleo lililopita tulisimulia askari wa Tanzania chini ya Luteni Kanali Benjamin Msuya walivyoingia mjini Kampala pamoja na kwamba hali ya hewa ilikuwa mbaya na mvua kubwa ilikuwa inanyesha.
Lakini kutokana na ari waliyokuwa nayo askari wetu,licha ya hali ya hewa kuwa mbaya lakini hawakuvunjika moyo kupambana.

Hatimaye JWTZ lilifanikiwa kuuweka mji huo katika himaya yao na kuhakikisha askari wa Iddi Amin wameshindwa vita.

Baadaye Msuya na askari wake waliamua kuhakikisha kuwa wamekalia vilima vyote vinavyoizunguka Kampala.

Baada ya kuzunguka mjini kutokana na kukosa ramani ya mji wa Kampala,huku wakikumbana na mtupiano wa risasi wa hapa na pale kutoka kwa askari wa Iddi Amin waliokuwa wamejificha kwenye majengo fulani fulani katika mji huo,hatimaye walifika katika kituo cha Redio Uganda.

Wanajeshi wa Tanzania waliliendea jengo la redio hiyo kwa uangalifu sana huku askari wengine wakililinda jengo refu la ghorofa lililokuwa upande wa pili wa barabara.

Askari wa Tanzania hawakuona ishara yoyote ya kuwapo kwa adui katika eneo hilo na Luteni Kanali Benjamin Msuya na baadhi ya askari wengine walikwenda moja kwa moja kufungua milango ya kituo hicho cha redio huku wengine wakivinjari mitaani.

Msuya alikuwa amepewa maelekezo ya kwamba asitoe matangazo yoyote ya redio iwapo atakuwa amekiteka kituo hicho cha redio.
Hata hivyo aliamua hatatangaza chochote, lakini alikwenda kwenye jengo la studio za redio hiyo kuona kama vifaa vyake vilikuwa vinafanya kazi.

Kwa uangalifu mkubwa, Msuya na baadhi ya askari wake waliingia ndani ya jengo hilo,na ilionekana kuwa jengo lilikuwa na chanzo chake cha umeme kwa sababu lilikuwa na umeme wakati sehemu nyingine za Jiji la Kampala hazikuwa na umeme.

Msuya na askari wake walianza kuchunguza vifaa vya studio hiyo,na wakati wakifanya hivyo,milio ya risasi ilisikika kwa sauti kubwa.

Ilikuwa ni vigumu kujua mara moja kama milio hiyo ilikuwa ikitoka ndani au nje ya jengo hilo.
Hata hivyo baadaye ikajulikana kuwa risasi hizo zilikuwa zikipigwa kutoka kwenye jengo refu.

Askari wa Tanzania walijibu mapigo kwa kulishambulia jengo hilo. Mapigano hayo yalidumu kwa muda wa takribani sekunde 30 na yalipokoma baadaye ni ama askari hao wa Iddi Amin walikuwa wameuawa au walijificha kwa sababu hawakuonekana tena.

Sasa giza lilikuwa limeshaingia na bado kulikuwa na vilima viwili kati ya saba vilivyoizunguka Kampala ambavyo vilitakiwa kutekwa usiku huo.
Maeneo ya mji wa Kampala ambayo yalikuwa hayajatekwa ni kilima cha Nakasero ambako kulikuwa na makao makuu ya polisi wa siri wa Iddi Amin waliojulikana kama "State Research Bureau" na makazi ya Amin na kilima cha Kololo.

Wakati Msuya akimaliza kukagua kituo cha redio, kikosi kingine kutoka kwenye brigedi yake kilikuwa kikiandaa shambulio.

Gari aina ya Land Rover likilivuta gari jingine aina ya Land Rover yote yakiwa na silaha yalionekana barabarani.
Inaelekea kuharibika kwa gari mojawapo kulisababisha kuchelewesha mpango wa askari wa Iddi Amin waliokuwa wakikimbia mji.

Shambulizi kutoka kwa askari wa Tanzania liliyafanya magari hayo yasimame na askari watatu waliovalia kiraia waliruka kutoka kwenye magari hayo, lakini waliuawa mara moja.

Katika gari mojawapo askari wa Tanzania walikuta mpango wa kivita kwa eneo lote la Kampala. Katika mpango huo mji wa Kampala ulikuwa umegawanya katika sehemu nyingi ndogondogo na kila sehemu ilikuwa imekabidhiwa kikosi chake cha kulinda,lakini wengi wa askari wa vikosi hivyo tayari walikuwa wamekwishakimbia.

Ilionekana pia kwamba hata Iddi Amin alikuwa katika mji huo jana yake,ilijulikana kuwa alizuru Hospitali ya Mulago na kuwaambia askari waliojeruhiwa na kulazwa katika hospitali hiyo kwamba wasiwe na wasiwasi kwa sababu mambo yote yalikuwa yanakwenda vizuri.

Njia ambayo Rais Nyerere alisema ibaki wazi ili Walibya wapate mwanya wa kupitia hiyo na waweze kuondoka Uganda ndiyo hiyohiyo aliyoitumia Amin kuondokea katika zile dakika za mwisho za utawala wake nchini Uganda.
Maofisa wengine wakubwa wa Serikali ya Amin walikuwa wamekimbia mapema zaidi kabla ya Amin mwenyewe.

Kila ofisa aliyekuwa anakimbia alimwachia maelekezo wa chini yake aendelee kuilinda Kampala.
Mtindo huo ukaendelea hadi walipokosekana maofisa wa kuwaongoza askari wa Amin na hivyo kubaki wakijiongoza wenyewe.

Msuya na askari wake walianza safari ya kuelekea Kololo na kwenye vilima vingine vilivyoizunguka Kampala.
Muda mwingi Msuya alikuwa kwenye mawasiliano ya redio kuwaweka askari wake pamoja.

Kila hatua sasa ilichukuliwa kwa uangalifu mkubwa. Askari wa Iddi Amin waliokata tamaa wangeweza kushambulia kutoka upande wowote hata kwenye majengo walimojificha.

Giza lilikuwa likiongezeka na Msuya hakujua kilipokuwa kilima cha Kololo.
Raia wa Uganda aliyekuwa akisaidia kutoa maelekezo ambaye alijulikana kwa jina moja tu la Godfrey naye hakutoa msaada sana.

Kwa mujibu wa simulizi fulani,askari wa Tanzania wakaweka kizuizi njia ya kuingia mjini ingawa hakukuwa na magari.

Baadaye likatokea gari moja ambalo walilisimamisha,ndani ya gari kulikuwa na mwanamke na mwanamume.
Alipohojiwa na Msuya ikajulikana kuwa alikuwa ofisa wa polisi wa Uganda.

Alipoulizwa aliko Iddi Amin, akasema hajui,Msuya akampiga kofi na kumuuliza tena,ni askari wangapi wa Amin wamebaki hapa mjini?

Akajibu kuwa hajui.

Akapigwa kofi jingine.
Mwanamke naye akaulizwa maswali,naye ikaonekana hana majibu.
Lakini hakupigwa.
Akamwamuru aende nyumbani na asitoke lakini yule ofisa wa polisi akashikiliwa kwa dakika nyingine kumi.

Baada ya kuona hana majibu ya maswali aliyoulizwa,naye aliruhusiwa kuondoka zake.

Wakiwa na njaa na kiu, askari wa Tanzania walielekea Kololo.
Baada ya kulitafuta eneo hilo kwa muda mrefu, hatimaye walilikuta.
Huko walijipanga na kuanza kuchimba mahandaki.
Saa tano usiku Msuya aliwaita maofisa wake na kupongezana kwa kuutwaa mji wa Kampala.

Wakazi wa Kololo walikuwa wamejifungia kwenye nyumba zao bila kutambua kuwa tayari mji wa Kampala ulikuwa umekombolewa na majeshi ya Tanzania.

Walipokuwa wakisikia milio ya buti za askari wakitembea walidhani ni askari wa Amin waliokuwa wakifanya doria katika maeneo yao.
Milio ya vifaru vilivyokuwa vikipita iliwatia hofu zaidi kiasi kwamba waliogopa kuwasha hata mishumaa na vibatari vyao.

Umeme ulikuwa umekatika maeneo yote ya viunga vya mji wa Kampala.

Baada ya mji wa Kampala kuangukia mikononi mwa JWTZ,nini kiliendelea!?

Endelea kutembelea ukurasa huu,ili kuendelea kuhabarika.

Itaendelea......
 
#HISTORIA_NA_KUMBUKUMBU_YA_VITA_YA_KAGER

Yusufu Lule aunda Serikali ya mpito.

#Sehemu_ya_23.

Katika toleo lililopita tuliona jinsi wakazi wa eneo la Kololo mjini Kampala walivyojifungia ndani wakati wanajeshi wa Tanzania wakipita usiku na vifaru vyao.
Hawakuwa wametambua kama Kampala ilikuwa imekombolewa na majeshi ya Tanzania.

Walidhani vishindo vya mabuti ya askari waliokuwa wakitembea na milio ya vifaru vilivyokuwa vinapita ni vya askari wa Amin.
Hata hivyo walikuja kugundua baadaye kuwa Kampala imekombolewa kutoka mikononi mwa utawala wa Iddi Amin.

Baada ya Jiji la Kampala kuangukia mikononi mwa majeshi ya Tanzania,hali haikutulia kama ilivyotazamiwa.
Usiku wa Jumanne ya Aprili 10 kuamkia Jumatano ya Aprili 11, 1979, maelfu ya wanajeshi wa Tanzania walikuwa wakivinjari katika jiji la Kampala.

Vikosi kadhaa vya Brigedi ya 208 iliyokuwa chini ya Brigedia Mwita Marwa vilikuwa kusini mwa mji huo.
Brigedi ya 207 ya John Butler Walden "Black Mamba" ilikuwa upande wa magharibi mwa jiji la Kampala.

Brigedi ya 201 chini ya Brigedia Imran Kombe ilikuwa imeweka kizuizi upande wa kaskazini.

Hadi mapambazuko ya Jumatano ya Aprili 11, 1979, wanajeshi wa Tanzania wakawa katika kila kona ya kila barabara iliyoingia katika Jiji la Kampala,ikiwa ni pamoja na barabara iliyoelekea Jinja.
Askari yeyote wa Iddi Amin ambaye alikuwa amesalia katika mji wa Kampala sasa alikuwa anawindwa na waliopatikana waliuawa.

Mapema Jumatano asubuhi,wapiganaji wa ukombozi wa Uganda, pengine kutokana na wengi wao kulewa usiku wa jana yake,walianza kuwaghasi raia waliokuwa wakipita na magari yao mitaani.
Lakini kiongozi wao,Kanali David Oyite Ojok alilazimika kuingia kwenye studio za Redio Uganda kuwatangazia waache kuwasumbua watu.

Kanali Ojok alitaka kutimiza ndoto yake ya kuwatangazia Waganda kuwa sasa wako huru dhidi ya Iddi Amin.
Lakini Profesa Yusuf Kironde Lule, kiongozi wa Umoja wa Kuikomboa Uganda (UNLF), akitambua ukaribu uliokuwapo kati ya Kanali Ojok na Dk Milton Obote, alihofia kuwa Ojok angetangaza kuwa Obote amerejea madarakani nchini Uganda.

Kanali Ojok alipokuta simu iliyokuwa ikifanya kazi katika studio za Redio Uganda,aliitumia kwa kupiga simu mbili jijini Dar es Salaam.

Simu moja alimpigia Rais Julius Nyerere na simu ya pili alimpigia Obote.
Ojok alikuwa amemwahidi Obote kuwa angempigia simu mara atakapokuwa amefika Kampala,na sasa alikuwa anatimiza ahadi yake.

Mwalimu Nyerere hakuwa ofisini kwake wakati Kanali Ojok akimpigia simu,lakini Ojok akaacha ujumbe kwa ofisa usalama aliyepokea simu hiyo kwamba Kampala imedhibitiwa.
Alipozungumza na Obote, Kanali Ojok alimwambia kuwa amenuia kutangaza kukombolewa kwa Kampala “kwa jina la UNLF”. Obote alimjibu kwamba hilo ni jambo jema.

Ingawa Kampala ilikuwa imeshakombolewa kutoka kwa Iddi Amin,milio ya risasi ya hapa na pale ilikuwa ikisikika mitaani na wakati mwingine milio ya mabomu nayo ilisikika.
Pamoja na yote hayo, mafundi mitambo wa Redio Uganda walifika kazini na kuendelea na kazi zao kama kawaida.

Ojok aliamua kutoa matangazo yake kupitia Redio Uganda.
Alitangaza kuwa utawala wa Amin nchini humo umeondolewa na kwamba sasa Kampala ilikuwa mikononi mwa UNLF.

Ojok alinukuliwa na jarida la Tarehe Sita akisema:

“Tunauomba umma wa Waganda kuamka na kuungana pamoja kuwaondoa kabisa wauaji wachache waliobakia.”

Aliendelea kusema:

“Tunawaomba wapenda amani wote wa Dunia hii kuwaunga mkono wakombozi wa Uganda na waulaani utawala uliopita wa kifashisti.”
Ojok aliwataka raia wa Kampala kuwa watulivu na kisha akawataka askari wa Iddi Amin “…popote walipo nchini Uganda wajisalimishe mara moja.”

Ingawa alitangaza hayo, mjini Dar es Salaam Profesa Lule ambaye alikuwa akiyasikiliza matangazo hayo ya Kanali Ojok kupitia Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), ambayo iliyarudia matangazo ya Ojok ya Redio Uganda,hakuyapenda sana.

Huenda ni kwa sababu hakusikia jina lake likitajwa katika matangazo yenyewe. Aliamini kuwa huu ndio wakati wake wa kusikika wakati wa kihistoria katika maisha yake na historia ya Uganda.

Kiuhalisia Profesa Lule alikuwa hotelini mjini Dar es Salaam wakati Ojok na wengine wakiwa katika uwanja wa mapambano dhidi ya utawala wa Iddi Amin kwa kipindi cha miaka kadhaa na sasa walifanikiwa kupigana hadi kuitwaa Kampala.

Profesa Lule aliamua kuandaa tangazo lake mwenyewe ambalo lingetolewa na Redio Uganda.
Tangazo hilo lilirekodiwa kwenye mkanda wa kaseti mjini Dar es Salaam na baadaye likatumwa Kampala Uganda kwa ajili ya Redio Uganda.

Ingawa hivyo tangazo lililonukuliwa na vyombo vya habari vya kimataifa ni lile la Kanali Ojok na si lile la Profesa Lule.

Katika mkanda wa kaseti uliorekodiwa Dar es Salaam na kupelekwa Kampala,kwa mujibu wa jarida la "Summary of World Broadcasts: Non-Arab Africa" la Ijumaa ya Aprili 13, 1979, Profesa Lule alisema:

“Najisikia heshima na faraja kuwatangazia muundo wa Serikali ya mpito kwa nchi yenu Uganda. Serikali yenu itakuwa kama ifuatavyo....”

Baada ya kujitaja mwenyewe kama Rais wa Serikali ya mpito ya Uganda na mawaziri wake aliowateua akiwa mjini Dar es Salaam,Profesa Lule alitaka kuwapo na utawala wa sheria,kisha akaahidi kuwa utafanyika Uchaguzi Mkuu nchini Uganda “mapema kadri hali itakavyoruhusu”.

Miongoni mwa waliotajwa katika baraza lake la mawaziri ni pamoja na Sam Sabagareka, Otema Alimadi, Paulo Mwanga, Dk Arnold Bisasi, A. Biararuha, Mathias Ngobi, Profesa Asavia Wandira (Elimu), Dani Wadada Nabudere (Utamaduni na Maendeleo ya Jamii), George Wilson Kanyeihamba (Sheria) na Luteni Kanali William Omaria.

Lakini siku moja baada ya matangazo hayo Iddi Amin alijibu,katika matangazo yake Amin alimjibu Ojok na si Profesa Lule.

Amin alikuwa akizungumza kutokea mahali fulani magharibi mwa Uganda.Inawezekana alikuwa akizungumza kupitia kituo fulani cha idhaa ya nje ya Redio Uganda au kwa kutumia magari ya matangazo ya redio aliyoyanunua kwa gharama akiwa madarakani.

Kwa mujibu wa gazeti la "The Washingtong Post" la Aprili 12, 1979 chini ya kichwa cha habari Uganda Capital Cuptured, Iddi Amin alinukuliwa akisema:

“Mimi Rais Iddi Amin Dada wa Jamhuri ya Uganda, napenda kukanusha matangazo yaliyotolewa na aliyekuwa Luteni Kanali wa jeshi, Oyite Ojok, kwamba eti Serikali yangu imepinduliwa na eti Serikali ya uasi imeundwa Uganda...”

Nini kilitokea?

I #HISTORIA_NA_KUMBUKUMBU_YA_VITA_YA_KAGERA:

Uporaji washamiri jijini Kampala.

#Sehemu_ya_24.

Baada ya Kanali David Oyite Ojok kutangaza kupitia Redio Uganda kuwa utawala wa Iddi Amin umeangushwa rasmi nchini humo,siku iliyofuata Amin alikanusha kupitia redio hiyo hiyo lakini akitangaza kutokea mahali fulani magharibi mwa nchi,labda kwa kutumia mojawapo ya magari ya matangazo ya redio aliyonunua kwa gharama kubwa wakati wa utawala wake.

Profesa Yusuf Lule naye alitangaza Serikali yake akiwa mjini Dar es Salaam.Wakati yote hayo yakitokea,uporaji ulitia fora mjini Kampala.
Ingawa ilitazamiwa kuwa baada ya Uganda kukombolewa mambo yangekuwa shwari,hali ilikuwa tofauti na matarajio.
Uporaji ulianza na kisha kuenea maeneo yote hususani katika mji wa Kampala.

Waporaji walionekana wajasiri sana na waliingia mitaani mapema Jumatano ya Aprili 11, 1979 pamoja na kwamba bado kulikuwa na milio ya risasi na mabomu katika mitaa ya Kampala na wanajeshi wa Jeshi la Kuikomboa Uganda (UNLA) walielekezwa kumpiga risasi mtu yeyote aliyekuwa mitaani ambaye hakuwa amevaa sare.

Kufikia jioni ya siku hiyo ikawa imeshakuwa kawaida kuona makundi ya waporaji wakitembea mitaani huku wamebeba mikononi na vichwani mwao mali walizopora.

Kabla ya giza halijaingia mitaa mingi ikawa imefurika watu kiasi kwamba hata magari yalishindwa kupita.
Maeneo yaliyowavutia zaidi waporaji ni nyumba zilizokimbiwa za maofisa wa Iddi Amin.

Lakini baada ya kumaliza kupora katika nyumba hizo,walihamia na kwenye maeneo mengine.

Askari wa Tanzania walibaki wakitazama hali inavyokwenda,lakini Luteni Kanali Benjamin Msuya alikerwa na hali hiyo na ingawa aliona ni lazima afanye chochote,hakuwa na namna ya kuweza kuzuia hali hiyo ya uporaji hata kama ingekuwa ni kwa kuwafyatulia risasi waporaji hao kwa sababu kwa kufanya hivyo askari wake wangelazimika kuwafyatulia risasi idadi kubwa ya raia.

Jambo ambalo Msuya hakulitaka ni kujenga chuki kati ya raia wa Uganda na askari wake.Aliwaamuru askari wake kuwasaidia raia kuingia katika majengo ili kuweka vizuri mali zilizokuwamo.
Lakini hali ikawa kinyume kabisa.
Askari wa Tanzania walipovunja mlango wa mojawapo ya maghala mjini Kampala lililokuwa karibu na njia ya reli walikuta kulikuwa na hifadhi kubwa ya sukari.

Kulikuwa na uhaba mkubwa wa sukari nchini Uganda kwa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya Vita vya Kagera havijazuka.
Kwa mujibu wa jarida la "New African Yearbook," kutokana na vibandiko vilivyokuwa kwenye mifuko iliyofungasha sukari hiyo, Amin alikuwa akiisafirisha kwenda Libya kwa kubadilishana na silaha zilizotumika vitani nchini humo.

Jarida la "Africa News" liliandika kuwa sukari hiyo ilikuwa imeandaliwa tayari kusafirishwa kupelekwa Libya.

Kitabu "cah Ethnicity, Nationalism, and Democracy in Africa" cha Bethwell Allan Ogot kinasema bidhaa za walaji kama sukari na chumvi zilikuwa adimu nchini Uganda kiasi kwamba haikushangaza baada ya utawala wa Amin kuanguka ndizo zilizoporwa zaidi.

Taarifa za kupatikana kwa sukari katika ghala hilo zilisambaa kwa haraka.Ndani ya dakika chache raia wengi wakawa wamepata taarifa hizo na maelfu wakawa wamefika eneo hilo ndani ya nusu saa ili nao wajipatie sehemu yao.

Kitabu cha "War in Uganda" kinasema katika uporaji huo,mama mmoja aliyekuwa amemfunga mwanawe mgongoni kwa kanga huku naye akijitahidi kujipatia sehemu yake katika uporaji wa sukari hiyo,mtoto huyo aliuawa baada ya kubanwa katika purukushani.

Mwanamume mmoja aliyejaribu kubeba mfuko wa kilo 50 kichwani naye alikufa kwa kukosa hewa kutokana na msongamano wa watu ulivyokuwa mkubwa.

Hadi kufikia hatua hii, kinaandika kitabu hicho kuwa askari wa Msuya walikuwa wakitazama waporaji walivyokuwa wakihangaika kujipatia sehemu ya bidhaa.

Siku iliyofuata, Alhamisi ya Aprili 12, 1979, uporaji ulikuwa umefikia hatua ya kutozuilika.
Sasa ukawa unafanywa si tu katika zile nyumba zilizokimbiwa,bali hata kwa zile zilizokuwa na watu.

Wenye nyumba hizo walishindwa kuwazuia waporaji na hivyo wakabaki wakiwaangalia bila msaada wowote,jinsi mali zao zilivyokuwa zinaporwa.

Kila duka, ghala, ofisi na kila nyumba iliporwa.
Wakati uporaji ukiendelea askari wachache wa Amin waliobakia bado walikuwa katika Jiji la Kampala.
Lakini sasa walikuwa wanatamani jambo moja tu kuondoka mjini Kampala kwa njia yoyote inayowezekana na kwa haraka inavyowezekana.

Askari hao walitamani kupata nguo za kiraia ambazo wangevaa waweze kuondoka mjini Kampala bila kutambuliwa kuwa ni wa Amin.
Njia pekee ambayo wangeweza kupata nguo hizo ni kwa kuwanyang’anya raia waliokuwa wamezivaa.

Njia rahisi zaidi ya kuwanyang’anya raia hao ilikuwa ni kwa kuwaua ikiwa wangekataa kuvua kwa hiari yao.
Hatimaye walianza kuingia mitaani maeneo ya raia wakiwa ama mmoja mmoja au katika makundi ya askari wachache wakitafuta nguo za kiraia,chakula na la maana zaidi kwao magari ambayo wangeweza kuyatumia kukimbia mji.

Walitumia silaha walizokuwa nazo kufanya uporaji wa mambo hayo. Raia ambao hawakutii matakwa ya askari hao na wengine ambao hawakupewa nafasi mbadala waliuawa.

Askari wa Tanzania waliokuwa wakifanya doria kwa kutembea kwa miguu mitaani na wengine kwenye magari aina ya Land Rover katika maeneo ya raia mara kadhaa walikumbana na askari wa Amin waliokuwa wakipora na kuwaua raia waliowapora.

Kurushiana risasi kulisikika mara kwa mara katika mitaa mbalimbali ya mji.
Milio ya risasi iliposikika, waporaji walijificha lakini wakawa wanaibuka tena baadaye.

Miili ya waliouawa ilibaki imelala mitaani ikioza na ilipofika mwisho wa wiki miili mingi ya raia wengi ilionekana mitaani.
Kitabu cha "War in Uganda" kinasema kikundi kimoja cha askari wa Amin kilichokuwa na silaha kiliingia nyumbani kwa watumishi wa Ubalozi wa Ufaransa mjini Kampala kwa nia ya kuwapora gari.

Watumishi hao ni Ricarda Hetsch na mumewe, Charles Hetsch.
Wakiwa na silaha zao walifika getini walielekeza silaha kwa Ricarda wakimtaka awakabidhi funguo za gari lake.
Kwa kuwa Ricarda naye alikuwa mzoefu wa kutumia silaha na alikuwa na bastola yake,ghafla aliichukua na kufyatua risasi tatu. Askari hao walijikuta wakichanganyikiwa wakaanza kukimbia ovyo.

Wakati Serikali ya mpito ikitangazwa kupitia Redio Uganda,uporaji ulikuwa umeshika kasi kuliko ilivyokuwa awali.
Kampala ilikuwa imekombolewa kutoka kwa Iddi Amin,lakini uporaji ulitia fora.

Itaendelea ........
 
#HISTORIA_NA_KUMBUKUMBU_YA_VITA_YA_KAGERA

1978-1979: Uhalifu waingia mitaani na kuzidi kushamiri.

#Sehamu_ya_25.

Toleo lililopita tuliona askari wa Iddi Amin waliobakia katika mji wa Kampala walivyohaha kutoroka bila kujulikana.

Waliingia mitaani maeneo ya raia wakiwa ama mmoja mmoja au katika makundi ya askari wachache wakitafuta nguo za kiraia,chakula na la maana zaidi kwao magari ambayo wangeweza kuyatumia kukimbia mji.

Pia walitumia silaha walizokuwa nazo kufanya uporaji na raia ambao hawakutii matakwa ya askari hao na wengine ambao hawakupewa nafasi ya mjadala waliuawa,hata hivyo hatimaye walielemewa.

Sasa endelea.....

Ukiacha uporaji uliokuwa ukiendelea na mtupiano wa risasi wa hapa na pale uliokuwa ukifanywa na askari wa Iddi Amin waliokuwa wanatafuta njia ya kuikimbia Kampala, baadhi ya wapiganaji wa Jeshi la Ukombozi wa Uganda (UNLA) nao walijikuta wakilipiza visasi kwa vibaraka wa Amin.

Baadhi ya waliokuwa wameukimbia utawala wa Iddi Amin lakini sasa wakawa wamerudi walianza kuwawinda na kuwaua wale ambao wao walidhani kuwa waliwasaliti au familia zao miaka iliyopita katika utawala wa Amin.

Askari wengine wa UNLA waliua kila Mnubi au Mkakwa waliyekutana naye.
Usiku wa Jumanne ya Aprili 10 kuamkia Jumatano, siku ambayo Kampala ilikombolewa,wafuasi wa Amin waliyakimbia makao makuu ya polisi wake wa siri "State Research Bureau SRB" yaliyokuwa eneo la Nakasero.

Lakini wakati wanaondoka walirusha mabomu ya mkono kwenye vyumba walimokuwa wafungwa ambao awali walikuwa wamenusurika kufa kwa njaa,mateso na adhabu za vifo.

Ilipofika asubuhi ya kesho yake maeneo ya maegesho ya magari kwenye ofisi za SRB yalikuwa yamefurika raia waliofika kuangalia kama kuna ndugu zao waliokuwa wanashikiliwa humo.

Baadhi ya walionusurika kufa walikuwa wamekonda kupita kiasi.
Wapo wengine waliotoka walijikuta wakipata tabu juani kutokana na kuona jua kwa mara ya kwanza katika kipindi cha muda mrefu kwa sababu walikuwa wamefungiwa ndani.

Kwa mujibu wa kitabu cha "Escape from Idi Amin’s Slaughterhouse" cha Wycliffe Kato,miili ya raia waliokuwa wanashikiliwa katika makao hayo makuu ya SRB ilikuwa imetapakaa karibu kila eneo.

Harufu kali ya miili iliyooza ilielekea kutovumilika.
Raia wa Uganda waliingia ndani ya vyumba vya mateso vya SRB kutafuta miili ya wapendwa wao.

Miili mingine ilikuwa ni ya watu ambao ndiyo kwanza walikuwa wameuawa saa chache kabla ya askari wa Amin kukimbia wakati mingine ilikuwa ni ya muda mrefu uliokuwa umepita.

Mingine ilikuwa imekatwa mikono na miguu.
Kitabu cha "War in Uganda" kinasema kwenye sakafu ya chini ya ardhi ya jengo hilo kulikuwa na silaha kali za kivita na mabomu yaliyokuwa na uwezo wa kuangamiza mji mzima.

Ikiwa mabomu hayo yangetumiwa kuvunja madaraja ya kusini mwa Uganda huenda yangewachelewesha askari wa Tanzania kwa miezi kadhaa kuifikia miji iliyoteka.

Ghorofa ya juu ya jengo hilo kulikuwa na kompyuta kadhaa na majalada yaliyokuwa na habari muhimu za kiitelijensia na nyingine zisizo za muhimu zilizohusu shughuli za maelfu kwa maelfu ya Waganda waliokuwa ndani na nje ya nchi na utiifu wao kwa Serikali ya Uganda.

Pia kulikuwa na maelfu kwa maelfu ya majalada yenye taarifa za wageni waliokuwa wakiishi Uganda au walioitembelea Uganda.

Kwa mujibu wa kitabu hicho,jalada moja lilionyesha kuwa wakala mmoja wa SRB alikuwa akilipwa posho ya Dola 58,500 za Marekani kwa ajili ya kumwezesha kupata taarifa.

Kitabu cha "War in Uganda" kimeandika kuwa faili moja katika maelfu ya mafaili yaliyokutwa katika ofisi hizo lilikuwa na muhtasari wa vikao vya siri vya baraza la mawaziri la Tanzania,moja likiwa na kiambato kilichosema

“Rafiki yetu wa Dar es Salaam anataka 5,000 nyingine mwishoni mwa mwezi ...

Inawezekana kilicho tatizo zaidi katika ghorofa ya juu ya ofisi za SRB ni nakala ya waraka wa siri wa jeshi la Tanzania ukieleza kinaganaga mpango wa kuishambulia Kampala.

Waraka huo ulionyesha njia zitakazotumika na kila mahali ambako kila kikosi kitakuwa ... muda uliowekwa katika mkakati huo ni wiki mbili hadi kuingia mji mkuu wa Uganda.”
Kwa jeshi lililokuwa likiulinda mji wake kama hilo la Amin,halikuwa na kitu cha thamani zaidi ya kupata mbinu za siri za jeshi la uvamizi.

Kwa jeshi lolote duniani ambalo lilikuwa limeshaupata mpango wa siri wa jeshi la adui ingekuwa ni rahisi kwao kuweka mtego na kuliangamiza jeshi la adui.

Lakini jeshi la Iddi Amin halikuweza kutumia taarifa hizo za kiitelijensia.
Huenda walizipata taarifa hizo wakiwa tayari wameshaelemewa na hivyo haikuwa rahisi kwao kuzitumia ilivyopaswa.
Isitoshe taarifa hizi hazikukutwa jeshini bali zilikutwa kwa polisi wa siri wa Amin.

Ilionekana kuwa SRB walikuwa mbali sana katika kukusanya taarifa za kiitelijensia.
Pengine tatizo lilikuwa katika kuzichanganua taarifa hizo na kuzifanyia kazi.
Kwa upande mwingine, Kanali Salim Hassan Boma na askari wake walifika kwenye Gereza la Luzira ambalo lilikuwa na sifa mbaya kwa mateso.

Liko kwenye viunga vya Kampala.
Maofisa na walinzi wote wa gereza hilo walikuwa wameshakimbia wakiwaacha wafungwa wakiwa wamefungiwa ndani ya gereza bila chakula na bila kujua kilichokuwa kikiendelea nje ya gereza.
Kanali Boma aliamuru gereza hilo lifunguliwe na wafungwa waondoke.
Miongoni mwa wafungwa hao alikuwamo kapteni wa ndege za kijeshi aliyepata mafunzo nchini Urusi.

Baada ya kuendesha ndege aina ya MiG-21 katika zile siku za mwanzo za vita, aligoma kuendelea na kazi na baadaye akakimbilia kijijini kwake ambako baadaye aligundulika na kukamatwa.

Mahakama ya kijeshi ilimhukumu kifo na Jumatano ya Aprili 11, 1979 siku ambayo Kampala ilikombolewa na majeshi ya Tanzania ndiyo ilikuwa tarehe iliyokuwa imepangwa yeye kuuawa kwa kupigwa risasi.

Aliposikia vishindo vya nyayo za miguu vikielekea lango la gereza alilokuwamo asubuhi ya Aprili 11, hakuwa na namna yoyote ya kujua kama hao waliofika gerezani hapo ni wauaji wake wamewasili kumchukua.

Lakini kwa mshangao akakuta ni binadamu waliokuja kumweka huru.
Askari wa Tanzania walihisi hawakuwa na la kufanya zaidi ya kuwaachia huru kila mfungwa waliyemkuta katika Gereza la Luzira kwa sababu hawakuwa na namna ya kuwalisha maelfu ya wafungwa na wakati huohuo wakiendelea na mapambano ya kumaliza vita.

Lakini kuachiwa kwa wafungwa hao kwa ujumla wao kulikuja kusababisha matatizo baadaye.
Baadhi ya wengine walioachiwa walikuwa wahalifu sugu ambao baadaye walichangia kuongezeka kwa uhalifu nchini Uganda.

Itaendelea hivi punde sehemu ya 26.
 
Safi
 
Ndugu zangu nilikuwa nahitaji kujua historia ya vita hivyo pamoja na jinsi wazanzibari walivyoshiriki.
Kuna mtu kaniambia kuwa bila ya wazanzibari na jeshi lao la nyuki tungeshindwa vibaya sana.
Kwa wanaojua ningependa kipata maoni yao
 
vita vya Kagera vilianza mwezi Oktoba 1978 mpaka Juni 1979.

katika kipindi hicho hakukuwa na jeshi la Wazanzibari linalojulikana kama "jeshi la nyuki."

aliyekusimulia huenda alimaanisha brigedi ya nyuki ya JWTZ ambayo makao yake makuu yako Zanzibar.

kabla vita vya Kagera havijaanza JWTZ ilikuwa na brigedi 4 kama ifuatavyo:--
1.Brigedi ya 401 / Tembo iliyokuwa Songea.
2.Brigedi ya 302 Dsm;
3.Brigedi ya 202/ Faru iliyokuwa Tabora
4.Brigedi ya 101 / Nyuki iliyokuwa Zanzibar.

vita vya Kagera vilipoanza Jeshi lilipangwa upya na ziliundwa brigedi zifuatazo.
1. Brigedi ya 201 -- iliongozwa na Brigedia.Imran Kombe.
2.Brigedi ya 205 -- iliongozwa na Brigedia.Herman Lupogo na baadae Brigedia.Muhidin Kimario.
3.Brigedi ya 206 -- iliongozwa na Brigedia.Silas Mayunga, baadae Brigedia.Roland Makunda.
4.Brigedi ya 207 -- iliongozwa na Brigedia.John Walden.
5.Brigedi ya 208 -- iliongozwa na Brigedia.Marco Mwita Marwa.
6.Brigedi ya Kagera -- iliongozwa na Brigedia.Ramadhani Haji Faki.
7.Brigedi ya Minziro -- iliongozwa na Brigedia.Ahmed Takadiri Kitete.

vita ilipiganwa kwa awamu mbili. awamu ya kwanza ilikuwa ni kuyaondoa majeshi ya Uganda toka ktk ardhi ya Tanzania. Operation hiyo iliitwa "operation chakaza" na iliongozwa na Brigedia.Tumainieli Kiwelu. awamu ya pili ni mapigano ndani ya ardhi ya Uganda na operation hiyo iliongozwa na Brigedia.David Musuguri.

mkuu wa majeshi CDF alikuwa ni Meja Jenerali.Abdalah Twalipo, mnadhimu mkuu wa jeshi CoS alikuwa Brigedia. Tumainieli Kiwelu, na Waziri wa Ulinzi alikuwa Rashid Mfaume Kawawa.
 
vita vya Kagera vilianza mwezi Oktoba 1978 mpaka Juni 1979.

katika kipindi hicho hakukuwa na jeshi la Wazanzibari linalojulikana kama "jeshi la nyuki."

aliyekusimulia huenda alimaanisha brigedi ya nyuki ya JWTZ ambayo makao yake makuu yako Zanzibar.

kabla vita vya Kagera havijaanza JWTZ ilikuwa na brigedi 4 kama ifuatavyo:--
1.Brigedi ya 401 / Tembo iliyokuwa Songea.
2.Brigedi ya 302 Dsm;
3.Brigedi ya 202/ Faru iliyokuwa Tabora
4.Brigedi ya 101 / Nyuki iliyokuwa Zanzibar.

vita vya Kagera vilipoanza Jeshi lilipangwa upya na ziliundwa brigedi zifuatazo.
1. Brigedi ya 201 -- iliongozwa na Brigedia.Imran Kombe.
2.Brigedi ya 205 -- iliongozwa na Brigedia.Herman Lupogo na baadae Brigedia.Muhidin Kimario.
3.Brigedi ya 206 -- iliongozwa na Brigedia.Silas Mayunga, baadae Brigedia.Roland Makunda.
4.Brigedi ya 207 -- iliongozwa na Brigedia.John Walden.
5.Brigedi ya 208 -- iliongozwa na Brigedia.Marco Mwita Marwa.
6.Brigedi ya Kagera -- iliongozwa na Brigedia.Ramadhani Haji Faki.
7.Brigedi ya Minziro -- iliongozwa na Brigedia.Ahmed Takadiri Kitete.

vita ilipiganwa kwa awamu mbili. awamu ya kwanza ilikuwa ni kuyaondoa majeshi ya Uganda toka ktk ardhi ya Tanzania. Operation hiyo iliitwa "operation chakaza" na iliongozwa na Brigedia.Tumainieli Kiwelu. awamu ya pili ni mapigano ndani ya ardhi ya Uganda na operation hiyo iliongozwa na Brigedia.David Musuguri.

mkuu wa majeshi CDF alikuwa ni Meaj Jenerali.Abdalah Twalipo, mnadhimu mkuu wa jeshi alikuwa Brigedia. Tumainieli Kiwelu, na Waziri wa Ulinzi alikuwa Rashid Mfaume Kawawa.
Kwa upande wa bara mpaka polisi na mgambo walishiriki vp kuhusu vikosi vya smz huko zanzibar ushiriki wao
 
Kwa upande wa bara mpaka polisi na mgambo walishiriki vp kuhusu vikosi vya smz huko zanzibar ushiriki wao

..Ni kweli kwamba vyombo vyote vya ulinzi na usalama vilichangia askari waliokwenda kupigana vita vya Kagera.

..Kwa hiyo polisi, magereza, mgambo, jkt, walikusanywa, wakapigwa msasa, na kupelekwa mstari wa mbele.

..Nina amini vikosi vya SMZ navyo vilichangia askari waliokwenda mstari wa mbele.

..Pia kila MKOA ulitakiwa kutoa VIJANA wa kujiunga na jeshi kwa ajili ya kumtoa Nduli Iddi Amin ktk ardhi yetu.

..Mashirika ya umma, na makampuni ya watu binafsi nayo yalitoa michango na huduma mbalimbali kusaidia majeshi yetu ktk mapambano dhidi ya adui aliyetuvamia.

..Kwa mfano, shirika la reli lilitoa mabehewa ya kusafirisha askari na vifaa. Pia yako makampuni ya mabasi ya watu binafsi ambayo yalisaidia kusafirisha askari.

..Wananchi walitoa mifugo, nafaka, na michango mbalimbali kwa ajili ya vita.

..Kwa ujumla, Watanzania tulikuwa na MUAMKO mkubwa wa kushinda vita ile.
 
..Ni kweli kwamba vyombo vyote vya ulinzi na usalama vilichangia askari waliokwenda kupigana vita vya Kagera.

..Kwa hiyo polisi, magereza, mgambo, jkt, walikusanywa, wakapigwa msasa, na kupelekwa mstari wa mbele.

..Nina amini vikosi vya SMZ navyo vilichangia askari waliokwenda mstari wa mbele.

..Pia kila MKOA ulitakiwa kutoa VIJANA wa kujiunga na jeshi kwa ajili ya kumtoa Nduli Iddi Amin ktk ardhi yetu.

..Mashirika ya umma, na makampuni ya watu binafsi nayo yalitoa michango na huduma mbalimbali kusaidia majeshi yetu ktk mapambano dhidi ya adui aliyetuvamia.

..Kwa mfano, shirika la reli lilitoa mabehewa ya kusafirisha askari na vifaa. Pia yako makampuni ya mabasi ya watu binafsi ambayo yalisaidia kusafirisha askari.

..Wananchi walitoa mifuko, nafaka, na michango mbalimbali kwa ajili ya vita.

..Kwa ujumla, Watanzania tulikuwa na MUAMKO mkubwa wa kushinda vita ile.
Na kwa kipindi hicho tulikuwa na jeshi la wanamaji tayari?
 
Ndio maana bongo wahitimu wa vyuo hawaajiriki kwa kucopy and kupaste hata kazi za masomo, yakitoka hapo, asilimia kubwa ni mazwazwa tu

kama kazi sio ya kwako, lazima umtabue mwadishi na kumtaja, sio unaiba halafu wakaimbiwa unatoa majibu yao ni matusi kwa kwenda mbele

Pia sema kama umeongezea utopolo wako ndani kazi ya mtu mwingine usiokuwa na ukweli wowote. Fiction
Hata huyo unayedai yake , amecopy bila kua acknowlegde lkn si kuna nukuu ya vitabu ana vinukuu.
Wivu tu. Ngoja tusome sie
 
Back
Top Bottom