Ukweli ni upi kuhusu chanzo cha vita ya Kagera?

stakehigh

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2019
Posts
39,365
Reaction score
39,579
Kutoka makala yenye episode ya arusha one radio, chanzo cha vita ni mwanajeshi wa uganda kufungwa tanzania, however katika makala za encyclopedia kuna taarifa kwamba, Nyerere alifadhili mapinduzi ya obote kurejea madarakni ambayo yalishindwa hivo amin akaamua kulipua kagera ikiwemo kiwanda cha kagera sugar

View: https://youtu.be/p_BWfsPgdSE?list=PLwboNetLZ6ALb0ybLBBq9Ex8_CtPh50vC

Kama ni taarifa ingine iweke
 
Who give a fly fuk about that during this period?
 
Kwa kifupi sana, Nyerere hakutaka kuona jumuia ya Afrika Mashariki ikisambaratika baada ya Idd Amin kumpindua Milton Obotte wakati akiwa kwenye mkutano wa Commonwealth kule Singapore.

Nyerere aliitoa hifadhi ya kisiasa kwa Obotte na wafuasi wake na kuwawezesha kuunda movement ya ukombozi wa Uganda lengo likiwa kumrudisha Obotte madarakani..

Waganda waliopata ufadhili wa Nyerere akiwemo Obotte mwenyewe ambaye binti yake Clare Obotte tulianza pamoja form one Mzizima 1975, Yoweri Kagutta Museveni alikuwa akiishi upanga akisoma mlimani na David Oyite Ojok na wenzake waliosoma pale Tumaini Secondary School.

Kitendo cha Nyerere kuwaunga mkono hawa wapigania uhuru na nia thabiti ya kumrudisha Obotte madarakani ndio kilichomfanya Idd Amin Daddah kuapa kuwafuata wapigania uhuru waliojificha Tanzania na ikiwezekana kutwangana kijeshi na Nyerere.

Maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Uganda kule Mutukula na Minziro ndiko walikokuwa wanajipenyeza kuingia Uganda na miaka ya 1972 tulishuhudia vita vya mpakani kabla Amin kuamua vita kamili mwaka 1978 na kuteka eneo la kaskazini la mto Kagera.
 
Kutoka makala yenye episode ya arusha one radio, chanzo cha vita ni mwanajeshi wa uganda kufungwa tanzania, however katika makala za encyclopedia kuna taarifa kwamba, Nyerere alifadhili mapinduzi ya obote kurejea madarakni ambayo yalishindwa hivo amin akaamua kulipua kagera ikiwemo kiwanda cha kagera sugar

View: https://youtu.be/p_BWfsPgdSE?list=PLwboNetLZ6ALb0ybLBBq9Ex8_CtPh50vC

Kama ni taarifa ingine iweke

Habari pekee inayosisimua taifa zima ni Samia kung'ang'ania kuongoza taifa lisilomtaka aliongoze.

Nguruwe mfugwaji kama wewe unahangaika kutafutiza vihabari visivyokuwa na umuhimu wowote kwa waTanzania wakati huu.

Samia amekwisha likoroga, ni lazima alinywe, hiyo ndiyo habari.
 
mkutano wa OAU kule Addis Abbaba Ethiopia.
Hii siyo kweli.
Nimesoma hayo yaliyofuata; yote hayana maelezo ya uzito uliotosheleza uwepo wa vita hiyo.

Idd Amin Dada alishadai sehemu ya Kenya; hadi Kisumu kuwa eneo la Uganda. Hilo lilimtisha sana Jomo, hadi kuomba msaada wa waingereza.

Alipogeukia Tanzania, hakutishia tu kuchukua sehemu ya mpakani, bali alitekereza kwa vitendo.

Of course, ni wazi kuwa Mwalimu Nyerere na Idd Amin Dada walikuwa hawapikiki chungu kimoja tokea mapinduzi yalipofanyika; lakini hiyo pekee haikuwa sababu ya vita kuwepo.
 
Hakuna sababu yoyoto ya msingi.Nyerere alitaka kumsaidia rafiki yake Milton Obote kurudi madarakani
 
Hii siyo kweli.
Kama si kweli kwa vyovyote utakuwa na moja au mbili ya sababu zilizomfanya Idd Amin kuivamia Tanzania.

Sikulazimishi kukubaliana nami lakini ungetoa sababu nyingine unayoamini kuwa ndiyo chanzo cha vita ile ungeutendea haki sana uzi huu na kukidhi kiu ya mtoa hoja kutaka kujua chanzo cha Amin kuivamia Tanzania.
 
Kutoka makala yenye episode ya arusha one radio, chanzo cha vita ni mwanajeshi wa uganda kufungwa tanzania, however katika makala za encyclopedia kuna taarifa kwamba, Nyerere alifadhili mapinduzi ya obote kurejea madarakni ambayo yalishindwa hivo amin akaamua kulipua kagera ikiwemo kiwanda cha kagera sugar

View: https://youtu.be/p_BWfsPgdSE?list=PLwboNetLZ6ALb0ybLBBq9Ex8_CtPh50vC

Kama ni taarifa ingine iweke

Chanzo cha vita ya Kagera ambacho hata hivyo, watawala hawakutaka kijulikane ni azma na nia ya Tz kumrejesha Obote Uganda aliyeishia kuwa kituko cha kukatisha tamaa.
 
Kama si kweli kwa vyovyote utakuwa na moja au mbili ya sababu zilizomfanya Idd Amin kuivamia Tanzania.

Sikulazimishi kukubaliana nami lakini ungetoa sababu nyingine unayoamini kuwa ndiyo chanzo cha vita ile ungeutendea haki sana uzi huu na kukidhi kiu ya mtoa hoja kutaka kujua chanzo cha Amin kuivamia Tanzania.
Usikimbilie "kwenye kulazimishana"; wakati siyo kweli kabisa kwamba Obote alipinduliwa akiwa kwenye mkutano wa OAU; hilo siyo kweli hata kidogo!

Hayo ya kwanini Idd Amin aliamua kuvamia eneo la mpakani wakati huo; hilo pia halina utata kwa kuwa hapakuwepo na maelewano kati ya nchi hizo mbili wakati huo; na kutokuwepo kwa maelewano, sababu mojawapo ni kuwa Obote alikuwa Dar; na serikali ya Tanzania haikuwahi kuyatambua mapinduzi ya Uganda. Sasa hilo nalo ni jambo gumu kulielewa?
 
Chanzo cha vita ya Kagera ambacho hata hivyo, watawala hawakutaka kijulikane ni azma na nia ya Tz kumrejesha Obote Uganda aliyeishia kuwa kituko cha kukatisha tamaa.
WEWE unamkumbuka Obote tu; lakini unasahau uwepo wa akina Lule na akina Binaisa!

Hali ya Uganda wakati huo ilikuwa ni tata sana.
 
Nawakumbuka wote. Umetaka kujua chanzo. Zaidi ya sisi kuwa tunamchokoza Amin ili kupata kisingizio cha kumchapa na kumpindua, hapakuwa na chanzo kingine. Maana, kama Amin angekuw akama ilivyodaiwa kuwa aliivamia Kagera, basi angeivamia Kenya aliyokuwa akiipa umeme kwanza.
 
Usikimbilie "kwenye kulazimishana"; wakati siyo kweli kabisa kwamba Obote alipinduliwa akiwa kwenye mkutano wa OAU; hilo siyo kweli hata kidogo!
Alipinduliwa na Idd Amin Daddah January 25, 1971 akiwa kwenye mkutano wa Commonwealth kule Singapore, nakiri kukosea kusema OAU lakini mengine yote yako sahihi.
 
Kwa kifupi sana, Nyerere hakutaka kuona jumuia ya Afrika Mashariki ikisambaratika baada ya Idd Amin kumpindua Milton Obotte wakati akiwa kwenye mkutano wa OAU kule Addis Abbaba Ethiopia.

Nyerere aliitoa hifadhi ya kisiasa kwa Obotte na wafuasi wake na kuwawezesha kuunda movement ya ukombozi wa Uganda lengo likiwa kumrudisha Obotte madarakani..

Waganda waliopata ufadhili wa Nyerere akiwemo Obotte mwenyewe ambaye binti yake Clare Obotte tulianza pamoja form one Mzizima 1975, Yoweri Kagutta Museveni alikuwa akiishi upanga akisoma mlimani na David Oyite Ojok na wenzake waliosoma pale Tumaini Secondary School.

Kitendo cha Nyerere kuwaunga mkono hawa wapigania uhuru na nia thabiti ya kumrudisha Obotte madarakani ndio kilichomfanya Idd Amin Daddah kuapa kuwafuata wapigania uhuru waliojificha Tanzania na ikiwezekana kutwangana kijeshi na Nyerere.

Maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Uganda kule Mutukula na Minziro ndiko walikokuwa wanajipenyeza kuingia Uganda na miaka ya 1972 tulishuhudia vita vya mpakani kabla Amin kuamua vita kamili mwaka 1978 na kuteka eneo la kaskazini la mto Kagera.
hio taarifa ya mwanajeshi kuvuka mpaka na kumwaga risasi zina ukwel?
 
Nawakumbuka wote. Umetaka kujua chanzo. Zaidi ya sisi kuwa tunamchokoza Amin ili kupata kisingizio cha kumchapa na kumpindua, hapakuwa na chanzo kingine. Maana, kama Amin angekuw akama ilivyodaiwa kuwa aliivamia Kagera, basi angeivamia Kenya aliyokuwa akiipa umeme kwanza.
Kenya alishatishia kuchukuwa eneo lote la mpakani toka Kaskazini hadi Kusini ikiwemo na Kisumu; lakini Kenyatta alikwishajihami kwa uwepo wa jeshi la Uingereza Kenya.

Hilo swala la sisi kumchokoza ili avamie mpakani tupate fursa ya kumpiga halileti mantiki yoyote.

Angekataa kuvamia je?

Pamoja na kwamba Tanzania haikutaka kushirikiana naye; lakini swala la kumchokoza, na kupanga kabisa kuwa atavamia mpaka ndipo tuingie vitani siyo sahihi.
 
Habari pekee inayosisimua taifa zima ni Samia kung'ang'ania kuongoza taifa lisilomtaka aliongoze.

Nguruwe mfugwaji kama wewe unahangaika kutafutiza vihabari visivyokuwa na umuhimu wowote kwa waTanzania wakati huu.

Samia amekwisha likoroga, ni lazima alinywe, hiyo ndiyo habari.
🤣 tuongezee bana mda wa kukaa madarakan acha uchoyo
 
Hii siyo kweli.
Nimesoma hayo yaliyofuata; yote hayana maelezo ya uzito uliotosheleza uwepo wa vita hiyo.

Idd Amin Dada alishadai sehemu ya Kenya; hadi Kisumu kuwa eneo la Uganda. Hilo lilimtisha sana Jomo, hadi kuomba msaada wa waingereza.

Alipogeukia Tanzania, hakutishia tu kuchukua sehemu ya mpakani, bali alitekereza kwa vitendo.

Of course, ni wazi kuwa Mwalimu Nyerere na Idd Amin Dada walikuwa hawapikiki chungu kimoja tokea mapinduzi yalipofanyika; lakini hiyo pekee haikuwa sababu ya vita kuwepo.
chanzo kikuu ni kipi?
 
Back
Top Bottom