RIWAYA: HISTORIA BATILI
MTUNZI & MWANDISHI: Jumaa Khatib Mdharuba(Jk)
EPISODE O18
★★★★★★★★★★★★★★★
Baada ya kufika maabara ile Hisham alikaa kwenye foleni ndogo aliyoikuta katika benchi lililokuwa karibu na mlango wa kuingia chumba cha vipimo..Mpaka alipofanikiwa kuingia katika chumba kile kidogo chenye meza kubwa na vifaa vya kuchukulia damu.. Akakutana na tabasamu zuri kutoka kwa daktari ambaye alionekana kumfahamu Hisham..
Karibu sana Mheshimiwa, naona leo umekuja kucheki afya Hisham moyo wake ulienda mbio sana sababu ya presha ya nini itakua hatma yake baada ya kupima..kitendo cha daktari kumuita Hisham mheshimiwa nacho kilimshtua sana..
Asante sana, kumbe unanifahamu? Hisham aliuliza kwa kuonyesha tabasamu, hakutaka mtu yeyote anayemfahamu ajue kuhusu afya yake..
Yaah..nakupata kaka Hisham, Manager wa Mambo Pub..ndo kiwanja changu cha kujidai kile baada ya uchovu wa hizi kazi Alifunguka Dokta yule akiwa na furaha..hakujua kuwa kwa Hisham tayari hilo ni tatizo..
Hisham aliangalia juu kama anayewaza jambo, kisha akarudisha mikono yake akiwa anajisachi mifukoni kama mtu aliyesahau kitu..
Samahani kidogo Dokta.. nakuja sasa hivi. Akatoka kwa kasi sana akaelekea moja kwa moja alipopack gari yake akazama ndani na kutokomea..
Akaelekea kwenye maabara ndogo iliyopo mitaa ya Mazimbu.. Jk Laboratory, akafika na kupokelewa vizuri na muhudumu mmoja wa kike ambaye hakuonesha dalili za kumfahamu, hapa hakukuta foleni, hivyo aliingia moja kwa moja maabara na kuonana na daktari ambaye baada ya kumueleza kuwa amekuja kupima HIV, daktari yule aliharakisha kuchukua damu ya Hisham kwa ajili ya vipimo..
Haikuchukua muda sana tangu Hisham aambiwe kusubiri hapo nje, akaitwa..
Daktari akamuangalia sana, kama anayetaka kusema kitu lakini anashindwa..
Hisham, una mke?
Yaah ninaye, mwaka wa saba sasa huu
Kwanini usije nae mkapima wote mkapata kuzitambua afya zenu kwa pamoja?
Wewe Dokta hebu acha siasa..mimi nimekuja kupima hapa unipe majibu nikafanye mambo mengine sikuja kufuata ushauri hapa.. Kama kawaida yake Hisham alishapanic..
★★★★★★★★★★★★★★★
Ni kumuua tu, unafikiri kuna kitu gani kingine? Mama Mdharuba alisema kwa kujiamini..
Khatib alianza kushangaa maneno ya mama yake, alihisi ameanza kuchanganyikiwa..
Mara zote nimekuwa nikikusikiliza na kukutii mama, lakini leo nakubishia kwakweli..hapo hauko sahihi..
Kwanini unasema hivyo mwanangu? Mama Mdharuba alirudi kuwa mpole tofauti na alivyotegemewa..
Mzee J4 si ndo yule aliyemponesha Kulwa siku ile wakati anaharisha, umesahau mama?!.. Sasa kesi yake unaipelekaje kwa Lesangwa? Hivi unavyomuona Mzee J4 ni mtu wa kumdhuru kirahisi namna hiyo? Mama katika hili hauko sahihi..fikiria upya.. Khatib aliongea maneno haya kwa hisia na kumfanya mama yake aanze kujiona ni kweli amekosea.. Ila kabla hajamruhusu kuongea akaendelea..
Halafuu..mama nilikwambia kuwa nisubiri nije tufanye mambo haya nikiwepo, lakini una haraka sana mama yangu..sasa angalia, unafikiri mi nitawezaje kujigawa?! Wewe unajua kuwa mimi nikirudi Canada siku hizi saba za mwanzo tangu nirudi natakiwa nifanye nini..wewe unajua..lakini nakushangaa sana unaongea na Sheikh Lesangwa tena, halafu unanambia bado siku tano..mimi nitajigawaje?? Khatib aliendelea kutupia lawama nzito kwa mama yake ambaye muda huu alishachoshwa na maneno ya mwanawe huyu wa kwanza na mwenye mafanikio makubwa!!
Mimi yote hayo nayafanya kwa ajili yako mwanangu, ni kwa ajili ya maisha yako na familia yako..sasa kama waniona mimi nakosea sawa..nitakuacha ufanye mwenyewe.. Mama mdharuba alikuwa amekasirika sana wakati huu, sura yake ilisadifu!! Khatib baada ya kuona hali hii aliamua kurudi chini na kumuomba mama yake msamaha na kuahidi kujitahidi kufanya yale aliyotakiwa kufanya kabla ya muda kuisha.. Ila aliendelea kumsisitiza mama yake kuwa jambo la Mzee J4 aliache tu..
**************
Baada ya pale, Khatib alielekea moja kwa moja kuonana na Noor.. Mtu aliyetambulika kama baba mdogo katika HISTORIA BATILI ya Khatib. Lengo la kuonana na Noor ni kupeana mustakabali wa mambo mengi yanayohusu mwenendo wao kibiashara na kiusalama..
Wakaamua wakutane Hotel kubwa ambayo watapata chakula wakati wakiendelea na mazungumzo yao..
In short kila kitu kiko sawa, kama nilivyokwambia kipindi kile kuwa Sauda lazima afe kwa sababu aliwekwa pale na Nuro, na yule Nuro ni wa kumuangali sana ndugu yangu..sijui tuko pamoja mpka hapo? Noor alikuwa akifunguka katika maongezi yale nyeti..
Yaah nakupata sana.. Na nilitekeleza hilo kama ulivyonielekeza..Sauda amekufa tayari, wala sikuchelewesha Alijibu Khatib ambaye alionekana kutekeleza maagizo kutoka kwa Noor kuhusu usalama wake..
Ahmed ndiye anayefuata katika hili, yeye anatakiwa kufa kabla hajaonana tena na Detective Rukia.. Noor aliongeza na kumfanya Khatib ashangae kidogo..ila kabla hajasema chochote Noor aliendelea..
Alikufuatilia ulipokuwa Canada..sasa kama amepata ujasiri huo unadhani anastahili kubaki?
Kwahyo baba, unataka kunambia Ahmed nilikua nae safarini?
Yaah..wamemzuia pale uwanja wa ndege wakimshutumu kukiuka baadhi ya vifungu vya kiusalama..lakini hiyo inatoa nafasi nzuri kwetu ya kumpoteza.. Noor alikazia point na kumfanya Khatib azidi kubaki mdomo wazi..
Na hili jambo la Mzee J4 niachieni mimi, hizo njia zenu za tradition haziwezi kumuondoa Mzee J4, mimi nitamuua ndani ya saa 48 kutoka sasa.. Ndivyo alivyomalizia Noor na kuweka nukta kubwa..
★★★★★★★★★★★★★★★
Tukutane Episode 019
mdharuba@gmail.com
+255718274130