RIWAYA: HISTORIA BATILI
MTUNZI NA MWANDISHI: Jumaa Khatib (Jk)
0718/0719/0756-274130
EPISODE O17
1⃣7⃣
★★★★★★★★★★★★★★★★
Dr Idd Fauz alishangazwa sana na sms ile, iliyokua imejieleza moja kwa moja kuwa Hamida alikua na hisia za mapenzi juu yake.. Alipigwa na butwaa..akikumbuka sababu ya yeye kufahamiana na Hamida, ni kweli alitenda wema, lakini sio wa kulipwa mapenzi na Hamida..isitoshe tayari alikua na mke na watoto wawili, ni jambo la hatari sana kujiingiza kwenye mapenzi na mwanamke mwingine ilhali alikua na mkewe aliyekua akimpenda sana na siku zote aliapa kutomsaliti..
Alizidi kuona mtihani mgumu juu yake, hakujua aijibu vipi sms ile licha ya kuwa zilishapita dakika tano sasa tangu ipokelewe kwenye simu yake..!! Akaamua kutoijibu, akakaa kimya. Na hata pale Hamida alipopiga simu dakika kumi baadae kwa sababu hajajibiwa meseji yake, aliona asiipokee.. Jambo la yeye kutakiwa kimapenzi lilishakua gumu kwake, alilifikiria saaana..hakupata majibu. Alikua akimfikiria sana mkewe Mariana ambaye alikua akiishi nae kama ndugu yake, walipendana, licha ya tatizo la akili ambalo alilipata miaka miwili iliyopita ambalo lilisababishwa na ajali ya gari ambayo ilimkuta Dr Idd wakati akiwa safarini kutoka Hospitali ya Bugando Mwanza ambapo ilifanyika semina ya siku tano ya madaktari Tanzania, akirudi nyumbani kwake Tanga. Dr Idd baada ya ajali ile damu yake ilivuja kidogo na kuufikia ubongo hivyo kumsababishia tatizo la akili ambalo lilidumu kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu..Lakini kipindi chote hiki, Mariana aliweza kuvumilia kukaa na 'chizi' huku akizidi kufanya maombi na matibabu mbalimbali ili mumewe arudi katika hali ya kawaida..
Dr Idd aliona malipo ya uvumilivu huu hayakupaswa kuwa usaliti kwa mkewe huyu..
Ingawa siku hiyo yote alikosa raha, alikosa kuwa na amani kwani alimuheshimu sana Hamida, hakutegemea kusikia kitu hiki kutoka kwake, ila baadae aliamua kufanya maamuzi ya kiume, akaamua kujibu sms ile kwa kuandika "Samahani sana, nina mke na watoto wawili, nampenda sana mke wangu, siwezi kumsaliti, plz, naomba tuendelee kuheshimiana..SIHITAJI MAPENZI NA WEWE" Kisha akaituma sms ile kwa Hamida..
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Hisham aliamua kuanza kufuatilia kwa makini amjue haswa mtumaji wa sms ile ni nani? Mwanzoni mawazo yake yalikua yakimtuma kuwa yule atakuwa boss wake, Khatib, lakini kadri muda ulivyoenda ndivyo alivyozidi kupingana na wazo hili..Wazo lililokuwa na nguvu kwa sasa ni Manager wa pale SauKhat Mr. Nira, ingawa alimfahamu Nira lakini sio saana kama vile alivyofahamiana na kuzoeana na Haroun..
Akafika SauKhat Investment Inc.., Fred hakuwa anamtambua Hisham, licha ya umaarufu alionao, hii ilitokana na Fred kuwa bize sana na mambo yake, na hakuwa na kawaida ya kwenda kiwanja chochote cha starehe hapa mjini..
Karibu sana boss..karibu sana..Naitwa Fred naweza kukusaidia.. Ndivyo Fred alivyomlaki Hisham..
Asante sana kaka, Vipi Manager nimemkuta? Hisham hakutaka kupoteza muda..
Hapana, Manager ni muda mrefu sasa anaumwa, hayupo kazini, lakini mimi ndio nipo nafasi yake, naweza kukusaidia..
Duuh..unataka kunambia Nira anaumwa?? Hisham alihamaki kitendo kilichomfanya Fred ashangae..Hisham moyo wake ulianza kwenda mbio kama saa iliyolegea mshale.. Maneno ya sms yakaanza kujirudia kichwani mwake.. Hisham alikuja hapa lengo lake lilikua kuonana na Nira, aongee nae kuhusu gari ambalo angedai anataka anunue, lakini mwisho kabisa ni kuchukua namba ya simu ya Nira ili afanye mawasiliano zaidi, lengo lake likiwa ni kuangalia kama namba itafanana na ile aliyoichukua kwa Regina..
Ndio boss..kumbe unamfaham..ndio huyo boss Nira anaumwa..
Daah..umenistua sana..kunambia Nira anaumwa..maana ni leo asubuhi nimempigia simu kwa namba yake ya Airtel sikumpata..ndio nikaona nije nimcheki hapa..bahati mbaya hata nyumbani kwake sipajui.. Hisham alizuga ili atakapoomba namba asije akapewa ya Airtel, kwani namba aliyosave kwenye simu yake ilikua Tigo..
Anatumia tigo pia, ni 0653686008.. Fred hakuona kama kuna haja ya kupoteza muda..akataja moja kwa moja namba ile ambayo ndiyo haswa iliyomleta Hisham pale..
Hisham akaisave tena namba ile, kisha akamuaga Fred, moja kwa moja akaelekea kwenye gari yake, akafungua mlango na kuzama ndani.. Hapa akapata muda muafaka sasa wa kuzifananisha namba mbili zile..
Laaahaulaaa..akakuta namba zinafanana..akaishiwa nguvu na kuegemea usukani wa gari yake..
Mawazo mengi sana yalianza kumtesa Hisham.. Akaanza kumfikiria Nira, kuwa ndiye alikua akimchukulia mkewe, alijisikia vibaya sana..Mawazo pia juu ya damu yake kutokubalika hospitali..akahisi huenda tayari ameshaathirika, akawaza pia alipotoka nae Regina miaka 7 iliyopita, alivyomgharamia..akaanza kujiona mjinga..
Ngoja nikapime kwanza, nikigundua nimeathirika atanikoma yule Mbwa..na huyu Nira pia nitamuua kwa mkono wangu mwenyewe hata kama anakaribia kufa..sheeenziiii... Alijisemea moyoni Hisham na kuondoa gari kwa kasi maeneo yale akielekea Maabara maarufu iliyopo mjini..
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Nilishaongea na Sheikh Lesangwa, ameweka mambo yote sawa, na kwa sasa sababu umekuja mwanangu ndio muda wa kuhakikisha tunafanikiwa katika yale tuliyoyapanga.. Khatib alipokea maelekezo haya kutoka nyumbani kwa mama yake, Mbezi jijini Dar.. Mama Mdharuba alikua akimwambia anachotakiwa kufanya baada ya kuwa amefika nyumbani..
Na sheikh Lesangwa ametoa maelekezo kuwa unatakiwa kuonana na Hamida ndani ya siku 7 tangu afanye hizi shughuli zake.. Na leo ni siku ya pili..kwahyo una siku tano tu mwanangu.. Mama Mdharuba aliongea haya huku Khatib akiwa kimya sana akimsikiliza kwa makin mama yake huyu ambaye mara zote alikua akimpa maagizo tu na sio kumuuliza maoni yake..
Halafu pia yule rafiki yako Hisham aliniambia kuwa Mzee J4 alimwambia kuwa alitaka uonane nae ukirudi..na yeye nimemwambia Lesangwa, amesema yule mzee atatusumbua sana..kwahiyo kitu cha kufanya hapa ni kimoja tu..ili tuaendelee kuishi kwa amani..
Kitu gani hicho mama? Khatib alivunja ukimya, akiwa na hamu ya kujua ni kitu gani kinaweza kumzima mzee J4 ambaye alishaonesha dalili za kuwa si mtu mzuri..
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Let's end up here today..
Watch out Episode 018
Whatsapp⬇
+255718274130