Hili la kuzuiliwa kwa maiti sababu ya bili kubwa mzizi wake ni huu, Wizara ya afya rudisheni utaratibu wa zamani

Feb 18, 2019
50
532
Haka ni katatizo kadogo sana ambako wizara inajua mzizi wake ni nini, kama hawajui basi nawajuza.

Kwanza hili tatizo huwezi kulisikia kwenye hospitali zifuatazo, kama lipo basi ni kwa udogo sana: Hospitali za Wilaya, Mikoa, Vituo vya Afya, Hospitali binafsi.

Hili tatizo utalikuta hospitali zifuatazo: Hospitali za Kanda[KCMC,Bugando,Mbeya ZRRH,Benjamin Mkapa(UDOM)] na Hospitali za Taifa[Muhimbili na Mloganzila]. Pia baadhi ya hospitali binafsi za rufaa zenye ubia na serikali.

Mzizi wa tatizo ni nini?: Utaratibu wa hizi hospitali za kanda na taifa ni kwamba huduma kwanza hata kama hauna pesa basi utalipa baadaye lakini standard ya wizara na nchi kwenye hizi hospitali ni kwamba mgonjwa anapewa priority ya matibabu kwanza kabla ya yote, na ndio maana kila kitu kinapatikana humohumo kuanzia vitendea kazi mpaka dawa. Pia aina ya vipimo na wataalamu kwenye hizi hospitali za kanda na taifa ni tofauti na kule level cha chini. Vipimo kama CT Scan, MRI nk ni gharama sana hivyo mwisho wa siku bill ya mgonjwa lazima itakuwa kubwa tuu.

Hospitali za level ya chini utaratibu wake uko tofauti kidogo, ukifika na mgonjwa wako basi utapewa list ya vitu vya kwenda kuleta, kuanzia vitendea kazi mpaka dawa, ni hospitali chache sana zenye utaratibu kama hospitali za kanda na taifa. Na huu ndio utaratibu waliozoea watanzania wengi. Hivyo wakipelekwa kwenye hizo hospitali kubwakubwa wanakutana na utaratibu mpya ambao hawajauzoea.

Kingine vipimo vya kwenye hizi hospitali za kanda na taifa ni gharama sana, na mara nyingi wagonjwa wanapewa rufaa kwa sababu ya kwenda kufanyiwa hivyo vipimo. Mtanzania ambaye amezoea kwenda na 50,000/= hospitali na anapata matibabu yake na chenji inabaki, leo hii akienda hospitali kubwa akaambiwa CT Scan moja tuu ni 150,000/=(mfano) lazima ashangae na hatokuelewa.

Dawa ya hili tatizo ni nini: Serikali irudishe utaratibu wa zamani kwa hizi hospitali, ndugu wapewe list ya vifaa na dawa za kununua kisha wavipeleke, wasipopeleka basi ni juu yao. Pia mgonjwa asifanyiwe vipimo mpaka pale ndugu wamelipa. Huu utaratibu umetumika toka enzi ana enzi na hakukuwa na kelele za maiti kuzuiliwa sababu ya bill. Pia tukumbuke watumishi wa afya wapo pale kuhudumia wagonjwa na si kuanza kukimbizana na wadaiwa sugu wa ndugu wa marehemu ambao wengine wakishazika tuu basi kulipa ndo majaaliwa. Bila kurudisha huu utaratibu wa zamani kuna siku watumishi wa afya wataingia matatizoni ama watatumbuliwa kwa kosa ambalo sio lao bali ni la watunga sera.

NB: Watanzania wengi tunajijua hulka zetu, tukipewa maiti tukazike bila kulipa deni basi ujue imekula kwa hospitali husika, kurudi kwetu kulipa ni majaaliwa ama kwa mbinde sana.
 
utaratibu ni mzuri tu ila serikali inatakiwa kubeba bili za watu wote waliofariki wakiwa wanapata matibabu hospitali. nadhani hili linawezekana, mwenda zake aliwahi kusema hii nchi ni tajiri sana.
 
Bima ya afya kwa kila raia ndio suluhisho...
Ilani ya chama itekelezwe.
Na hii ndiyo dawa pekee kwa sasa. Ni wakati sasa serikali ya ccm kutekeleza sera ya bima ya afya kwa watanzania wote.

Na hakuna asiye fahamu ya kwamba mwanzilishi wa hili wazo ni Mh. Tundu Lissu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka wa jana 2020, kabla ya ccm kulibeba kichwa kichwa!!

Ni wakati wao sasa kulitekeleza.
 
utaratibu ni mzuri tu ila serikali inatakiwa kubeba bili za watu wote waliofariki wakiwa wanapata matibabu hospitali. nadhani hili linawezekana, mwenda zake aliwahi kusema hii nchi ni tajiri sana.

Ndiyo sera ilivyo kwa sasa, wizara husika inasema wale ambao hawana uwezo wawe exempted wao watacover hizo gharama, na raia wameshajua kwa hiyo wakiona mgonjwa wao ni wa kufa tuu hawajigusi, na akifa mkazuia maiti wanampandia hewani waziri.

Upande wa pili wa shilingi ni kwamba wizara hizo pesa haizitoi, na hospitali zilishaambiwa zijiendeshe zenyewe kibiashara, hivyo mwisho wa siku hospitali inajikuta mapato na matumizi hayabalance, matumizi yanakuwa makubwa kuliko matumizi.
 
Hospital ndogo ndogo matatizo hayo hayapo maana wagonjwa wanaohitaji vipimo vikubwa wapo rufaani. Suluhu ya ili tatizo ni kuwekeza kwenye afya kuanzia dawa, vifaa tiba, wataalam bila kusahau bima bima bima bima
 
Dah....hivi kwanini usitumike utaratibu Kama wa mafundi wengine? Yaani unalipa baada ya mgonjwa kupona....akifa imekula kwa hospital 🤣🤣🤣🤣
 
Haka ni katatizo kadogo sana ambako wizara inajua mzizi wake ni nini, kama hawajui basi nawajuza.

Kwanza hili tatizo huwezi kulisikia kwenye hospitali zifuatazo, kama lipo basi ni kwa udogo sana: Hospitali za Wilaya, Mikoa, Vituo vya Afya, Hospitali binafsi.

Hili tatizo utalikuta hospitali zifuatazo: Hospitali za Kanda[KCMC,Bugando,Mbeya ZRRH,Benjamin Mkapa(UDOM)] na Hospitali za Taifa[Muhimbili na Mloganzila]. Pia baadhi ya hospitali binafsi za rufaa zenye ubia na serikali.

Mzizi wa tatizo ni nini?: Utaratibu wa hizi hospitali za kanda na taifa ni kwamba huduma kwanza hata kama hauna pesa basi utalipa baadaye lakini standard ya wizara na nchi kwenye hizi hospitali ni kwamba mgonjwa anapewa priority ya matibabu kwanza kabla ya yote, na ndio maana kila kitu kinapatikana humohumo kuanzia vitendea kazi mpaka dawa. Pia aina ya vipimo na wataalamu kwenye hizi hospitali za kanda na taifa ni tofauti na kule level cha chini. Vipimo kama CT Scan, MRI nk ni gharama sana hivyo mwisho wa siku bill ya mgonjwa lazima itakuwa kubwa tuu.

Hospitali za level ya chini utaratibu wake uko tofauti kidogo, ukifika na mgonjwa wako basi utapewa list ya vitu vya kwenda kuleta, kuanzia vitendea kazi mpaka dawa, ni hospitali chache sana zenye utaratibu kama hospitali za kanda na taifa. Na huu ndio utaratibu waliozoea watanzania wengi. Hivyo wakipelekwa kwenye hizo hospitali kubwakubwa wanakutana na utaratibu mpya ambao hawajauzoea.

Kingine vipimo vya kwenye hizi hospitali za kanda na taifa ni gharama sana, na mara nyingi wagonjwa wanapewa rufaa kwa sababu ya kwenda kufanyiwa hivyo vipimo. Mtanzania ambaye amezoea kwenda na 50,000/= hospitali na anapata matibabu yake na chenji inabaki, leo hii akienda hospitali kubwa akaambiwa CT Scan moja tuu ni 150,000/=(mfano) lazima ashangae na hatokuelewa.

Dawa ya hili tatizo ni nini: Serikali irudishe utaratibu wa zamani kwa hizi hospitali, ndugu wapewe list ya vifaa na dawa za kununua kisha wavipeleke, wasipopeleka basi ni juu yao. Pia mgonjwa asifanyiwe vipimo mpaka pale ndugu wamelipa. Huu utaratibu umetumika toka enzi ana enzi na hakukuwa na kelele za maiti kuzuiliwa sababu ya bill. Pia tukumbuke watumishi wa afya wapo pale kuhudumia wagonjwa na si kuanza kukimbizana na wadaiwa sugu wa ndugu wa marehemu ambao wengine wakishazika tuu basi kulipa ndo majaaliwa. Bila kurudisha huu utaratibu wa zamani kuna siku watumishi wa afya wataingia matatizoni ama watatumbuliwa kwa kosa ambalo sio lao bali ni la watunga sera.

NB: Watanzania wengi tunajijua hulka zetu, tukipewa maiti tukazike bila kulipa deni basi ujue imekula kwa hospitali husika, kurudi kwetu kulipa ni majaaliwa ama kwa mbinde sana.
Itafaa kwa baadhi maana Wengine unakuta ni ajali ...ndugu hawajulikani mpaka waje waonekane ni siku ya tatu au ya nne sasa apo si majeruhi watakufa..
 
Back
Top Bottom