NHIF msicheke na nyani mtavuna mabua

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
862
1,097
Ni ukweli usiopingika kwamba hizi private hospitals zinaiba sana kupitia bima za afya za wananchi...na pale mfumo wowote ukibuniwa ukaonekana kuwabana vita inakuwa kubwa sana.

Ukweli ni kwamba hospitali nyingi za binafsi survival yao inategemea NHIF. Zipo njia mbalimbali zinazotumiwa na hospitali hizi kuiba au kutengeneza biashara hivyo kuathiri maana ya bima;

1. Kutoa vipimo vingi makusudi kwa mgonjwa na kwa bei ya juu..ili mradi mtu NHIF basi kama ana homa atapimwa kifua,Uti, nk na lazima akutwe na UTI!!!

2. Mgonjwa akija na kadi ya NHIF gharama za matibabu ni tofauti na yule anayelipa cash...na hii nazungumzia out patient yaani mgonjwa wa nje.

NHIF iangalie pia wenzao wanafanyaje ili kuzuia matumizi mabaya na wizi kwa watoa huduma.

Wizara pia iletewe mapendekezo ya bei hasa kwenye upimaji na huduma mbalimbali, haiwezekani kufanya dialysis kwenye kituo kimoja itofautiane kwa zaidi ya asillmia 100.
 
Hasa hapo umeandika nini? Unataka kusema kuwa kwa kupunguza gharama watoa huduma wataiba kama kweli walikuwa ni majizi? Hapa umeharisha. Serikalini mnakaa mnakula kodi za walala hoi, then unakuja unaandika upupuu. Hospitali za serikali mishahara inatoka hazina ambako mnatumia kodi za walala hoi. Private wanajitegemea, na hawapati ruzuku kutoka serikalini. Hapo hapo serikali inakuambia eti kwa nini unalipa mshahara mdogo. Kama mmeamua kuua sekta binafsi, semeni, siyo kuja kuhara hapa.
 
Sekta binafsi ya wizi hata ikifa hakuna shida yoyote... mfumo wa bima unasaidia wote wenye vipato na wasio na vipato ... mnapofanya wizi wenu mnaharibu uwezo wa bima kusaidia watu wengi zaidi.... kama unaona wewe upo sawa weka hiyo taasisi yako hapa tuwavue nguo. Mmezoea kula fedha za NHIF ambazo watumishi wanalazimika kukatwa.... mnaweka gharama za juu inafika mahala mtu ana bima lakini bado anatakiwa kutoa cash
 
Back
Top Bottom