Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Mimi 2017 sitaisahau natoka Gairo - Dar kufika Moro ukiwa unaiacha morogoro mjini kuna njia imenyooka sana aisee nikaanza ligi lori mimi na IST mimi mdogo wangu, shemeji yangu na bi mkubwa aisee lori la mafuta BIL aisee niliiga kulifata nyuma aisee jamaa aliwahi kurudi kulia baada ya ku overtake aisee ile siku sitaisahau jamaa aliekua anakuja kwa mbele yangu na fuso hakupunguza mwendo lori nalo liovertake halikupunguza mwendo unakanyaga accelerator hadi chini gari ipo pale pale sijui ilikuaje lakini niliwahi kurudi kushoto nikalichomekea hilo lori nililokua nalipita baada ya jambo lile ilibidi nipaki pembeni nikojoe niliapa sitaanzisha ligi tena...barabarani wala kumfata mtu nyuma akihama na wewe unahama ni hatari sana
Achana kabisa na tabia ya mtu akichomoka nawewe unachomoka, hiyo itakuuwa haraka sana mkuu
 
Mwenye mark x alikuwa muoga maana hapo akuna chuma ya kufata the x alaf mkuu ww ulikuwana gari gani ujasema ili nione kama kweli ligi ilikuwa na vyuma
Wakuu, nimezoea sana kutembea safari ndefu haswa Dar-Kahama-Geita na Dar-Mwanza, mara chache Dar-Bukoba.
Mara nyingi napenda kusafiri jioni au asubuhi sana.

Hizo route nilizozitaja hapo juu hazina Magari madogo mengi usiku, zaidi ya malori na mafuso. So huwa hatujui mambo ya ligi kabisa.

Kuna hii route ya Arusha-Dar na ligi huwa inaanzia pale Njia panda ya Himo, wakuu kuna watu wanapenda kushindana sana, kwenye barabara.

Juzi kati hapa tumetoka Arusha kwenda Dar tulivyofika Pale Njia Panda ya Himo, kulikuwa kuna gari kama tatu ndogo, Mark x nyeupe, Murano moja nyeusi na Alphad ya Silver, plan niliyokuwa nayo nikupoteza muda pale Njia Panda, at least usumbufu upungue barabarani kumbe zile gari zilikuwa zinatafuta abiria wa Dar, mimi kwenye gari ninayoendesha tulikuwa watatu. Sikuwa na wazo la kuchukua abiria.

Ilivyofika saa kumi na mbili kama na nusu hivi yule jamaa wa Alphad akang'oa, baada ya kama dakika kumi, Mark X akang'oa.
Hapo nimepaki upande wa pili wa barabara.

Ukapita tena muda kidogo Murano akang'oa...Tukamaliza mambo yetu tukaanza kuondoka, nilijua nikipiga mashine vizuri nitaenda kuwatoa kabla hata hawajafika Same!!
Tumeanza kutembea sio kwa speed kali hiyo jioni jioni ya saa moja bado watu ni wengi barabarani na mibasi + magari makubwa mengi yakitoka Dar kuja Moshi, Arusha.

Haikuchukua dakika nyingi saana kufika Mwanga, nikaiona ile Murano ndio inaondoka, nikajua labda alikuwa anaongezea abiria, nikawa nimempita mbele kabla ya Kisaranga nikaipita na ile Mark x, Alphad sikuiona. Giza linazidi kuongezeka naona na barabara inapungua jam.

Tumepita Lembeni kwenye Kivuko cha treni jamaa wa Mark X akaovertake kwa speed kali kuianza Tambarare flan hivi kuelekea Same, hapo ndio ikawa shughuli hakuniacha mbali sana, kabla ya sehemu inaitwa mgagao Murano akaniovertake akaenda akaovertake na mark x..

Baada ya Murano kunipita nikagundua Mark X kaongeza speed zaidi kwasababu alianza kuniacha kwa mbali kidogo.

Nikagundua hawa watu kama vile wanafanya ligi hapo road, nikaamua na mimi kujihusisha nao, ule mtiti haukuwa wa kawaida Tukaanza kutembea sasa pita nikupite ikaanza, jamaa wa Mark X tulikuwa tunamuacha sana...

Mpinzani wangu mkubwa alikuwa jamaa wa Murano, hadi tunafika Korogwe, kwenye kona yakuelekea Old Korogwe, kuna beria, tukamkuta jamaa wa Alphad pale na gari nyingine ndogo mbili, zote zinaenda Dar, ebwana eeh kama ni ligi ndio ilikuwa kama vile inaanza piga nikupige,

Jamaa walikuwa wanatoa changamoto sana, hata kusinzia huwezi muda wote unawaza kumtangulia aliyeko mbele yako na kutokukubali aliyeko nyuma yako akupite! Huu mfumo ulifanya tukafika Dar mapema sana! Huu utaratibu wa Ligi kwenye hii barabara sijui kama ni wa kila siku, Kuna mashindano sana.

Ni barabara yenye ligi tena matata sana.
Kuna MwanaJf anayependa ligi barabarani, share na sisi.
 
Mkuu naona umeongelea wrx kuna kitu inaitwa wild ni s.t.i iliwah mchapa wrx adi mwenye w.r.x akapunguza mwendo maana ulikuwa ni mwendo wa kuguza bati sahani zinasoma
Ukiwa na Wrx sti mpk unaweza kupizi kwa utamu wa ligi za barabarani.
 
Nimecheka sana kunavideo ilisambaa ya hapa hapa bongo jamaa ana crown athlete alipigwa na golf akiwa 180 af wanaongea jamaa anasema daaaah kunawanaume[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Inaonekana mkuu ukiona hizo 220km/h sijui 240km/h zinakupagawisha balaa,ukikutana na ki golf-gti polo kana 300km/h kuna uwezekano ukaogopa kwenda nako ligi kisa umeona dashboard yake kana speed 300.
 
Back
Top Bottom