Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Mwezi uliopita kuna noah iliingia nyuma ya trela la trekta ambalo halikuwa na taa wala reflector maeneo ya vijiji flani kabla ya Kabuku! Ilikuwa ligi hivyo hivyo, usiku ni mbaya sana kukimbia speed kubwa
Unakimbia kwa tahadhari.
 
Safi, kuna mtu alijiunga yeye tulikutana kwenye junction ya segera akitokea Tanga, Mercedes yake ilikuwa inakimbia sana! aliniovertake pale Michungwani, nilifanikiwa kwenda kumwona tena kwenye ile Beria ya Mkata. Itakuwa ndio wewe bila shaka
Naaam ni Mimi mkuu[emoji134]
 
Nakumbuka nilifanya ligi moja Matata na nisoyemjua barabarani siku niliyotoka kupiga kura, mwaka 2015....

Barabara iliyohusika ni Ali Hassan Mwinyi kuanzia hapa mataa ya Serena hadi Bagamoyo Road maeneo ya Tegeta.

Mida ilikuwasaa kumi jioni.

Chanzo cha ligi, alinichomekea kiboya bin kibabe halafu akanioneshea like, nshakuchomekea utanifanya nini sasa.... mmaamaaeee nilimkanyagia mafuta nahisi alienda kumeza cofta kwa vumbi nililomuachia. Shida yangu niko mbishi sana...

Siku husika ilikuwa jumapili watu sio wengi barabarani na siku ya uchaguzi hivo barabara ilikuwa nyeupeee.

Gari alilotumia mleta ligi mwenzangu kama sijasahau ilikuwa Altezza maana ilikuwa hizi gari za chini. Mimi nilikuwa na Grand Car (yaani gari ya juu halafu iko branded grand uchomaji wake wa mafuta uko sawia na V8 hukoo).

Siku hizi nimekua kiasi nimepunguza ukorofi na ubishi, ligi za barabarani almost nimeziacha.

Ligi niliyobakia nayo ni ya Mahaba na Mziki tuu. Mtu akiwa tayari tufanye ligi ya kucheza mziki kuanzia saa nne usiku hadi jogoo la saa kumi alfajiri linawika bila kupumzika.....

Kasinde Platinum Matata.
We mmama wewe, una mbwebwe sana
 
Gari yangu ya kwanza kabisa ya kichovu toyota caldina, hapo natoka Moshi kuja dar na sina uzoefu sana na route za mbali, jamaa wa vits naye akaamua eti kunianzishia ligi, mimi niko 110 kph ananipita speed then mbele anaenda anapaki, nikipita tu huyu tena. Ama kweli ukiwa mchovu hata wachovu watataka ligi na wewe. Sasa hivi hata BMW akileta ligi na mimi ajipange kweli kweli, japo sita sahau kamwe dharau nilizoonyeshwa na vits kipindi nina gari la kichovu
[emoji23][emoji23]aiseee nimecheka sana
 
Vijana wadogo kama Wewe hamfai kuendesha magari, usipende kushindana endesha kwa kadri unavyoweza na uzoefu wako kwahiyo barabara
Wakuu, nimezoea sana kutembea safari ndefu haswa Dar-Kahama-Geita na Dar-Mwanza, mara chache Dar-Bukoba.
Mara nyingi napenda kusafiri jioni au asubuhi sana.

Hizo route nilizozitaja hapo juu hazina Magari madogo mengi usiku, zaidi ya malori na mafuso. So huwa hatujui mambo ya ligi kabisa.

Kuna hii route ya Arusha-Dar na ligi huwa inaanzia pale Njia panda ya Himo, wakuu kuna watu wanapenda kushindana sana, kwenye barabara.

Juzi kati hapa tumetoka Arusha kwenda Dar tulivyofika Pale Njia Panda ya Himo, kulikuwa kuna gari kama tatu ndogo, Mark x nyeupe, Murano moja nyeusi na Alphad ya Silver, plan niliyokuwa nayo nikupoteza muda pale Njia Panda, at least usumbufu upungue barabarani kumbe zile gari zilikuwa zinatafuta abiria wa Dar, mimi kwenye gari ninayoendesha tulikuwa watatu. Sikuwa na wazo la kuchukua abiria.

Ilivyofika saa kumi na mbili kama na nusu hivi yule jamaa wa Alphad akang'oa, baada ya kama dakika kumi, Mark X akang'oa.
Hapo nimepaki upande wa pili wa barabara.

Ukapita tena muda kidogo Murano akang'oa...Tukamaliza mambo yetu tukaanza kuondoka, nilijua nikipiga mashine vizuri nitaenda kuwatoa kabla hata hawajafika Same!!
Tumeanza kutembea sio kwa speed kali hiyo jioni jioni ya saa moja bado watu ni wengi barabarani na mibasi + magari makubwa mengi yakitoka Dar kuja Moshi, Arusha.

Haikuchukua dakika nyingi saana kufika Mwanga, nikaiona ile Murano ndio inaondoka, nikajua labda alikuwa anaongezea abiria, nikawa nimempita mbele kabla ya Kisaranga nikaipita na ile Mark x, Alphad sikuiona. Giza linazidi kuongezeka naona na barabara inapungua jam.

Tumepita Lembeni kwenye Kivuko cha treni jamaa wa Mark X akaovertake kwa speed kali kuianza Tambarare flan hivi kuelekea Same, hapo ndio ikawa shughuli hakuniacha mbali sana, kabla ya sehemu inaitwa mgagao Murano akaniovertake akaenda akaovertake na mark x..

Baada ya Murano kunipita nikagundua Mark X kaongeza speed zaidi kwasababu alianza kuniacha kwa mbali kidogo.

Nikagundua hawa watu kama vile wanafanya ligi hapo road, nikaamua na mimi kujihusisha nao, ule mtiti haukuwa wa kawaida Tukaanza kutembea sasa pita nikupite ikaanza, jamaa wa Mark X tulikuwa tunamuacha sana...

Mpinzani wangu mkubwa alikuwa jamaa wa Murano, hadi tunafika Korogwe, kwenye kona yakuelekea Old Korogwe, kuna beria, tukamkuta jamaa wa Alphad pale na gari nyingine ndogo mbili, zote zinaenda Dar, ebwana eeh kama ni ligi ndio ilikuwa kama vile inaanza piga nikupige,

Jamaa walikuwa wanatoa changamoto sana, hata kusinzia huwezi muda wote unawaza kumtangulia aliyeko mbele yako na kutokukubali aliyeko nyuma yako akupite! Huu mfumo ulifanya tukafika Dar mapema sana! Huu utaratibu wa Ligi kwenye hii barabara sijui kama ni wa kila siku, Kuna mashindano sana.

Ni barabara yenye ligi tena matata sana.
Kuna MwanaJf anayependa ligi barabarani, share na sisi.
 
Hiyo scania ya Sauli weka mbali na watoto imekaa vizuri hata ikipita kwenye matuta inaunafuu mkubwa kuliko basis lolote kwasasa
licha ya changamoto za barabarani, kwa upande wa ligi za mabasi ya abiria nasikia kwa sasa anayesumbua route ya dar - mwanza ni tungis express na anayesumbua route ya dar - mbeya ni sauli express. imefika kipindi mpaka watu wanabet kuhusu haya mabasi.

View attachment 1222485View attachment 1222488
 
Ligi za barabarani ndio ilikuwa michezo yangu but toka nimeoa na kuwa na familia nimepunguza manake naogopa kupasua nyanya/kupata ajali.....
Hereinbelow is one of my race nikiwa na Crown Athlete....
I was a dumb mthefcker racer...
 

Attachments

  • IMG_20190619_164213.jpg
    IMG_20190619_164213.jpg
    68.4 KB · Views: 43
Hahahaha mkuu vuta BMW hutojutia speed. Chuma kizito balance ya kutosha
mzee baba yani swala sio aina ya gari hahahaha baba swala ni pale upo kabah 160km/h mara pah kitu umeona kinapita barabarani unakikwepa sasa ayahhhh weeeee ndiyo basi tena hiyo..naongea hivyo imeshanitokea...huwa mnasaemaga nyosha goti ukiona mbwa yani hiyo ndiyo mbaya anapindua gari juu chini
 
Usiku sio salama kwa ligi.

Si rahisi kuona zaidi ya 200M, ukiwa speed zaidi ya 100kph, ni ngumu kukwepa hatari ya ghafla.

Usishindane na watu wa magazeti, hao wanapita hiyo njia kila siku tena usiku. Wanaifahamu vizuri sana.

Na usiku kuna ajali nyingi sana za uzembe na kukosa umakini.

Kuwa makini, usishindane na usiemjua.
Raha ya ligi upambane na usiemjua.....
 
Mwezi uliopita kuna noah iliingia nyuma ya trela la trekta ambalo halikuwa na taa wala reflector maeneo ya vijiji flani kabla ya Kabuku! Ilikuwa ligi hivyo hivyo, usiku ni mbaya sana kukimbia speed kubwa
Kuna watu wengi wamekufa kwa mwendo huo. Mimi nimenusurika zaidi ya mara 10 kwa ajali za aina hiyo.

1. Pale Ruvu nimenusurika kugonga gari yenye taa moja nikidhani pikipiki.

2. Igunga, nilinusurika kulivaa lori lililopaki pembeni.

3. Wami, nilinusurika kulivaa lori liliharibika katikati ya barabara.

Na mengine mengi tu. Usiku ni risk sana kukimbia kama huifahamu njia vizuri.
 
Ligi za barabarani ndio ilikuwa michezo yangu but toka nimeoa na kuwa na familia nimepunguza manake naogopa kupasua nyanya/kupata ajali.....
Hereinbelow is one of my race nikiwa na Crown Athlete....
I was a dumb mthefcker racer...
Naona warning lights za kutosha hapo kwenye dashboard.

Una amani kabisa ukiwa na hizo lights na umemaliza kisahani?
 
Back
Top Bottom