Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

[emoji28][emoji28][emoji28] wenye vyombo vya usafiri wanazingua sana
Ahaaa tulikuwa na boss Kiduku Lilo tukiwa na gari letu tukaona watu wanapIga honi na vitu vitu vyao tukaamua tuwapishe coz hawa wanaopenda ligi ni hatari kwa tunaoendesha magari.
Jamani nachangamsha genge tu.
 
Wakuu, nimezoea sana kutembea safari ndefu haswa Dar-Kahama-Geita na Dar-Mwanza, mara chache Dar-Bukoba.
Mara nyingi napenda kusafiri jioni au asubuhi sana.

Hizo route nilizozitaja hapo juu hazina Magari madogo mengi usiku, zaidi ya malori na mafuso. So huwa hatujui mambo ya ligi kabisa.

Kuna hii route ya Arusha-Dar na ligi huwa inaanzia pale Njia panda ya Himo, wakuu kuna watu wanapenda kushindana sana, kwenye barabara.

Juzi kati hapa tumetoka Arusha kwenda Dar tulivyofika Pale Njia Panda ya Himo, kulikuwa kuna gari kama tatu ndogo, Mark x nyeupe, Murano moja nyeusi na Alphad ya Silver, plan niliyokuwa nayo nikupoteza muda pale Njia Panda, at least usumbufu upungue barabarani kumbe zile gari zilikuwa zinatafuta abiria wa Dar, mimi kwenye gari ninayoendesha tulikuwa watatu. Sikuwa na wazo la kuchukua abiria.

Ilivyofika saa kumi na mbili kama na nusu hivi yule jamaa wa Alphad akang'oa, baada ya kama dakika kumi, Mark X akang'oa.
Hapo nimepaki upande wa pili wa barabara.

Ukapita tena muda kidogo Murano akang'oa...Tukamaliza mambo yetu tukaanza kuondoka, nilijua nikipiga mashine vizuri nitaenda kuwatoa kabla hata hawajafika Same!!
Tumeanza kutembea sio kwa speed kali hiyo jioni jioni ya saa moja bado watu ni wengi barabarani na mibasi + magari makubwa mengi yakitoka Dar kuja Moshi, Arusha.

Haikuchukua dakika nyingi saana kufika Mwanga, nikaiona ile Murano ndio inaondoka, nikajua labda alikuwa anaongezea abiria, nikawa nimempita mbele kabla ya Kisaranga nikaipita na ile Mark x, Alphad sikuiona. Giza linazidi kuongezeka naona na barabara inapungua jam.

Tumepita Lembeni kwenye Kivuko cha treni jamaa wa Mark X akaovertake kwa speed kali kuianza Tambarare flan hivi kuelekea Same, hapo ndio ikawa shughuli hakuniacha mbali sana, kabla ya sehemu inaitwa mgagao Murano akaniovertake akaenda akaovertake na mark x..

Baada ya Murano kunipita nikagundua Mark X kaongeza speed zaidi kwasababu alianza kuniacha kwa mbali kidogo.

Nikagundua hawa watu kama vile wanafanya ligi hapo road, nikaamua na mimi kujihusisha nao, ule mtiti haukuwa wa kawaida Tukaanza kutembea sasa pita nikupite ikaanza, jamaa wa Mark X tulikuwa tunamuacha sana...

Mpinzani wangu mkubwa alikuwa jamaa wa Murano, hadi tunafika Korogwe, kwenye kona yakuelekea Old Korogwe, kuna beria, tukamkuta jamaa wa Alphad pale na gari nyingine ndogo mbili, zote zinaenda Dar, ebwana eeh kama ni ligi ndio ilikuwa kama vile inaanza piga nikupige,

Jamaa walikuwa wanatoa changamoto sana, hata kusinzia huwezi muda wote unawaza kumtangulia aliyeko mbele yako na kutokukubali aliyeko nyuma yako akupite! Huu mfumo ulifanya tukafika Dar mapema sana! Huu utaratibu wa Ligi kwenye hii barabara sijui kama ni wa kila siku, Kuna mashindano sana.

Ni barabara yenye ligi tena matata sana.
Kuna MwanaJf anayependa ligi barabarani, share na sisi.
Napenda sana ila nikiwa peke yangu,nikishakuwa na familia nyie piteni tu kwa raha zenu...
 
Napenda sana ila nikiwa peke yangu,nikishakuwa na familia nyie piteni tu kwa raha zenu...
Familia ni muhimu sana, ila kuna member wengine ni washabiki wa ligi.
 
Ligi za Moshi - Arusha - Mto wa Mmbu tuachie hizo ligi mkuu nina kitu cha BMW hakijawahi kuniangusha, wajapan wanapata tabu sana. Wengine wanahisigi wanafukuzwa na majambazi.

Gari za kijapan naziitaga Prey namfukuza hapo nyuma huku naangalia dash board nitamani nikiona yupo 170 mbishi 180 basi hapo gear box naitupia kwenye sport mode kitu kinashtuka, nawasha indicator ya kuovertake napita kwa kasi ya ajabu naitafuta 200 nahakikisha mpumbavu haoni taa za breki.

Naenda mbele napark namsubiri apite tena . Wengine wakiona nimesimama hahahaha wanaogopa wanapark pembeni wanasikilizia.

Wabongo waoga sana
[emoji28][emoji28][emoji28] kuna kipindi flan nilipanda gari moja ya tour, kutoka Ngorongoro pale getini kuja Arusha town, jamaa alinipa lift kiroho safi!! Nahisi alikuwa amevuta bangi kidogo, kwasababu alikuwa rafu sana.
Ameshuka kwenye ule mlima kutoka Karatu kuingia mto wa Mbu kama kichaa, kutoka Mto wa mbu to Makuyuni kuna vizibiti mwenda vya chini (downs). Huyu jamaa alikuwa anazipiga balaa, aisee!! Nilivumilia sana kwa kweli.

Hizi gari za kijapani sio comfortable cars especially hizi Land cruiser hardtop
 
Ligi tamu kuanzia saa 10 jioni kutafuta kale kagiza cha saa 1 kasoro baba unakutana na V8 flani STK dereva anayejitambua, ligi inakuwa tamu sana. Yeye anaamini v8 inachanja mbuga na 220 yake mnyama BMW unasoma 240 halafu boss wake amelala hahahaha au na yeye anapenda ligi dereva anamwambia kuna mshezi anakuja kasi hapo nyuma unaona boss anachungulia kwenye mirror unaona v8 inaanza kuchanganya 180- 190 anachezea hapo kijana namuashia indicator napita anapagawa.

Mara mbele mteremko sipiti asije akasema nimetumia advantage ya mteremko nasubiria muinuko tunavyoanza kukamata tambarare basi napita.

Mjerumani nyoko sana BMW forever
Ndio ukute uko kwenye uwanja mpana sasa na njia unaijua vizuri.
Kuna siku nilikuwa natoka Shelui kuelekea Misigiri, kuna mshenzi aliniovertake nikiwa kwenye 190km/h.
Alienda kuua Ng'ombe kadhaa, mita chache kabla ya kuanza kushuka Senkeke, speed kali mida ya jioni ya saa kumi na saa kumi na moja, ni hatari sana kwasababu ya mifugo.

Ligi za barabarani ni tamu sana.
Naikubali sana BMW
 
Gari yangu ya kwanza kabisa ya kichovu toyota caldina, hapo natoka Moshi kuja dar na sina uzoefu sana na route za mbali, jamaa wa vits naye akaamua eti kunianzishia ligi, mimi niko 110 kph ananipita speed then mbele anaenda anapaki, nikipita tu huyu tena. Ama kweli ukiwa mchovu hata wachovu watataka ligi na wewe. Sasa hivi hata BMW akileta ligi na mimi ajipange kweli kweli, japo sita sahau kamwe dharau nilizoonyeshwa na vits kipindi nina gari la kichovu
 
licha ya changamoto za barabarani, kwa upande wa ligi za mabasi ya abiria nasikia kwa sasa anayesumbua route ya dar - mwanza ni tungis express na anayesumbua route ya dar - mbeya ni sauli express. imefika kipindi mpaka watu wanabet kuhusu haya mabasi.

a83e97be5c56163355cc6bcdd83b2b3a.jpeg
671b6614fc4e376718e6537d54b653b2.jpeg
 
Back
Top Bottom