Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Hahah mzee baba una kumbukumbu balaa, kuna uzi mwingine huyu mchizi alisema Dar-Mwz anatumiaga masaa 7 tu hahah.

Dar to Mwz ni km 1175 maana yake on average alikua anatembea 170km/h,Tz hii hii na barabara zake hahah.
Hili tulishalifanyia hesabu,
Haliwezekani.
 
Nakumbuka nilifanya ligi moja Matata na nisoyemjua barabarani siku niliyotoka kupiga kura, mwaka 2015....

Barabara iliyohusika ni Ali Hassan Mwinyi kuanzia hapa mataa ya Serena hadi Bagamoyo Road maeneo ya Tegeta.

Mida ilikuwasaa kumi jioni.

Chanzo cha ligi, alinichomekea kiboya bin kibabe halafu akanioneshea like, nshakuchomekea utanifanya nini sasa.... mmaamaaeee nilimkanyagia mafuta nahisi alienda kumeza cofta kwa vumbi nililomuachia. Shida yangu niko mbishi sana...

Siku husika ilikuwa jumapili watu sio wengi barabarani na siku ya uchaguzi hivo barabara ilikuwa nyeupeee.

Gari alilotumia mleta ligi mwenzangu kama sijasahau ilikuwa Altezza maana ilikuwa hizi gari za chini. Mimi nilikuwa na Grand Car (yaani gari ya juu halafu iko branded grand uchomaji wake wa mafuta uko sawia na V8 hukoo).

Siku hizi nimekua kiasi nimepunguza ukorofi na ubishi, ligi za barabarani almost nimeziacha.

Ligi niliyobakia nayo ni ya Mahaba na Mziki tuu. Mtu akiwa tayari tufanye ligi ya kucheza mziki kuanzia saa nne usiku hadi jogoo la saa kumi alfajiri linawika bila kupumzika.....

Kasinde Platinum Matata.
@kasie natamani nikuone tuu my dear
 
Wakuu, nimezoea sana kutembea safari ndefu haswa Dar-Kahama-Geita na Dar-Mwanza, mara chache Dar-Bukoba.
Mara nyingi napenda kusafiri jioni au asubuhi sana.

Hizo route nilizozitaja hapo juu hazina Magari madogo mengi usiku, zaidi ya malori na mafuso. So huwa hatujui mambo ya ligi kabisa.

Kuna hii route ya Arusha-Dar na ligi huwa inaanzia pale Njia panda ya Himo, wakuu kuna watu wanapenda kushindana sana, kwenye barabara.

Juzi kati hapa tumetoka Arusha kwenda Dar tulivyofika Pale Njia Panda ya Himo, kulikuwa kuna gari kama tatu ndogo, Mark x nyeupe, Murano moja nyeusi na Alphad ya Silver, plan niliyokuwa nayo nikupoteza muda pale Njia Panda, at least usumbufu upungue barabarani kumbe zile gari zilikuwa zinatafuta abiria wa Dar, mimi kwenye gari ninayoendesha tulikuwa watatu. Sikuwa na wazo la kuchukua abiria.

Ilivyofika saa kumi na mbili kama na nusu hivi yule jamaa wa Alphad akang'oa, baada ya kama dakika kumi, Mark X akang'oa.
Hapo nimepaki upande wa pili wa barabara.

Ukapita tena muda kidogo Murano akang'oa...Tukamaliza mambo yetu tukaanza kuondoka, nilijua nikipiga mashine vizuri nitaenda kuwatoa kabla hata hawajafika Same!!
Tumeanza kutembea sio kwa speed kali hiyo jioni jioni ya saa moja bado watu ni wengi barabarani na mibasi + magari makubwa mengi yakitoka Dar kuja Moshi, Arusha.

Haikuchukua dakika nyingi saana kufika Mwanga, nikaiona ile Murano ndio inaondoka, nikajua labda alikuwa anaongezea abiria, nikawa nimempita mbele kabla ya Kisaranga nikaipita na ile Mark x, Alphad sikuiona. Giza linazidi kuongezeka naona na barabara inapungua jam.

Tumepita Lembeni kwenye Kivuko cha treni jamaa wa Mark X akaovertake kwa speed kali kuianza Tambarare flan hivi kuelekea Same, hapo ndio ikawa shughuli hakuniacha mbali sana, kabla ya sehemu inaitwa mgagao Murano akaniovertake akaenda akaovertake na mark x..

Baada ya Murano kunipita nikagundua Mark X kaongeza speed zaidi kwasababu alianza kuniacha kwa mbali kidogo.

Nikagundua hawa watu kama vile wanafanya ligi hapo road, nikaamua na mimi kujihusisha nao, ule mtiti haukuwa wa kawaida Tukaanza kutembea sasa pita nikupite ikaanza, jamaa wa Mark X tulikuwa tunamuacha sana...

Mpinzani wangu mkubwa alikuwa jamaa wa Murano, hadi tunafika Korogwe, kwenye kona yakuelekea Old Korogwe, kuna beria, tukamkuta jamaa wa Alphad pale na gari nyingine ndogo mbili, zote zinaenda Dar, ebwana eeh kama ni ligi ndio ilikuwa kama vile inaanza piga nikupige,

Jamaa walikuwa wanatoa changamoto sana, hata kusinzia huwezi muda wote unawaza kumtangulia aliyeko mbele yako na kutokukubali aliyeko nyuma yako akupite! Huu mfumo ulifanya tukafika Dar mapema sana! Huu utaratibu wa Ligi kwenye hii barabara sijui kama ni wa kila siku, Kuna mashindano sana.

Ni barabara yenye ligi tena matata sana.
Kuna MwanaJf anayependa ligi barabarani, share na sisi.
I see kila ninaposoma uzi wako mwili unanisisimka. Hizo ndio zangu. Napenda hizo ligi balaa. Moyo hautaki hizi ligi kabisa,lakini nafsi inataka balaa. Kawaida sitakagi gari liwe mbele yangu. Huwa natokaga mbeya saa 12 asubuhi. Huku nyuma hakuna ligi sana, Ligi unakuja kuikuta huku moro baada ya trafick kupungua barabarani. Na huwa sitakagi kubeba abiria. Kuna siku nimechukua abiria wa3 pale moro,nilikuwa natoka dar to mbeya. Kulikuwa na mdada mmoja na jamaa yake walifika hoi na jamaa yake,si kwa kutapika huko. I see jamaa wanatembea jioni. Ikitokea wakatoa tochi siku moja njiani utashuhudia ajali kama 100 hivi siku hiyo. Ni juzi tu hapo kuna jamaa alileta tred hapa ya yule mwanajeshi aliepata ajali na IST pale mikumi. Kidogo hapo ikanitisha,siku kadhaa hizi nimesafiri safiri kwa bus. Lakini now natamani wiki ijayo naenda town itabidi niinuke tu na mpira wangu. Maana hakuna namna sasa
 
Hii barabara ya Dar to Mbeya siipendi kabisa.
Sijui kwanini sijawahi kuizoea kabisa.
 
niliwahi kuliukiza hili siku moja.
nikaambiwa wapinzani wao inluding kisbo huwa wanatoa mpunga kwa traffic ili tungis adhibitiwe.

matokeo yake huwa anasimamishwa mara kwa mara njiani ili achelewe kungia mwanza.
hv wanapata faida gani kwa mambo haya yote..maana mchuano huwa siyo wa kitoto!
 
Hii barabara ya Dar to Mbeya siipendi kabisa.
Sijui kwanini sijawahi kuizoea kabisa.
Barabara moja tamu sana mzee. Haina sana sehemu zenye usumbufu. Ukimudu tu kona za iyovi iyovi (japo nazo zina utamu wake,unalala kabisa na 120,unaibukia 130,unanyoosha kwa 140) na kitonga huko kwingine ni tambarale tu kama kumbusu msichana. Ukitokea dar,ukipita kitonga tu kipande kirefu cha iringa to igawa hapo unakaribia mbeya kimetandikwa mkeka wa maana,wamenikwaza tu kwenye vituta,hapa na hapa.
 
Bora ubaki tuu na hamu yako usinione, utakuwa disappointed. Niko togauti na maelezo ya humu jukwaani, kizee mithili ya Bi. Kidude.
Yeye hatajali ubibi kizee,atakachoangalia yeye ni kufikiria nyuma ya pazia,nondo unazoshuka nazo,hizo tu ndio zitampa mzuka,mzee ataendelea kusukuma ndani mashine (namaanisha kuendesha gari) [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Aahahahhaaa unanipandisha mzuka ujue...

Nimejikuta naanza kuruka makida makida aahahahhahaaa
 
Wakuu nimetoka Dar saa 12:30 asubuhi ndio naingia double road kuishika A town.
IMG_20191012_121337.jpeg
 
A Town...
Pamoja na kuwa ni mchana, nimetumia Saa sita na nusu.
IMG_20191012_122647.jpeg
 
Aahahahhaaa unanipandisha mzuka ujue...

Nimejikuta naanza kuruka makida makida aahahahhahaaa
Na ulivyoliweka hilo tabasamu la kichokozi hapo. Watu wanakupigia hesabu za kiutuuzima. Siku moja ulisema ni wewe mwenyewe. Siku ya siku tu wewe hapa nitaanza na ung'eng'e kwanza,tutageukia kizuru,nakuja kuua na hiki cha kwetu,wa kumuangusha tembo. Ile unapiga na magoti ya kukubembeleza
 
Mnyamwezi mie eehehehee mzigo mzito haswaaa, wanaopiga hesabu wajipangeee aahahahahhaa

Matata K.
 
Waaapiiii... Tweendee tuu nnavopenda safari miee mradi tuu kuwe na gari.... Aahahahhahaaa
Gari sio inshu. Shida pa kukubamba. Hivi ukute unaongea uko ng'ambo kwa madiba
 
Back
Top Bottom