Hii sasa ni pupa, ni papara

Angalia wasije wakakuita CDM.
Maana Tanzania kuna kaugonjwa kanaitwa CDM na CCM, kuna watu eti wanaitwa wapinga kila kitu.

Kila swali huwa lina jibu sahihi, Tujitahidi kuishi kwa uhalisia na sio hisia.
 
Angalia wasije wakakuita CDM.
Maana Tanzania kuna kaugonjwa kanaitwa CDM na CCM, kuna watu eti wanaitwa wapinga kila kitu.

Kila swali huwa lina jibu sahihi, Tujitahidi kuishi kwa uhalisia na sio hisia.

Umeona eeh?

Mara kibao tu humu nimemchana Magufuli!

Lakini hilo watu hawalikumbuki.

Wanachokumbuka wao ni mimi kumuunga mkono Magufuli kwenye mambo machache.

Sasa wanadai eti akili zimerudi kana kwamba ziliondoka!
 
Kwa ujumla sioni ubaya wa juhudi za kulifufua shirika letu la ndege.

Ni jambo jema tu.

Ila hii ya kununua lidege likubwa kama hilo li Dreamliner, sioni tija yake kwa sasa.

Wangeanza ufufuzi wa hilo shirika kidogo kidogo na hizo ndege ndogo ndogo.

Halafu baadaye baada ya kutengeneza faida ndo wangehitimu kwenye hayo makubwa makubwa ya masafa marefu.

Kununua dege la masafa marefu na kulirusha kwenye safari fupi za ndani ni uwendawazimu!

Kuna kila dalili hilo li Dreamliner litakuwa grounded.

Hii serikali imechemka kabisa hapa!

No two ways about it.
Hawa jamaa hawana Mpango Kazi wala Mpango Biashara.... Wanachofanya ni kutafuta sifa tu.......
 
Man, mbona huwa unaeleweka sana tu. Uzuri wako panapohitaji pongezi, utapongeza, ukiona mambo hayapo shwari napo huwa haufi na tai shingoni, unaweka bayana dukuduku lako.

Tatizo kuna watu kama yuko upande flani anajifunga kitambaa abaki upande mmoja tu, mambo hayaendi hivyo.
Well said mkuu.
 
No Business Plan no business. A business Helps you to make mistakes in Papers Than in Actual Business
 
Mkiwa humu mnauvua ulumumba, mkisimama kwenye madhabahu mnatukuza fikra za mwenyekiti
Bigg up Nyani Ngabu wewe ni mhenga nakuheshimu sana na naheshimu upeo wako ulitukuka unavyoanza kupambanua zuri na baya (sio lazima usifie / uponde vyote) ila haki lazima isimame
 
Very interesting. Angalau kuna mjadala wa aina hii. Katika biashara zisizoendana na malengo ya kisiasa ya “kuwapasha wapinzani” na “kuwapatisha taabu sana” ni hii ya usafiri wa anga.

Shirika la ndege hufufuliwa na kujengwa kwa kuanzia na mpango makini wa biashara. Ununuzi wa ndege hufanywa kimkakati hasa kwa kutumia mikataba sahihi ya malipo ikiwa ni pamoja na “Capetown Convention” inayotoa unafuu mkubwa kwa nchi masikini. Idadi na aina ya ndege hutegemea mpango wa biashara.

Itakuwa vyema kama ndugu zetu wahusika wakituthibitishia kuwa walitumia na wanaendelea kutumia nyenzo sahihi kufufua ATC. Kama lengo pekee ni “kuwadolisha” na “kuwapatisha taabu sana” wapinzani aka CHADEMA basi imetosha. Turudi mezani tuangalie jinsi ya kurekebisha mambo; kuweka serious business plan na kuzitumia ndege zilizopo kwa manufaa ya kibiashara itakavyowezekana. Tukishindwa, si hoja, ET itaendelea kutuletea watalii kama kawa.
 
Mkiwa humu mnauvua ulumumba, mkisimama kwenye madhabahu mnatukuza fikra za mwenyekiti
Bigg up Nyani Ngabu wewe ni mhenga nakuheshimu sana na naheshimu upeo wako ulitukuka unavyoanza kupambanua zuri na baya (sio lazima usifie / uponde vyote) ila haki lazima isimame

Shukran jazilan.
 
Nadhani ulikuwa usingizini. Zamani ulikuwa na mawazi supa. Au kuna NYANI NGABU tofauti na ninayemjua. Huu uandishi sio wako. Umeandikiwa?

Huyu "Ngabu" si ndiye aliyechangia majuzi kuwa "fulani" yalimsibu kwa kuwa "He talks too much?" Nikadhani anaona kwa kina! Leo haikubali dreamliner moja? Mbona ya pili na ya tatu zinakuja miaka 2 ijayo? Mbona hii ya sasa imechota theluthi 2 ya abiria wa ndege nchini mpaka "Jeti ya haraka" wamekuwa waungwana? Nauli za usafiri wa ndege zimeshuka kwa sasa. Nadhani huko mbele tutaona faida ya kununua sasa.
 
Nasikia tumenunua Airbus....

Sijui hii itakuwa inapiga masafa ya wapi?? Mtwara labda?
 
Back
Top Bottom