SoC02 Hii ni sauti ya dada yako, rafiki yako naitwa Judith Kaunda, karibu unisikilize

Stories of Change - 2022 Competition

Judithkaunda

Member
Aug 21, 2022
90
228
Wakati wa balehe kuna changamoto nyingi sana, binafsi nimekumbana na mengi. Mengine yakinisibu moja kwa moja, mengine nikijionea kwa macho, kati ya mengi niliyoona kwa macho, lilinitisha lile la mapenzi ya jinsia moja.

Kama uliipita vyema balehe yako, basi na tumshukuru Mungu. Balehe nd’o ujana wenyewe ambao wahenga walitutahadhalisha kuwa ni maji ya moto.

Wanawake kwa wanawake dhidi ya wanaume kwa wanaume, mapenzi ya jinsia moja kwa wanaume yameonyesha madhara ya wazi zaidi katika jamii. Kalamu yangu inajikita katika upande huu tishio zaidi. Ninayaandika haya nikiwa tayari ni mama mwenye watoto jinsi ya kiume.

Ushoga upo, ulikuwepo na utaendelea kuwepo ikiwa hatutazungumza pasi na kuoneana aibu.
Nami nasema nawe pasi na aibu, aya moja kwenda nyingine.

Wazazi tusipofanya bidii sasa hivi tutatengeneza tatizo kubwa baadae hawa watoto wetu ndio Taifa la kesho, unapowaangalia watoto wako unaiona wapi kesho yao? Unatengeneza kizazi cha aina gani hapo baadae?.

Wazazi tujitahidi kufanya wajibu wetu kuwalea watoto wetu, kuwapa mahitaji pekee haitoshi kumfanya mwanao kuwa unavyotamani awe, tusiwaachie wasaidizi wa kazi na walimu majukumu yetu yote. Tusiwanyime kuwa waalimu kwa watoto wetu, lakini wasiwe waalimu wa kila kitu. Inagharimu

Wakati mzuri wa kumtengeneza mtoto wako na kumfundisha ili akuelewe vizuri ni pale anapokuwa bado mdogo ili kumtengenezea mazoea, usisubiri akue zaidi itakuwa ngumu kumuweka sawa. Kisha ule usemi wa ‘samaki mkunje angali mbichi’ ukaanza kupambana nao na kumkunja samaki angali mbishi na amekomaa. Utamvunja

Kwanza tukubaliane kwamba Ushoga upo na ni tatizo kubwa hivyo tuwekeze zaidi kwenye fikra zao na tuwape maarifa ya kutatua matatizo yao kwa sababu kujiamini kunajengwa na ufahamu alionao juu ya jambo hilo. Tuwafundishe kitu ambacho unatamani ungefundishwa ulipokuwa mdogo na wazazi wako ili kuwa bora, na umwambie ambacho ulitamani kuambiwa kipindi cha nyuma.

Na wewe pia uwe mfano mzuri kwake azione tabia nzuri kutoka kwako ni rahisi kwao kujifunza kwa kuangalia kuliko kusikiliza. Unapomnunulia kitabu na kumuhimiza asome wakati huo wewe umejikita na matumizi ya simu muda wote ataona ni adhabu kwa sababu hajawahi kukuona unasoma vitabu.

Kwa ulimwengu wa sasa mitandao ya kijamii haikwepeki na tusipo wafundisha watajifunza wenyewe au akifundishwa na mtu mwingine hujui atakutana na nini huko. Tusiwaepushe na mitandao kwa kuwaambia ‘intaneti’ ni mbaya wakati wewe unatumia, atakuwa na maswali mengi sana na atatafuta majibu yake. Watoto ni watu wa kutafuta mambo mapya kila uchwao.

Tuwafundishe watoto wetu uzuri na faida ya intanet na matokeo chanya ya kutumia mitandao vizuri. Hawatasahau daima

Mzazi bado naongea na wewe, zingatia MIPAKA ya simu janja yako. Yumkini ni kweli kabisa katika simu yako hakuna video na picha za hovyo, ni amani na salama kumruhusu mwanao awe mmiliki mwenza kwa kujua kila kona. Lakini jikumbushe, ikiwa ameizoea simu yako kiasi hicho, vipi siku akikutana na simu ya mjomba Athumani inayofanana na yako, akapekenyua na kukutana na video za hovyo katika ‘folda la koneksheni’. Sio balaa hilo?...

Ibada njema siku zote huanzia nyumbani. Ukimpa mwanao mipaka katika simu yako, asilani abadani hawezi kuigusa simu ya ‘Anko’ Suma wa ‘koneksheni’.

Mzazi usiishi kimazoea, zama hizo katuni zilikuwa katuni kweli. Maana halisi ya kiburudisho kwa watoto, siku hizi dunia imeongeza madoido katika mzunguko wake. Hizohizo katuni zimeanza kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja.

Mzazi usimwache mwanao aangalie kila aina ya katuni, kama unayo nafasi anza kuiangalia kwanza wewe hiyo katuni kabla haujamkabidhi ‘Rimoti’ mwanao. Usijione unapoteza muda, ni heri kupoteza hizo dakika sitini kuweka tahadhali kulikoni aibu na huzuni ya milele.

Wazungu walitueleza kwa kimombo kuwa ‘Charity begins at home’ na mimi leo sibanduki nyumbani kwako mzazi. Ninaamini hilo nd’o jiko la mema na mabaya tunayoyaona mtaani.

Mzazi lainisha lugha na kauli zako mzazi. Kumfokea mtoto na kumcharaza wakati wa kumkanya juu ya janga hili sugu la wazawa na wakuja, haitakuwa msaada toshelezi. Bali kumjaza hofu na kumvunjia daraja la uhuru wa kukueleza anayopitia.

Sema na mtoto kirafiki, weka masikhara ikibidi wakati wa kusema naye juu ya janga hili la mapenzi ya jinsia moja.

Tusiwaogopeshe watoto wetu wanatakiwa kujivunia na kufurahia mazingira ya nyumbani usimfanye akakosa uhuru wa kuuliza chochote kwako. Kuna watoto wanapitia matatizo makubwa lakini hawawezi kusema kwa sababu wanajua wataadhibiwa kana kwamba hawakutakiwa kukosea au kupata tatizo hilo.

Mzazi, wewe ndio muandaaji wa kwanza wa stori ya maisha ya mtoto wako, tuwafundishe kusema hapana, tuwafundishe nidhamu na kanuni watakazo zifuata hata wakiwa mbali na wazazi. Tuwakumbushe thamani na fahari ya kuwa wanaume thabiti.

Ewe mama taifa linatengenezwa tumboni mwako na mtoto mpumbavu ni mzigo wa mamaye.

Tuwatengenezee mazingira watoto wetu waendelee kutuamini, kama ambavyo mtoto mdogo akichokozwa anakimbilia kwako kushtaki akiamini wewe ni wa upande wake siku zote. Hii ni imani kubwa waliyoweka kwetu. Tujivunie na wao wajivunie sisi.

Ni kweli umri wake umesogea kiasi na unaogopa hata kuongea naye jambo hilo, usiache! Ukimuonea aibu sasa, usianguke katika sonona baadaye. Mlinde ni mwanao ulimleta duniani akiwa uchi na ukamuhudumia usimuonee aibu hata wakati amelala mvizie umpekue kama yuko salama. Yanayotokea mtaani ni mengi sana mzazi mwenzangu, usikae kizembe. Kilinde kizazi chako.

Baba ni mtatuzi wa matatizo yake hivyo ndivyo anaamini mtoto na anaamini baba anamiliki kila kitu, hata akiona ndege anasema ni ya baba hata kama hujawahi kumiliki baiskeli, sauti yako ina mamlaka wape tumaini wanakuamini sana.

Wafundishe utii, maana yule anayemsikiliza sana ana ushawishi mkubwa wa kumbadilisha, kuwa mfano mzuri kwake aone fahari ya jinsia aliyotunukiwa na Mungu, imani utakayo mtengenezea itamsaidia hadi watakapokua mbali na wewe ili apambane kadri awezavyo kuutetea uanaume wake.

Tunaona ni kawaida na tumeshazoea watoto wetu wa kiume kulala chumba kimoja, tuwajulishe wajue nini cha kufanya wakiwa pamoja na nini hawatakiwi kufanya wakiwa pamoja. Hakuna mahali ambapo hatutalipia gharama, tuwe makini na tunachopandikiza kwa watoto wetu.

Simama kwenye nafasi yako kuokoa kizazi chako kutoka kwenye laana ya uzinzi. Kizazi tunacholea sasa ndicho kitaamua ushoga uendelee au vinginevyo. Mimi ntajitahidi kusimamia kizazi changu ushoga usiwepo.

Mfahamishe dunia inataka watu wanao jiamini. Na ukiwa karibu yake mnong’oneze kuwa michezo yote duniani inayo matokeo ya aina tatu. Ushindi, kufungwa na kutoa sare. Kasoro mchezo wa USHOGA TU! Wenye matokeo matatu ya ajabu.

AIBU, MARADHI na LAANA.

WAKO MWANDISHI
JUDITH KAUNDA
 
Mwenyezi Mungu akuongoze uliesoma chapisho langu usitoke Bure. Na uwe mfano mzuri kwa Jamii yako, mwambie na rafiki Ako na Usisahau kunipigia kura ili huduma hii iwafikie wengi zaidi.
 
sante dada ake kwa fundisho zuri 🙏
 
Back
Top Bottom