Bajeti yote ya Tanzania kwa mwaka wa fedha 2006/2007 ni TSH.4,850,588,000,000 (shilingi trilioni 4, bilioni 850, na milioni 588). Hizi ni fedha nyingi, kwani ni kasi cha sh. 138,588 kwa kila Mtanzania.
Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ni TSH. 239,650,710,000 (shilingi bilioni 239, milioni 650 na elfu 710)
Bajeti ya Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia ni TSH. 167,610,218,000 (shilingi bilioni 167, milioni 610 na elfu 218)
Ukujumlisha bajeti za wizara hizo mbili za Elimu, unakuta bajeti yote ya Elimu Tanzania ni TSH. 407,260,928,000 (shilingi bilioni 407, milioni 260 na elfu 928). Hii ni 8.396% ya bajeti yote ya Tanzania. Ni sehemu ndogo sana ya bajeti yote, na hili lina matatizo makubwa.
Augustine Moshi