Hii ndio sababu kwanini wahuni, watu tunaowaona wadhambi wengi wataingia mbinguni kuliko watakatifu wa kidigitali

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,603
15,401
Hawa jamaa waliopinda, wahuni, wezi, vibaka na watu wa aina hii licha ya ukorofi wao huwa wakibanwa kwenye kona ni wapole sana na wepesi kutubu.

Nakumbuka ajali moja ya Bajaji abilia wote walikuwa wamelewa chakali lakini wakiwa majeruhi walikuwa wanatubu na kumuomba Mungu fasta kabla hawajadedi mmoja baada ya mwingine.

Hawa wengi wataingia mbinguni kupitia dirisha la yule jambazi aliyetubu msalabani. Alisema tu "Unikumbuke katika ufalme wako" hapohapo akapata fursa hiyo wala hakuekuendeshwa sala ya toba na mwokozi.

Hakulisti maovu yake. Na wengi wanapokaribia kufa hutoa kauli za namna hii na Mungu huwa anawapa nafasi.

Walokole, watu wa dini sana na wafiadini mbalimbali wengi watapata shida kwa sababu ya kiburi na kujihesabia haki. Wengi wamedanganywa kuwa hawana dhambi hivyo atakufa kama mtakatifu bila kuomba rehema na msahama mwisho wa siku inakula kwake. Hawa ndio Yesu atawakataa, kusema siwajui.

Kitu cha kujifunza. Pamoja na mambo yako yote, usisahau kumwambia Mungu akukumbuke, akupe rehema zake. Hata ukibanwa kwenye engo ambayo opsheni yako ni kifo tu. Ingia kifona na kauli hii Mungu unikumbuke katika ufalme wako.

Ni hilo tu mkuu.
Fanyia kazi litakusaidia.
 
Kuna jamaa likua punga mtaa ulimchukia sana. Siku alipoumwa na kuzidiwa sana alimuita mchungaji wakaomba pale, akaomba msamaha kwa waliokuwepo, akaokoka siku mbili mbele akadanja.
 
Kuna jamaa likua punga mtaa ulimchukia sana. Siku alipoumwa na kuzidiwa sana alimuita mchungaji wakaomba pale, akaomba msamaha kwa waliokuwepo, akaokoka siku mbili mbele akadanja.
Huyu alizunguka sana. Alitakiwa kusema tu kama yule mwamba msalabani. Bwana nirehemu au unikumbuke. Tiketi tayari. Kwenda mbinguni ni simpo sana watu hawajui tu.
 
Mkuu! Yule mharifu msalabani alipata neema za kutubu mbele za Mungu! Sio wote wanapata neema kama hiyo! Ukiwa unaishi maisha ya dhambi na kukataa wokovu ukasubiri umebanwa unakaribia kufa eti ndo utubu na kujihesabia haki kuwa ndo utaenda mbinguni unajidanganya.

Hao unaowaita walokole ambao matendo yao yanawakana sio walokole! Mlokole anaushuhuda! Japo wapo wengine mnawakwaza wanapoamua ku-fight back mnaanza kuwanyoshea kidole! Kwavyovyote vile tusijiesabie haki! Anayetuhesabia haki ni Mungu.
 
Kuna jamaa likua punga mtaa ulimchukia sana. Siku alipoumwa na kuzidiwa sana alimuita mchungaji wakaomba pale, akaomba msamaha kwa waliokuwepo, akaokoka siku mbili mbele akadanja.
Hiyo inakubalika umemkiri Kristo mbele ya watu wengi! Sio unatenda madhambi alafu unajifariji nikikaribia kufa natubu! Uingii mbinguni! Wokovu ni sasa na ishi kulingana na toba!
 
Mkuu! Yule mharifu msalabani alipata neema za kutubu mbele za Mungu! Sio wote wanapata neema kama hiyo! Ukiwa unaishi maisha ya dhambi na kukataa wokovu ukasubiri umebanwa unakaribia kufa eti ndo utubu na kujihesabia haki kuwa ndo utaenda mbinguni unajidanganya! Hao unaowaita walokole ambao matendo yao yanawakana sio walokole! Mlokole anaushuhuda! Japo wapo wengine mnawakwaza wanapoamua kufight back mnaanza kuwanyoshea kidole! Kwavyovyote vile tusijiesabie haki! Anayetuhesabia haki ni Mungu
Ni kweli lakini, mwenyezi Mungu huwa anatoa kachansi flani kwa kila anayekaribia kufa.
Yule jamaa hakutubu. Alimwambie tu Yesu amkumbuke. Hii sentensi kuitamka inahitaji nanoseconds tu unakula tiketi ya uzima.

Pamoja na yote, hii fursa watu wasiisahau.
 
Hiyo inakubalika umemkiri Kristo mbele ya watu wengi! Sio unatenda madhambi alafu unajifariji nikikaribia kufa natubu! Uingii mbinguni! Wokovu ni sasa na ishi kulingana na toba!
Yule mwizi alikuwa myahudi. Anajua mambo ya Mungu lakini hakutubu hadi alipokaribia kudanja. Hili limeandikwa kutukumbusha unaweza kutenda maovu ila Mungu atakuvizia hadi sekunde ya mwisho ili utubu akuokoe.

Hataki mtu yoyote apotee. Ndio maana wanaoenda mbinguni ni wengi kuliko warakaoingia motoni mkuu.
 
Ndio mana yatupasa tujizuie kuhukumu, dakika za mwisho ndio zitakazo amua hatima yako tuombe Mwenyez Mungu atujalie mwisho uliokuwa mwema
 
Hakuna anaejua atakufa lini mkuu, hiyo kukiona kifo ni bahati ya watu wachache.
Ndio maana story ya yule jambazi na Yesu inatufundisha lazima na sisi tutafute maneno mafupi ya fasta ya kutamka unapoona una nafasi sufuri ya kuendelea kuwa hai. Naamini hata katika ajali, huwa kuna hata tusekunde 0.0002 ambatwo mola huwa anaachia waja wake. Sasa ukiwa na mentality za kuwaita wachungaji wakubishe, utakosa hii fursa.
 
Ndio mana yatupasa tujizuie kuhukumu, dakika za mwisho ndio zitakazo amua hatima yako tuombe Mwenyez Mungu atujalie mwisho uliokuwa mwema
Ni kweli kabisa. Wengi sana wataingia mbinguni kwa window ya last chance.

Idd amin
Osama bin laden
Hitler
Makahaba sugu
Mashoga na sponsors wao

Wengi sana. Hivyo lazima tukae mkao wa kuwa karibu na sentensi za kutumia sekunde za mwisho mola anazotupa.
 
somo hili ni fundisho kwa imani na makaniss yanayosusia maiti kisa wahusika walikuwa wadhambi. Unaweza kuwa umesusia mtu ambaye anasiti ya mbele katika ufalme alafu wewe ukaambiwa sikujui maana ulisusia watu wangu watakatifu walitubu sekunde za mwisho
 
Hao walokole hao aiseee wanaojiita walokole n watu wanafki na cjui kwann wanajihesabiaga Wana HAKI na kujiona wtt wa MUNGU ingali wengi wao Wana roho mbayà na chukii za waz wazi..
 
Ni kweli lakini, mwenyezi Mungu huwa anatoa kachansi flani kwa kila anayekaribia kufa.
Yule jamaa hakutubu. Alimwambie tu Yesu amkumbuke. Hii sentensi kuitamka inahitaji nanoseconds tu unakula tiketi ya uzima.

Pamoja na yote, hii fursa watu wasiisahau.
Unajua watu wanamchukulia poa yule muhalifu msalabani ya kwamba aliingia mbinguni kimasihara! Sio kweli! Kiwango kikubwa cha udhalilishaji cha kumshushia hadhi mtu kwa kiwango cha chini ni kifo cha msalabani! Aliyekuwa anahukumiwa kifo hicho alikuwa anaitwa mlaaniwa! Yaani ni uovu kiwango cha kulaaniwa na kufa kifo cha aibu! Unavuliwa nguo na kufedheheshwa katika kiwango cha chini kabisa kuliko mtu yeyote aliyehai anaweza kufedheheshwa! Alafu cha pili ni kwamba hao waalifu kutokana na uhalifu wao wanajiona wako sawa na huyo muhalifu (Yesu). Katika mazingira kama hayo alafu utambue kuwa huyo aliyekatikati yenu eti ni Mungu muumba mbingu na kuomba toba kwake akusaidie kuingia mbinguni! Inahitaji mafunuo ya ndani yasiyo ya kawaida! Hivyo, kitendo cha huyo muhalifu kuomba toba na rehema kwa Yesu msalabani katika mazingira hayo kilikuwa na uzito sawa na haki ya kuingia mbinguni! Tusichulie poa! Maaana hakuna kinyonge kitaingia mbinguni! Ufunuo 21:27
 
Unajua watu wanamchukulia poa yule muhalifu msalabani ya kwamba aliingia mbinguni kimasihara! Sio kweli! Kiwango kikubwa cha udhalilishaji cha kumshushia hadhi mtu kwa kiwango cha chini ni kifo cha msalabani! Aliyekuwa anahukumiwa kifo hicho alikuwa anaitwa mlaaniwa! Yaani ni uovu kiwango cha kulaaniwa na kufa kifo cha aibu! Unavuliwa nguo na kufedheheshwa katika kiwango cha chini kabisa kuliko mtu yeyote aliyehai anaweza kufedheheshwa! Alafu cha pili ni kwamba hao waalifu kutokana na uhalifu wao wanajiona wako sawa na huyo muhalifu (Yesu). Katika mazingira kama hayo alafu utambue kuwa huyo aliyekatika yenu eti ni Mungu muumba mbingu na kuomba toba kwake akusaidie kuingia mbinguni! Inahitaji mafunuo ya ndani yasiyo ya kawaida! Hivyo, kitendo cha huyo muhalifu kuomba toba na rehema kwa Yesu msalabani katika mazingira hayo kilikuwa na uzito sawa na haki ya kuingia mbinguni! Tusichulie poa! Maaana hakuna kinyonge kitaingia mbinguni! Ufunuo 21:27
Umeandika kitaalam sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom