Hii ndio Orodha ya makundi ya watu wanaohitaji Katiba Mpya na wasiohitaji

Umetumia methodology gani kubaini makundi hayo? Mawazo binafsi si tafiti

Nimehoji watu wa makundi niliyoyataja Mkuu.

Nimefanya kautafiti kadogo.

Sample niliyoichukua ni participants 100 Kwa mikoa ya Morogoro, Dar, Iringa, Mbeya NK.

Wapo niliowahoji,
Wapo Kwa kuwatazama tuu nikiwa kijiweni nk
 

Iko hivyo
 
Katiba inaumhimu wake ila si kwa kila kitu,

Mwanadamu si wa kudhibitiwa na katiba pekee, Ni nidhamu na kupenda haki ndiyo tunu kwa kila taifa

Ukitaka kufahamu kwamba katiba sio mwarobaini, Jifunze kwa vitabu vya Mungu vilivyoahidi adhabu kali kuliko katiba zote za duniani, lakini wanadamu wanazivunja kila siku amri na katiba ya maisha ya baada ya haya, sembuse katiba isiyoziba mianya yote, la mwanadamu haliwezi kuwa Perfect 💯, Mtatengeneza katiba, lakini kutapatikana tu watu watakaoona mianya ya katiba hiyo na watajinufaisha kupitia udhaifu huo, hii ni lazima,

Katiba inahitajika, ila siyo dawa ya wavunja katiba, na wala haitasababisha tuishi kama peponi, Kwani Africa nzima hakuna nchi zenye katiba nzuri na bora?

Je kwao kukoje?

Tuitafuteni katiba kwa maelewano, Wale wanaoitaka, wasiitake kwa nguvu, wale wasiopenda wasiwazuie wanaoitaka kwa nguvu

Tujadiliane kwa upendo, ingawa kwangu mimi siiwekei umhumu na kuipa matumaini makubwa mno

Tujifunze kwa katiba za vyama vyetu,

Mungu Ibariki Tanzania
 
Uko sahihi. Ila, pamoja na wengi kutojua maana ya katiba na wengine kunufaika na katiba iliyopo; mazingira ya kijamii, kiuchumi na kisiasa Tanzania kwa sasa yanadai katiba mpya. Hii ninaifananisha na enzi za kudai uhuru. Ni aslimia ndogo sana ya raia wakati ule (Nyerere na raia wachache wengine) walijua maana na umhimu wa uhuru. Kwa uchache wao walipambana hadi uhuru ukapatikana. Hivyo hivyo, kwa uchache wetu, tuendelee kupambana hadi katiba mpya ipatikane. Tusichoke kupayuka: TUNATAKA KATIBA MPYA!!!?
 

Umenena
 
Hata kipindi cha Nyerere waliotaka vyama vingi walikuwa 20% tu ,haijalishi wanaotaka ni asilimia ngapi hata kama ni mmoja tu anataka na akawa na hoja zenye mashiko basi ana haki yake.

-Kuna mambo mengi sana ya hovyo yaliyopo kwenye katiba hii ambayo yanahitaji kuondolewa,eg kuna ulazima wa kuwa na utitiri wa RC,RAS,DAS,DC etc na kuongeza gharama kwa taifa? Rasimu ya Warioba ilikuwa nzuri maana ilikusanya maoni ya wananchi.
 
Pengine niwakumbushe, kupata Katiba nzuri ni kitu kimoja na kuheshimu Katiba ni kitu kingine. Katiba hii mbovu ya sasa yule Mwendazake alikuwa anaivunja anavyotaka. Tumpongeze kwanza huyu Samia ambaye anaiheshimu pamoja na mapungufu yake.

Kuna haja ya elimu ya Katiba kwa wananchi na kujenga utamaduni wa kuheshimu Sheria na taratibu. Maana tukipata Katiba mpya na ikashindwa kuheshimiwa, tutakuwa tumevikosea vizazi vijavyo
 
Ndiyo mkuu, lakini kipengele hiko ni sehemu ya mtu kuwa na ajira!! kumbuka hilo mkuu
 
Mazuzu mengi ya ccm hayajui hata faida ya katiba wao wanachojua ni mwenyekiti kasemaje yenyewe utasikia ndiiiiiiiooooooooooooo hata yakiambiwa leo kunya hapana yataitikia hivyo hivyo sababu yamekalili!
 

Uko sahihi kabisa
 
Zote ni nchi
Ndugu Crimea kinachowaumiza Kenya pamoja na katiba yao nzuri ni zaidi issue ya ukabila (ambayo haikuletwa na katiba) lakini ni aina ya mfumo wa uchumi waliorithi kutoka kwa Muingereza (ubepari) ulisababisha land grubbing hivyo kuwaacha wengi wakiwa hawana ardhi na kutegema matajiri wachache! Lakini hii katiba yao inawapa nguvu ya juu ya kuwawajibisha viongozi wao! kitu ambacho tunakosa hapa Kwetu!
 

Upo sahihi Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…