Chombo pekee cha kudai katiba mpya ni Vyama vya Siasa Wananchi nani atawakusanya ili wadai katiba mpya?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,487
2,351
CCM Watanzania tunataka KATIBA MPYA .Acheni kupotosha kuwa Eti KATIBA sio ya VYAMA bali ya WANANCHI wakati Wananchi hao hao wapo kwenye HIVYO VYAMA.

VYAMA ni LAZIMA viwasemee WANANCHI wa NCHI hii,Vyama lazima Viwaelimishe Wananchi hawa Faida ya KATIBA MPYA kwani Kwenye Vyama kuna Wasomi wengi Wenye Uelewa wa Masuala ya Sheria.

Je, Wananchi wakitaka KUDAI KATIBA MPYA mnataka WAANDAMANE? Nani atawaunganisha hao WANANCHI wa NCHI Nzima ili WASEME tunataka KATIBA MPYA?

Nakipongeza sana Chama cha UPINZANI wa Dhati kabisa CHADEMA kwa kutoa ELIMU ya KATIBA na kuwasemea WANANCHI kuwa WANATAKA KATIBA MPYA.
 
kitakachowaunganisha wanainchi kutoka kwenye hivyo vyama vya siasa, na hususani hicho ulichokipongeza, ni vipaumbele vya msingi vinavyogusa maisha na maslahi yao moja kwa moja 🐒

huwezi kwenda kumshawishi mwanainchi anaehitaji maji, huduma bora za Afya, elimu, kilimo, biashara n.k akuunge mkono kudai katiba ili kurekebisha sheria za uchaguzi, mgombea binafsi, madaraka ya raisi, tume ya uchaguzi n.k🐒

utapiga kelele sana, utapata ghadhabu na muhemko sana, utawabeza na kuwadhihaki sana wanainchi kwamba hawajielewi, kama ilivyokawaida ya chama hicho ukipendacho kikikataliwa na wanainchi, mathalani kwenye sanduku la kura, kwa sababu vipaumbele vya chama chako dhidi ya katiba mnayoidai na vipaumbele vya wanainchi dhidi ya katiba wanayoitaka havisikilizani 🐒
 
Back
Top Bottom