Hii ndio Lamborghini ya kwanza kuingia bongo

Hii ndio Lamborghini ya kwanza kuingia bongo

hiyo sio ya kwanza kaka coz ipo nyingine ni nyeusi no zake ni T537 BEF,nimeshindwa kutundika picha yake coz natumia cm,ila ni kali hatari
Sasa wewe unabisha nini???T537 BEF na T526ARY ipi ni yakwanza wabongo kwa kubisha anweza kukubishia hata kiwembe akasema ni panga!!:bange::majani7:
 
Mfuko wake unamruhusu kufanya alichofanya, kama mimi nilivyoweza kununua baiskeli aina ya Avon, ndio mfuko wangu jamani tusimuonee wivu wa kitoto.
 
Najaribu kuangalia vyema naona ipo barabarani nadhani inatembea lakini kama macho yangu hayakosei sioni kama kuna mtu ndani. samahani lakini

labda ameli-program limfikishe nyumbani halafu yeye kalala usingizi, na litamuamsha likimfikisha, hahahhaa....
Acha mimi niendeshe evade gari langu la kimasikini.

Conquest-Vehicles-Evade.jpg
attachment.php
 
..mbaya zaidi huku bongo tunajua hammer,vx,benz na vigari vyetu tunavyopigana pasi na daladala kila siku, bilioni moja niitupe kwenye gari !! wakati ka vx keusi tu trafiki wanakaogopa ??

Hapo kwenye bold nimecheka sana. Lazima trafiki waogope VX V8 kwa sababu ndimo waajiri wao 'wanamoishi', kuanzia wabunge, mawaziri, wakurugenzi, wakuu wa polisi, wakuu wa jeshi n.k. Kuwa la Lmborghini na hizi pasi za daladala ni majanga tu!
 
hiyo sio ya kwanza kaka coz ipo nyingine ni nyeusi no zake ni T537 BEF,nimeshindwa kutundika picha yake coz natumia cm,ila ni kali hatari

Wewe hauoni hata hizo tofauti ya registration number? Umeambiwa ya kwanza kuingia nchini.
 
Sifa za kijinga!
Utaliendesha kwa barabara zipi na utajaza mafuta yapi?
 
Umepotea sana jembe, upo!?
nipo mkuu mambo mengi ila najitahidi hivyo hivyo mara moja moja kuja kuwawashia moto kule nyumbani kwenu cc
kama leo nimetoka kumchokoza secretary teh teh
 
Hapa umesema kweli, bado matuta yaliyojaa kila kona, hadi mitaani yapo, me hapa altezza linanitoa jasho, kwenye matuta natamani nilie, naenda kulinyanyua bila kupenda, sembuse hili hata kwenye kijishimo kupita mbinde
Inashangaza kwa mtu aliye na akili timamu kufanya kitu cha kipuuzi kama hiki. Mtu unapata prestige gani kuendesha gari kama hili Bongo? Au labda uwe unaendesha kwenye parking lot yako maana hapa jijini na hii milima Kilimanjaro (matuta yasiyopimwa ubora) na maziwa ya ghafla (mashimo yaliyojaa maji barabarani) si mtu unajitakia kifo tu na Kigali kama hiki?
 
aisee tukitoka wote home si tunaendesha gari..na mimi nilie na Toyota corolla 100
 
Nilichokigundua hapa wachangiaji wengi wanazungumzia gari kutokana na financial position zao na upeo wao mdogo kuhusu magari,ubora wa gari ni pamoja na engine perfomance + driving experience,na tatizo la wabongo wengi wanakimbilia kununua magari yenye perfomance ndogo na wakifikiri magagri yote yanafanana,kama huyo jamaa mwenye hiyo Lamborghini ungekuwa mna fahamiana nae ningekushauri umuombe akuazime hiyo gari u-drive kwa angalau 10kms then ungejua kuwa hizo gari zenu mmnazoendesha si lolote si chohote,gari kuuzwa kwa zaidi ya sh.bilioni moja kama alivosema Young Master ni lazima iwe ina something very different to other cars,just imagine mwingine ana-compare na Vitz,anyways poleni najua ni ufahamu mdogo wa magari ndio unawafanya mtoe hizo comments.
 
Preta its all about standing out the crowd, si umeona mpaka Young Master katupia picha ya gari, je angekuwa kanunua ist? nani angeweka picha hapo? kumiliki gari kama hiyo inamaana nyingi mfano wewe kutoa bilioni moja kununua gari sio tatizo,pia inaonesha kazi uanyofanya inalipa, wewe sio mtu mdogo au wa kawaida,

kwa sisi vijana mbona mademu watajileta wenyewe tu...

yani kuna sababu zaidi ya milioni moja kuwa na dude kama lambo au veyron bugatti, kina jayz wana private jet yao...
sasa wewe una dola milioni kadhaa kwa benki una makampuni yanaingiza mpunga daily afu unaendesha gari ya kimbwela si watasema umepewa masharti na mganga
 
Last edited by a moderator:
Na TRA aliwaambia thamani yagari hiyo ili akipe kodi stahiki au Shigongo anauza magazeti.
 
Back
Top Bottom