KERO Kwanini Hospitali ya Wilaya ya Ubungo haiwaruhusu wagonjwa kuingia na simu kwa baadhi ya wodi, Je, ndiyo Sheria inataka hivyo?

KERO Kwanini Hospitali ya Wilaya ya Ubungo haiwaruhusu wagonjwa kuingia na simu kwa baadhi ya wodi, Je, ndiyo Sheria inataka hivyo?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba tuwasilishe changamoto ya Hospital ya Wilaya ya Ubungo kutowaruhusu wagonjwa kuingia na simu wodini (wodi ya wazazi na emergency kwa watoto).

Hii ni hatari sana kwani ni kumnyima mgonjwa haki ya kuwasiliana na ndugu zake, na endapo akapata changamoto yoyote kabla ya ndugu kumtembelea basi mgonjwa hatapata msaada wowote.

Na mbaya zaidi ni afya ya Mama na mtoto ambaye ndio inahitaji udharura muda wowote. Yaani kimsingi Mama anaingia hatakiwi kuwa na simu kabisa

Naomba hii changamoto iwasilishwe kwa wahusika kuona kwan ni hii hospital hii tu? Au kuna waraka wowote wa serikali kupitia Wizara ya Afya?

Maana hakuna TANGAZO lolote la katazo ila walinzi (migambo) wanaolinda hapo muda wote wapo Kupambana na kunyang'anya simu wagonjwa wengine ambao hawana taarifa za hilo katazo.
 
Mheshimiwa PM wa JMHTZ alitoa mawasiliano yake wazibueni maskio hao
 
Naunga mkono. Hamna kuingia na simu wodi la wazazi. Sababu ni privacy ya wagonjwa.
 
Hii ni hatari sana kwani ni kumnyima mgonjwa haki ya kuwasiliana na ndugu zake, na endapo akapata changamoto yoyote kabla ya ndugu kumtembelea basi mgonjwa hatapata msaada wowote.
Sasa wewe utansaidia nini? Mtu yupo hospital kwenye msaada we utafanya nn ebu waache wataalamu wafanye vyao. Wake zenu wakiwa humo wakaanza kuwarecord wenzao je. Hongera kwa ujauzito btw.
 
Naunga mkono. Hamna kuingia na simu wodi la wazazi. Sababu ni privacy ya wagonjwa.
Umeelewa lakini? Privacy ipi hiyo kwamba mgonjwa aruhusiwi kuwasialiana na ndugu?

Privacy wanaficha nini?
 
Back
Top Bottom