..ni kweli Dr.Mahiga amefanya kazi nje na ana exposure tofauti na ile aliyokuwa nayo JK.
..lakini kuna wana-CCM kama Prof.Tibaijuka, Prof.Muhongo, Mh.Kagasheki, Mh.Omari Nundu, Dr.Salim Salim, Dr.Daudi Balali, Prof.Benno Ndulu, ambao nao tunaweza kusema wana exposure kama ya Dr.Mahiga, au hata zaidi.
..zaidi nadhani tunaposema mtu ana-exposure ya kufanya kazi na kuishi nje ya nchi, tunategemea mtu huyo atakuwa hapendezwi na hawezi kuvumilia jinsi CCM inavyoendesha nchi hii.
..sasa mimi kitendo cha mtu kuishi na kufanya kazi nje ya nchi halafu bado akaendelea kuwa mwanachama mtiifu wa CCM, kiasi cha kutafuta uongozi ndani ya CCM, hakinipi matumaini hata kidogo. Kwangu mimi that is a big, huge NEGATIVE.
..Binafsi ningemuamini Dr.Mahiga kama angetafuta uongozi kupitia vyama vya upinzani vilivyoko sasa hivi. Kama anaona Dr.Mahiga anaona vyama vya upinzani vilivyopo havifai, basi angeweza kabisa kuanzisha chama chake mwenyewe.
NB:
..Binafsi namheshimu sana Prof.Lipumba kwa kujitoa mhanga kuongoza chama cha upinzani. Huyu angebaki CCM leo angekuwa anakula kuku kwa mrija. Mwingine ni Zitto Kabwe. Kijana mdogo, raised by a single mother, ana ujasiri wa kuanzisha chama na kusimamia kile anachokiamini.
..Lakini tuna watu kama kina Warioba, Salim, Mahiga, whom the country has given so much, lakini wamejikunyata na wameshindwa kusimama kidete kupinga ufisadi na udhulumati unaoendelea nchi nzima.
cc
Mkandara,
Nyani Ngabu,
Jasusi,
Kimweri,
Nguruvi3,
ZeMarcopolo,
Mzee Mwanakijiji,
Kapwela, Zero, Mchambuzi