Hii ndio Familia ya Agustino Mahiga

Hii ndio Familia ya Agustino Mahiga

Huyu mahiga hafai na hawezi kuwa president wa nchi Hi sana sana anapoteza muda wake.
hajui chochote kuhusu hali halisi ya tz, alafu hao watoto wa obay na masaki washapitwa sahv hakuna kuogopana sjui huyu mtoto wa masaki wala huyu wa obay.

----- anafahamika kwa kauli zake:becky:
 
Mzee najua uko very passionate na huyu POSH BOY MAHIGA lakini acha uwongo kuhusu January kukosa security clearence kuwa naibu waziri.

Again hujaelewa, nimesema imegomea nikimaanisha it's as high as what Naibu waziri can have. do you honestly think Clearance ya Naibu waziri na Mkurugenzi wa TISS ziko sawa?

Am passionate about any credible candidate, someone who will raise the bar of presidency, not making it a laughing stock
 
wewe mapenzi yanakupofusha mkuu,

Sasa kama ni ishu ya uwezo binafsi, si aanzishe timu inaitwa MESI acheze mwenyewe nafasi zote toka golini na afunge, si anauwezo bwana, au huyu astronout si arushe roketi yake mwenyewe mpaka huko angani? mkuu unasikia unachokisema lakini??

ndio maana hata katika tuzo waungwana hawaachi kuwashukuru wenzao, kwa maana bila ya watu hakuna mtu,

Narudia tena, ni hatari sana kukaa chumbani kwako na kujiaminisha kua hakuna kama wewe, kuna wengine wengi tu zaidi yako, pia naamini katika watanzania 50 milion, kunao mahiga na zaidi yake kama 20 million, ni mgawanyo wa majukumu tu mkuu, ndio maana huoni wote tukifanya kazi moja, ushaona wapi watu wote ni marais? sio kwamba hakuna wenye uwezo wa kua rais, kwahiyo huyo aliekua rais ndio anauwezo kuliko wengine, hapana, ni katika ile hali ya kibinadamu tu kwamba hatuwezi fanya jambo moja wote kwa wakati mmoja hivyo tunateua mmoja atusaidie kufanya kwa niaba yetu.

Naamini kuna watu ambao they could have done better than him. na wapo hapa Tanzania, tena kule ndoombo meru,

Nimeshawazoea watu wa sampuli zako. Mkiishiwa hoja mnaanza vioja. Kama unaamini watanzania wenye uwezo wa kuwa maraisi wazuri ni zaidi ya 20 walioongoza nia basi u are beyond help. being president needs the correct preparation and credentials, umeshapita wakati wa UHURU ambapo kila mwenye college education aliweza kuwa kiongozi wa serikali.

Unaongelea mgawanyo wa majukumu halafu unaanza porojo za kila mmoja kuwa raisi. Unasema kuna watanzania milioni 20 wanafaa kuwa maraisis, wakati hao wenye elimu ya chuo kikuu tu hawafiki milioni 20, au hujui vigezo vya kuteuliwa kuwa raisi wa Jamhuri?

Kama umeshawahi kufanya kazi na statistics unaweza kufanya deduction ya kujua ni watu wangapi wanafaa kwa hiyo kazi baada ya kufanya elimination ya factors nyengine.

Ukishaweka kigezo cha lazima awe na uzoefu na maswala ya kimataifa lets say kw amuda usiopungua miaka 5, unatoka kwenye millions of potential candidates to a few hundred, kadri unavyoweka vigezo ndio unavyofanya elimination ya wenye uwezo wa kuwa maraisi. Kama hujui hivyo basi la ziada. hata hao wa ndoombo meru wanafaa.maana hujui hata vigezo vilivyowekwa ni vipi.
 
1.
2.
3.
4.
5.
Wapendwa mbona mnapanick? Hivi ikitokea akapatikana Kiongozi mzuri si wote tutafaidika? Msianze mapema kuwakashifu watu. Wapeni nafasi wapimwe tuone nani ni nani. Kwa wakati huu nawaambieni Nchi inahitaji mgombea msafi sana, Kama posho kuleni lakini isaidieni nchi ipate Kiongozi atakayefaa bila kujali atatoka wapi, kama yuko CCM apewe, kama ni UKAWA Apate, lakini kigezo kiwe weledi na usafi, mtu amabaye ataweza kuitoa nchi kwenye ufisadi atatusaidia

Point mkuu
 
Kitu muhimu kwa Tanzania sasa hivi ni kujaribu upinzani watu tungehamasishana tuuondoe utawala wa CCM, na upinzani uje ndo kingekua kitu cha msingi kujadili viongozi sijui watia nia wa CCM ni kupoteza muda

Hilo nakubaliana kabisa na wewe.

CCM miaka nenda miaka rudi wapo madarakani na hakuna nafuu yoyote ile.

Hakuna hata mtu anayehoji je, kasi mpya, ari mpya, na nguvu iliyaleta hayo maisha bora kwa kila Mtanzania?

Akina nani hao ambao maisha yao yameboreka katika miaka 10 iliyopita?

Haya, turudi nyuma kidogo...enzi uwazi na sijui usawa ule. Hivi kulikuwepo na kitu kama hicho kweli au tulikuwa tunalishwa (na kumeza) maneno matamu tu?

I am sick with CCM's lip service and I am ready for a real change. A clean break from the past.

But sadly I don't see that happening anytime soon in my lifetime especially with the time of people we have who are too pliant and very easy to hoodwink.
 
Muulizeni bei ya nyanya au kilo ya sembe kiasi gani kama atawajibu

Hapo mako makuu ya CCM kaenda juzi. Mnataka kutuaminisha kuwa mtu anayenunua suti za dola elf 10 anajua hali halisi za wa Tanzania?

Inakuwaje balozi anavaa suti za ghali kuliko rais wa nchi? Sasa hapo bosi nani?

Kwani kaona tabu gani kukaa kimya na kuendelea kuandika articles zake kwenye magazeti ya udaku? Angekuwa ana akili hivyoo bas kwa nini alikuwa haandiki hizo makala zake kwenye majarida ya foreign policy yenye heshima kama vile Africa Journal of International Affairs, International Studies Quarterly, International Security, Foreign Affairs, Foreign Policy etc? Mnataka kutuaminisha kuwa huyu ana akili kuliko Asha Rose Migoro na Libereta Mulamula? Mindhali kaamua kuingia kwenye hiki kinyanganyiro na anaishi kwa pesa za walipa kodi bas ajue tutaendelea kumfanyia vetting maisha yake Public na Private. And he cant stand the heat he should stay out of the kitchen.

Eti afisa Usalama wa Taifa!! so what? kuna maofisa wangapi wapo na wana qualifications kuliko zake na hawajapewa hizo nafasi. Huyu narudia kuwa kama walivyo mabalozi wetu wengi, he's out of touch na hatumtaki. Kama kanuna aende akaombe kazi ya contract kwa Ban Ki Moon.

Tulimkataa Salim Ahmed Salim ndio itakuwa huyu?
Hoja zako za kitoto sana. Kajipange upya.
 
Kama hiyo orodha ndefu hukuielewa si uulize? Uliza hawa ni akina nani? Lakini itakuwa ni uchovu tu maana google ipo na ndo utagundua contribution yao iko mbali zaidi ya Obama. Mimi nimewaangalia. Hawa ndo wameigeuza Dunia hakika na ni ukweli hawakusoma Harvard!

Jamani huyo Obama ndo kipimo chenu?

Again unarukia mbele ya mjadala usiokuhusu bila kupata total context ya kilichoongelewa. I was referring to smarts of a Havard educated professor as a plug for his relatively thinner experience. Sasa kina january Elimu za mashaka, Vyeo walivyopata wamependelewa na uwepo wa wazazi wao, na bado performance mbovu, with short experience he has gathered. Leo hii mnataka kumpa majukumu mazito zaidi, wakati kuna solid performer with excellent track record and unquestionable intelligence.

Ukiona mtu anampigia debe mtu wa style za Makamba jua kala hela zake, au ana matatizo ya kufanya analysis.
 
Hilo nakubaliana kabisa na wewe.

CCM miaka nenda miaka rudi wapo madarakani na hakuna nafuu yoyote ile.

Hakuna hata mtu anayehoji je, kasi mpya, ari mpya, na nguvu iliyaleta hayo maisha bora kwa kila Mtanzania?

Akina nani hao ambao maisha yao yameboreka katika miaka 10 iliyopita?

Haya, turudi nyuma kidogo...enzi uwazi na sijui usawa ule. Hivi kulikuwepo na kitu kama hicho kweli au tulikuwa tunalishwa (na kumeza) maneno matamu tu?

I am sick with CCM's lip service and I am ready for a real change. A clean break from the past.

But sadly I don't see that happening anytime soon in my lifetime especially with the time of people we have who are too pliant and very easy to hoodwink.

Lakini ukiangalia watu ambao wangetegemewa kua mstari wa mbele kuhamasisha kupigia kura upinzani ndio hawa wanaendekeza ushabiki usio na tija, tena wameweka mbele u vyama ambao kimsingi hausaidii kitu au manufaa yoyote yale...
 
Huu ndio msimu wenyewe wa Kampeni and all gloves are off. Kamapeni zikiisha tutaombana radhi. Kwa sasa hebu tuache tumchambue huyu jamaa kama wanavyochambuliwa wengine. Why give him a preferential treatment? kama yeye na hiyo team yake hapo Masaki hawawezi kujibu wakodishe mercenaries waje kumjibia lakini sisi tunaendelea kukamua kama kawaida.

Na sisi we have all the time in the world kwa ajili ya JAMIIFORUMS. Afterall WE EAT, BREATHE, SLEEP JAMIIFORUMS.

Mpaka sasa hujaja na hoja ya maana inayoaddress mambo ya msingi ambayo ni uchumi, rushwa ma ufisadi, elimu afya. Unamhukumu wakayi hujamba nafasi. Je unatumia benchmark gani ku conclude kwamba hafai. Leta utafiti unaosema wanaovaa suti nzuri nzuri hawafai kuwa viongozi. Leya utafiti unaosema walipeleka watoto shule nzuri nzuri wakaelimik hawafai kuwa viongozi. Acha porojo ongea kwa facts
 
Lakini ukiangalia watu ambao wangetegemewa kua mstari wa mbele kuhamasisha kupigia kura upinzani ndio hawa wanaendekeza ushabiki usio na tija, tena wameweka mbele u vyama ambao kimsingi hausaidii kitu au manufaa yoyote yale...

I've given up.

Acha tu maCCM yaendelee kutawala.

We deserve every bit of them and then some.
 
Exposure ya Kikwete siyo sawa na ya Mahiga hata Kidogo. Kikwete hajawahi kusoma wala kukaa nje ya nchi kwa muda mrefu. Hii exposure ya kwenda kikazi au kozi ya miezi 2-3 siyo exposure kubwa kama watu wanavyopenda kufikiria. Exposure ya Kikwete unayoizungumzia ni wakati akiwa Waziri wa Foreign Affairs!!? Kwangu exposure ni kupata fulsa wa kuishi na kufanya kazi na watu wengine kwa muda murefu, probably 2 to 3 three years!!

Exactly my point.

Sasa mtu atapewa choice ya kumchagua Balozi Mahiga na Mwigulu Nchemba, atamchagua Mwigulu kwa exposure gani aliyo nayo? Kwa hiyo local jockeying for position?

Kikwete tumemuona tangu anaingia foreign anafundishwa mambo ya foreign na Dim. Kwa hiyo sioni tunachopingana katika kusema Kikwete hana exposure. That is the point I was making when I said hecould nit answer Bob Geldof.
 
Nimemsikiliza jamaa kwenye hiyo lecture;Ana upeo mkubwa sana na anailewa vizuri sana Tanzania, historia yetu tulikotoka, challenges zetu, tulipo na tunakotakiwa kwenda. Kwa kifupi kati ya wote waliojitokeza upande wa CCM he is way on his own level. But sad wapiga kura ni watanzania wale wale waliowachagua kina JK
 
Kama kawa mtanzania ni kichwa cha mwendawazimu kila msusi hupendelea kujifuzia kwake kusuka...."unafiki,usaliti,uwongo na ubinafsi utatumaliza...
 
Exactly my point.

Sasa mtu atapewa choice ya kumchagua Balozi Mahiga na Mwigulu Nchemba, atamchagua Mwigulu kwa exposure gani aliyo nayo? Kwa hiyo local jockeying for position?

Kikwete tumemuona tangu anaingia foreign anafundishwa mambo ya foreign na Dim. Kwa hiyo sioni tunachopingana katika kusema Kikwete hana exposure. That is the point I was making when I said hecould nit answer Bob Geldof.

..ni kweli Dr.Mahiga amefanya kazi nje na ana exposure tofauti na ile aliyokuwa nayo JK.

..lakini kuna wana-CCM kama Prof.Tibaijuka, Prof.Muhongo, Mh.Kagasheki, Mh.Omari Nundu, Dr.Salim Salim, Dr.Daudi Balali, Prof.Benno Ndulu, ambao nao tunaweza kusema wana exposure kama ya Dr.Mahiga, au hata zaidi.

..zaidi nadhani tunaposema mtu ana-exposure ya kufanya kazi na kuishi nje ya nchi, tunategemea mtu huyo atakuwa hapendezwi na hawezi kuvumilia jinsi CCM inavyoendesha nchi hii.

..sasa mimi kitendo cha mtu kuishi na kufanya kazi nje ya nchi halafu bado akaendelea kuwa mwanachama mtiifu wa CCM, kiasi cha kutafuta uongozi ndani ya CCM, hakinipi matumaini hata kidogo. Kwangu mimi that is a big, huge NEGATIVE.

..Binafsi ningemuamini Dr.Mahiga kama angetafuta uongozi kupitia vyama vya upinzani vilivyoko sasa hivi. Kama anaona Dr.Mahiga anaona vyama vya upinzani vilivyopo havifai, basi angeweza kabisa kuanzisha chama chake mwenyewe.

NB:

..Binafsi namheshimu sana Prof.Lipumba kwa kujitoa mhanga kuongoza chama cha upinzani. Huyu angebaki CCM leo angekuwa anakula kuku kwa mrija. Mwingine ni Zitto Kabwe. Kijana mdogo, raised by a single mother, ana ujasiri wa kuanzisha chama na kusimamia kile anachokiamini.

..Lakini tuna watu kama kina Warioba, Salim, Mahiga, whom the country has given so much, lakini wamejikunyata na wameshindwa kusimama kidete kupinga ufisadi na udhulumati unaoendelea nchi nzima.


cc Mkandara, Nyani Ngabu, Jasusi, Kimweri, Nguruvi3, ZeMarcopolo, Mzee Mwanakijiji, Kapwela, Zero, Mchambuzi
 
Back
Top Bottom