Hii kitu huwa inauma lakini pia huwa inahamasisha kupambana

mweatu

Member
Jul 13, 2015
16
47
Pale ambapo upo mkoani na unapambana kupata ajira, halafu unapata interviews za Dar mara kadhaa, na unafikia kwa washikaji zako huko Dar ambao kiasi fulani maisha wameyaweza.

Ni wa umri wako, wengine hata classmates. Unakuta wana mijengo saafi, usafiri, unakaa pale comfortably unakula, unakunywa unapewa na pocket money kabisa.

Then kila ukienda interview, hamna kitu. Sometimes hata oral interview hufiki. Unakuja umeinama, kichwa chini, na unarudi zako mkoani.

Halafu unapewa na nauli, then unaagizwa ukawatafutie ekari za ardhi za kutosha huko kijijini ili wawekeze huko pia eg ekari 100, 150, duh!.

Duh! Ngoja tuendelee kuwapigia makofi wenzetu, ipo siku itakuwa zamu yetu pia kupigiwa makofi.

Tuendelee kupambana
 
Nilikuwa naongea na CEO mmoja wa Benki kubwa nchini akaniambia hata yeye alivyomaliza chuo alikuwa anashindia mikate tu geto, maisha yalikuwa magumu kinyama lakini alitoboa.

Hiyo kawaida tu.
Dawa ni kutowaonea wivu waliotangulia, shirikiana nao uvuke
 
Asanteni wadau kwa ushauri na kunipa moyo. Kwa wale wenzangu wote ambao bado hatujapata ajira kama mimi, tusikate tamaa tuendelee kupambana, ipo siku. Nimepokea pia mawazo ya plan B eg kupanda miti etc.
Shukrani pia ziwafikie hao washkaji zangu hasa wale wa Dar, muendelee kuwa na moyo huo wa kutusupport. Tunaamini usumbufu huu hautadumu wa siku zote, one day mambo yatakaa sawa
 
Nimeupenda huu ushauri,ikiwezekana ufanyie kazi.
Pia endelea kuishi fresh na washikaji,one day yes
 
Mwaetu umeandika ya moyoni haswa,
Pole,
Kila mtu na wakati wake,
Usikate tamaa wewe ni mtu mkuu,
Kinywa chako kina nguvu,
Endelea kujinenea na kujiwazia mazuri.
 
Pale ambapo upo mkoani na unapambana kupata ajira, halafu unapata interviews za Dar mara kadhaa, na unafikia kwa washikaji zako huko Dar ambao kiasi fulani maisha wameyaweza.

Ni wa umri wako, wengine hata classmates. Unakuta wana mijengo saafi, usafiri, unakaa pale comfortably unakula, unakunywa unapewa na pocket money kabisa.

Then kila ukienda interview, hamna kitu. Sometimes hata oral interview hufiki. Unakuja umeinama, kichwa chini, na unarudi zako mkoani.

Halafu unapewa na nauli, then unaagizwa ukawatafutie ekari za ardhi za kutosha huko kijijini ili wawekeze huko pia eg ekari 100, 150, duh!.

Duh! Ngoja tuendelee kuwapigia makofi wenzetu, ipo siku itakuwa zamu yetu pia kupigiwa makofi.

Tuendelee kupambana
Inauma sana hakika unaweza ukasema f.uc.k the creator kama una roho ndogo
 
Back
Top Bottom