Audi A4 Gari Moja Ya Kichawi Sana, Twende Pamoja utanielewa

Samatime Magari

Senior Member
Feb 10, 2017
103
387
1652765086063.png


Audi A4 ni line ya compact executive cars ambazo zimekua kwenye uzalishaji tangu 1994 huko German na Audi ambayo ni subsidiary ya Volkswagen Group, Subsidiary yani ni kama CCM na ACT hivi [Jokes] Tuendelee.
.
Generation zake zimekua coded B5[1994-2001], B6[2000-2006], B7[2004-2009], B8[2008-2016] na B9[2016-Todate]... . Audi A4 imekuja na shape za sedan [Kama Taxi], station wagon [Kama Probox].. . Convertible version [inafunguka juu] na coupe [Kile cha wachoyo cha milango miwili].
.
1652765206158.png
1652765237350.png
1652765258606.png

.
Sasa kwa leo tutaenda kugusa generation ya Pili [B6 2000-2006] na Tatu [B7 2004-2009] as kwa sasa ndo nyingi zinanunuliwa na bei zake ni nzuri, Tutaanza na B6 Kaa vizuri andaa popcorn zako za Laki moja na juice uanze kula madini...
.
Audi A4 B6 ina umbo la kuvutia [sports Looks] na ni moja ya classy looking car, Ikishindanishwa duniani na BMW 3 -Series na Mercedes Benz C-class. Kwa nje ina muonekano very unique ikipewa taa kama macho ya Rehema Chalamila na nyuma ikipewa curves nzuri za kuvutia...
.
Kwa na ndani nafasi ni kubwa na mnakaa mkiwa comfortable kabisa, Legroom ipo ya kushosha pale mbele abiria mrefu miguu inakaa vizuri na hata kwa upande wa abiria kuko poa pia Ila ukiwa mrefu sana kuanzia kiunoni kuja juu kichwa kinaweza gusa kwenye roof...
.
Seats zake zimepangwa vizuri[well elevated and extra padded] ili kukupa comfortability zaidi unapokua ndani ya chombo, Ukija kwenye dashboard imekaa poa sana option zake zimepangwa vizuri, maandishi yakipewa rangi nyekundu yenye kuvuti, niweza sema German kwa interiors wako vizuri sana.

1652765373926.png
1652765507413.png
1652765586236.png


B6 imekuja imekuja ikiwa na engine option kadhaa kwa Petrol na Diesel. Tukianza na Petrol kuna Inline-four [cylinder] petrol engine 1.6L, 1.8L 20v Turbo, 2.0L 20v, 2.0L FSI 16v, then kuna V6 petrol engine 2.4L V6 30v, 3.0L V6 30v, V8 petrol engine 4.2L V8 40v [V ni Valve]...
.
Diesel engine kuna Inline-four [cylinder] engine 1.9L I4 TDI, V6 diesel engine na 2.5L V6 TDI, Hizi engine zote ziko linked na Transmission za 5-speed Manual, 6-speed Manual. Kwa automatic Transmission kuna 5-speed Automatic na 6-speed Automatic..
.
Kuna codes zimetumika katika majina ya hizi engine mfano TDI ni Turbocharged Direct Injection, Kwa lugha nyepesi ni engine ambayo ina turbo na intercooler kwenye compressor ya turbo ndo inakua na hili Jina. Hizi ni kwa engine za Diesel, na Pia kuna mfumo wa TFSI..
.
1652765662578.png
1652765724785.png
1652765814038.png


TFSI hii ni mfumo unaotumika sana na engine za Audi [Petrol Engine] ukimaanisha turbo fuel stratified injection (TFSI). Yani turbo inakua introduced kwa mafuta yanayoingizwa kwa pressure katika combustion chamber na kuchoma instantly. Pia ukiona Audi imeandikwa Quattro Inamaanisha hiyo gari inaendesha tyre zote nne [All wheel drive] na gari ina element za racing...
.
Hili ni neno la ki Italia likimaanisha nne na pia Q inatumika na Group maarufu la rally huko duniani toka miaka ya 80, Sasa Tofauti ya TSFI na TDI ni kwamba TSFI yuko faster Anachanganaya mapema na anakula mafuta zaidi na kumtunza ni rahisi...
.
Wakati TDI yeye ni mzito anatumia mafuta kidogo [economy] na ni gharama kumtunza ukilinganisha na mwenzake, Kwenye matunzo huwa hatuko vizuri ndo maana tunatumia engine za Petrol na wewe nakushauri tumia Petrol tu...
.
Hizi mifumo Lengo ni kuipa gari nguvu ya ziada kama hauna uhitaji na hizo nguvu hakuna haja ya kuchukua hizo engine, Sio una gari top speed 260Km/Hr na hujawahi hata kufika 160Km/Hr, huo ni uharibifu tu its much better ukachukua engine za kawaida tu [nitashare huko mbele]...
.
Gari iko chini haifai kufukia mashimo hasa ukiwa speed, Iko very stable barabarani yani haichezi hata kidogo hata ukiwa kwenye high speed. Kwenye kona ndo tamu zaidi gari imetulia mpaka unasikia raha, Nikukumbushe ukiwa speed ukiona shimo/speed bumps pita taratibu gari iko na sensors za kutosha kama majipu ukilitumbua tu mpaka lije kupona ni issue..
.

1652765927268.png
1652765984874.png
1652766213913.png


Standard Features kwa B6 ni Electronic Stability Programme (ESP) system, Hii inasaidia gari kuwa Stable pamoja na anti-lock braking system (ABS), ABS kama huijui niambie nikupe Link ya Kavishe Ujifunze, Pia kuna brake assist, and electronic brakeforce distribution (EBD)...
.
Kwa hii generation B6[2000-2006] kama unazipenda chukua kuanzia 2002++, Hapo ndo walifanya maboresho kuanzia kwenye body na machine wakiipa gari muonekano mzuri zaidi na engine zenye nguvu ila zikiwa zinatumia mafuta vizuri, Sasa twende kwa Dada ake B7...
.
B7 Hii ni generation ya 3 ikianza mwaka [2004-2009] na hapa kuna maboresho makubwa zaidi, tunaweza sema hapa imefanyika heavy facelifted. Front grille mpangilio wake ulibadirishwa ukawa mrefu gari ikapewa shape ya trapezoidal [Juu ndogo chini imejaa kama kiuno cha nyigu vile]..
.
1652766344079.png
1652766423749.png
1652766503750.png


Ukija kwa setting za kwenye steering zikawa revised, suspension zikaguswa pia, Infotainment ya hii B7 ni balaa tupu iko na option za kutosha. Kwanza pale kati chini kwenye gear umepewa access ya kumonitor option zote za gari ukiwa na screen kwa mbele inayokudirect...
.
Navigation system na chassis electronics [Vifaa vya umeme ambavyo viko mounted na chasis], Pamoja na Electronic Stability Programme (ESP) system viliboreshwa. Dashboard na Interiors hazikuguswa sana ila vilifanyiwa minor detailing[kupewa muonekana mzuri zaidi wa kuvutia]..
.
Engines nazo zilipata maboresho pia mwaka 2005 ndo ikaja TFSI kama nilivyooleza hapo nyuma before ilikua ni FSI, Yaani Fuel Stratified Injection bila Turbo, na hii ilifanyika kwa engine za 2.0 4 cylinder na 3.2 V6 Petrol Engine. Hapa na power output iliguswa pia ikawa na 197hp na 252hp..
.
Hizi engines zote zinatumia valve nne kwa cylinder moja, tofauti na engine za nyuma zilizokua na valve 5, Valve kwa lugha nyepesi kabisa ni kifaa juu ya cylinder kinachoratibu mchanganyiko wa hewa na mafuta ili kupata combustion..
.
1652766608523.png
1652766733358.png
1652766916062.png
1652766990841.png


Pia kuna 2.0 Turbocharged Direct Injection [TDI] diesel engine ikiwa combined na Pumpe Duse [Unit Injector} with 16 Valves. Wakati kubwa yake ya 2.5 TDI V6 Diesel engine ilikuwa superseded na 3.0 V6 TDI ikiwa inatoa 201 Hp na 2005 ikawa upgraded to 230Hp kwa model za 2006...
.
Audi ni moja ya gari ambayo huwa nawashauri wateja kama wanakaa miji mikubwa kama Dar/Mwanza/Arusha/Dodoma nk ndo wanunue. Ila kama uko Songwe au katavi huko upatikanaji wa mafundi na vipuri inaweza kuwa changamoto. Na kwa miji mikubwa hata mafundi ni kuwa nao makini usije kutana na Fundi Michael...
.
Audi ni Slay queen mrembo akiwa na urembo mwingi wa gharama za juu na hapendi shida. Kama una rough driving na barabara unazotumia ni za kimara Bonyokwa hii gari haifai. Gari inaweza kupa pressure Kama za Slay queen Birthday inatokea mara 4 kwa mwaka na umri uko hapo hapo..
.
1652767071078.png
1652767176329.png
1652767260757.png


Ila ni slay queen very reliable and durable ukimtunza, consumption yake ya mafuta ni nzuri sana ukija kwenye speed performance yake ni super. Kwenye Mafuta hapa inategemea na engine iliyofungwa lakini wasitani Audi A4 anatumia 5.8-6.1L/100K Yani anaenda 16.6-17.2Km/L...
.
Full Tank ni 54L acceleration yake ni sekunde 9 tu from 0-100Km, Sasa ukiangalia performance gari inayokupa haya matumizi ya ni mazuri tu. Kwenye maintenance iko poa sio ya kutisha though iko juu uki compare na toyota, Parts zake zinapatikana na bei sio mbaya sana...
.
Sema kama uchumi wako bado ni wa kuunga unga achana nayo hii gari inataka uchumi ulionyooka. Sio unapewa proforma invoice ya birthday unaanza kukumbuka birthday ya mwisho ilikua lini au unaona kama imejirudia ndani ya mwaka mmoja, Any way tuendelee...
.
Audi A4 matatizo common ni kuwasha warning light mara kwa mara sababu ya sensor nyingi [Ila hili sio tatizo gari nyingi za kisasa ziko hivyo] . Transmission issues ukitumia vilainishi sivyo na engine itasumbua kama ikikosa service . Hii gari haikopeshi wala haicarry forward..
.
Yani ukiipa vitu sivyo utapata majibu mapema tu, Muhimu kusoma Owners manual kupata taarifa muhimu za jinsi ya ku maintain gari na jinsi ya kui operate. Kwenye Engine na gear box hakikisha unatumia vilainishi OG ambavyo viko recommended na manufacture ku avoid matatizo ..
.
Engine nzuri ni za petrol under cc 2000 yani 2.0L, Hizi zote zinakupa Performance nzuri[speed/pooling]. Na pia they are easy to maintain kibongo bongo hasa kwa wadau wa uchumi wa join the chain. Ila kama unahitaji nguvu zaidi you can go for bigger engine za V6 zitakufaa..

1652767531344.png
1652768351704.png
1652769093865.png

.
Diesel engine they are a bit expensive and complicated kuzi maintain though ziko economy, Ndo maana kama umenotice Africa gari ndogo za diesel ni chache sana hata supplier wa nje wanalijua hili, Ila zinapatikana kama uko fresh mfuko uko vizuri you can opt them ziko poa pia...
.
Audi A4 Kama unahitaji kuagiza mpaka unaishika Price range ni 15-19M Kutokana na mwaka wa matengenezo plus features na condition ya gari husika. Kama unahitaji wasiliana nasi kwa number 0714547598 au Ofisini Kigamboni Kisiwani Kwa Mkorea mbele kama unaenda Kibada utakua sorted na hitaji lako litatimizwa ...
.
1652768805666.png
1652768896513.png
1652769004562.png

.
Tunafanya kazi na dealers wa Japan,UK, etc, dealers wanaotupa gari nzuri zenye ubora kwa ajili yako, Tutafanya machakato wako wa kupata gari kuwa salama na unaojali muda wako na unaokupa gari la thamani ya pesa yako. Kama uko mkoani unaweza agiza gari pia ukiwa huko huko...
.
Tupe hitaji lako na budget yako tutakushauri na kukutafutia gari kulingana na mahitaji yako na kipato chako, Ukiipenda utatumiwa invoice [at cost] utafanya malipo huko huko mpaka gari itafika ikiwa cleared unakuja kuchukua au unaletewa ulipo. Maana gari ukinunua kwa kukurupuka ni
.
Maana gari ukinunua kwa kukurupuka ni Liability moja mbaya sana ambayo itakunyonya damu wakati inakuchekea, Natumaini umejifunza kitu kama Jibu ni ndio basi unaweza share na wengine wapate haya Madini...
.
Asante sana
Samatime
Mob; 0714547598

1652765307912.png
 
TFSI hii ni mfumo unaotumika sana na engine za Audi [Petrol Engine] ukimaanisha turbo fuel stratified injection (TFSI). Yani turbo inakua introduced kwa mafuta yanayoingizwa kwa pressure katika combustion chamber na kuchoma instantly.

Simply tu....

TFSI ni Direct injection with turbo.

Ni kama D4 ya toyota uiongeze turbo.
 
Sasa Tofauti ya TSFI na TDI ni kwamba TSFI yuko faster Anachanganaya mapema na anakula mafuta zaidi na kumtunza ni rahisi...
.
Wakati TDI yeye ni mzito anatumia mafuta kidogo [economy] na ni gharama kumtunza ukilinganisha na mwenzake

Engine za Diesel hazijatengenezwa kwa ajili ya High revs hata dashboard zake zinajieleza clearly.

Angalia RPM ya gari ya petrol na RPM ya gari ya diesel hakuna usawa.

Ila nakuapia ukiitune engine engine ya Diesel. Basi engine ya petrol ni mchumba.
 
... Mkuu hebu fafanua japo kiduchu kuhusu D4 engines za Toyota; kuna ubishi mwingi miongoni mwa mafundi wa chini ya miembe kwamba ni injini za ovyo sana na hata gari ikiwa na aina hiyo ya injini kuuzika ni msala. Msaada tafadhali.
hahahahahah mafundi hawazipendi D-4 sababu hazitaki ubabaishaji kuanzia sheli mpaka kwenye oil zake. Pia zina mfumo wa umeme ambao haukawilii kuloga🤣
 
Back
Top Bottom