mng'ato
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 29,195
- 49,117
Ilirudishwa mkuu.ndiyo mkiambia hii nchi imechoka muelewe, siyo mnalalamika hapa halafu oktoba mnarudisha thithiem madarakani.
Ilirudishwa mkuu.ndiyo mkiambia hii nchi imechoka muelewe, siyo mnalalamika hapa halafu oktoba mnarudisha thithiem madarakani.
"Morning ndessa" siku hizi sizioni sana barabarani.Yupo sana anakaa usa, huyu ndiyo anawatia machungu wenzake coz huyu ni mfanyabiashara jumla, hiace zilizoandikwa ndesa ndiyo zake full wax saa kumi hesabu imetimia gari zinaoshwa.
Fuso za mchanga za kutosha, nyumba za kupanga usiseme lkn jamaa bado anakomaa na kupiga mkono magari na haachi hata buku.
Kumbe hii ya kupeleka hesabu ni ya kitambo tu,tangu awamu ya 4 wanapeleka hesabu bado hazija jaa tu?Aisee nilijua Dar tu kumbe mpaka A-TOWN. Siku moja nilikuwa kwenye hotel moja mitaa ya mbagala napata breakfast nikawasikia wanasema wameambiwa wapeleke faini makosa saba kila siku yaani sio chini ya 210,000/=Tsh kwa siku. Kwa usumbufu walio nao hawa jamaa ni lazima utembee na fedha mfukoni unapoendesha gari.
Hahah ila watu wenye roho ngumu wanadumu sana,tangu ameanza kulalamikiwa mpk leo anadunda tu mamaeee.Huyo mwenye matege ipo siku alitukamata akasema yy ana roho mbaya kama sura yake so hata tukimchukia haisaidii sababu anajijua yy ni mbaya
Wako watumiaji wa barabara ambao ni maafisa wa takukuru na usalama wa taifa na wanashuhudia vitendo hivyo
Hahah ila watu wenye roho ngumu wanadumu sana,tangu ameanza kulalamikiwa mpk leo anadunda tu mamaeee.
Jamaa juzi aliwaweza ngaramtoni ya chini
Inawezekana mkuu,maana amedumu sana aisee pamoja na malalamiko yote hayo.Labda anapeleka kamisheni kubwa kwa wakubwa
Mkuu hii thread ni ya zamani enzi za JK lkn mpk leo traffic ni kero tu.Hamjui kama xmas tar 25?
Huo ni uboya traffic police muache uonevu kwa maslahi binafsiHuwajui vizuri Trafiki wa Arusha wewe eeh?,watakugusa tu,labda uwe na mkonge tu ndo hutasumbuliwa,otherwise,watakushambulia wote na wanataka pesa yako kwa ulazima,hata kama ni kubambikiziwa kakitu.
Ok poa ila ndo tar zao barabarani kukamia madereva.Mkuu hii thread ni ya zamani enzi za JK lkn mpk leo traffic ni kero tu.
Ni kweli mkuu hizi tarehe ni noma sana aisee.Ok poa ila ndo tar zao barabarani kukamia madereva.
Siku zote najiuliza hivi hii takukuru yetu huwa inang'ata mpaka ipewe amri ?Wakuu naandika hii maada nikiwa na hasira isiyozuilika.
Hata kama Ni usalama wa barabarani sasa huu ni upumbavu.Rushwa imekuwa logo yao ya kazi hata kama unakila kitu kwenye gari.Imefikia hatua kama huna hela Arusha kamwe hutaendesha gari hata kama gari lingekuwa jipya hutothubutu.Mbaya zaidi kama unatokea kisongo unaenda Kia imekula kwako kila mita 600wapo.
Anzia uwanjani Kisongo wapo,TANAPA,kona Mbauda,mataa ya Esso,kona ya TCA,Mianzini,Sanawari,kwa Mrefu,Daraja la Nduruma,,shamba la mbegu,Kilala,Makumira university,Usa River ,Maji ya Chai,Kikatiti,Funga kazi Ni King'ori kuna kadada kana miguu kama vibua kapenda rushwa mbaya na kengine kana matege kapo Arusha mjini hako ndo kiboko,nafikiri Arusha inaongoza Kwa kuwa na matrafiki wengi kuliko maaskari wa kawaida.
Kilichobaki ni kuwalipua kwenye vyombo vya habari au kuchukuwa hatua mkononi tu,tumechoka.Siku hizi mimi huwa sisimami kabisa.Haya matrafiki yana njaa kama dumuzi.
Sasa wanajamvi tuwachukulie hatua gani zingine za ziada kukomesha upuuzi huu maana mimi naweza kuja vunja mtu miguu.
Nina hasira sana.