Hi mambo nipe number yako basi

Hi mambo nipe number yako basi

Unamwambia akupe yake utamtafuta,hapo ndo asahau o unaweza mnyima kistaarabu tu
 
Huwezi kuombwa namba kama sio mzuri na zaidi huoneshi dalili ya kukataa iwapo utatongozwa.

Wanawake wengi Simu zao ziko ki-kazi zaidi...!

Hapa mnajivunga tu....!!

Huyohuyo uliyempa namba yako, akimaliza maongezi tu, utasikia...."NITUMIE VOCHA BASI"...!!
 
ukiwanyima eti wanasema umepiga teke bakuli la mshahara (husband material)

hivi kwa styl hiyo hata nikikukubali uwe mume inamaana umejaza costa kwakutonfoza hivo na ni kiashiria kwamba tupo wengi.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hii tabia unakutana na mtu kwenye bus mnasalimiana tu baada ya hapo anaomba number ya simu. Hata kanisani unakuta na mtu mnasalimiana hasa wanaume anaomba number. Kwenye seminar, mnamaliza tu seminar unaombwa bumber.

Kwa mtazamaji wangu kutoa number ni kama kumpa mtu go ahead ya mtongozo.

Mnakionaje hili?
Kwani kuna shida gani?mbona hata wapaka kucha rangi mnawapa bila kuomba?
 
Huyo wa kanisani anaomba kwa nia njema ili muhendeleze maombia.
 
Inakera kweli mi niilikuwa nasafiri kutoka moshi kuja dar, nilikaa na kaka mmoja alinisumbua mpk niliona gari linapunguza mwendo ukikaa kimya anakuforce kuongea mby zaidi alikuwa ananuka mdomo.
Bahati nzuri basi lilikuwa halijajaa nikajihamisha taraatibu akanifata tena ananishika nilimropokea mropoko mmoja abiria wote wakanitolea machoo mwenyewe aliondoka akarudi kukaa kwenye siti yke...alikuwa km jambazi anatishaaa hatar
 
Mtongozo kuikubali au kuikataa ni uamuzi na msimamo wa mtu. Vile vile namba kuitoa ni uamuzi wa mtu, uzuri huwa wanaomba na si kulazimisha!!!
Nmekupenda bureeee kwa point yako!!! Naomba namba yako....
 
Sasa mungu katukutanisha leo tusipopeana namba si ndio itakuwa hatuonani tena tutarudi dunia ya nyerere ya jioni anapitaga pale hujui leo kapata Lav 4 kapita juu kwa ju namba ndio mpango mzima usisite kutoa namba bahati na majuto vinaanzia hapo wewe hujui yako ipi
 
NYIE AKILI YENU IMEKAA UKISALIMIWA...UKIOMBWA NAMBA...UKIPIGWA...MTU ANAKUTAKA ATAKUTONGOZA....MUEGE NA POSITIVITY SOMETIMES...
 
Hakuna ubaya unampa tu namba aisee, kama huhitaji mtongozo wake unampa namba ya gari tu, kisha unamwambia simu yangu haina charge nitafute badae basi hivyo tu yaan ya nn kuumiza kichwa kwa kitu ambacho huhitaji
Kwan kuna no cm inaanza T
 
Ukiona wanaume wa kila aina wanakuomba omba no ovyo ovyo ujue huna value. Sisi wanaume huwa tunaogopa kuomba nu kwa mwanamke anayeonekana anajiheshimu na nzuri. Sasa wewe mtu kakuona sekunde mbili tu kakuomba number ujue kaisha kudegrade na kakuona wewe mwepesi sana.
Ukiona demu anaombwa no hovyohovyo ujue analipa na kila me anataman ampate lkn ndo hivo tena.......
 
Back
Top Bottom