Hebu Kwanza: Hawa Saudi Arabia Vipi?

Hebu Kwanza: Hawa Saudi Arabia Vipi?

Uko sawa kwa kiwango kikubwa, lakini Kusema kuwa wananunua silaha kwa sababu ya sera na sio mahitaji ni generalisation isio sahihi kabisa.

Threats alizonazo Saudi kutoka kwa Yemen, Iran n.k, ndio zinampelekea anunue silaha kwa Marekani., so wananunua silaha sio kwa sera bali ni mahitaji halisi ya kijeshi
Sasa mahitaji ndiyo hayo sasa ya kukabiliana na hao Houthi, sasa ni kipi kinachomliza wakati silaha zote anazo!

Maelezo ya T 14 yanashawishi sana kutokana na hali inavyojionyesha sasa hivi.
 
Kama ni sera mbona hawanunui silaha muhimu za Urusi au China?
Ngoja nikupe mfano wa silaha ambazo Saudi anaweza nunua nje na hajanunua.

1. Saudia hana class ya drones ambazo Turkey anazo ila US hana. Hizo zingemsaidia sana tu, maana Israel anazo kama Heron ila Saudia hawezi miliki Israeli made weapons systems.

2. Saudia angeweza kununua air defense systems za China especially HQ-9 family ila itamgombanisha na Marekani. Hii ingesaidia kuwa na integrated air defense badala kumtegemea Marekani kama Mungu. What if mfumo ukawa penetrated au US ikamuwekea sanctions maana yake miundombinu ya mafuta ikae wazi?

3. Saudia anahitaji ndege kama Su-34 ya Urusi ambayo ni fighter bomber kwa mazingira yake hapo jangwani na maadui zake hivyo vikundi. Badala yake hawezi nunua anabaki na ndege kama F-15 na Typhoons.

4. Saudi inahitaji anti drones systems kutoka nchi mbali mbali hata China ila inajiogopa ogopa. Inasubiri solutions kutoka US pekee, au kidogo Europe au ndani ya NATO ila haiko huru kuchagua.

Kaone inachofanya Egypt. Haipangiwi, leo inanunua ndege Ufaransa, kesho inanunua US, keshokutwa inajadiliana na China, juzi iliongea na Urusi. Hii ni kuzuia siku inapigana na Israel isitokee Marekani ikazuia supply kwa silaha ilizotengeneza kama ilivyofanya kwa Iran wakati Saddam Hussein anawavamia.
Game theory in action , I aonekane saudia hajielewi hii nadharia ya mchezo , au wakati anakubali ndoa na us hakuwa na uelewa huo , akuanticipate a future .
 
Jeshi la Saudi Arabia ni model sawa na jeshi la Libya ya Gaddafi na jeshi la Syria ya Bashar al Assad.

Kuna tawala ambazo majeshi yao kuwa na nguvu sio kipaumbele, bali kipaumbele ni majeshi yao kuwa watiifu. Kwahiyo tawala hizo hufanya sabotage kuhakikisha majeshi hayawi na nguvu, uhuru, akili, uongozi shupavu na utayari wa vita ili kusitokee mapinduzi.

Vikosi competent pekee huwa ni kikosi cha kulinda serikali, bunge, mahakama na ikulu na wale protection unit ya kiongozi wa nchi. Hizo special forces pekee ndio huwa imara kila kona na huongozwa na the most trusted people kama mabinamu na wapwa wa watawala.

The rest ni vikosi oya oya mafunzo sifuri, coordination hamna, utayari hamna, na vinaongozwa na machawa tu wala sio makamanda wenye uwezo.

Model hiyo ya jeshi huwa inanunua silaha nyingi kumtisha adui wa nchi jirani aogope kuleta uchokozi. Na huwa majeshi hayo yanakwepa sana confrontation za nje ili uwezo wake usijulikane waziwazi. Huwezi wasikia sijui wamelinda amani au wameshiriki joint task force, sana sana Saudi Arabia itatuma hela, inunue silaha kisha nchi maskini zinazojiamini ndio zitumie huo msaada kwenye kulinda amani.

Mara ya mwisho Gaddafi anajaribu kumsaidia Iddi Amin majeshi yake yalipigwa na JWTZ. Ni majeshi njaa yaliyokuwa na sifa nilizotaja hapo juu, ila yana silaha nzuri.
Vilevile Gaddafi alishindwa vita ya Chad wakati Chad ni maskini tu na Jenerali Derby akiongoza vikosi kwa silaha nyepesi kabisa. Gaddafi na kuvaa magwanda kila siku maisha yake yote hajawahi pigana vita yoyote akashinda.

Ambacho hayo majeshi yanajua vizuri ni kupiga raia. Wana mbinu za kila aina za kupiga raia na kukamata watu, jambo ambalo majeshi kama ya UK au France yanaweza fundishwa nao.

Vilevile ni sera ya Saudi Arabia kununua silaha nyingi kwa washirika kwa makubaliano italindwa. Last time inakaribia kuvamiwa alikuwa ni Saddam Hussein aliyekuwa na silaha nyingi na jeshi la kawaida tu, alivyoivamia Kuwait na kukaribia kuivamia Saudia ambayo haikuwa na silaha kabisa ndipo Mfalme wa Saudi akaanzisha defense policy ya kununua silaha nyingi na kuweka kambi za superpower ili jirani mwenye fujo aogope kukuvamiwa.

That policy worked well, mpaka Iran ilipopata makombora na drones makundi kama Houthi yakapewa.
Naam ,nje ya mada hivi hipi ni superior power ya jeshi la kagame ni ipi na je sifa inazomwagiwa ni hype tu au ni kweli ndiyo jeshi tishio Afrika mashariki?

Na pia ningependa kufahamu sifa ya JWTZ
 
Houthi wamefugwa mpaka kufikia hapa. Ni sawa na Nigeria ilivyowafuga Boko Haram na kujiendekeza.

Kitu kingine, ni rahisi zaidi kushambulia kuliko kujilinda. Na haijawahi tokea popote duniani silaha ya kushambulia ikawa na bei kubwa kuliko silaha ya kujilinda.

Unaweza kusoma hadi ukawa Professor kwa kutumia mamia ya mamilioni, nikakuua kwa sumu ya panya inayouzwa mia tano. Ila ili uhakikishe chakula chako hakitiwi sumu hata ya panya au ikiwemo ijukikane ni teknolojia inayotumia mamilioni vilevile.
Ww jamaa ndo tatizo lako ,yaani wauthi walio pambana na karibia na mataifa yote ya Kiarabu Kwa miaka 8,kavumilia mashambulizi ya marekani na uingereza Kwa zaidi ya mwezi, wakavumilia mashambulizi ya Israel leo hii wapo wanaipelekea moto saudia utasemaje walifungwa na kuendelezwa?

Kabla ya kuibeza Saudia kwanza tuambie hiyo marekani yenyewe ambaye ndo mwenye hizo silaha zimemsaidia nn mpaka Sasa kwenye vita yake na Iran.
Marekani ana Kila aina ya rundo la mifumo ya ulinzi na mifumo ya hapo mashariki ya kati mbona kambi zake zimefumuliwa na kuharibiwa na vidrone uchwara vya Iran?

Hoja hapa ni kuwa dunia ya sasa vita imebadilika sana.
 
Mkuu...
Umeeleza upande mmoja tu, kwamba jeshi la Saudia ni dhaifu tokana na suala zima la kisiasa...

Lakini kuna mambo muhimu ya kuzingatia ...
Hebu tuzungumzie pia mbinu za kivita, usaidizi wa silaha na teknolojia kutoka Iran...

Pia Houthis wanapata intel, mafunzo , silaha , vipuri n.k kutoka Iran...
Iran imewapa Houthis teknolojia ya wao wenyewe kutengeneza makombora na drones, Saudia wao wanategemea interceptor za patriot zinazogharimu mamilioni ya dollar kutoka US...

Iran inafahamika vyema kwa mbinu za kivita hasa kutumia silaha na mbinu za gharama nafuu lakini zenye madhara makubwa...

Ni kweli jeshi la Saudia ni dhaifu, lakini Houthis pia wapewe credit, wapo vizuri kimbinu na kivita...

Hata Israel na jeshi lake imara wanapelekana sana na Hezbollah achilia Hamas...
Mkuu kwanza kuachane na Saudia je huyo Marekani mwenye hizo silaha zimemsaidia nini kwenye vita yake na Iran?
 
Kuna nchi duniani inayowashinda waSaudi katika ununuzi wa silaha za kivita, silaha za kisasa kabisa!

Sasa hawa wa Houthi wanapata wapi hata uthubutu tu wa kuzozana na Saudi Arabia kiasi kwamba makombora yanapigwa hadi ndani mwa Riadh, na nusra mengine yaende Mecca!

Kwa nini Saudi walielie na kuomba msaada kukabiliana na hawa Houthi. Kuna nini kinatokea hadi hali iwe tete kiasi hiki?
Kwani wakiandaa vidola kama bilioni mbili hivi, akina Lucas Mwashamba, Tlaatlaah hawawezi kweli kwenda kutoa msaada huko na kutuacha nasi hapa JF tupate hewa kidogo?
Houthi kisilaha wanaunda silaha kupitia teknolojia ya Iran. Na wanaunda kila aina ya silaha zenye ufanisi. Wale sio bokoharam au alshabab wanaopigana kwa silaha za kuunga unga. Houthi ni sawa na Iran mtoto kisilaha na kivita.
 
Kuna nchi duniani inayowashinda waSaudi katika ununuzi wa silaha za kivita, silaha za kisasa kabisa!

Sasa hawa wa Houthi wanapata wapi hata uthubutu tu wa kuzozana na Saudi Arabia kiasi kwamba makombora yanapigwa hadi ndani mwa Riadh, na nusra mengine yaende Mecca!

Kwa nini Saudi walielie na kuomba msaada kukabiliana na hawa Houthi. Kuna nini kinatokea hadi hali iwe tete kiasi hiki?
Kwani wakiandaa vidola kama bilioni mbili hivi, akina Lucas Mwashamba, Tlaatlaah hawawezi kweli kwenda kutoa msaada huko na kutuacha nasi hapa JF tupate hewa kidogo?
Inaitwa assymetric warfare, Houthi hawapigani na Saudi Arabia kwa vita standard za kawaida...ni vita ya kuvizia, kupiga na kujificha kwa kutumia silaha za bei Chee kama drones na rockets, unakuta wanajificha katikati ya raia au kwenye mapango au milima jangwani, na wanalenga miundombinu ya kiuchumi sio l jeshi
So Saudi Arabia yeye kupigana nao inatakiwa awalenge wao sio miundombinu ya kiuchumi ya Yemeni au makazi ya raia ambalo wanajificha, ama itanoekana anafanya ugaidi, ndio maana vita Inakuwa ngumu kwa Saudia
 
Usianzishe ugomvi wa mawe na huku unaishi nyumba ya vioo.
Wahouth hawana cha kupoteza wale, Saudia inapigana nae kimbinu zaidi ya kutumia manguvu..
 
Inaitwa assymetric warfare, Houthi hawapigani na Saudi Arabia kwa vita standard za kawaida...ni vita ya kuvizia, kupiga na kujificha kwa kutumia silaha za bei Chee kama drones na rockets, unakuta wanajificha katikati ya raia au kwenye mapango au milima jangwani, na wanalenga miundombinu ya kiuchumi sio l jeshi
So Saudi Arabia yeye kupigana nao inatakiwa awalenge wao sio miundombinu ya kiuchumi ya Yemeni au makazi ya raia ambalo wanajificha, ama itanoekana anafanya ugaidi, ndio maana vita Inakuwa ngumu kwa Saudia
ACHA UONGO. Houthi hawajifichi katikati ya raia kama unavyodai. Houthi wanapigana direct confrontational war na majeshi mamluki ya Saudi Arabia. Mocha na Haiyz zilichukuliwa kwa mtutu wa bunduki wa cross fire. Kiufupi Houthi amewazidi mbinu za kivita Saudi Arabia ila USITUDANGANYE eti houthi wanajificha nyuma ya raia ACHA UONGO.
 
Mkuu...
Umeeleza upande mmoja tu, kwamba jeshi la Saudia ni dhaifu tokana na suala zima la kisiasa...

Lakini kuna mambo muhimu ya kuzingatia ...
Hebu tuzungumzie pia mbinu za kivita, usaidizi wa silaha na teknolojia kutoka Iran...

Pia Houthis wanapata intel, mafunzo , silaha , vipuri n.k kutoka Iran...
Iran imewapa Houthis teknolojia ya wao wenyewe kutengeneza makombora na drones, Saudia wao wanategemea interceptor za patriot zinazogharimu mamilioni ya dollar kutoka US...

Iran inafahamika vyema kwa mbinu za kivita hasa kutumia silaha na mbinu za gharama nafuu lakini zenye madhara makubwa...

Ni kweli jeshi la Saudia ni dhaifu, lakini Houthis pia wapewe credit, wapo vizuri kimbinu na kivita...

Hata Israel na jeshi lake imara wanapelekana sana na Hezbollah achilia Hamas...
Hezbollah na Hamas karata Yao kuu ni kujificha katikati ya raia, Israel ipate wakati magumu kuwashambulia, akishambulia apate lawama anajua watoto,
 
Leo wameona drone ya wahouthi ikipita kwenye msikiti wao pendwa tena haijafanya kitu ikashuka kidogo kisha ikaenda zake😆😆😆😆😆😆😆😆😆
Wameiomba dunia iwasaidie maana Allah wao hakufanya chochote
 
Sasa maslaha ya mabilioni yananunuliwa ya nini, kutishia watu au?

Kwa kweli inashangaza sana hawa Saudia kulizwa kiasi hiki na Hothi.

Jambo jingine linaloshangaza ni vipi washirika wa Saudi, Turkey na Pakistani, mbona hawaji kusaidia?
Uwezo wa mapigano ni pamoja na kuwa na askari wenye moyo wa kupigana,udhoefu wa mapigano,uongozi imara,uzalendo mkuu hao washirika wapo kimaslahi zaidi wanaogopa kujiingiza kwenye vita ambavyo vitaharibu uchumi wao
 
Inaitwa assymetric warfare, Houthi hawapigani na Saudi Arabia kwa vita standard za kawaida...ni vita ya kuvizia, kupiga na kujificha kwa kutumia silaha za bei Chee kama drones na rockets, unakuta wanajificha katikati ya raia au kwenye mapango au milima jangwani, na wanalenga miundombinu ya kiuchumi sio l jeshi
So Saudi Arabia yeye kupigana nao inatakiwa awalenge wao sio miundombinu ya kiuchumi ya Yemeni au makazi ya raia ambalo wanajificha, ama itanoekana anafanya ugaidi, ndio maana vita Inakuwa ngumu kwa Saudia
Hii ya kujificha kwa raia mshaifanya ndio sababu ya kujificha kushindwa kwenu mzee
Marekani aliripua shule pale iran napo vipi walijificha majeshi
Karipua juzi tu karipua sherehe napo vipi kulikua na jeshi
Karipua miundo mbinu napo vipi mzeee
Kiufupi saudia hana tofauti na bwana wake marekani wameshindwa kujilinda mbele ya hao wamba!!!
 
Ww jamaa ndo tatizo lako ,yaani wauthi walio pambana na karibia na mataifa yote ya Kiarabu Kwa miaka 8,kavumilia mashambulizi ya marekani na uingereza Kwa zaidi ya mwezi, wakavumilia mashambulizi ya Israel leo hii wapo wanaipelekea moto saudia utasemaje walifungwa na kuendelezwa?

Kabla ya kuibeza Saudia kwanza tuambie hiyo marekani yenyewe ambaye ndo mwenye hizo silaha zimemsaidia nn mpaka Sasa kwenye vita yake na Iran.
Marekani ana Kila aina ya rundo la mifumo ya ulinzi na mifumo ya hapo mashariki ya kati mbona kambi zake zimefumuliwa na kuharibiwa na vidrone uchwara vya Iran?

Hoja hapa ni kuwa dunia ya sasa vita imebadilika sana.
Marekani mara ya mwisho kuwa in a state of war ni 1945.

Ni sawa na Tanzania ipeleke kikosi cha wananajeshi 120 Congo, wakutane na waasi 2,800 wa M24. Waasi wawapige wanajeshi wa Tanzania kisha utoke ushikikie bendera kwamba M24 wameishinda vita Tanzania. Wakati Watanzania waliopo Namtumbo hawajui hata kama kuna mapigano, huku watu wa M24 wamejimaliza, wamejitutumua mpaka mwisho kuwa wana vita kali sana.

Iran ilipigana vita ya kujimaliza. Vita ambayo imemuua Ayatollah, mkuu wa usalama wa taifa, mkuu wa Airforce, mkuu wa Army, Chief of Staff, mkuu wa makombora, maofisa wengine wengi sana. Ila Marekani hata declaration ya vita haina, hata Congress haijawahi kaa kikao special kujadili vita.

Saudi Arabia vile vile. Haijawahi kuwa na declaration ya vita dhidi ya Houthi. Tufanye Houthi wawe taifa la Yemen lote. Kisha waingie vitani na nchi jirani hapo ndio utasema wanaweza ila sio kujificha mbele ya raia ili nchi inayochokozwa ikipiga na kuporomosha majengo mtoe vilio kwamba inafanya genocide kama mnavyoilaumu Israel. Hapo ikiachwa mseme inapigana na mataifa mengi.

Taleban walikuwa hivi hivi wanaonekana wanajua wakati Afghanistan ina serikali. Wanapigania uraiani wamevaa kanzu kutoka msikitini, ukiwapiga unaua raia wasio na hatia. Baada ya kuchukua madaraka ni jeshi moja disorganized vibaya mno haliwezi pigana na jirani yeyote pale. Pakistan, Iran, Turkmenistan, Uzbekistan, Tajikistan na China wote hawa ni majirani wa Afghanistan ambao hawezi wapiga.

Kuwa gaidi au ni jambo jepesi sana. Kurusha bomu sokoni ukiwa umevaa jezi na umeshikilia begi la mitumba ni rahisi, twende sasa uvae sare za jeshi na uheshimu sheria za vita ushambuliane na jeshi la adui na upige military targets tu uone mziki wake.

Kwa akili zako ulitaka Houthi wakishambulia miundombinu ya mafuta, basi na Saudi Arabia ishambulie fuel depots za Yemen?
Hiyo tit for tat anaiweza Israel tu, unashambulia kutokea andaki lililopo shuleni, anashusha shule nzima ya watoto 300 ili abomoe andaki lenye makombora 10.
 
Back
Top Bottom