Jeshi la Saudi Arabia ni model sawa na jeshi la Libya ya Gaddafi na jeshi la Syria ya Bashar al Assad.
Kuna tawala ambazo majeshi yao kuwa na nguvu sio kipaumbele, bali kipaumbele ni majeshi yao kuwa watiifu. Kwahiyo tawala hizo hufanya sabotage kuhakikisha majeshi hayawi na nguvu, uhuru, akili, uongozi shupavu na utayari wa vita ili kusitokee mapinduzi.
Vikosi competent pekee huwa ni kikosi cha kulinda serikali, bunge, mahakama na ikulu na wale protection unit ya kiongozi wa nchi. Hizo special forces pekee ndio huwa imara kila kona na huongozwa na the most trusted people kama mabinamu na wapwa wa watawala.
The rest ni vikosi oya oya mafunzo sifuri, coordination hamna, utayari hamna, na vinaongozwa na machawa tu wala sio makamanda wenye uwezo.
Model hiyo ya jeshi huwa inanunua silaha nyingi kumtisha adui wa nchi jirani aogope kuleta uchokozi. Na huwa majeshi hayo yanakwepa sana confrontation za nje ili uwezo wake usijulikane waziwazi. Huwezi wasikia sijui wamelinda amani au wameshiriki joint task force, sana sana Saudi Arabia itatuma hela, inunue silaha kisha nchi maskini zinazojiamini ndio zitumie huo msaada kwenye kulinda amani.
Mara ya mwisho Gaddafi anajaribu kumsaidia Iddi Amin majeshi yake yalipigwa na JWTZ. Ni majeshi njaa yaliyokuwa na sifa nilizotaja hapo juu, ila yana silaha nzuri.
Vilevile Gaddafi alishindwa vita ya Chad wakati Chad ni maskini tu na Jenerali Derby akiongoza vikosi kwa silaha nyepesi kabisa. Gaddafi na kuvaa magwanda kila siku maisha yake yote hajawahi pigana vita yoyote akashinda.
Ambacho hayo majeshi yanajua vizuri ni kupiga raia. Wana mbinu za kila aina za kupiga raia na kukamata watu, jambo ambalo majeshi kama ya UK au France yanaweza fundishwa nao.
Vilevile ni sera ya Saudi Arabia kununua silaha nyingi kwa washirika kwa makubaliano italindwa. Last time inakaribia kuvamiwa alikuwa ni Saddam Hussein aliyekuwa na silaha nyingi na jeshi la kawaida tu, alivyoivamia Kuwait na kukaribia kuivamia Saudia ambayo haikuwa na silaha kabisa ndipo Mfalme wa Saudi akaanzisha defense policy ya kununua silaha nyingi na kuweka kambi za superpower ili jirani mwenye fujo aogope kukuvamiwa.
That policy worked well, mpaka Iran ilipopata makombora na drones makundi kama Houthi yakapewa.