Hebu Kwanza: Hawa Saudi Arabia Vipi?

Hebu Kwanza: Hawa Saudi Arabia Vipi?

Hezbollah na Hamas karata Yao kuu ni kujificha katikati ya raia, Israel ipate wakati magumu kuwashambulia, akishambulia apate lawama anajua watoto,
Si kweli...
Israel ilizidiwa mbinu na Hamas...
Kama Hamas wanajificha katikati ya raia, wale mateka wa Israel waliofichwa ndani ya Gaza na Hamas... nao walikuwa wamefichwa katikati ya raia?

Inakuwaje walitafutwa ikashindikana kuwapata, kama wangelikuwa miongoni mwa raia, kwa intel ya Israel na walivyojaza MOSSAD ndani ya Gaza, basi wale wangepatikana tu...

Sasa nikuulize kama Hamas waliweza kuficha mateka huko kusikojulikana na intel yote ya Israel wakashindwa kuwapata, je Hamas wao kama wao wanashindwa pia kujificha kusikojulikana kama hao mateka....

IDF imezidiwa mbinu kwa kiasi kikubwa, ukisema wapambane vita ya ardhini na hivyo vikundi jeshi la IDF litapoteza askari wengi sana na ushindi hutopatikana...

The only way, ni kuua raia na kupiga makazi ya watu hasa pale wanapoona mchezo ni mgumu ili kupelekea ceasefire kwa lazima na pengine kufanya adui aogope....

Mfano vita ya Hezbollah, IDF inaua raia, hii imepelekea jeshi la serikali kuingia mtafaruku na Hezbollah.. ndivyo Israel inachofanya.... airforce ndio wanachotegemea , tofauti na hapo ni weupe sana...
 
Mkuu kwanza kuachane na Saudia je huyo Marekani mwenye hizo silaha zimemsaidia nini kwenye vita yake na Iran?
Zimempa hasara tu...
Huwezi kuamini kwamba US imechelewa kutambua kwamba vita imebadilika...

Silaha zake luxury, gharama na anazo zipigia chapuo ili kuziuza na kutengeneza uchumi it's finally zimekosa majibu mbele ya mbinu za kivita na silaha za waajemi...

Niseme tu silaha za Iran zimeonekana effective na superior kuliko silaha za kimarekani kwenye hio vita...
 
Kupigana vita na makundi ya Aina ya houthi nk sio kazi rahisi kama watu wanavyofikiri, makundi ya Aina ile Kwanza silaha Yao kubwa ni kuishi na jamii, hakuna namna Utaweza kuwashinda Hadi pale utakapoamua kuua na kutesa watu wengi wasio na hatia. Ili uue mmoja itakubidi uue au kutesa wasio na hatia Mia moja na Saudi Arabia hayuko tayari Kwa Hilo.

US, Israel na ubabe wao wote wa teknolojia wameua watu wengi wasio na hatia kuliko idadi ya wanachama wa hivyo vikundi katika kupambana vita na hao Magaidi, Israel yeye ndio kabisa anapiga Tu makombora as long akipata taarifa kuwa mahali Fulani wako Magaidi basi anafumua Tu haijalishi kuna Nani. Yani mentality ya kupambana na ugaidi inatofautina baina ya Mataifa.

Kingine ni kwamba Saudi Arabia anategemea Sana taarifa za kijasusi kutoka Israel, US. Mfumo wa ukusanyaji taarifa wa kiitelijensia wa Saudi Arabia hauko imara, uko compromised Sana Kwa maana ya kwamba Hapa Katikati kabla hujafika kule juu wako maafisa Wana target na malengo binafsi yanayosukumwa na Imani za kidini, tofauti za mitazamo ya kisiasa na kiutawala nk, hawako pamoja na ndani ya hiyo hiyo Intelligent ring kuna Israel assets ambao wanahujumu humo ndani ili instability iendelee kuwepo iwape Faida ya kusonga mbele...Kumbuka hapo hapo ndani ya Saudi Arabia wapo wahafidhina wanasapoti harakati wanazofanya Houthi na pesa wanazo kama kawaida....

Kingine cha mwisho vita ni gharama na inaua uchumi, Saudi Arabia hayuko tayari kuharibu uchumi wake. Saudi Arabia Hana ubavu wa kuvumilia mashambulizi ya Houthi bila msaada wa US na US kachomoa kwenye Hilo so kaamua atulie tu.
 
Marekani mara ya mwisho kuwa in a state of war ni 1945.

Ni sawa na Tanzania ipeleke kikosi cha wananajeshi 120 Congo, wakutane na waasi 2,800 wa M24. Waasi wawapige wanajeshi wa Tanzania kisha utoke ushikikie bendera kwamba M24 wameishinda vita Tanzania. Wakati Watanzania waliopo Namtumbo hawajui hata kama kuna mapigano, huku watu wa M24 wamejimaliza, wamejitutumua mpaka mwisho kuwa wana vita kali sana.

Iran ilipigana vita ya kujimaliza. Vita ambayo imemuua Ayatollah, mkuu wa usalama wa taifa, mkuu wa Airforce, mkuu wa Army, Chief of Staff, mkuu wa makombora, maofisa wengine wengi sana. Ila Marekani hata declaration ya vita haina, hata Congress haijawahi kaa kikao special kujadili vita.

Saudi Arabia vile vile. Haijawahi kuwa na declaration ya vita dhidi ya Houthi. Tufanye Houthi wawe taifa la Yemen lote. Kisha waingie vitani na nchi jirani hapo ndio utasema wanaweza ila sio kujificha mbele ya raia ili nchi inayochokozwa ikipiga na kuporomosha majengo mtoe vilio kwamba inafanya genocide kama mnavyoilaumu Israel. Hapo ikiachwa mseme inapigana na mataifa mengi.

Taleban walikuwa hivi hivi wanaonekana wanajua wakati Afghanistan ina serikali. Wanapigania uraiani wamevaa kanzu kutoka msikitini, ukiwapiga unaua raia wasio na hatia. Baada ya kuchukua madaraka ni jeshi moja disorganized vibaya mno haliwezi pigana na jirani yeyote pale. Pakistan, Iran, Turkmenistan, Uzbekistan, Tajikistan na China wote hawa ni majirani wa Afghanistan ambao hawezi wapiga.

Kuwa gaidi au ni jambo jepesi sana. Kurusha bomu sokoni ukiwa umevaa jezi na umeshikilia begi la mitumba ni rahisi, twende sasa uvae sare za jeshi na uheshimu sheria za vita ushambuliane na jeshi la adui na upige military targets tu uone mziki wake.

Kwa akili zako ulitaka Houthi wakishambulia miundombinu ya mafuta, basi na Saudi Arabia ishambulie fuel depots za Yemen?
Hiyo tit for tat anaiweza Israel tu, unashambulia kutokea andaki lililopo shuleni, anashusha shule nzima ya watoto 300 ili abomoe andaki lenye makombora 10.
Saudia ,UAE na wale waarabu pale gulf states... hakuna ambae ana jeshi la maana...

Saudia na UAE kuna askari wengi mamluki, hao mamluki wakiondoka ndipo jeshi litakuwa sawa na migambo wa jiji kimafunzo na uwezo....

Hao waarabu waambie kula tende na kuendesha Lamborghini, kukimbiza magari jangwani na kuishi maisha ya starehe... ni wazito na wana vitambi na utapiamlo kwa ajili ya kula biriani za ngamia na vyakula vitamu vitamu...

Hakuna jeshi hapo UAE, Qatar , Saudia wanategemea zaidi mamluki, ndio maana baada ya Houthis kuwapiga kidogo wanaomba msaada...

Nashangaa mnamumunya maneno, silaha hazisaidii chochote kama askari ni mdebwedo...

Vijana ambao walipaswa wawe wakakamavu, wabishi na wenye uzalendo... wao wanatambua starehe tu, mambo laini laini...

Hapo UAE vijana wa hapo ndipo utashangaa na hizo kanzu zao, ni wanywa whiskey za gharama na wine, malaya na wanavuta unga, wakute kwenye yacht party zao, ama kwenye majumba yao... wakila shisha huku wamezungukwa na wanawake..

Ji Wanafiki tu hao...

Taifa lenye vijana kama hao hawawezi kupambana na jeshi la Iran lenye vijana wazalendo, wakakamavu, wenye elimu na walizoea mazingira magumu , nasema wamezoea mazingira magumu sababu Iran ipo kwenye vikwazo kwa karibu miaka 50, vijana ambao wapo active jeshini na wenye nguvu kazi wengi wamezaliwa kipindi nchi inapitia vikwazo...
 
Marekani mara ya mwisho kuwa in a state of war ni 1945.

Ni sawa na Tanzania ipeleke kikosi cha wananajeshi 120 Congo, wakutane na waasi 2,800 wa M24. Waasi wawapige wanajeshi wa Tanzania kisha utoke ushikikie bendera kwamba M24 wameishinda vita Tanzania. Wakati Watanzania waliopo Namtumbo hawajui hata kama kuna mapigano, huku watu wa M24 wamejimaliza, wamejitutumua mpaka mwisho kuwa wana vita kali sana.

Iran ilipigana vita ya kujimaliza. Vita ambayo imemuua Ayatollah, mkuu wa usalama wa taifa, mkuu wa Airforce, mkuu wa Army, Chief of Staff, mkuu wa makombora, maofisa wengine wengi sana. Ila Marekani hata declaration ya vita haina, hata Congress haijawahi kaa kikao special kujadili vita.

Saudi Arabia vile vile. Haijawahi kuwa na declaration ya vita dhidi ya Houthi. Tufanye Houthi wawe taifa la Yemen lote. Kisha waingie vitani na nchi jirani hapo ndio utasema wanaweza ila sio kujificha mbele ya raia ili nchi inayochokozwa ikipiga na kuporomosha majengo mtoe vilio kwamba inafanya genocide kama mnavyoilaumu Israel. Hapo ikiachwa mseme inapigana na mataifa mengi.

Taleban walikuwa hivi hivi wanaonekana wanajua wakati Afghanistan ina serikali. Wanapigania uraiani wamevaa kanzu kutoka msikitini, ukiwapiga unaua raia wasio na hatia. Baada ya kuchukua madaraka ni jeshi moja disorganized vibaya mno haliwezi pigana na jirani yeyote pale. Pakistan, Iran, Turkmenistan, Uzbekistan, Tajikistan na China wote hawa ni majirani wa Afghanistan ambao hawezi wapiga.

Kuwa gaidi au ni jambo jepesi sana. Kurusha bomu sokoni ukiwa umevaa jezi na umeshikilia begi la mitumba ni rahisi, twende sasa uvae sare za jeshi na uheshimu sheria za vita ushambuliane na jeshi la adui na upige military targets tu uone mziki wake.

Kwa akili zako ulitaka Houthi wakishambulia miundombinu ya mafuta, basi na Saudi Arabia ishambulie fuel depots za Yemen?
Hiyo tit for tat anaiweza Israel tu, unashambulia kutokea andaki lililopo shuleni, anashusha shule nzima ya watoto 300 ili abomoe andaki lenye makombora 10.
Kwa hiyo bunge la marekani kutokujadili vita ya Iran ndo linalo zuia marundo ya kapoko ya marekani yaliyo jazana hapo mashariki ya kati yashindwe kufanya kazi dhidi ya vidrone vya bei rahisi vya Irani?
Au bunge lingejadili hiyo vita ndo marekani ingeshinda vita ambavyo mpaka Sasa vimeikalia kooni hali ya kuwa alivianzisha Kwa mbwembwe?
Ebu ww tuambie ni silaha gani ambayo Marekani hajaitumia kwenye vita hii ili tujue kuwa kweli yeye hakujimaliza.
Kwa hiyo Kwa wahuthi hoja Yako imebadilika kutoka Kwa Saudia kuwa na jeshi dhaifu mpaka Kwa wahuthi wanajikimga nyuma ya raia?
Aya niambie Kwa hiyo maneno yaliyo tekwa na wahuthi walikuwa wametanguliza raia mbele yao kupigana na vibaraka wacsaudia ?
Ww jamaa huwa unajifanya smart lakini ni bonge moja la kilaza.
 
Naona unatumia nguvu kubwa kutaka kutetea uovu
Suala la marekani na israhell kushambulia makazi ama sehemu za raia na kusingizia unayoyasema hayo ni kawaida
Sisi tunayajua zamani kama wanayafanya sasa mpaka taasisi walizoziunda zinasema tunayoyasema sisi kila mara na kila wakati
Marekani kaua wanafunzi shule hakuna hata kiberiti kilichopatikana pale shule
Kaenda kaua watu harusini hakuna hata baruti ilopatikana
Kaenda kuripua mashine zinazotoa chumvi kwenye maji hajatosheka karipua madaraja haijatosha karipua mpaka vyuo vikuu
Iran haikutaka vita ila imejikuta vitani na haikua na namna zaidi ya kujilinda marekani haijawahi kutangaza ipo vitani ila wanaokufa wanajeshi wa marekani kambi zinazoripuliwa za marekani mpaka leo WSP limesema idadi ya mizoga ya marekani imeongezeka
Iran licha ya kupitia magumu yakuuliwa ulowataja kaonesha zaidi ya ukomavu
Israhell licha ya kufanya hayo unayoyasema mpaka Lei hamas ipo na hizbullah ipo
Mwisho juzi sijui ndio bungee sijui nini la marekani limelight kura marekani ama Turampet awaondoe wanajeshi wa marekani kwenye vita na iran wao wanajua kama wapo vitani ila wewe unasema hawapo vitani
Shkamoo wabongo 🙏🙏🙏
 
Kupigana vita na makundi ya Aina ya houthi nk sio kazi rahisi kama watu wanavyofikiri, makundi ya Aina ile Kwanza silaha Yao kubwa ni kuishi na jamii, hakuna namna Utaweza kuwashinda Hadi pale utakapoamua kuua na kutesa watu wengi wasio na hatia. Ili uue mmoja itakubidi uue au kutesa wasio na hatia Mia moja na Saudi Arabia hayuko tayari Kwa Hilo.

US, Israel na ubabe wao wote wa teknolojia wameua watu wengi wasio na hatia kuliko idadi ya wanachama wa hivyo vikundi katika kupambana vita na hao Magaidi, Israel yeye ndio kabisa anapiga Tu makombora as long akipata taarifa kuwa mahali Fulani wako Magaidi basi anafumua Tu haijalishi kuna Nani. Yani mentality ya kupambana na ugaidi inatofautina baina ya Mataifa.

Kingine ni kwamba Saudi Arabia anategemea Sana taarifa za kijasusi kutoka Israel, US. Mfumo wa ukusanyaji taarifa wa kiitelijensia wa Saudi Arabia hauko imara, uko compromised Sana Kwa maana ya kwamba Hapa Katikati kabla hujafika kule juu wako maafisa Wana target na malengo binafsi yanayosukumwa na Imani za kidini, tofauti za mitazamo ya kisiasa na kiutawala nk, hawako pamoja na ndani ya hiyo hiyo Intelligent ring kuna Israel assets ambao wanahujumu humo ndani ili instability iendelee kuwepo iwape Faida ya kusonga mbele...Kumbuka hapo hapo ndani ya Saudi Arabia wapo wahafidhina wanasapoti harakati wanazofanya Houthi na pesa wanazo kama kawaida....

Kingine cha mwisho vita ni gharama na inaua uchumi, Saudi Arabia hayuko tayari kuharibu uchumi wake. Saudi Arabia Hana ubavu wa kuvumilia mashambulizi ya Houthi bila msaada wa US na US kachomoa kwenye Hilo so kaamua atulie tu.
Hapa umeandika uongo mwingi sana mzee
Kwanza houthi wanakua magaidi kwa vigezo gani
Pili saudia ipo tayari ni vile uwezo hawana wao wala mabwana zao hawana
Saudia marekani israhell na vibaraka wenzao wengine walipigana na Houth zaidi ya miaka 7 sijui 8 ila hakuna walichokipata
Hatimae wakaona waingie nao makubaliano ambayo khatimae ndio yamevunjika mara hii tena kwa saudia kuanza kuwashambulia hao hao wahouthi
Kama hawako tayari kwanini walianza mashambulizi dhidi ya hao houthi
Saudia hawateteteeki kwenye hili
 
Kwa hiyo bunge la marekani kutokujadili vita ya Iran ndo linalo zuia marundo ya kapoko ya marekani yaliyo jazana hapo mashariki ya kati yashindwe kufanya kazi dhidi ya vidrone vya bei rahisi vya Irani?
Au bunge lingejadili hiyo vita ndo marekani ingeshinda vita ambavyo mpaka Sasa vimeikalia kooni hali ya kuwa alivianzisha Kwa mbwembwe?
Ebu ww tuambie ni silaha gani ambayo Marekani hajaitumia kwenye vita hii ili tujue kuwa kweli yeye hakujimaliza.
Kwa hiyo Kwa wahuthi hoja Yako imebadilika kutoka Kwa Saudia kuwa na jeshi dhaifu mpaka Kwa wahuthi wanajikimga nyuma ya raia?
Aya niambie Kwa hiyo maneno yaliyo tekwa na wahuthi walikuwa wametanguliza raia mbele yao kupigana na vibaraka wacsaudia ?
Ww jamaa huwa unajifanya smart lakini ni bonge moja la kilaza.
Kuna muda ukisikiliza hoja za T14 Armata unabakia kushangaa tu maana kuna muda anajizonga mwenyewe
Juu kule kakwambia saudia ategemee ant drone kutoka marekani
Marekani ambayo hata yeye kashindwa kuzitumia hizo ant drone kulinda kambi zako hapo ME marekani ambayo imeshindwa kutumia hizo ant drone kuzuia meli zisishambuliwe pale hormuz ambapo anasema anapamiliki yeye kwasasa
Yaani kuna muda kumuelewa mwamba inataka ufanye kazi kwelii
 
Hapa umeandika uongo mwingi sana mzee
Kwanza houthi wanakua magaidi kwa vigezo gani
Kwangu Mimi Gaidi(Magaidi) ni mtu au kikundi chochote kile kinacholenga watu na miundombinu Yake Kwa lengo wanalojua wao Kwa expense ya wasio na hatia mfano wa Magaidi wengine ni IDF, US (US forces), Al Qaida, nk.

Hatimae wakaona waingie nao makubaliano ambayo khatimae ndio yamevunjika mara hii tena kwa saudia kuanza kuwashambulia hao hao wahouthi
Kama hawako tayari kwanini walianza mashambulizi dhidi ya hao houthi
Saudia hawateteteeki kwenye hili
Saudia alichofanya ni kama alivyofanya au anavyofanya Iran, Israel na US pindi Tu maslahi Yao yanapoguswa...Alichofanya Saudia ni kulenga kulinda Mpaka wake wa kusini dhidi ya take over ya Houthi Yemeni, Hapa ni suala la kutumika vibaya madhehebu ya kidini ya kishia na kisunni in expense ya wasio na hatia thus why Mm naona mataifa kama Qatar, Saudi, Iran nk ni nchi zinazoongeza kukua Kwa ugaidi duniani coz how comes mnakubali kugawanywa na US & Israel?
 
Kwangu Mimi Gaidi(Magaidi) ni mtu au kikundi chochote kile kinacholenga watu na miundombinu Yake Kwa lengo wanalojua wao Kwa expense ya wasio na hatia mfano wa Magaidi wengine ni IDF, US (US forces), Al Qaida, nk.

Saudia alichofanya ni kama alivyofanya au anavyofanya Iran, Israel na US pindi Tu maslahi Yao yanapoguswa...Alichofanya Saudia ni kulenga kulinda Mpaka wake wa kusini dhidi ya take over ya Houthi Yemeni, Hapa ni suala la kutumika vibaya madhehebu ya kidini ya kishia na kisunni in expense ya wasio na hatia thus why Mm naona mataifa kama Qatar, Saudi, Iran nk ni nchi zinazoongeza kukua Kwa ugaidi duniani coz how comes mnakubali kugawanywa na US & Israel?
Walau kwa mara ya kwanza nimeipata tafsiri ya gaidi inayoeleweka

Ahsante sina chakuongeza mkuu
 
Kuna muda ukisikiliza hoja za T14 Armata unabakia kushangaa tu maana kuna muda anajizonga mwenyewe
Juu kule kakwambia saudia ategemee ant drone kutoka marekani
Marekani ambayo hata yeye kashindwa kuzitumia hizo ant drone kulinda kambi zako hapo ME marekani ambayo imeshindwa kutumia hizo ant drone kuzuia meli zisishambuliwe pale hormuz ambapo anasema anapamiliki yeye kwasasa
Yaani kuna muda kumuelewa mwamba inataka ufanye kazi kwelii
Huyu jamaa ni bonge la kilaza japo kuwa anajifanya kuwa smart.
 
Hii ya kujificha kwa raia mshaifanya ndio sababu ya kujificha kushindwa kwenu mzee
Marekani aliripua shule pale iran napo vipi walijificha majeshi
Karipua juzi tu karipua sherehe napo vipi kulikua na jeshi
Karipua miundo mbinu napo vipi mzeee
Kiufupi saudia hana tofauti na bwana wake marekani wameshindwa kujilinda mbele ya hao wamba!!!
Aaah huyo bwege achana naye. Habari zinaonesha wazi kabisa wanajeshi wa Saudi Arabia wakikamatwa mateka na Houthi. Haiyz na Mocha imechukuliwa kwa mtutu wa bunduki askari mamluki wakiinua mikono kusalimu amri. Halafu huyo FALA anakwambia eti wanajificha nyuma ya raia.
 
Kwangu Mimi Gaidi(Magaidi) ni mtu au kikundi chochote kile kinacholenga watu na miundombinu Yake Kwa lengo wanalojua wao Kwa expense ya wasio na hatia mfano wa Magaidi wengine ni IDF, US (US forces), Al Qaida, nk.
Basi kwa Houthi hawako kwenye tafsiri ya ugaidi. Maana sehemu kubwa wanayolenga ni kambi za jeshi za Saudi Arabia.
Saudia alichofanya ni kama alivyofanya au anavyofanya Iran, Israel na US pindi Tu maslahi Yao yanapoguswa...Alichofanya Saudia ni kulenga kulinda Mpaka wake wa kusini dhidi ya take over ya Houthi Yemeni, Hapa ni suala la kutumika vibaya madhehebu ya kidini ya kishia na kisunni in expense ya wasio na hatia thus why Mm naona mataifa kama Qatar, Saudi, Iran nk ni nchi zinazoongeza kukua Kwa ugaidi duniani coz how comes mnakubali kugawanywa na US & Israel?
Saudi Arabia ndiye aliyeanza huu ugomvi kwa kuweka blockade Yemeni tangu 2021. Haijatosha akaanza kushambulia wenzake walipoanza kuondoa blockade. Hivyo hapa mchokozi ni Saudi Arabia.
 
Kupigana vita na makundi ya Aina ya houthi nk sio kazi rahisi kama watu wanavyofikiri, makundi ya Aina ile Kwanza silaha Yao kubwa ni kuishi na jamii, hakuna namna Utaweza kuwashinda Hadi pale utakapoamua kuua na kutesa watu wengi wasio na hatia. Ili uue mmoja itakubidi uue au kutesa wasio na hatia Mia moja na Saudi Arabia hayuko tayari Kwa Hilo.

US, Israel na ubabe wao wote wa teknolojia wameua watu wengi wasio na hatia kuliko idadi ya wanachama wa hivyo vikundi katika kupambana vita na hao Magaidi, Israel yeye ndio kabisa anapiga Tu makombora as long akipata taarifa kuwa mahali Fulani wako Magaidi basi anafumua Tu haijalishi kuna Nani. Yani mentality ya kupambana na ugaidi inatofautina baina ya Mataifa.

Kingine ni kwamba Saudi Arabia anategemea Sana taarifa za kijasusi kutoka Israel, US. Mfumo wa ukusanyaji taarifa wa kiitelijensia wa Saudi Arabia hauko imara, uko compromised Sana Kwa maana ya kwamba Hapa Katikati kabla hujafika kule juu wako maafisa Wana target na malengo binafsi yanayosukumwa na Imani za kidini, tofauti za mitazamo ya kisiasa na kiutawala nk, hawako pamoja na ndani ya hiyo hiyo Intelligent ring kuna Israel assets ambao wanahujumu humo ndani ili instability iendelee kuwepo iwape Faida ya kusonga mbele...Kumbuka hapo hapo ndani ya Saudi Arabia wapo wahafidhina wanasapoti harakati wanazofanya Houthi na pesa wanazo kama kawaida....

Kingine cha mwisho vita ni gharama na inaua uchumi, Saudi Arabia hayuko tayari kuharibu uchumi wake. Saudi Arabia Hana ubavu wa kuvumilia mashambulizi ya Houthi bila msaada wa US na US kachomoa kwenye Hilo so kaamua atulie tu.
Hapa bro umeongopa 90%.
Houthi wanapigana kama jeshi kamili na maeneo yao ya kambi zao yapo pembezoni kwa mji na milimani NJE NA RAIA. Pia huwa hawajifichi bali wanapigana vita za uso kwa uso. Miji miwili,bandari mbili na visiwa viwili walivinyakua kwa mtutu wa bunduki. Houthi sio kama Hamas na Bokoharam. Houthi wana operate kwa rank za jeshi na kwa battalion.
-Kuhusu houthi kuwa gaidi hapa ndio UONGO mwingine. Houthi ni kundi ambalo lilikua chama cha siasa tangu 1994. Ila kilishika silaha kikiungwa mkono na 90% ya raia wa Yemeni ambao walikua hawautaki utawala wa MANSOUR 2014. Ila tamaa ya Mansour akaomba usaidizi Saudia,UAE na Marekani dhidi ya raia wa nchi yake ambao HAWAMTAKI. Saudi Arabia ilifanya ukatili wa kuweka blockade misaada ya vyakula na madawa kisa tu raia 90% wapo nyuma ya Houthi. Matokeo yake 2 millions innocent children wakafa kwa magonjwa na malnutrition. Hapo nani GAIDI!?
 
Kuna nchi duniani inayowashinda waSaudi katika ununuzi wa silaha za kivita, silaha za kisasa kabisa!

Sasa hawa wa Houthi wanapata wapi hata uthubutu tu wa kuzozana na Saudi Arabia kiasi kwamba makombora yanapigwa hadi ndani mwa Riadh, na nusra mengine yaende Mecca!

Kwa nini Saudi walielie na kuomba msaada kukabiliana na hawa Houthi. Kuna nini kinatokea hadi hali iwe tete kiasi hiki?
Kwani wakiandaa vidola kama bilioni mbili hivi, akina Lucas Mwashamba, Tlaatlaah hawawezi kweli kwenda kutoa msaada huko na kutuacha nasi hapa JF tupate hewa kidogo?
Wajua Marekani ndio watengenezaji na wauza silaha wakubwa kuliko mwingine yeyote na wana silaha za kisasa sana nasikia na siku hizi wanazo zinazopiga toka anga za juu (space lesser wepons)
Cha ajabu wamepigana na Wataliban wa Afghanistan kwa miaka ishrini mwisho wa kakubali kushindwa. Silaha za Wataliban zilikuwa bunduki za AK 47 na bazooka tuu.
Hali ilukuwa hivyo hivyo Vietnam. Laos na Cambodia Marekani walikimbia kwa aibu kubwa.
Muhimu ni ujasiri wa wapiganaji na sio silaha pekee.
 
Basi kwa Houthi hawako kwenye tafsiri ya ugaidi. Maana sehemu kubwa wanayolenga ni kambi za jeshi za Saudi Arabia.
Houthi nao pia wamekuwa wakishambulia Civilian Infrastructures zile Oil processing & Pipeline facilities za Saudi Aramco alizoshambulia Houthi ni nini zile?, unafikiri ni watu wangapi waliathirika na shambulizi Hilo moja Tu nililotolea mfano, Acha Tu land mines ambazo wamezitega zinavyoharibu utaratibu wa kawaida wa mambi...Houthi ni kundi la kigaidi kama lilivyo IDF na wengine.
 
Hapa bro umeongopa 90%.
Houthi wanapigana kama jeshi kamili na maeneo yao ya kambi zao yapo pembezoni kwa mji na milimani NJE NA RAIA. Pia huwa hawajifichi bali wanapigana vita za uso kwa uso. Miji miwili,bandari mbili na visiwa viwili walivinyakua kwa mtutu wa bunduki. Houthi sio kama Hamas na Bokoharam. Houthi wana operate kwa rank za jeshi na kwa battalion.
-Kuhusu houthi kuwa gaidi hapa ndio UONGO mwingine. Houthi ni kundi ambalo lilikua chama cha siasa tangu 1994. Ila kilishika silaha kikiungwa mkono na 90% ya raia wa Yemeni ambao walikua hawautaki utawala wa MANSOUR 2014. Ila tamaa ya Mansour akaomba usaidizi Saudia,UAE na Marekani dhidi ya raia wa nchi yake ambao HAWAMTAKI. Saudi Arabia ilifanya ukatili wa kuweka blockade misaada ya vyakula na madawa kisa tu raia 90% wapo nyuma ya Houthi. Matokeo yake 2 millions innocent children wakafa kwa magonjwa na malnutrition. Hapo nani GAIDI!?
Haijalishi Una operate Kwa mfumo kamili wa kijeshi namna gani, ni sawa na IDF Leo hii useme Kisa ni Jeshi basi sio Magaidi wakati movements wanazofanya ni za kigaidi kabisa, Houthi wamekuwa wakiweka landmines na kusumbua Sana watu, sasa huo si ugaidi Tu kama wa kina Marekani?...
 
Haijalishi Una operate Kwa mfumo kamili wa kijeshi namna gani, ni sawa na IDF Leo hii useme Kisa ni Jeshi basi sio Magaidi wakati movements wanazofanya ni za kigaidi kabisa, Houthiayo wamekuwa wakiweka landmines na kusumbua Sana watu, sasa huo si ugaidi Tu kama wa kina Marekani?...
Hakuna civilian area ambayo Houthi wameweka landmines,usipende kuongopa kaka.
Landmines Houthi wameweka maeneo yao ya kijeshi na sio maeneo ya kiraia.
Huwenda una tafsiri yako ya maana ya ugaidi ila kwa tafsiri ya kimataifa Houthi hakuna tukio la kigaidi walilolifanya.
 
Back
Top Bottom