HE saved me,HE gave me the second chance!

Halafu kuna wapumbavu humu JF wanaleta mada za kijinga,eti hakuna MUNGU,niliwatukana eti cha ajabu nikawa banned kwa siku 8,nisipate access ya JF,sasa natoa amri ni marufuku kwa mtu yoyote asiyemwabudu MUNGU kuwa member wa JF,kama wapo humu ambao hawatambui uwepo wa MUNGU,nawapa siku 30 kuanzia leo waokoke,kama hawataki basi waondoke JF kwa amani,wasipoondoka,JF itakufa,na itakuwa mwisho wa uhai wa JF,na kama JF itaendelea kuwepo na member wasiotambua uwepo wa MUNGU,basi tukio lisilo la kawaida litatokea,hebu tusubiri mtaona!
MUNGU awasamehe bure na kuwabadilisha mapema kabla hawajaharibikiwa zaidi.
 
Pole sana,mwili umesisimuka,hii ajali niliiona kwenye tv noah aliharibika kabisa.Zingatia ibada MUNGU amekupa second chance kurebisha yale uliyokuwa ujayaweka sawa
 
Hiyo ajali nilipata habari zake humu Jf, kumbe mkuu na wewe ulikuwemo? Pole kwa maswahibu yaliyokusibu Jaguar...

Oohhh ndo ile noah waliweka picha yake humu daah...Mungu mkubwa
 
Last edited by a moderator:
Pole sana mkuu na hongera, ila hata ukimwi wewe huwezi kupata una kinga.
 
Ilikuwa 08/11/2013 saa kumi na moja na robo alfajir Jaguar nilipanda gari aina ya noah iliyokuwa ikitokea GAIRO kuelekea MOROGORO MJINI.Nilianza safari yangu kuanzia kijiji cha DAKAWA na nilikuwa nawahi suala muhimu sana mjini MORO.
Nilipoingia ndani ya ile noah,kwanza nilikosa siti ikabidi nijiminye kwenye buti nyuma na kufanya jumla ya abiria wawili waliokaa kwenye buti,mimi na dada mmoja.
Abiria wengi niliowakuta walikuwa wamejifunika mashuka ya kimasai wakiendelea kuuchapa usingizi.Kilichotokea baada ya robo saa tangu nipande ile noah ni kiza kitupu kwangu mpaka sasa kwani nilipoteza fahamu kwa siku mbili.
Kwa stori nilizopewa na abiria wa noah iliyokuwa nyuma yetu ni kwamba mbele yetu lilikuwa basi la adventure kigoma-Dar.Tulipofika maeneo ya dakawa ranchi,yule dereva wa basi akachukua uamuzi wa ku-overtake FUSO iliyokuwa mbele yake na dervA wetu Masoud(R.I.P) akaunga tela bila kufanya uchunguzi.Ile Adventure inarudi kushoto,noah yetu uso kwa uso na scania lori.
Maskini,watu 7 walipoteza maisha pale pale akiwemo dereva masoud na yule abiria mwenzangu niliyekuwa naye kwenye buti na wengine watatu hospitalini na kufanya jumla kuu kuwa kumi.Inasemekana mimi Jaguar baada ya mzinga ule,buti la noah lilifunguka nami nikatoka nje ya gari,nikatembea hatua kadhaa kwenda kando ya barabara kisha nikaanguka chini na kupoteza fahamu.Nilirudisha fahamu zangu ndani ya hospitali ya mkoa MORO baada ya siku mbili.
Nikiangalia idadi ya waliopoteza maisha(10) na majeruhi (3),wawili hao wengine wakiwa na hali mbaya,mimi sijavunjika hata kidole,kwa kweli sielewi nimrudishie nini MUNGU wangu kwa muujiza huu!ninaandika hivi huku nikikiri kutoka moyoni kwamba nimekuwa mbali mno na ibada,nimeasi kanisa kwa muda mrefu,lakini mwenyezi MUNGU hakujali hilo,akanipa nafasi ya pili kubadilika,TUACHE MUNGU AITWE MUNGU,hawezi kufananishwa na kitu chochote,uweza,wema na huruma zake hazina mfano wala mipaka.
Nimeguswa!.
Mkuu Jaguar, you have the powers ndani yako. Huyo Mungu unayemtaja amekuoakoa yuko ndani yako!. Ametokea kukuokoa tuu bila ya wewe kumtuma, sasa baada ya kumjua kuwa yuko ndani yako, mtume chochote, au muombe chochote utapata!.

Kilichokutokea ni kuwa your sub-concious mind iliiona ajali kabla, astarar body ikaicontrol physical body, ikaufungua mlango, ikakutoa nje kabla kidogo ya ajali, then within a split of a second, ajali ikatokea, ikakulaza chini, na kukupotezea fahamu ili usijue nini kilitokea!.

Baada ya kuyajua haya, sasa shikamana na Mungu, uyafanye makubwa na sio tena ukiwa usingizini bali ukiwa macho huku unajitambua!. Kila anayepewa a second chance, anapewa for a purpose!, pata muda utulie, muulize Mungu kusudio lake kwako ni lipi!, utaisikia sauti itakuambia upasayo kutenda!, go for it!.
Pasco
 
Nimeguswa!.
Mkuu Jaguar, you have the powers ndani yako. Huyo Mungu unayemtaja amekuoakoa yuko ndani yako!. Ametokea kukuokoa tuu bila ya wewe kumtuma, sasa baada ya kumjua kuwa yuko ndani yako, mtume chochote, au muombe chochote utapata!.

Kilichokutokea ni kuwa your sub-concious mind iliiona ajali kabla, astarar body ikaicontrol physical body, ikaufungua mlango, ikakutoa nje kabla kidogo ya ajali, then within a split of a second, ajali ikatokea, ikakulaza chini, na kukupotezea fahamu ili usijue nini kilitokea!.

Baada ya kuyajua haya, sasa shikamana na Mungu, uyafanye makubwa na sio tena ukiwa usingizini bali ukiwa macho huku unajitambua!.
Pasco
100% mkuu,nakubaliana na wewe!
 
Mkuu Jaguar

Pole sana kwa yote. Hakika unahitaji kumshukuru Mungu kwa nusra uliyopata.

Nakutakia heri ili kupona salama trauma uliyonayo.
 
Last edited by a moderator:
Halafu kuna wapumbavu humu JF wanaleta mada za kijinga,eti hakuna MUNGU,niliwatukana eti cha ajabu nikawa banned kwa siku 8,nisipate access ya JF,sasa natoa amri ni marufuku kwa mtu yoyote asiyemwabudu MUNGU kuwa member wa JF,kama wapo humu ambao hawatambui uwepo wa MUNGU,nawapa siku 30 kuanzia leo waokoke,kama hawataki basi waondoke JF kwa amani,wasipoondoka,JF itakufa,na itakuwa mwisho wa uhai wa JF,na kama JF itaendelea kuwepo na member wasiotambua uwepo wa MUNGU,basi tukio lisilo la kawaida litatokea,hebu tusubiri mtaona!

Tanzania kuna atheist basi hawa mchwara wasiojielewa wanawaiga tu wazungu kila kitu,

amesoma viblaa blaaa vya Darwinism basi na yeye keshakuwa atheist.
 
Halafu kuna wapumbavu humu JF wanaleta mada za kijinga,eti hakuna MUNGU,niliwatukana eti cha ajabu nikawa banned kwa siku 8,nisipate access ya JF,sasa natoa amri ni marufuku kwa mtu yoyote asiyemwabudu MUNGU kuwa member wa JF,kama wapo humu ambao hawatambui uwepo wa MUNGU,nawapa siku 30 kuanzia leo waokoke,kama hawataki basi waondoke JF kwa amani,wasipoondoka,JF itakufa,na itakuwa mwisho wa uhai wa JF,na kama JF itaendelea kuwepo na member wasiotambua uwepo wa MUNGU,basi tukio lisilo la kawaida litatokea,hebu tusubiri mtaona!

Psssssss! Dude are you out of your mind?
 
Watu kama wewe ni janga kwa Dunia. Hivi unadhani kama Mungu angetaka watu wote wamuamini angeshindwa??
 
Mkuu pole kwa ajali na mwenyezi Mungu apewe sifa.
 
Mkumbuke muumba wako siku za ujana wako tena kabla hazijaja siku zilizo mbaya. Pole kwa janga lililokupata. Endelea kumtumaini Mungu anampango na wewe.
 
Halafu kuna wapumbavu humu JF wanaleta mada za kijinga,eti hakuna MUNGU,niliwatukana eti cha ajabu nikawa banned kwa siku 8,nisipate access ya JF,sasa natoa amri ni marufuku kwa mtu yoyote asiyemwabudu MUNGU kuwa member wa JF,kama wapo humu ambao hawatambui uwepo wa MUNGU,nawapa siku 30 kuanzia leo waokoke,kama hawataki basi waondoke JF kwa amani,wasipoondoka,JF itakufa,na itakuwa mwisho wa uhai wa JF,na kama JF itaendelea kuwepo na member wasiotambua uwepo wa MUNGU,basi tukio lisilo la kawaida litatokea,hebu tusubiri mtaona!

Sijawahi kukubali unabii kama huu,unadhani Mungu mwenyewe hajui kuwa hawa watu wanaexist? Then kwanini awaache waendelee kuishi?(U cn refer King..ge), mfano JF ife ili...? Nyie ndo mnafanya watu wadhani kuwa religious ppl aren't intelligent,unavojinadi kuwa uliwatukana hao walosema hakuna Mungu,ulikuwa sahihi? Ndivyo Mungu wako anavyosema? uwatukane? Hivi mlipoambiwa mkawafanye watu kuwa wanafunzi ilimaanishwa kwa kutoa amri ya siku 30 kama mahakama eeeh...? Mh....haya ngoja tusubir amri ya siku 30 tuone kama itkuwa na back up ya Mungu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom