HE saved me,HE gave me the second chance!

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,413
2,000
Ilikuwa 08/11/2013 saa kumi na moja na robo alfajir Jaguar nilipanda gari aina ya noah iliyokuwa ikitokea GAIRO kuelekea MOROGORO MJINI.Nilianza safari yangu kuanzia kijiji cha DAKAWA na nilikuwa nawahi suala muhimu sana mjini MORO.

Nilipoingia ndani ya ile noah,kwanza nilikosa siti ikabidi nijiminye kwenye buti nyuma na kufanya jumla ya abiria wawili waliokaa kwenye buti,mimi na dada mmoja.

Abiria wengi niliowakuta walikuwa wamejifunika mashuka ya kimasai wakiendelea kuuchapa usingizi.Kilichotokea baada ya robo saa tangu nipande ile noah ni kiza kitupu kwangu mpaka sasa kwani nilipoteza fahamu kwa siku mbili.

Kwa stori nilizopewa na abiria wa noah iliyokuwa nyuma yetu ni kwamba mbele yetu lilikuwa basi la adventure kigoma-Dar.Tulipofika maeneo ya dakawa ranchi,yule dereva wa basi akachukua uamuzi wa ku-overtake FUSO iliyokuwa mbele yake na dervA wetu Masoud(R.I.P) akaunga tela bila kufanya uchunguzi.Ile Adventure inarudi kushoto,noah yetu uso kwa uso na scania lori.

Maskini,watu 7 walipoteza maisha pale pale akiwemo dereva masoud na yule abiria mwenzangu niliyekuwa naye kwenye buti na wengine watatu hospitalini na kufanya jumla kuu kuwa kumi.

Inasemekana mimi Jaguar baada ya mzinga ule,buti la noah lilifunguka nami nikatoka nje ya gari,nikatembea hatua kadhaa kwenda kando ya barabara kisha nikaanguka chini na kupoteza fahamu.Nilirudisha fahamu zangu ndani ya hospitali ya mkoa MORO baada ya siku mbili.

Nikiangalia idadi ya waliopoteza maisha(10) na majeruhi (3),wawili hao wengine wakiwa na hali mbaya,mimi sijavunjika hata kidole,kwa kweli sielewi nimrudishie nini MUNGU wangu kwa muujiza huu!ninaandika hivi huku nikikiri kutoka moyoni kwamba nimekuwa mbali mno na ibada,nimeasi kanisa kwa muda mrefu,lakini mwenyezi MUNGU hakujali hilo,akanipa nafasi ya pili kubadilika,TUACHE MUNGU AITWE MUNGU,hawezi kufananishwa na kitu chochote,uweza,wema na huruma zake hazina mfano wala mipaka.
 
ram

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,108
2,000
Aisee... sifa na shukrani tumpe Mungu, pole na hongera kwa kutoka mzima, Mungu ana makusudi na wewe, soma zaburi 116 iwe faraja kwako na zaburi 91 ujue kwamba Alwayz Mungu yupo nasi kila iitwapo leo
 
Blessed

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
3,118
2,000
Ilikuwa 08/11/2013 saa kumi na moja na robo alfajir Jaguar nilipanda gari aina ya noah iliyokuwa ikitokea GAIRO kuelekea MOROGORO MJINI.Nilianza safari yangu kuanzia kijiji cha DAKAWA na nilikuwa nawahi suala muhimu sana mjini MORO.
Nilipoingia ndani ya ile noah,kwanza nilikosa siti ikabidi nijiminye kwenye buti nyuma na kufanya jumla ya abiria wawili waliokaa kwenye buti,mimi na dada mmoja.
Abiria wengi niliowakuta walikuwa wamejifunika mashuka ya kimasai wakiendelea kuuchapa usingizi.Kilichotokea baada ya robo saa tangu nipande ile noah ni kiza kitupu kwangu mpaka sasa kwani nilipoteza fahamu kwa siku mbili.
Kwa stori nilizopewa na abiria wa noah iliyokuwa nyuma yetu ni kwamba mbele yetu lilikuwa basi la adventure kigoma-Dar.Tulipofika maeneo ya dakawa ranchi,yule dereva wa basi akachukua uamuzi wa ku-overtake FUSO iliyokuwa mbele yake na dervA wetu Masoud(R.I.P) akaunga tela bila kufanya uchunguzi.Ile Adventure inarudi kushoto,noah yetu uso kwa uso na scania lori.
Maskini,watu 7 walipoteza maisha pale pale akiwemo dereva masoud na yule abiria mwenzangu niliyekuwa naye kwenye buti na wengine watatu hospitalini na kufanya jumla kuu kuwa kumi.Inasemekana mimi Jaguar baada ya mzinga ule,buti la noah lilifunguka nami nikatoka nje ya gari,nikatembea hatua kadhaa kwenda kando ya barabara kisha nikaanguka chini na kupoteza fahamu.Nilirudisha fahamu zangu ndani ya hospitali ya mkoa MORO baada ya siku mbili.
Nikiangalia idadi ya waliopoteza maisha(10) na majeruhi (3),wawili hao wengine wakiwa na hali mbaya,mimi sijavunjika hata kidole,kwa kweli sielewi nimrudishie nini MUNGU wangu kwa muujiza huu!ninaandika hivi huku nikikiri kutoka moyoni kwamba nimekuwa mbali mno na ibada,nimeasi kanisa kwa muda mrefu,lakini mwenyezi MUNGU hakujali hilo,akanipa nafasi ya pili kubadilika,TUACHE MUNGU AITWE MUNGU,hawezi kufananishwa na kitu chochote,uweza,wema na huruma zake hazina mfano wala mipaka.

to God be the glory Jaguar,tunamshangiria BWANA kwa mujiza wako!
 
Last edited by a moderator:

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,413
2,000
Ila Yule jamaa aliiba simu yangu moja aliwapanikisha sana mkeo wangu na Ndugu zangu. alikuwa anawapigia na kuwaambia direct, 'Ndugu yenu kafa katika ajali,njooni mchukue mwili wake'.Mama yangu mzazi kasafiri kutoka Tunduma mpaka Morogoro akiomboleza safari nzima.
 
TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
9,824
2,000
Hiyo ajali nilipata habari zake humu Jf, kumbe mkuu na wewe ulikuwemo? Pole kwa maswahibu yaliyokusibu Jaguar...
 
Last edited by a moderator:

SAID KIGUA

Member
Aug 28, 2013
11
20
Allah akbar allah akbar akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa pole sana. Pole sana sana kwani bila mungu hakuna linalowezekana
 
Truth guy.

JF-Expert Member
Oct 30, 2013
398
0
Halafu kuna wapumbavu humu JF wanaleta mada za kijinga,eti hakuna MUNGU,niliwatukana eti cha ajabu nikawa banned kwa siku 8,nisipate access ya JF,sasa natoa amri ni marufuku kwa mtu yoyote asiyemwabudu MUNGU kuwa member wa JF,kama wapo humu ambao hawatambui uwepo wa MUNGU,nawapa siku 30 kuanzia leo waokoke,kama hawataki basi waondoke JF kwa amani,wasipoondoka,JF itakufa,na itakuwa mwisho wa uhai wa JF,na kama JF itaendelea kuwepo na member wasiotambua uwepo wa MUNGU,basi tukio lisilo la kawaida litatokea,hebu tusubiri mtaona!
 
Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,413
2,000
Allah akbar allah akbar akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah akbar allah mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa mungu ni mkubwa pole sana. Pole sana sana kwani bila mungu hakuna linalowezekana
Hakika daima na milele!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom