Hayati Magufuli aliweza kuwatisha waovu, mifumo iliamka kufanya kazi

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,135
22,640
Salaam, Shalom.

Ili pawe na Amani, huna budi kuwatisha waovu, KAZI hii ya kuhakikisha waovu hawachezei Sharubu za Serikali, Mungu alimsaidia Hayati Magufuli kuifanya kazi hiyo kwa ufasaha.

Maeneo yafuatayo, alidhibiti kwelikweli;

1. MTANDAO WA WIZI WA PESA ZA UMMA

Tumesikia Rais Samia analalamika Badala ya kuamrisha mifumo, asema kuwa umerudi mtandao wa kuiba pesa za umma, yaani pesa inatoka hazina kuja halmashauri, wanatokea watu, wanachepusha pesa hizo zinaingia katika account zao, na pesa hizo ni za mikopo tuliyokopa!

Miradi aliyeanzisha Magu, ilienda kwa kasi sababu ya ufuatiliaji wa karibu na wezi walidhibitiwa hasa.Usingeweza kukwiba pesa ya umma ukabaki salama.

2. UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA.

Katika kipindi chake, majambazi walienda likizo, hilo litoshe kutupa kujua kazi kubwa aliyoifanya hasa katika kuifanya mifumo ya ulinzi na Usalama kutenda kazi Kwa viwango vya juu.

3. KUDHIBITI MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA

Kabla ya Magufuli kuingia madarakani, Nchi yetu ilikithiri kwa kutapakaa kwa dawa za kulevya, lakini baada ya miaka kadhaa, mateja wengi walijisalimisha katika sobber houses, sababu kuu ikiwa ni kuadimika Kwa dawa za kulevya mtaani. Hilo litoshe kutuonyesha jinsi ambavyo palifanyika kazi kubwa underground.

4. UTAKATISHAJI FEDHA

Pesa haramu, chafu zilizotokana na biashara ovu ya kuiba pesa za umma, uuzaji dawa za kulevya, biashara chafu za ukwepaji kodi, zilidhibitiwa kwa kiasi kikubwa, jambo hilo lilileta mtikisiko kwenye Uchumi kwa kuwa Kwa namna moja au ingine, pesa hizo zilisaidia kutengeneza ajira sekta binafsi.

5. MFUMO WA EFD ULIFANYA KAZI

Vituo vya mafuta kwa Mfano, vyenye kuingiza pesa nyingi, hazikuwa zikitoa EFD, na walipobanwa kutoa risiti, walitishia kugoma.

Ujasiri wa Magufuli, ulisaidia wafanyabiashara hao kurudi mezani na kukubali kutoa EFD bila masharti.

6. UFANISI KATIKA MIFUMO YA UTOAJI MIZIGO BANDARINI

Ni katika uongozi wa Hayati Magufuli, document za kutoa Mzigo bandarini zilipungua, mwanzoni palikuwa na utitiri wa karatasi na mizunguko iliyochelewesha ufaulishaji mizigo bandarini.

Scana ya ukaguzi wa vitu vinavyopita bandarini ULIFANYA KAZI utawala wa Magufuli, alipambana kweli kweli na ufanisi ulionekana.

HITIMISHO

Pamoja na mapungufu wa kibinadamu na makosa kadhaa aliyoifanya Hayati Magufuli, itoshe kusema, Mungu alimwezesha kukaa katika KITI cha maamuzi sawasawa na kuhakikisha mifumo inafanya KAZI. Magufuli hakulalamika, alichukua hatua.

OMBI: Wananchi tunaomba atokee kiongozi atakayefuta BETTING nchini, hivi sasa, vijana wa CCM+ CDM na wasio na vyama wametekwa na jinamizi hili, HAYATI Magu hakuliweza hili. Maisha hayajawahi kuwa Bahati nasibu.

Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya Rais Magufuli.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo Tanzania🇹🇿.

Amen.
 
Salaam,Shalom.

Ili pawe na Amani, huna budi kuwatisha waovu, KAZI hii ya kuhakikisha waovu hawachezei Sharubu za Serikali, Mungu alimsaidia HAYATI Magufuli kuifanya KAZI hiyo Kwa ufasaha.

Maeneo yafuatayo, alidhibiti Kweli Kweli.

1. MTANDAO WA WIZI WA PESA ZA UMMA.

Tumesikia Rais Samia analalamika kuwa umerudi mtandao wa kuiba pesa za umma, yaani pesa inatoka hazina kuja halmashauri, wanatokea watu, wanachepusha pesa hizo zinaingia katika account zao, na pesa hizo ni za mikopo tuliyokopa!!

Miradi aliyeanzisha Magu, ilienda Kwa Kasi sababu ya ufuatiliaji wa karibu na wezi walidhibitiwa Hasa.

2. UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA.

Katika kipindi chake, majambazi walienda likizo, Hilo litoshe kutupa kujua KAZI kubwa aliyoifanya Hasa katika kuifanya mifumo ya ulinzi na USALAMA kutenda KAZI Kwa viwango vya juu.

3. KUDHIBITI MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA.

Kabla ya Magu kuingia madarakani, Nchi yetu ilikithiri Kwa kutapakaa Kwa dawa za KULEVYA, lakini Baada ya miaka kadhaa, mateja wengi walijisalimisha katika sobber houses, sababu kuu ikiwa ni kuadimika Kwa dawa za KULEVYA mtaani. Hilo litoshe kutuonyesha jinsi ambavyo palifanyika KAZI kubwa underground.

4. UTAKATISHAJI FEDHA.

Pesa haramu, chafu zilizotokana na biashara ovu ya kuiba pesa za umma, uuzaji dawa za KULEVYA, biashara chafu za ukwepaji kodi, zilidhibitiwa Kwa kiasi kikubwa, jambo Hilo lilileta mtikisiko kwenye Uchumi Kwa kuwa Kwa namna Moja au ingine, pesa hizo zilisaidia kutengeneza ajira sekta binafsi.

5. MFUMO WA EFD ULIFANYA KAZI.

Vituo vya mafuta Kwa Mfano, vyenye kuingiza pesa nyingi, hazikuwa zikitoa EFD, na walipobanwa Kutoa risiti, walitishia kugoma.

Ujasiri wa Magufuli,ulisaidia wafanyabiashara hao kurudi mezani na kukubali Kutoa EFD bila masharti.

6. UFANISI KATIKA MIFUMO YA UTOAJI MIZIGO BANDARINI.

Ni katika uongozi wa HAYATI Magufuli, document za Kutoa Mzigo bandarini zilipungua, mwanzoni palikuwa na utitiri wa karatasi na mizunguko iliyochelewesha ufaulishaji mizigo bandarini.

Scana ya ukaguzi wa vitu vinavyopita bandarini ULIFANYA KAZI utawala wa Magu, alipambana Kweli Kweli na ufanisi ulionekana.

HITIMISHO.

Pamoja na mapungufu wa kibinadamu na makosa kadhaa aliyoifanya HAYATI Magufuli, itoshe kusema, Mungu alimwezesha kukaa katika KITI Cha maamuzi sawasawa na kuhakikisha mifumo inafanya KAZI.

Magufuli hakulalamika, alichukua hatua.

Tunamshukuru Mungu Kwa zawadi ya Rais Magu.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.

Amen
Watakuambia majizi yaliogopa kuwekwa kwenye viroba kinyume na haki binadamu
 
Aliwapa nguvu wanyoofu na kuwafifisha wezi. Leo hii ukilalamikiwa kwa unyoofu wako unashughulikiwa na mamlaka badala ya kupewa nguvu.
Wengine walilalamika kuwa wauza drugs hawatendewi HAKI,

Zamani ilikuwa, ukikamatwa Mzigo wa drugs, polisi wakiwa na mtuhumiwa, njiani watapigiwa simu na mkubwa na kuambiwa wausindikize Mzigo sehemu husika wakiulinda,

Magufuli alifanikiwa kudeal na mtandao wa dawa za KULEVYA Kwa mkono wa CHUMA.

Huo ndio Hasa uongozi.
 
Watakuambia majizi yaliogopa kuwekwa kwenye viroba kinyume na haki binadamu
Kwamba Kuna HAKI za binadamu za kutetea wauza unga?

Watu wanaoharibu nguvukazi ya Taifa Kwa kuwadidimiza kwenye lindi la dawa za kulevya wanataka HAKI Gani?

Jambazi anayeuwa wananchi wasio na HATIA, unaweza tumia HAKI Gani za binadamu kumpokonya silaha?
 
Chadema walimuogopa na kumchukia zaid utadhani alikua Mwenyekiti wa Taifa 🐒
Wezi wengi wamo ndani ya chama chenu, WAPINZANI Wachache walitumika tu.

Ujenzi wa BWAWA la JNHP ulipingwa Kwa nguvu na watu ndani ya Serikali ukichagizwa na viongozi wa upinzani kukwamisha Magu.

Maslah ya nchi yanatakiwa yatangulizwe mbele,

Uchama hautatufikisha kokote.
 
Salaam, Shalom.

Ili pawe na Amani, huna budi kuwatisha waovu, KAZI hii ya kuhakikisha waovu hawachezei Sharubu za Serikali, Mungu alimsaidia Hayati Magufuli kuifanya kazi hiyo kwa ufasaha.

Maeneo yafuatayo, alidhibiti kwelikweli;

1. MTANDAO WA WIZI WA PESA ZA UMMA

Tumesikia Rais Samia analalamika kuwa umerudi mtandao wa kuiba pesa za umma, yaani pesa inatoka hazina kuja halmashauri, wanatokea watu, wanachepusha pesa hizo zinaingia katika account zao, na pesa hizo ni za mikopo tuliyokopa!

Miradi aliyeanzisha Magu, ilienda kwa kasi sababu ya ufuatiliaji wa karibu na wezi walidhibitiwa hasa.Usingeweza kukwiba pesa ya umma ukabaki salama.

2. UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA.

Katika kipindi chake, majambazi walienda likizo, hilo litoshe kutupa kujua kazi kubwa aliyoifanya hasa katika kuifanya mifumo ya ulinzi na Usalama kutenda kazi Kwa viwango vya juu.

3. KUDHIBITI MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA

Kabla ya Magufuli kuingia madarakani, Nchi yetu ilikithiri kwa kutapakaa kwa dawa za kulevya, lakini baada ya miaka kadhaa, mateja wengi walijisalimisha katika sobber houses, sababu kuu ikiwa ni kuadimika Kwa dawa za kulevya mtaani. Hilo litoshe kutuonyesha jinsi ambavyo palifanyika kazi kubwa underground.

4. UTAKATISHAJI FEDHA

Pesa haramu, chafu zilizotokana na biashara ovu ya kuiba pesa za umma, uuzaji dawa za kulevya, biashara chafu za ukwepaji kodi, zilidhibitiwa kwa kiasi kikubwa, jambo hilo lilileta mtikisiko kwenye Uchumi kwa kuwa Kwa namna moja au ingine, pesa hizo zilisaidia kutengeneza ajira sekta binafsi.

5. MFUMO WA EFD ULIFANYA KAZI

Vituo vya mafuta kwa Mfano, vyenye kuingiza pesa nyingi, hazikuwa zikitoa EFD, na walipobanwa kutoa risiti, walitishia kugoma.

Ujasiri wa Magufuli, ulisaidia wafanyabiashara hao kurudi mezani na kukubali kutoa EFD bila masharti.

6. UFANISI KATIKA MIFUMO YA UTOAJI MIZIGO BANDARINI

Ni katika uongozi wa Hayati Magufuli, document za kutoa Mzigo bandarini zilipungua, mwanzoni palikuwa na utitiri wa karatasi na mizunguko iliyochelewesha ufaulishaji mizigo bandarini.

Scana ya ukaguzi wa vitu vinavyopita bandarini ULIFANYA KAZI utawala wa Magufuli, alipambana kweli kweli na ufanisi ulionekana.

HITIMISHO

Pamoja na mapungufu wa kibinadamu na makosa kadhaa aliyoifanya Hayati Magufuli, itoshe kusema, Mungu alimwezesha kukaa katika KITI cha maamuzi sawasawa na kuhakikisha mifumo inafanya KAZI. Magufuli hakulalamika, alichukua hatua.

Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya Rais Magufuli.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo Tanzania🇹🇿.

Amen.
Anatokea mjinga mmoja anasema Bi Hangaya anaupiga mwingi
 
Wezi wengi wamo ndani ya chama chenu, WAPINZANI Wachache walitumika tu.

Ujenzi wa BWAWA la JNHP ulipingwa Kwa nguvu na watu ndani ya Serikali ukichagizwa na viongozi wa upinzani kukwamisha Magu.

Maslah ya nchi yanatakiwa yatangulizwe mbele,

Uchama hautatufikisha kokote.
wezi wa wa pesa za join the chain mpaka leo hawajakamatwa dah 🐒

na wapo tu ata kwenye maandamano walikuepo aise 🐒
 
Salaam, Shalom.

Ili pawe na Amani, huna budi kuwatisha waovu, KAZI hii ya kuhakikisha waovu hawachezei Sharubu za Serikali, Mungu alimsaidia Hayati Magufuli kuifanya kazi hiyo kwa ufasaha.

Maeneo yafuatayo, alidhibiti kwelikweli;

1. MTANDAO WA WIZI WA PESA ZA UMMA

Tumesikia Rais Samia analalamika kuwa umerudi mtandao wa kuiba pesa za umma, yaani pesa inatoka hazina kuja halmashauri, wanatokea watu, wanachepusha pesa hizo zinaingia katika account zao, na pesa hizo ni za mikopo tuliyokopa!

Miradi aliyeanzisha Magu, ilienda kwa kasi sababu ya ufuatiliaji wa karibu na wezi walidhibitiwa hasa.Usingeweza kukwiba pesa ya umma ukabaki salama.

2. UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA.

Katika kipindi chake, majambazi walienda likizo, hilo litoshe kutupa kujua kazi kubwa aliyoifanya hasa katika kuifanya mifumo ya ulinzi na Usalama kutenda kazi Kwa viwango vya juu.

3. KUDHIBITI MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA

Kabla ya Magufuli kuingia madarakani, Nchi yetu ilikithiri kwa kutapakaa kwa dawa za kulevya, lakini baada ya miaka kadhaa, mateja wengi walijisalimisha katika sobber houses, sababu kuu ikiwa ni kuadimika Kwa dawa za kulevya mtaani. Hilo litoshe kutuonyesha jinsi ambavyo palifanyika kazi kubwa underground.

4. UTAKATISHAJI FEDHA

Pesa haramu, chafu zilizotokana na biashara ovu ya kuiba pesa za umma, uuzaji dawa za kulevya, biashara chafu za ukwepaji kodi, zilidhibitiwa kwa kiasi kikubwa, jambo hilo lilileta mtikisiko kwenye Uchumi kwa kuwa Kwa namna moja au ingine, pesa hizo zilisaidia kutengeneza ajira sekta binafsi.

5. MFUMO WA EFD ULIFANYA KAZI

Vituo vya mafuta kwa Mfano, vyenye kuingiza pesa nyingi, hazikuwa zikitoa EFD, na walipobanwa kutoa risiti, walitishia kugoma.

Ujasiri wa Magufuli, ulisaidia wafanyabiashara hao kurudi mezani na kukubali kutoa EFD bila masharti.

6. UFANISI KATIKA MIFUMO YA UTOAJI MIZIGO BANDARINI

Ni katika uongozi wa Hayati Magufuli, document za kutoa Mzigo bandarini zilipungua, mwanzoni palikuwa na utitiri wa karatasi na mizunguko iliyochelewesha ufaulishaji mizigo bandarini.

Scana ya ukaguzi wa vitu vinavyopita bandarini ULIFANYA KAZI utawala wa Magufuli, alipambana kweli kweli na ufanisi ulionekana.

HITIMISHO

Pamoja na mapungufu wa kibinadamu na makosa kadhaa aliyoifanya Hayati Magufuli, itoshe kusema, Mungu alimwezesha kukaa katika KITI cha maamuzi sawasawa na kuhakikisha mifumo inafanya KAZI. Magufuli hakulalamika, alichukua hatua.

Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya Rais Magufuli.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo Tanzania🇹🇿.

Amen.
Baada ya kuwatisha waovu ndio
Akakwapua matrilioni yaliyomfukuzisha CAG au?
 
wezi wa wa pesa za join the chain mpaka leo hawajakamatwa dah 🐒

na wapo tu ata kwenye maandamano walikuepo aise 🐒
Hujawahi kumiliki akili,

Pesa za join the chain ni sawa na michango ya hiari ya harusi au vikoba,

Na CHADEMA haikusanyi Kodi Wala kuendesha Serikali.
 
Back
Top Bottom