Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,608
Viongozi wa kisiasa wana kazi ngumu sana. Kutakiwa kumridhisha kila wanayemuongoza kwa kadri ya uwezo binafsi, ni mtihani mgumu. Ni vigumu kwa kila anayeongozwa na kiongozi fulani kuwa na mtazamo ule ule kama wa mtu mwingine.
Naamini kabisa kwamba hayati John Magufuli hakuwa na sifa ya kiongozi mwenye diplomasia. Hakuwa na nguvu ya ushawishi wa mwanasiasa, yule wa asili. Alijawa na jazba na ile hali ya kutopenda kubishiwa hata kama mwisho wa mjadala hoja zake pengine zingeimarishwa kuliko alivyodhani. Hayati hakuwa na ile sifa aliyokuwa nayo mwasisi Julius Nyerere ya kuamini katika ushawishi wa hoja zinazotolewa.
Udhaifu wa JPM wa kukosa nguvu ya kidiplomasia ulifidiwa vyema na uwezo mkubwa wa kiutendaji. Uwezo wa kutoa maagizo na kuyafuatilia kwa ukali pasipo kuchekeana, ilikuwa ndio nguvu yake iliyomuwezesha kuanzisha miradi mikubwa na kuweka msukumo wa kuhakikisha inafikia hatua ya kumalizika.
Legacy ya JPM ipo katika uwezo wa kuthubutu kufanya maamuzi magumu. Suala la makinikia linaweza kuonekana ni jepesi lakini watangulizi wa hayati JPM walionekana kukosa uwezo wa kuwaambia wazungu wawekezaji kwamba hapa sisi tunasema hapana na hapa tunataka kifanyike hiki na hiki kwa faida yenu na yetu. Mabilioni ya pesa ambayo tunayapata kwenye mgao wetu baada ya kukaa mezani na kubadilisha mfumo mzima wa umiliki wa biashara ndio legacy yenyewe.
Ni rahisi kusema kwamba vitu vinavyojengwa kwa pesa ya kodi haviwezi kuwa legacy lakini mbona haikuwa rahisi kwa shirika la ndege kufufuliwa mpaka zikaanza kwenda India na kwingineko?. Mbona treni ya mwisho kwenda mpaka Moshi ilifanya hivyo miaka ya 1990 katikati?.
Mbona haikuwa rahisi kuzikarabati meli maziwani na watu wakiendelea kufa kwa kuzama na mitumbwi kila kukicha?. Mbona haikuwa rahisi kutekeleza kwa vitendo maamuzi ya kuhamia Dodoma tangu 1970 mwanzoni?, uthubutu wa JPM katika kutekeleza kile kinachowakera wengi ndio legacy yenyewe.
Hakujaliwa uwezo wa siasa za ushawishi lakini kukosa sifa hiyo hakuwezi kuyafanya yote aliyoyafanya kwa nguvu kubwa yasiwe na sifa ya kuwa legacy yake. Ukiwaambia wote watakaokwenda kufaidika na viwanda vya kupandisha thamani ya dhahabu ndani ya Tanzania kwamba JPM hakuacha legacy wanaweza wakakushangaa.
Ni rahisi sana kusema kuwa kodi zetu zinapofanya kazi yale matokeo yanayopatikana hayawezi kuitwa legacy. JPM ameacha urathi wa uthubutu. ameacha legacy ya ujasiri, ule moyo wenye kujivunia cha kwako mwenyewe hata kama kipo sawa sawa na nguo yenye viraka (vidabwada).
Apumzike kwa amani Hayati John Magufuli. Wenye kutazama masuala kwa kina wanajua ni kitu gani alikifanya kwa uwezo wake wote.